EVERTON wanakaribia kumrudisha tena Romelu Lukaku katika dimba lao la Goodison Park.
Mbelgiji huyo ni mshambuliaji chaguo la
kwanza la kocha Roberto Martinez majira haya ya kiangazi na anatarajia
kukamilisha usajili wake ndani ya saa 48 zijazo.
Martinez, aliyekuwa anamfikiria demba Ba
kama mbadala wa Lukaku, hakukubaliana na mshahara aliodai wa paundi
elfu 80 kwa wiki, na sasa anataka kumshawishi mbelgiji mwenye miaka 21
kumwaga wino katika kikosi chake cha msimu ujao.
Nyota wa mkopo: Lukaku alifanya vizuri alipokuwa Goodison Park mwaka jana na sasa Martinez anahitaji huduma yake tena.
Rada: Roberto Martinez amemweka Lukaku
kuwa chaguo la kwanza katika usajili wa majira haya ya kiangazi baada ya
kuonesha kiwango kikubwa msimu uliopita.
Inafahamika kuwa maandalizi makubwa ya kumrudisha Everton yamekamilika baada ya kurejea kutoka Austria walipoweka kambi.
Lukaku alikuwa anatarajia kusaini
Atletico Madrid, lakini kwa bahati mbaya ikawa tofauti kwasababu hakuwa
chaguo la kwanza la kocha Diego Simeone.
Wolfsburg pia walionesha nia kubwa ya
kumsajili kama ilivyokuwa kwa Tottenham, lakini Lukaku alifurahia maisha
Goodison na anapenda kuendelea kuisaidia klabu hiyo mpaka kufuzu ligi
ya mabingwa.
Majanga: Mshambuliaji huyu wa Ubelgiji
ameshindwa kuonesha kiwango cha kuivutia klabu yake mama (Chelsea) tangu
alipojiunga mwaka 2011.
Mkali: Mshambuliaji huyu aliifungia mabao 15 Everton msimu uliopita na alikuwa ndiye mfungaji bora wa klabu.
Martinez pia amefanya mazungumzo ya kumrudisha mchezaji aliyekuwa kwa mkopo, Monaco, Lacina Traore.
Pia yupo katika makubaliano ya kumsajili kiungo wa Bosnia ,Muhamed Besic, mwenye miaka 21, anayekipiga klabu ya Ferencvaros.
0 comments:
Post a Comment