HOME »
» ALIYECHEZA KOMBE LA DUNIA ATUA AZAM FC,
NI ALIYEFUNGA BAO LA ‘AJABU’ OLIMPIKI 2008 BEIJING
MSHAMBULIAJI
wa kimataifa wa Haiti, aliyecheza Kombe la Mabara mwaka ya Dunia la
FIFA jana nchini Brazil, Leonel Saint-Preux ametua Azam FC kwa ajili ya
kujiunga nayo kwa msimu ujao.
Kocha
Joseph Marius Omog raia wa Cameroon amesema amekuwa na mchezaji huyo
kwa siku mbili na atahitaji muda zaidi kumuona kabla ya kuamua kumsajili
au la.
Mshambuliaji
huyo aliyezaliwa Machi 12, mwaka 1985 in Cap-Haitien mara ya mwisho
alichezea klabu ya FELDA United F.C. ya Ligi Kuu ya Malaysia.
 |
| Mshambuliaji wa Haiti ametua Azam FC, je atasajiliwa? |
 |
| Hapa anacheza Kombe la Mabara dhidi ya Hispania |
Kisoka, Saint-Preux alianzia Zenith ya kwao, ambako alikuwa mkali wa mabao katika Ligia ya nchini humo.
Saint-Preux alisaini Minnesota Thunder ya Daraja la Kwanza Marekani Aprili 15, mwaka 2009, kabla ya kuhamia Hanoi ya Vietnam.
Machi 2010 alisiani mkataba wa awali na Aztex, lakini akatemwa baada ya kueli vipimo vya afya.
Kimataifa
Saint-Preux, alianzia kuchezea timu za vijana za Haiti wa umri tofauti.
Alikuwemo kwenye kikosi cha Haiti kilichofuzu michezo ya Olimpiki mwaka
2008 mjini Beijing, akifunga bao la kukumbukwa kutoka umbali wa mita 40
timu yake ikishinda 2-1 dhidi ya Canada.
Alianza
kuchezea timu ya wakubwa ya Hati mwaka 2007. Alifunga bao lake la
kwanza timu ya taifa ya Haiti Novemba 19, mwaka 2008 katika sare ya 1-1
Surinam. Haiti ilifungwa 10-0 na Hispania kwenye michuano hiyo.
0 comments:
Post a Comment