Naibu Waziri wa Habari, Vijana , Utamaduni na Michezo Mheshimiwa Juma Nkamia (kushoto) na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana , Utamaduni na Michezo Sihaba Nkinga(kulia) wakibadlishana mawazo leo mjini Dodoma wakati wa maandalizi ya kilele cha mbio za Mwenge wa Uhuru kinachotarajiwa kufanyika Oktoba 14 katika Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma ambapo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dokta Jakaya Mrisho Kikwete atakuwa mgeni rasmi.
Mfugaji wa Vipepeo kutoka mkoani Tanga Jane William akitoa ufafanuzi leo kwa wananchi waliofika katika maonyesho ya wiki ya vijana kwenye Uwanja wa Barafu mjini Dodoma jinsi ya ufugaji wa vipepeo kwa ajili ya biashara. Moanyesho hayo ni sehemu ya maadhimisho ya kilele cha Mwenge wa Uhuru ambapo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dokta Jakaya Mrisho Kikwete atakuwa mgeni rasmi.
Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Bibi Joyce Fissoo akitoa maelezo kwa Maafisa Utamaduni mbalimbali juu ya hatua wanazozichukua katika kukagua filamu za kuziwekea madaraja na stika za Mamlaka ya Mapato Tanzania ili kujenga uchumi wa Nchi. Maelezo hayo ameyatoa leo mjini Dodoma wakati wa wiki ya vijana ikiwa ni kuelekea kilele cha Mwenge wa Uhuru ambapo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dokta Jakaya Mrisho Kikwete atakuwa mgeni rasmi.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana , Utamaduni na Michezo Sihaba Nkinga (kulia ) akipata ufafanuzi wa hotuba na maandishi mbalimbali yaliyomo katika kitabu cha Mwalimu Nyerere cha Freedom and Unity leo mjini Dodoma wakati wa maonyesho ya wiki ya vijana . Kushoto ni Afisa Mipango Msaidizi wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere Edgar Atubonekisye (kulia) . Maonyesho hayo yanaenda sanjari na Kilele cha Mwenge wa Uhuru ambapo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dokta Jakaya Mrisho Kikwete atakuwa mgani rasmi tarehe 14.10.2015 mjini Dodoma.
0 comments:
Post a Comment