MATUKIO KATIKA PICHA YALIYO WEZA KUVUTIA DUNIANI KOTE

Asante kwa kututembelea mbeyagreennews kwa taarifa zaidi endelelea kututembela kila siku ,saa,dakika usipitwe na matukio kem kemu

MATUKIO KATIKA PICHA YALIYO WEZA KUVUTIA DUNIANI KOTE

Asante kwa kututembelea mbeyagreennews kwa taarifa zaidi endelelea kututembela kila siku ,saa,dakika usipitwe na matukio kem kemu

MATUKIO KATIKA PICHA YALIYO WEZA KUVUTIA DUNIANI KOTE

Asante kwa kututembelea mbeyagreennews kwa taarifa zaidi endelelea kututembela kila siku ,saa,dakika usipitwe na matukio kem kemu

MATUKIO KATIKA PICHA YALIYO WEZA KUVUTIA DUNIANI KOTE

Asante kwa kututembelea mbeyagreennews kwa taarifa zaidi endelelea kututembela kila siku ,saa,dakika usipitwe na matukio kem kemu

MATUKIO KATIKA PICHA YALIYO WEZA KUVUTIA DUNIANI KOTE

Asante kwa kututembelea mbeyagreennews kwa taarifa zaidi endelelea kututembela kila siku ,saa,dakika usipitwe na matukio kem kemu

Saturday, 31 May 2014

KULALA CHUMBA CHENYE MWANGA MKALI HUSABABISHA UNENE

lightKama ulikuwa hujui ngoja nikufahamishe, Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa huko nchini Uingereza umebaini kuwa kulala chumba chenye mwanga uliopitiliza kumehusishwa na mtu kuongeza unene wa kupindukia.

Timu ya watafiti kutoka Taasisi ya saratani ya jijini London imebaini kuwa wanawake wana nafasi kubwa ya kuongezeka unene kwa kulala vyumba vyenye mwanga mkubwa.
Hata hivyo utafiti huo unaonya kuwa hakuna ushahidi wa kutosha kuwa sasa watu waanze kununua mapazia mazito au ulazima wa kuzima taa wakati wa kulala.
Sasa jiulize kibongobongo hii imekaaje kutokana na mazingira ya nyumba zetu?

AFARIKI HOSPITALI BAADA YA KUCHELEWESHWA TOPEWA HUDUMA YA AFYA

mwanamke Unaweza kudhani matukio haya hutokea katika hospitali za kawaida tu. Hii ni ya kusikitisha zaidi na imetokea katika hospitali kubwa nchini Uingereza. 
Picha hii ya mwisho inamuonyesha mwanamke mmoja aliyekuwa amezidiwa hospitali na akashindwa kupatiwa dawa hadi kuamua kupiga magoti hospitali akibembeleza apatiwe dawa ya maumivu tu kutokana na kuzidiwa kwake lakini wauguzi hawakumsaidia chochote hadi umauti ulimkuta. mwanamke2 Siku mbili baada ya kutelekezwa na maafisa wa hospitali, mwanamama huyo Margaret Lamberty alipoteza maisha baada ugonjwa wake unaotibika kumzidi kutokana na kushindwa kupatiwa msaada. Margaret alifikishwa hospitali ya chuo kikuu cha A&E North Staffordshire nchini Uingereza na wanafamilia yake akiwa na maumivu makali ya tumbo, Mtoto wake kike aitwaye Laura amesema kuwa baada ya kufika hospitalini hapo wauguzi walikuwa wakimuangalia tu bila kumpa msaada wowote ndipo mama yake akaamua hadi kupiga magoti akiwaomba wampatie dawa ya maumivu lakini hakusikilizwa na mtu. mwanamke3 Hospitali hiyo imekumbwa na kashfa kubwa kwa sasa baada ya kifo cha mwanamke huyo ambapo familia inapanga kuishtaki kwa kushindwa kutimiza wajibu wao hadi kusababisha kifo cha ndugu yao.

RAIS MPYA WA MALAWI AAPISHWA RASMI LEO


 
Peter Muthirika anayeongoza chama cha DPP ndiye rais mteule nchini Malawi
Rais mpya wa Malawi Peter Mutharika ameapishwa rasmi baaada ya kucheleweshwa kwa matokeo ya uchaguzi kufuatia madai ya udanganyifu na wizi wa kura.
Mutharika aliibuka mshindi wa uchaguzi huo baada ya kujipatia zaidi ya asilimia 36 ya kura zilizopigwa.
Rais anayeondoka mamlakani Joyce Banda alikuwa katika nafasi ya tatu.
Banda amewataka wafuasi wake kuheshimu matokeo hayo.
Mahakama kuu ilipinga ombi la kura kuhesabiwa upya baada ya Banda kudai kuwa kumekuwa na udanganyifu mkubwa katika shughuli hiyo.
Peter Mutharika aliwahi kuhudumu kama waziri wa maswala ya kigeni na ndugu ya aliyekuwa rais wa taifa hilo marehemu Bingu wa Mutharika aliyefariki mwaka 2012 akiwa afisini.
Mwandishi wa BBC Baruan Muhuza amesema kutoka mjini Blantyre kuwa Profesa Peter Mutharika ameshinda uchaguzi huo kwa kupata asilimia 36.4 ya kura zote akifuatiwa na Dr Lazarus Chakwera mwenye asilimia 27.8 huku Rais anayemaliza muda wake Dr Joyce Banda akishika nafasi ya tatu kwa asilimia 20.2 na Atupele Muluzi amekuwa wa nne na asilimia 13.7
Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi Jaji Mackson Mbendera amesema uchaguzi huo ulikumbwa na changamoto nyingi lakini mwishowe nchi ikalazimika kupata kiongozi wake na akawaomba wananchi kuwa na utulivu .

ASILIMIA 25 YA WALIMU HUFUNDISHA' MAKOROKOCHO'

 

Dar es Salaam. Wakati Serikali ikiahidi kuboresha elimu nchini kwa kuhakikisha inaajiri walimu wa kutosha, imebainika kuwa asilimia 25 ya walimu huwafundisha wanafunzi mambo yasiyo ya msingi.
Ripoti ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (Unesco), iliyozinduliwa Dar es Salaam hivi karibuni, imebainisha kuwa wakati wananchi wakilalamika kuwa elimu inayotolewa haimsaidii mwanafunzi kupata ajira nzuri, wanafunzi hawajifunzi mambo ya msingi yatakayowasaidia kupambana na changamoto za maisha.(FS)
Akizindua ripoti hiyo, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk Shukuru Kawambwa alisema kuwa ripoti hiyo imeweka wazi ukubwa wa tatizo la ufundishaji, akieleza kwamba jumla ya watoto milioni 250, duniani wanakosa mafunzo ya msingi ya kusoma, kuandika na kuhesabu, ingawa wanaingia darasani.
“Tanzania kama sehemu ya dunia, haijakwepa tatizo hilo. Baadhi ya watoto wetu wamekuwa wakimaliza shule za misingi bila ya kuwa na ujuzi huo. Hii ni hali ya kushtua, inayohitaji nguvu za pamoja za wadau wote wa elimu duniani,” alisema Kawambwa.
Alibainisha kwamba ripoti hiyo imependekeza mpango wa elimu mwaka 2015, uzingatie ubora utakaotokana na mipango sahihi inayotekelezeka akitaka tatizo la walimu lipatiwe ufumbuzi wa kudumu kwa lazima ili kuwanusuru wanafunzi.
“Kama suala la walimu halitapatiwa ufumbuzi sasa, tofauti kwenye ufundishaji itakuwepo kwa vizazi vingi huku ikitoa tafsiri mbaya dhidi ya jitihada za kuondoa umaskini duniani na kufikiwa kwa maendeleo endelevu,” alisema Dk Kawambwa.
Aliongeza kuwa kwa namna hali ilivyo sasa, Serikali inalazimika kuhakikisha inaajiri walimu wenye dhamira ya kweli ya kufundisha na kutoa elimu bora.
Ripoti ya Unesco inaeleza kuwa licha ya kuwepo kwa mafanikio ya kuridhisha katika kipindi cha miaka kumi iliyopita, wananchi masikini ndiyo walioathirika zaidi na tatizo la utoaji elimu mbaya sababu ikiwa kutokuwepo kwa walimu wenye mafunzo ya kutosha.
Unesco ilisema kuwa kutokana na matatizo ya walimu, wanafunzi 130 milioni wanaosoma shule za msingi duniani, hawana uwezo wa kusoma hata sentensi moja, jambo linalowafanya washindwe kujiunga na sekondari.
“Matatizo ya elimu siyo tu yanaathiri malengo ya watoto ya baadaye, lakini pia uchumi wa Serikali hizo. Gharama ya watoto 250 milioni kutosoma elimu ya msingi ni Dola 129 bilioni za Marekani,(Sh 212.85 bilioni), ambayo ni asilimia kumi ya matumizi ya dunia katika elimu,” inasema ripoti hiyo. 
Ripoti hiyo imelinukuu shirikali lisilo la Serikali la Uwezo, linaloeleza kuwa asilimia 26 ya wanafunzi wa darasa la tatu ndiyo wanaoweza kusoma vizuri hadithi ya Kiswahili ya darasa la pili.
Akizungumza na gazeti hili kuhusu takwimu hizo, Mratibu wa Uwezo-Taifa, Zaida Mgalla alisema kuwa asilimia 44 ya wanafunzi wa darasa la tatu walifaulu jaribio la hisabati la darasa la pili, huku asilimia 11 pekee wakifaulu kusoma hadithi ya Kiingereza.
Zaida alisema walimu wamekata tamaa ya kufundisha kutokana na Serikali kushindwa kuwatimizia mahitaji ya msingi, huku pia heshima yao ikishuka mbele ya jamii.
“Walimu hawaheshimiwi, wanapigwa na wanafunzi, mtoto akipigwa na mwalimu anapiga simu polisi waje kumkamata mwalimu. Kwa hiyo walimu wamewasusa wanafunzi na wazazi nao wapo bize na kazi,” alisema Zaida.
Pia alisema wanafunzi hawafundishwi mambo ya msingi kutokana na walimu kutojua kitu wanachofundisha.
Hata hivyo, Unesco imeimwagia sifa Tanzania kwa kuongeza idadi ya wanafunzi  waliomaliza shule ya msingi kati ya mwaka 2000 na 2007, lakini ikasema kuwa asilimia 27 ya wanafunzi hao hawakujifunza mambo ya msingi.(CHANZO: MWANANCHI)
Vijana milioni 175 katika nchi zenye kipato cha chini na cha wastani ambao ni sawa na robo ya vijana duniani, hawana uwezo wa kusoma na kuandika. Katika nchi zilizopo chini ya Jangwa la Sahara, asilimia 40 hawajui kusoma wala kuandika.
“Ripoti inathibitisha kwamba lazima mtoto asome miaka minne ili aweze kujua kusoma na kuandika vizuri; kati ya wale waliosoma miaka minne au chini ya hapo, asilimia 77 hawawezi kusoma sentensi,” inasema ripoti hiyo.
Akisoma hotuba ya makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kwa mwaka 2014/2015 bungeni, Dodoma, Dk Kawambwa alisema kuwa vyuo vya Serikali na umma vimefanikisha upatikanaji wa walimu wapya 36,000 waliohitimu na kuajiriwa.
“Kati ya idadi hiyo, walimu wa masomo ya sayansi na hisabati ni 2,364, ngazi ya cheti 17,928, ngazi ya stashahada 5,416 na ngazi ya shahada 12, 994.  Ofisi ya Waziri Mkuu - Tamisemi imewaajiri na kuwapanga katika halmashauri mbalimbali nchini, hivyo kuendelea kupunguza kwa kiasi kikubwa tatizo la uhaba wa walimu ngazi mbalimbali,” alisema.
Waziri huyo alisema kuwa baada ya ajira ya walimu hao kufanyika, kwa sasa, taifa litabaki na upungufu wa walimu 30, 949 wa shule ya msingi na walimu 24, 596 wa sekondari katika masomo ya sayansi na hisabati.
Mhadhiri wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT), Emmanuel Mallya alisema kuwa walimu wanashindwa kuwafundisha wanafunzi mambo ya msingi kutokana na kukosa ubunifu wa kutumia mifano iliyopo kwenye jamii husika.
Pia alisema baadhi ya walimu waliingia katika taaluma hiyo baada ya kufeli katika masomo mengine, hivyo hawana uwezo mkubwa wa kuchambua mambo mapya na muhimu kwa wanafunzi hao.

MYIKA AISHUKIA SERIKALI UTOROSHAJI FEDHA NJE YA NCHI

 

    Msemaji wa kambi hiyo, John Mnyika ambaye amesema katika kipindi cha miaka 39 kuanzia 1970 hadi 2008, Sh9.6 trilioni zilitoroshwa kiharamu kwenda nje.
    Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, imeilipua Serikali kwa kushindwa kudhibiti utoroshwaji mkubwa wa fedha kwenda nje.
    Msemaji wa kambi hiyo, John Mnyika alisema katika kipindi cha miaka 39 kuanzia 1970 hadi 2008, Sh9.6 trilioni zilitoroshwa kiharamu kwenda nje.
    "Utoroshaji wa fedha hizi unasadikiwa kutokana na ukwepaji wa kodi, na misamaha mikubwa ya kodi," alisema Mnyika na kuongeza; "Fedha nyingine zilitokana na usiri mkubwa wa mikataba baina ya wawekezaji na Serikali, upotoshaji wa bei katika biashara na rushwa katika mikataba na wawekezaji" alisema.
    Mnyika alisema Serikali ya CCM haiwezi kukwepa kuwajibika kwa sababu utoroshaji wa mapesa yote haya umefanyika wakati na CCM ipo madarakani, " alisema.
    Mnyika alifafanua, utoroshaji huo wa fedha ulifanyika kwa mafungu na kutolea mfano mwaka 1980, Dola 570. 6 milioni zilitoroshwa.
    Fedha hizo zilitoroshwa wakati hayati baba wa Taifa mwalimu Jullius Nyerere akiwa madarakani na dola 1,566 milioni zikatoroshwa 1985 wakati wa Rais Ali Hassan Mwinyi.
    "Jambo la kusikitisha zaidi mwaka 2002 zilitoroshwa jumla ya Dola za Marekani 1,1010 milioni katika kipindi ambacho Rais Benjamin Mkapa yuko madarakani," alisema Mnyika.
    Mnyika alisema kambi hiyo imesikitishwa na kitendo cha Bunge kushindwa kuisimamia kikamilifu Serikali hususan Wizara ya Nishati na Madini.
    Alisema fedha zote zilizotoroshwa nchini tangu mwaka 1970 mpaka 2008 zinaweza kurejeshwa nchini kwa kuanzia na kuzibaini zilipo.
    "Uchunguzi wa kina ufanyike kuzuia fedha hizo katika akaunti za benki zilipotunzwa nje ya nchi na hatimaye kurejesha fedha hizo nchini," alisema.
    Kitengo cha Financial Intelligence Unit (FIU) cha Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kimetakiwa kukusanya taarifa za kiintelijensia na kuziwasilisha Takukuru ili uchunguzi ufanyike.
    Chanzo: Mwananchi

    MWANAFUNZI WA KIDATO CHA PILI AFARIKI DUNIA BAADA YA KUGONGWA NA GARI


    msangi 
    TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI
    “PRESS RELEASE” TAREHE 31.05.2014.
    • MWANAMKE MMOJA AUAWA KWA KUKATWA NA KITU CHENYE NCHA KALI SEHEMU MBALIMBALI ZA MWILI NA MUME WAKE.
    • MTU MMOJA AUAWA NA KUNDI LA WANANCHI WALIOAMUA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI KWA TUHUMA ZA WIZI.
    • MWANAFUNZI WA DARASA LA TATU AFARIKI DUNIA BAADA YA KUDONDOKA NA KISHA KUKANYAGWA NA POWERTILLER.
    • MWANAFUNZI WA KIDATO CHA PILI AFARIKI DUNIA BAADA YA KUGONGWA NA GARI.
     JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA WATU WANNE KUTOKANA NA TUHUMA MBALIMBALI.
     KATIKA TUKIO LA KWANZA:
    MWANAMKE MMOJA ALIYETAMBULIKA KWA JINA LA CHRISTINA HAYOLA (35) MKAZI WA KIJIJI CHA LIWALANJE, ALIKUTWA AMEUAWA KWA KUKATWA KITU CHENYE NCHA KALI KICHWANI, KIFUANI NA MGUU WA KULIA  NA MUME  WAKE AITWAYE MUSSA NSAGAJE @ MWAULAMBO.
    MWILI WA MAREHEMU ULIKUTWA MNAMO TAREHE 30.05.2014 MAJIRA YA SAA 06:00 ASUBUHI HUKO KATIKA KIJIJI CHA MAGAMBA, KATA YA ISANZA, TARAFA YA IGAMBA, WILAYA YA MBOZI MKOA WA MBEYA. INADAIWA KUWA CHANZO CHA TUKIO HILO NI UGOMVI ULIOTOKANA NA WIVU WA KIMAPENZI ULIOTOKEA WAKIWA KILABUNI USIKU.
     MTUHUMIWA ALIKIMBIA MARA BAADA YA TUKIO. JUHUDI ZA KUMTAFUTA ZINAENDELEA.
    KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA ZA MAHALI ALIPO MTUHUMIWA WA TUKIO HILI AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI AKAMATWE NA HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAKE, VINGINEVYO AJISALIMISHE MWENYEWE.
     KATIKA TUKIO LA PILI:
     MTU MMOJA ALIYETAMBULIKA KWA JINA LA ABDI SANGA (20) MKAZI WA ISANGA ALIUAWA KWA KUPIGWA SEHEMU MBALIMBALI ZA MWILI WAKE  NA KUNDI LA WANANCHI WALIOAMUA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI WAKITUMIA SILAHA ZA JADI FIMBO, MAWE NA RUNGU.
     TUKIO HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE 31.05.2014 MAJIRA YA SAA 03:45 USIKU WA KUAMKIA LEO HUKO ENEO LA FOREST YA ZAMANI KATA YA FOREST, TARAFA YA  SISIMBA JIJI NA MKOA WA MBEYA. INADAIWA KUWA CHANZO CHA TUKIO HILI NI TUHUMA ZA WIZI BAADA YA  MAREHEMU NA MWENZAKE MMOJA AMBAYE ALIFANIKIWA KUKIMBIA KUINGIA NYUMBANI KWA KASSIM ISSA (28)  MKAZI WA FOREST NA KUIBA VITENGE VYENYE THAMANI YA  TSHS 70,000/=,  MHANGA ALIPIGA KELELE ZA KUOMBA MSAADA, HIVYO KUNDI LA WATU WALIJITOKEZA NA KUMSHAMBULIA. 
     KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA TABIA YA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA INA MADHARA MAKUBWA NA BADALA YAKE WAWAFIKISHE WATUHUMIWA WANAOWAKAMATA KWA TUHUMA MBALIMBALI KATIKA MAMLAKA HUSIKA KWA HATUA ZAIDI ZA KISHERIA.
     KATIKA TUKIO LA TATU:
     MWANAFUNZI WA DARASA LA TATU KATIKA SHULE YA MSINGI IBUMILA ALIYETAMBULIKA KWA JINA LA FATINA FESTO @ MWANDOSYA (12) MKAZI WA KIJIJI CHA MAHONGOLE ALIFARIKI DUNIA PAPO HAPO BAADA YA  KUDONDOKA KUTOKA  KWENYE POWER TILLER ILIYOKUWA IKIENDESHWA NA AIZACK MWASHANGWA (22) MKAZI WA MAHONGOLE.
    TUKIO HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE 30.05.2014 MAJIRA YA SAA 15:30 ALASIRI HUKO KATIKA KIJIJI CHA IBUMILA-MAHONGOLE, KATA YA SONGWE-IMALILO, TARAFA YA RUJEWA, WILAYA YA MBARALI, MKOA WA MBEYA. WAKATI TUKIO HILO LINATOKEA MAREHEMU NA WENZAKE WALIKUWA WANATOKA KUVUNA MPUNGA WA SHULE. CHANZO CHA AJALI KINACHUNGUZWA. DEREVA ALIKIMBIA NA KUACHA POWER TILLER MARA BAADA YA TUKIO.
     KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA ZA MAHALI ALIPO MTUHUMIWA [DEREVA] AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI AKAMATWE NA HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAKE, VINGINEVYO AJISALIMISHE MWENYEWE.
    KATIKA TUKIO LA NNE:
    MWANAFUNZI WA KIDATO CHA PILI KATIKA SHULE YA SEKONDARI MAKONGOLOSI ALIYEMBALIWA KWA JINA LA ADEN PETER @NGOMBE (17) MKAZI WA MAKONGOLOSI AMEFARIKI DUNIA PAPO HAPO BAADA YA KUGONGWA NA GARI LENYE NAMBA ZA USAJILI T.117 APK/T.150 AVM AINA YA SCANIA LILILOKUWA LIKIENDESHWA NA DEREVA AITWAYE ALLY MOSHI (35) MKAZI WA MBARALI.
    TUKIO HILO LA AJALI LIMETOKEA MNAMO TAREHE 30.05.2014 MAJIRA YA SAA 13:00 MCHANA HUKO KATIKA KIJIJI NA KATA YA MAKONGOLOSI, TARAFA YA KIWANJA WILAYA YA CHUNYA MKOA WA MBEYA KATIKA BARABARA YA MAKONGOLOSI/LUPA. CHANZO CHA AJALI DEREVA ALIKUWA AMELEWAPOMBE. MTUHUMIWA AMEKAMATWA NA GARI LIPO KITUO CHA POLISI – MAKONGOLOSI.
     KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI WATUMIAPO VYOMBO VYA MOTO HASA KWA KUZINGATIA SHERIA NA ALAMA ZA BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI. AIDHA ANAENDELEA KUTOA WITO KWA WATEMBEA KWA MIGUU KUFUATA NA KUZINGATIA ALAMA ZA USALAMA BARABARANI IKIWA NI PAMOJA NA KUTEMBEA PEMBENI MWA BARABARA NA KUVUKA KATIKA MAENEO YENYE VIVUKO VYA KUVUKIA ILI KUEPUKA AJALI
    TAARIFA YA MISAKO:
    KATIKA MSAKO WA KWANZA:
    JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAMSHIKILIA MTU MMOJA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA MWIYULEGHE MBUGHI (60) MKAZI WA KIJIJI CHA ITENTULA AKIWA ANAMILIKI BILA KIBALI SILAHA /BASTOLA MOJA AINA YA   BABY YENYE NAMBA 946663 ILIYOTENGENEZWA NCHINI UBELGIJI IKIWA NA RISASI TATU [03] KWENYE MAGAZINE.
    MTUHUMIWA ALIKAMATWA MNAMO TAREHE 30.05.2014 MAJIRA YA SAA 01:00 USIKU WA KUAMKIA LEO HUKO KATIKA KIJIJI CHA ITENTULA, KATA YA   BARA, TARAFA YA ITAKA, WILAYA YA MBOZI, MKOA WA MBEYA. MTUHUMIWA ALIKUWA AMEKUFICHA SILAHA HIYO CHUMBANI NDANI YA   NYUMBA YAKE. TARATIBU ZA KUMFIKISHA MAHAKAMANI ZINAENDELEA.
     KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA KWA JAMII KUACHA KUJIMILIKISHA SILAHA KINYUME CHA SHERIA NA BADALA YAKE WAFUATE TARATIBU ZA UMILIKAJI WA SILAHA KIHALALI.
    KATIKA MSAKO WA PILI:
    JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAMSHIKILIA MTU MMOJA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA DEZDERIS JACKSON (30) MKAZI WA KIJIJI CHA SAZA AKIWA NA KETE 17 ZA BHANGI KWENYE KIBANDA CHA KUUZA SABUNI SAWA NA UZITO WA GRAM 85.
    MTUHUMIWA ALIKAMATWA MNAMO TAREHE 30.05.2014 MAJIRA YA SAA 11:00 ASUBUHI HUKO KATIKA KIJIJI CHA SAZA, KATA YA   MKWAJUNI,   TARAFA YA   KWIMBA, WILAYA YA CHUNYA, MKOA WA MBEYA. MTUHUMIWA NI MTUMIAJI NA MUUZAJI WA BHANGI.
    KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA KUTUMIA DAWA ZA KULEVYA KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI.
    KATIKA MSAKO WA TATU:
    MTU MMOJA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA EVA WILSON (23) MKAZI WA KIJIJI CHA BWAWANI ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA AKIWA ANAUZA  POMBE KALI ZILIZOPIGWA MARUFUKU NA SERIKALI[VIROBA] AINA YA  BOSS PAKETI 51.
    MTUHUMIWA ALIKAMATWA MNAMO TAREHE 30.05.2014 MAJIRA YA SAA 14:00 MCHANA HUKO KATIKA KITONGOJI NA KIJIJI CHA BWAWANI, KATA YA MAKONGOLOSI, TARAFA YA   KIWANJA, WILAYA YA CHUNYA, MKOA WA MBEYA.
    KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII HASA WAFANYABIASHARA KUACHA KUJIHUSISHA NA UUZAJI WA BIDHAA ZILIZOPIGWA MARUKUFU NA SERIKALI KWANI ZINA MADHARA KIAFYA KWA WATUMIAJI.
    KATIKA MSAKO WA NNE:
    MTU MMOJA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA ESTER MWALUGAJA (34) MKAZI WA KIJIJI CHA MAMBA-F ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA AKIWA   POMBE HARAMU YA MOSHI [GONGO] UJAZO WA LITA MBILI [02].
    MTUHUMIWA ALIKAMATWA MNAMO TAREHE 30.05.2014 MAJIRA YA SAA 14:00 MCHANA HUKO KATIKA KITONGOJI CHA MTANDE, KIJIJI CHA MAMBA -F, KATA YA   MAMBA, TARAFA YA   KIPEMBAWE, WILAYA YA CHUNYA, MKOA WA MBEYA.
    TARATIBU ZA KUWAFIKISHA MAHAKAMANI WATUHUMIWA ZINAENDELEA.

                KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA KUTUMIA POMBE HARAMU YA MOSHI [GONGO] KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI. AIDHA ANATOA WITO KWA JAMII KUENDELEA KUTOA TAARIFA ZA WATU WANAOJIHUSISHA NA MTENGENEZAJI NA UUZAJI WA POMBE HARAMU YA MOSHI.
    Imesainiwa na:
    [AHMED Z. MSANGI – SACP]
    KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.

    SERIKALI YATOA ZAIDI YA SHILINGI 6.7 BILIONI KUJENGA HOSPITALI YA RUFAA SINGIDA

    DSC_0473 
    Katibu Mkuu wa CCM Taifa Abdulrahamani Kinana akiongozwa na Mkuu wa Moa wa Singida Dk, Parseko Kone, Katibu Tawala Lianna Hassan na viongozi wengine wa Mkoa wa Singida kukagua hatua iliyofikiwa ya ujenzi wa hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Singida, wakati Kinana alipokuwa Mkoani Singida kwa ziara ya kikazi ya siku saba.

    MKUU wa Mkoa wa Singida,Dk.Parseko Vicent Kone amesema serikali imetoa zaidi ya shilingi 6.7 bilioni kwa ajili ya kugharamia ujenzi wa hospitali ya rufaa ya mkoani hapa iliyoko kijiji cha Madewa nje kidogo ya Singida mjini.
    Dk.Kone amesema hospitali hiyo itakapokamilika,itahudumia wagonjwa kutoka mikoa yote ya kanda ya kati.
    Mkuu huyo alitoa rai hiyo wakati akitoa akitoa taarifa yake kwa katibu mkuu CCM taifa,Abrahamani Kinana aliyetembelea hospitali hiyo hivi karibuni.
    Amesema mkoa umetegewa eneo la ekari 283 kwa ajili ya uendelezaji wa mradi wa hospitali hiyo, ambayo itakuwa ya mfano hapa nchini.
    Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dk Dorothy Gwajima amesema lengo la mradi huo ni kuimarisha huduma za afya mkoani pamoja na mikoa jirani.
    DSC_0429 
    Katibu Mkuu wa CCM akiweka saini kwenye kitabu cha hospitali ya Rufaa huku Naibu Katibu Mkuu wake Mwigulu Nchemba na mkuu wa Mkoa wa Singida Kone wakishuhudia.
    Dk.Gwajima amesema mradi huo utakapomalizika,utakuwa na majengo 29 yatakayotumika kutoa huduma mbali mbali.
    Mganga huyo mkuu,amesema changamoto inayowakabili ni pamoja na uhaba wa watumishi,nyumba za kuishi watumishi na ufinyu mdogo wa bajeti ya dawa kutoka bohari kuu ya madawa (MSD).
    Kwa upande wake Kinana,alitumia fursa hiyo kumpongeza Dk.Kone kwa utendaji kazi wake ambao umesaidia kujengwa kwa hospitali hiyo.
    DSC_0446
    Mganga mkuu wa hospitali ya Mkoa wa Singida (RMO) Bi. Doroth Bwajima akisoma taarifa ya ujenzi wa hospitali hiyo.
    Amesema baada ya mradi huo kukamilika mkoa wa Singida utaondokana na matatizo ya huduma za afya.
    “Ili kumuunga mkono Dk.Kone kwa hili jambo nzuri la ujenzi wa hospitali ya rufaa ambayo itasaidia Watanzania wengi kupata huduma ya afya kwa kiwango kizuri,nitahakikisha nina muunganisha na baadhi ya marafiki zangu wa ndani na nje ya nchi ili waweze kusaidia kumalizika kwa ujenzi wa hospaitali hii inayovutia”,amesema Kinana.
    DSC_0453Mganga mfwawidhi wa hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Singida, Dkt Joseph Malunda, akiwaonesha michoro ya hospitali hiyo viongozi walioambatana na Kinana.
    DSC_0463 
    Viongozi mbalimbali wa mkoa huo wakimsikiliza Dkt Malunda.


    (Picha na Zainul Mzige wa modewjiblog).
    Na Nathaniel Limu, Singida

    MSHAMBULIAJI RICKIE LAMBERT AWASILI LIVERPOOL KUPIMA AFYA


    On his way: Rickie Lambert (left, next to Adam Lallana) has arrived at Liverpool for his medical

    MZAZI WA SERGIO KUN AGUERO ASEMA MWANAE ANAPENDA KWENDA BARCELONA


    Passion: Sergio Aguero's father claims he would 'love' to go to Barcelona amid reports of a £31m bid
    Keen: New Barcelona head coach Luis Enrique is an admirer of Aguero and is driving the Catalans' bid
    Aguero mwenye miaka 25, ana uhusiano mzuri na nyota wa Barcelona, Lionel Messi na Enrique anaamini kuwa kuwaweka pamoja kunaweza kuisaidia klabu na Argentina kwa ujumla.
    Mkataba wa Aguero utamalizika mwaka 2017, lakini klabu yake inaweza kumuuza zaidi ya paundi milioni 36 walizotumia kumsajili mwaka 2011.
    Aguero alikuwa na msimu mzuri Etihad licha ya kuwa na majeruhi. Alifunga magoli 28 na kuwasaidia Man City kubeba kombe la ligi kuu na Capital One.
    Star: Aguero scored 28 goals in 34 games last season as Man City won the Premier League and League Cup

    MBEYA CITY FC YACHAPWA 1-0 NA VICTORIA UNIVERSITY ROBO FAINALI



     DSCF5413
    Na Baraka Mpenja, Dar es salaam

    Imechapishwa Mei 31, 2014, saa 1:52 usiku
    WAWAKILISHI wa Tanzania katika michuano ya CECAFA Nile Basin Cup, Mbeya City fc wameaga mashindano hayo baada ya kufungwa bao 1-0 dhidi ya Victoria University ya Uganda katika mchezo wa robo fainali uliomalizika dakika chache zilizopita mjini Khartoum.
    Mbeya City wametolewa katika michuano hiyo wakiwa wameshinda mechi moja, kufungwa moja na kutoka suluhu mechi moja katika hatua ya makundi.
    Lakini wamepoteza mechi ya pili katika mashindano haya baada ya kufungwa hatua ya robo fainali na kufungashiwa virago.
    Afisa habari wa Mbeya City fc, Freddy Jackson amesema wanashukuru kwa kilichotokea kwani ndio matokeo ya mpira wa miguu.
    Freddy amesema wachezaji wamejitahidi kucheza kwa juhudi, lakini hawakuwa na bahati.
    “Ndugu tunashukuru kwa maombi yenu,  alichotupangia mungu ndicho tulichopata.  Mechi imemalizika , Mbeya city O victoria 1, hivyo basi tumeyaaga mashindano”. Amesema Freddy.

    UGANDA YATINGA HATUA INAYOFUATA , RWANDA YAIKANYAGA LIBYA 3-0


    Football - 2014 Fifa World Cup Qualifier - Uganda Vs Angola - Mandela Stadium - Namboole - Kampala 

    UGANDA The Cranes imefanikiwa kusonga hatua inayofuata katika michuano ya kuwania kupangwa hatua ya makundi kusaka tiketi ya kucheza fainali za kombe la mataifa ya Afrika, AFCON 2015 nchini Morocco baada ya kufanikiwa kuiondosha Madagascar kwa wastani wa mabao 2-2, lakini Uganda wamenufaika kwa faida ya bao la ugenini.
    Uganda jioni hii wameibuka na ushindi wa bao 1-0 mjini Kampala katika mchezo wa marudiano, na mechi ya kwanza walilala kwa mabao 2-1 nchini Madagascar.
    Kusoma zaidi bofya www.bkmtata.blogspot.com
     Na Baraka Mpenja, Dar es salaam

    Friday, 30 May 2014

    MATOKEO RASMI YA MALAWI PETER MUTHARIKA ASHINDA UCHAGUZI

     
    Peter Muthirika anayeongoza chama cha DPP ndiye rais mteule nchini Malawi
    .............................................................................
    Hatimaye Malawi imepata Rais mpya baada ya mivutano ya kisheria kwa wiki nzima. 

    Mwandishi wa BBC Baruan Muhuza amesema kutoka mjini Blantyre kuwa Profesa Peter Mutharika ameshinda uchaguzi huo kwa kupata asilimia 36.4 ya kura zote akifuatiwa na Dr Lazarus Chakwera mwenye asilimia 27.8 huku Rais anayemaliza muda wake Dr Joyce Banda akishika nafasi ya tatu kwa asilimia 20.2 na Atupele Muluzi amekuwa wa nne na asilimia 13.7
    Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi Jaji Mackson Mbendera amesema uchaguzi huo ulikumbwa na changamoto nyingi lakini mwishowe nchi ni lazima ipate kiongozi wake na kuwaomba wananchi kuwa na utulivu .

    Kesi Mahakamani
    Awali Jaji Kenyata Nyirenda wa mahakama kuu mjini humo jana usiku alitoa uamuzi kuwa hawezi kuvunja sheria kwa kuruhusu tume iongeze muda wa kuhesabu upya kura kwenye maeneo yenye utata.

    Na kwamba sheria inaitaka tume kutangaza matokeo ndani ya siku nane na si vinginevyo.

    Uchaguzi wa Malawi ulifanyika Mei 20 nchini kote lakini siku moja tu baada ya kupiga kura, malalamiko yakiambatana na mapingamizi ya kisheria yakatawala kwenye mahakama kuu za Lilongwe na Blantyre.

    KILI MUSIC TOUR YAPAMBA MOTO MKOANI MWANZA

     wasanii wawasili kwenye Kili Music Tour

    KILI MUSIC TOUR 2014 MWANZA (10)
    Baadhi ya wasanii watakaotoa burudani katika tamasha la Kili Music Tour litakalofanyika katika Uwanja wa CCM Kirumba JIjini Mwanza Jumamosi. Show hii inayodhaminiwa na Bia ya Kilimanjaro Premium Lager ni ya pili kati ya kumi zitakazofanyika katika mikoa mbali mbali nchini.na Baathi ya m
    KILI MUSIC TOUR 2014 MWANZA (15)
    IMG_8514
    Meneja wa Bia ya Kilimanjaro Premium Lager, George Kavishe akizungumza na waandishi wa habari kuhusu tamasha la Kili Music Tour litakalofanyika katika Uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mbeya Jumamosi huku akiwa ameameongozana na baadhi a wasanii watakaotoa burudani katika tamasha hilo kubwa.

    ANGALIA AJALI YA DIRECTOR GEORGE TYSON

    Gari alilopata nalo ajali Director George Tyson na picha za saa 4 kabla ya tukio

    Screen Shot 2014-05-31 at 3.46.30 AM 
    Dj Choka ambae kwa sehemu kubwa alikua kwenye safari moja ya Dodoma na Marehemu George Tyson, ameandika kwenye http://djchokamusic.com/ kwamba Marehemu alikuwa yupo kijiji cha Chilonwa Chamwino kwenye utoaji wa madawati katika shule ya msingi Chaula iliyopo Dodoma.
    Baada ya kumaliza shughuli hii huku akiwa kama producer wa The Mboni Show mauti yalimkuta majira ya saa 12 jioni ikiwa ni saa 4 tu toka tuanze safari ya kurudi Dar es Salaam maeneo fulani hivi kama unataka kukaribia GAIRO mjini.
    Kwenye gari walikuwa watu 8 ila yeye pekee ndio aliyepoteza maisha ila wengine wamepata majeraha mwilini akiwemo dereva wa gari hilo ambapo kwa sasa mwili wa marehemu umehifadhiwa hapa Morogoro katika hospital ya mkoa Morogoro baadae asubuhi safari ya kurudi Dar es Salaam itaanza.
    Screen Shot 2014-05-31 at 3.46.12 AM
    Screen Shot 2014-05-31 at 3.46.38 AM
    Screen Shot 2014-05-31 at 3.46.50 AM
    Kwenye hii safari, George Tyson aliambatana na mtangazaji Mboni Masimba wa The Mboni show.
    Screen Shot 2014-05-31 at 3.46.58 AM
    Screen Shot 2014-05-31 at 3.47.07 AM

    KURASA ZA MAGAZETI MAY 31 2014 MBEYAGREENNEWSBLOG

    .






    .
    .
    .
    .
    .
    .
    .
    .
    .
    .
    .
    .
    .
    .
    .
    .
    .
    .
    .
    .
    .
    .
    .
    .
    .
    .
    .
    .
    .
    .
    .
    .


    .
    .
    .
    .
    .
    .
    .
    .
    .
    .

    PETER MUTHARIKA WA DPP ASHINDA UCHAGUZI NCHNI MALAWI

     

    DPP CANDIDATE PETER MUTHARIKA HAS WON  ELECTION  TONIGHT WITH MORE THAN 1.9 MILLION VOTES AGAINST THE INCUMBENT PRESIDENT JOYCE BANDA WHO SCORED ONLY 1 MILILION VOTES. (FRIDAY SIMBAYA) (SOURCE: AL JAZEERA NEWS)

    FIFA YAWATAKA HISPANIA KUBADILISHA JEZI ZAO

      KWA SABABU WALIZOTOA SASA ZINAFANANA NA ZA UHOLANZI

    HISPANI wametakiwa kubadilisha jezi zao Kombe la Dunia baada ya FIFA kuamua jezi zao za sasa zinafanana na za Uholanzi.
    Wasambazaji wa nguo za Hispania, Adidas wamesema jana kwamba FIFA wameagiza Hispania ichapishe jezi ya tatu- nyeupe - ambayo wataitumia katika mchezo wao wa kwanza na Brazil.

    Clash: Spain's new kit, modelled by Andres Iniesta, Xabi Alonso and Pedro (left) is too similar to Holland's kit, worn by Gregory van der Wiel (right)
    Clash: Spain's new kit, modelled by Andres Iniesta, Xabi Alonso and Pedro (left) is too similar to Holland's kit, worn by Gregory van der Wiel (right)
    Mgongngano: Jezi mpya za Hispania, znazoonyeshwa na Andres Iniesta, Xabi Alonso na Pedro (kushoto) zinafanana sana na za Uholanzi

    FIFA intaka kila timu iwe na aina mbili za jezi katika kila pea kwa ajili ya mashindano hayo - moja yenye range nyepesi na nyingine nzito. 
    Jezi za Hispania ni nyekundu kwa mechi za nyumbani na nyeusi kwa mechi za ugenini, wakati Uholanzi kwa kawaida huvaa range ya chungwa nyumbani na bluu ugenini waliyopanga kuvaa dhidi ya Hispania wakati timu hizo zitakapokutana katika mechi za Kundi B Juni 13. 

    ZITTO KABWE AFUNGUKA ATOA UFAFANUZI MZURI KUHUSU TANAPA NA NSSF


    Nasikitika kwamba katika hali niliyonayo ya kumwuguza mama yangu naingizwa kwenye siasa za majitaka.

    Kampuni ya LekaDutigite inamilikiwa na wasanii. Gombe Advisors ni kampuni isiyofanya faida (Company limited by guarantee) na haina maslahi yeyote ya kibiashara.

    Wasanii wa Kigoma wamefanya kazi na TANAPA na NSSF, kazi ambazo zinajulikana na zipo.

    Leo mpigie simu mfanyakazi yeyote wa NSSF utasikia kazi ya wasanii hao. Kwa namna yeyote ile hii ni ishara ya kukosa ubinaadam maana waliyoyasema wanajua sina faida yeyote ya kifedha Leo wala kesho kwa LekaDutigite na Gombe Advisors.

    Kipindi ambacho mama yangu yupo mahututi, tena mjumbe wa kamati kuu ya chama chao, pole ninayopewa ndio hiyo.

    Hakuna namna ya kukosa ubinaadamu zaidi ya hivi.

    Zitto Zuberi Kabwe: Hata hivyo, ni vema CAG afanye ukaguzi haraka sana na Mimi binafsi nitawajibika iwapo itaonekana kwa namna yeyote ile nina maslahi ya kifedha katika LekaDutigite na gombe advisors.

    By Zitto Kabwe

    ---------------------------

    Maelezo zaidi kutoka kwa Zitto Kabwe