Saturday, 3 August 2013

WANANCHI NA WAKAZI WA MBALIZI MBEYA WAGOMBANIA MAFUTA BAADA YA LORI KUPINDUKA

 

 Lori lenye namba za usajili  T97 AJL lenye tela namba T746 BKF lilipo acha njia na kupinduka na kuziba njia

Lori  likishindwa kupita baada ya Mafuta kumwagika Barabarani na kusababisha barabara kushindwa kupitika
Magari yakipita kwa shida baada ya Lori kudondoka
Askari wakijitahidi kukabiliana na watu waliokuwa wanachota mafuta
Shughuli za uokoaji zikiendelea kulia ni Dereva wa Lori hilo baada ya kunusurika
Dereva wa gari hilo Hassan Abdi (35) akiwa haamini kilicho tokea baada ya Kunusurika kifo


YALE YALE!!! Wananchi  wenye ndooo Haya.... Wenye Madumu haya .... wenye Masefuria haya... wote walikuwepo kuchota Mafuta kama inavyo onekana ... bila kujali kama yaweza kulipuka 
Wananchi Mbalimbali wakiwa wanapata shida kupita baada ya Lori kudondoka

Askari wa zima moto wakiwa wanaendelea na Juhudi za kuondoa mafuta barabarani kwa maji 
Wananchi mbalimbali wakiwa wanaondoka na Mafuta... huku wengine wakiendelea kuchota
Wakina mama... Watoto... Vijana na wazee wakiwa wanapata shida jinsi ya kupita baada ya ajali



Ezekiel Kamanga
Watu wawili wamenusurika kifo baada ya roli la mafuta lenye namba za usajili T 978 AJL lenye tela namba T 746 BKE Aina ya SCANIA walilokuwa wakisafiria kutoka DAR ES SALAAM kwenda ZAMBIA kuacha njia na kupinduka katika mteremko wa MBALIZI barabara MBEYA TUNDUMA.
Dereva ametambuliwa kwa jina la HASSAN ABDI 35 na msaidizi wake SAIMON SOVELA 23 ambao walikuwa wametokea DAR ES SALAAM kuelekea ZAMBIA likiwa limejaa shehena ya mafuta
Kwa mujibu wa Dereva amesema kuwa gari hilo ghafla lilipoanza kuteremka mteremko liliharibika mfumo wa breki na mbele yake kukiwa na magari matano baada ya kuona kuwa angesababisha maafa makubwa aliamua kulichepusha pembeni ndipo lilipoacha njia na kupinduka na kumwaga shehena ya mafuta.
Kikosi cha zimamoto kilifika eneo la tukio na kuhakikisha usalama wa eneo hilo kuhofia mlipuko wa moto ambao ungeweza kutokea kutokana na baadhi ya wananchi kuanza kuchota mafuta yaliyokuwa yanatiririka.
Pamoja na juhudi za Jeshi la Polisi kudhibiti wananchi kutochota mafuta lakini wananchi walikaidi na kuendelea kuchota mafuta.
Ajali hiyo ilisababisha adha kubwa kwa wasafiri waliokuwa wana pita barabara hiyo wakiwemo wagonjwa na waliokuwa wanawahi usafiri wa ndege majira ya saa saba mchana.

Habari na mbeya yetublog

0 comments: