Harare. Baada ya kumalizika kwa Uchaguzi Mkuu wa Zimbabwe huku Rais Robert Mugabe akiibuka kidedea kwa mara ya saba, waangalizi wa Umoja wa Ulaya (EU), Umoja wa Afrika (AU), na Jumuiya ya Kiuchumi ya Kusini mwa Afrika (SADC), wametofautiana kuhusu matokeo hayo.
Wakati waangalizi AU na SADC wakisema uchaguzi huo ulikuwa huru na haki, wenzao wa EU wamesema kulikuwa na kasoro kadhaa.
Hata hivyo, AU na SADC walisema kulikuwa na hitilafu katika daftari la wapigakura kwani baadhi hawakuruhusiwa kupiga kura wakati walikuwa na haki ya kufanya hivyo.
Waangalizi wa EU wameeleza wasiwasi wao juu ya
kutokukamilika kwa ushiriki wa wapigakura na kwamba kulikuwa na udhaifu
kwenye mchakato wa upigaji kura pamoja na ukosefu wa uwazi.
Kwa upande wake, Tume ya Uchaguzi ya Zimbabwe
(ZEC), ilisema uchaguzi ulikuwa huru na wa haki, licha ya hitilafu
mbalimbali zilizojitokeza.
Mwenyekiti wa Tume hiyo, Solomon Zwana, alisema iwapo kuna chama ambacho hakijaridhishwa na matokeo, kinaweza kufuata njia za kisheria.
“Tuna imani vyama vitaheshimu ahadi walizoweka
kwamba watafuata njia za kisheria na si kuanzisha vurugu. Hilo ndilo
tumaini letu na ujumbe wetu kwa wadau wa kisiasa,” alisema Zwana.
Zuma wa kwanza kumpongeza Mugabe
Rais wa Afrika Kusini, Jacob Zuma amempongeza Rais
mteule wa Zimbabwe, Robert Mugabe kwa kuchaguliwa tena kuliongoza taifa
hilo la Kusini mwa Afrika.
Katika salamu zake, Rais Zuma aliwataka wapinzani kukubaliana na matokeo hayo kwa ajili ya kudumisha amani nchini humo.”
Zuma anaonekana kutofautiana na misimamo ya Marekani, Uingereza na Australia, zilizokataa kukubaliana na ushindi wa Mugabe.
Uchaguzi wa Zimbabwe umemrudisha madarakani Mugabe
kwa ushindi wa asilimia 61 dhidi ya aliyekuwa Waziri wake Mkuu, Morgan
Tsvangirai aliyeambulia asilimia 34.
Na Mwandishi Wetu, Mwananchi
Posted Jumatatu,Agosti5 2013
Na Mwandishi Wetu, Mwananchi
Posted Jumatatu,Agosti5 2013
0 comments:
Post a Comment