MATUKIO KATIKA PICHA YALIYO WEZA KUVUTIA DUNIANI KOTE

Asante kwa kututembelea mbeyagreennews kwa taarifa zaidi endelelea kututembela kila siku ,saa,dakika usipitwe na matukio kem kemu

MATUKIO KATIKA PICHA YALIYO WEZA KUVUTIA DUNIANI KOTE

Asante kwa kututembelea mbeyagreennews kwa taarifa zaidi endelelea kututembela kila siku ,saa,dakika usipitwe na matukio kem kemu

MATUKIO KATIKA PICHA YALIYO WEZA KUVUTIA DUNIANI KOTE

Asante kwa kututembelea mbeyagreennews kwa taarifa zaidi endelelea kututembela kila siku ,saa,dakika usipitwe na matukio kem kemu

MATUKIO KATIKA PICHA YALIYO WEZA KUVUTIA DUNIANI KOTE

Asante kwa kututembelea mbeyagreennews kwa taarifa zaidi endelelea kututembela kila siku ,saa,dakika usipitwe na matukio kem kemu

MATUKIO KATIKA PICHA YALIYO WEZA KUVUTIA DUNIANI KOTE

Asante kwa kututembelea mbeyagreennews kwa taarifa zaidi endelelea kututembela kila siku ,saa,dakika usipitwe na matukio kem kemu

Friday, 28 June 2013

LORI LA MAFUTA LA ANGUKA KIBAHA WATU NA MADUMU YAO MKONONI

Picture
Lori moja la kubebea bidhaa ya mafuta ya vyombo vya moto likiwa limeanguka eneo la Kongowe, Kibaha kama lilivyokutwa na mpiga picha jioni ya leo. Wananchi wanaonekana na vyombo vya kubebea, wamelizungukaa kana kwamba hawajali hatari inayoweza kutokea kama zilivyotokea nyingine siku zilizopita.

CHEKA NA UTANI WA MBEYAGREENNEWS.BLOGSPORT.COM

     Picture

Thursday, 27 June 2013

UEFA EURO 2016 KUFANYIKA NCHINI UFARANSA



UEFA EURO 2016 ITAFANYIA NCHINI UFARANSA, AMBAPO LOGO KWA AJILI YA MICHUANO HIYO IMESHATOLEWA.
 

MWANANCHI TATHIMINI MIAKA MIWILI YA BUNGE:JE? WABUNGE WETU WAMEWAJIBIKA IPASAVYO

Swali muhimu kwa mwananchi yeyote, Je, Mbunge wangu aliwakilishaje maslahi yangu Bungeni? Njia moja ya kutathmini utendaji wa Wabunge ni kutazama idadi ya ushiriki wao Bungeni.

       Muhtasari unaoitwa Je, waliwajibika? Tathmini ya miaka miwili ya Bunge 2010-2012 uliyoandaliwa na Twaweza kwa kushirikiana na Centre for Economic Prosperity (CEP).

Muhtasari unachambua data zinazopatikana kwenye       tovuti ya Bunge, kuhusu ushiriki wa kila Mbunge wakati wa vikao vya Bunge. Bunge ndio mhimili wa demokrasia, likiwakilisha wapiga kura katika namna 
wanavyohusiana na dola. Twaweza na CEP zinatoa tathmini ya utendaji wa Wabunge kwa ujumla, kwa kila chama, kwa kila Mbunge na kwa aina ya ushiriki.

Uchambuzi umeonyesha kwamba Wabunge wanaotoka katika vyama vidogovidogo na vyenye viti vichache huwa na wastani wa juu zaidi wa ushiriki. Tathamini hii inazingatia ushiriki uliofanywa na Wabunge katika miaka miwili ya kipindi cha ubunge cha 2010 – 2015. Wabunge wanaweza kushiriki kwa namna tatu: kwa kuuliza maswali ya msingi, maswali ya nyongeza na kutoa michango. 
         Katika namna zote hizi, TLP ambacho kina mbunge mmoja na NCCR-MAGEUZI watano, vilikuwa na kiwango kikubwa zaidi chaa ushiriki kwa Mbunge. Hata hivyo, ukiondoa vyama vidogovidogo vyenye chini ya asilimia 5 ya uwakilishi Bungeni, CHADEMA kinafanya vema zaidi, kikifuatiwa na CUF na CCM.

 

KONGAMANO LA WAZI NA UZINDUZI WA MPANGO WA KULETA MATOKEO MAKUBWA SASA KWA WIZARA YA NISHATI NA MADINI

KONGAMANO LA WAZI NA UZINDUZI WA MPANGO WA KULETA MATOKEO MAKUBWA SASA KWA WIZARA YA NISHATI NA MADINI

Waziri wa Nishati na Madini, Mhe. Profesa Sospeter Muhongo (Mbunge), anawaalika wadau wote wa Sekta ya Nishati na Madini kote nchini kwenye kongamano la wazi litakalofanyika siku ya Jumatano Julai 3, 2013 kwenye Ukumbi wa Mlimani City, Mwenge Jijini Dar es Salaam, kuanzia saa 3.00 asubuhi hadi saa 11.00 jioni.

Mada kuu ni kujadili, kushauri na kutoa maoni juu ya miradi mikubwa ya kitaifa ya sekta ya nishati itakayotekelezwa na Wizara ya Nishati na Madini kwa kipindi cha miaka mitatu, Julai 2013 – Disemba 2015 ili kuliwezesha Taifa kufikia Matokeo Makubwa Sasa (Big Results Now).

Wadau wanaoalikwa ni pamoja na:

Mabenki washirika, Wakandarasi kwenye sekta ya Umeme, Wahandisi kutoka Taasisi na Vyuo Vikuu nchini, Mashirika ya Kiserikali na yasiyo ya kiserikali, Wawakilishi kutoka Makampuni mbalimbali, Migodi, Viwanda vikubwa na vidogo na wananchi wote kwa ujumla.

Hakuna kiingilio kwenye uzinduzi huo.

“Matokeo Makubwa sasa kwa maendeleo ya Mtanzania”

Imetolewa na:
Katibu Mkuu, Wizara ya Nishati na Madini

 

Tuesday, 25 June 2013

JAJI BOMANI AVIONYA VYOMBO VYA USALAMA KUA VIFUATE MISINGI YA SHERIA



http://www.mwananchi.co.tz/image/view/-/1638570/highRes/434731/-/guqhon/-/jaji_bomani.jpg
Mwanasheria Mkuu mstaafu wa Tanzania Jaji Mark Bomani, amevitaka vyombo vya ulinzi na usalama vya nchi hiyo kufuata misingi ya sheria katika utendaji wao wa kazi. 

Jaji Bomani amevitaka pia vyombo vya usalama vya Tanzania kuzingatia sheria katika matumizi ya silaha kwenye matukio mbalimbali wanayokabiliana nayo. 
              Kauli hiyo ameitoa wakati wa Kongamano la Maadili ya Waandishi wa Habari lililofanyika jijini Dar es Salaam likiwa na kaulimbiu ya 'Wajibu wa Vyombo vya Habari Kupambana na Kauli za Chuki na Itikadi Kali.' 
Mwanasheria Mkuu mstaafu wa Tanzania ameongeza kuwa, kumekuwa na tabia ya baadhi ya vyombo vya dola kuwapiga watu bila kufuata sheria ambazo zinakataza kufanya hivyo, lakini mambo hayo yanatokana na uelewa mdogo. 
   Amesema,  hata maandamano na mikutano yoyote inapozuiwa pia ni lazima vigezo na sheria zifuatwe ili kila mmoja au kinachofanyika kimezingatia sheria na si uonevu au upendeleo.

ANCELOTTI ATUA HISPANIA AWA MENAGER MPYA WA REAL MADRID



http://www.libero.pe/sites/default/files/imagecache/Resize_img_full_node/nodo_imagen_principal/oker.jpg
VIGOGO wa Hispania, Real Madrid wametangaza katika tovuti yao kuingia Mkataba wa miaka mitatu na kocha Mtaliano, Carlo Ancelotti ambaye atatambulishwa kwa Waandishi wa Habari Jumatano.

Real madrid imethibitisha carlo Ancelotti ataondoka paris-saint-German kuja kurithimikoba ya 
Jose morinho aliyeondoka mapema mwezi huu.Madrid iliamua mara moja kumchukua Ancelotti, kufuatia Mourinho kutimkia Chelsea, lakini PSG awali iligoma kumuachia kocha huyo mwenye umri wa miaka 54.
    
  Hata hivyo,wamekubali skumruhusu Ancelotti kuondoka baada ya kumteua Laurent Blanc kurithi mikoba yake, ambaye wamemtangaza leo.
   "Real Madrid itamtambulisha Carlo Ancelotti kama kocha wao mpya kwa misimu mitatu ijayo, Jumatano ya Juni 26,"imesema taarifa ya klabu hiyo katika tovuti yao.

"Shughuli itafanyika Santiago Bernabeu katika Royal Box saa 7:00 mchana.  Kisha Carlo Ancelotti atakuwepo mapema."

      Ancelotti amekuwa kocha wa PSG tangu Desemba 2011 na ameiongoza timu hiyo kutwaa taji lao la tatu laLigue 1 kihistoria kwa mara ya kwanza ndani ya miaka 19.
Awali alizifundisha kwa mafanikio Chelsea na AC Milan, wakati pia alifundisha Juventus, Parma na Reggiana katika hatua zake za mwanzoni za ukocha.

WAFUNGWA 4 WANYONGWA NCHINI NIGERIA

 
 
 
Wafungwa wanne wamenyongwa kusini mwa Nigeria, katika kile maafisa wanasema kuwa hukumu ya kwanza ya kunyongwa kutekelezwa kwa miaka saba.
Kamishna wa haki katika jimbo la Edo, Henry Idahagbon, aliambia waandishi wa habari kuwa wafungwa hao walinyongwa baada ya kuhukumiwa kifo kwa makosa ya wizi wa mabavu na mauaji.
Shirika la Amnesty International lilisema kuwa hatua hiyo ya uwanyonga wafungwa ni jambo la kuhuzunisha sana kwa watetezi wa haki za binadamu nchini Nigeria.
Zaidi ya wafungwa 1,000 nchini Nigeria wanaaminika kuhukumiwa kifo .

   Vyombo vya habari nchini humo vinasema kuwa Rais Goodluck Jonathan hivi karibuni aliwataka magavana wa majimbo kutia saini vibali vya hukumu ya kifo katika jitihada za serikali kupunguza visa vya uhalifu.
     
         Bwana Idahagbon alisema kuwa wananume wanne walinyongwa katika gereza la Benin baada ya mahakama kuamuru wanyongwe siku ya Jumatatu.
Alisema kesi zote za rufaa, hazikuweza kufua dafu na hukumu zao tayari zikuwa zimetiwa saini -mbili na magavana wa Edo Governor Adams Oshiomhole, huku nyingine zikitiwa saini na magavana wa majimbo mengine.

            Ikiwa itathibitishwa , hatua hii ya kunyongwa ni ishara ya kurejea kwa sheria kali ya hukumu ya kunyongwa nchini Nigeria.
Wahudumu wa magereza ndio waliotekeleza hukumu ya kunyongwa , kitengo cha serikali wala sio jimbo la Edo.
Kulikuwa na ripoti za kutatanisha kuhusu hali ya mfungwa wa tano.

       Chino Obiagwu wa kitengo cha sheria na mradi wa kuwasaidia wafungwa hao alisema kuwa mwanaume huyo alinyongwa.
Hukumu ilicheleweshwa kwa muda kwa sababu za kiufundi lakini baadaye wakapashwa habari kwa njia ya barua pepe, alisema bwana Obiagwu.

             Lakini bwana Idahagbon alisema mwanaume huyo hakunyongwa kwa sababu hukumu yake ilisema kuwa auawe kwa kupigwa risasi.
Hata hivyo shirika la Amnesty International limesema kuwa limepokea habari zinazoweza kuthibitisha kuwa wafungwa wanne walinyongwa mjini Benin.

 

MZEE MANDELA HALI BADO NITETE YUPO MAHUTUTI

 

Hali ya Mandela inasemekana kuwa mbaya
Familia ya rais mstaafu Nelson Mandela, imemtembelea hospitalini, mzee Mandela ambaye anasifika kwa vita alivyopigana dhidi ya utawala wa wazungu nchini nAfrika Kusini.
     Hali ya Mandela inasemekana kuwa mbaya sana na hakuna habari zaidi zimetolewa kuhusu ikiwa imeimarika tangu ilipotangazwa Jumapili jioni.
       Amekuwa akiugua ugonjwa wa mapafu mara kwa mara na hii ni mara ya tatu kwa Mandela kulazwa hospitalini mwaka huu.
Rafiki na jamaa wameendelea kukusanyika katika hospitali alikolazwa Mandela mjini Pretoria kumtakia afya njema mzee Mandela.
   
      Mmoja wa waliomtembelea Mandela , mfanyabiashara Calvin Hugo, aliawachilia huru njiwa weupe, kama heshima yake kwa Mandela anaeyendelea kuugua hospitalini.
Alisema kitendo chake kilikuwa ishara ya, hatua ya Mandela kuikwamua nchi ya Afrika Kusini kutoka kwa mkoloni.

    Baadhi ya jamaa zake wamekusanyika nyumbani kijijini eneo la Qunu, kujadili kile wanachosema ni habari muhimu sana.

TAARIFA KWA UMMA : KUHAMISHWA KWA OFFISI YA MAKAO MAKUU YA BODI YA MIKOPO YA ELIMU YAJUU

Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu inawajulisha wadau wake wote kuwa Ofisi yake ya Makao Makuu inahama kutoka Jengo la TIRDO, Barabara ya Kimweri, Msasani kwenda Kiwanja Na.. 8, Kitalu Na. 46, Barabara ya Sam Nujoma, Mwenge, Dar es Salaam kufikia Juni 30, 2013.

Katika kipindi cha kuhama, Bodi itahakikisha huduma zinarejea katika hali ya kawaida ndani ya siku chache.

Aidha uombaji wa mikopo kwa njia ta mtandao upo kama kawaida, na hivyo waombaji wa mikopo wanaweza kuendelea na utaratibu wa kuomba mikopo. Hata hivyo, huduma ya simu kwa waombaji wa mikopo imesitishwa kwa muda wakati mitambo ikifungwa na huduma itaendelea kama kawaida kuanzia Jumanne Juni 25, 2013.

Bodi inaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaotokea wakati ikijiweka sawa katika makazi mapya.

Imetolewa na:

Mkurugenzi Mtendaji,
Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu,
Kiwanja Na.. 8, Kitalu Na.. 46, Barabara ya Sam Nujoma, Mwenge
S.L.P. 76068, Dar es Salaam, Tanzania.

Simu: +255 22 2669036/2669037
Faksi: +255 22 2669039
Barua pepe:
info@heslb.go.tz
Tovuti : www.heslb.go.tz


 

ASKARI ALINICHANIA NGUO NIKABAKI UCHI MBELE YA BABA YANGU (ARUSHA)

Nukuu za alichokisema Wema Malisa baada ya kufukuwa na Polisi Juni 18, 2013 katika Uwanja wa Soweto, Arusha ambapo watu kadhaa walikukusanyika ili kuwaaga watu wanne waliokufa kwenye mlipuko wa bomu katika mkutano wa CHADEMA, Jumamosi ya Juni 15, 2013 katika uwanja uo huo.
Picture: Wema Malisa
Wema Malisa
Nilikuwa namfuata baba yangu ambaye ni kada wa CHADEMA. Kutokana na ulemavu wake nilihofu angepata matatizo kama vurugu zingezuka.

Nilikuta uwanja ukiwa umefurika wananchi wakiwasikiliza viongozi wa Chadema. Viongozi hao ni Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema ambaye alihutubia na kumwachia Tundu Lissu naye akamwachia Said Arfi. Alipomaliza kuwataka wanachama hao waelekee Hospitali ya Mount Meru, ndipo mabomu yakaanza kulipuliwa.

Nilimwambia baba tuondoke lakini tulikuwa tumeshachelewa, polisi walikuwa wametuzingira. Bomu la pili liliangukia mbele yetu. Askari mmoja akasema ‘laleni chini’, tukalala tukidhani 
tutakuwa salama. Lakini walikuja askari na kutupiga marungu mwili mzima mimi na baba.

Ghafla akatokea askari mwingine akawakataza wasitupige, tukadhani tumeokoka. Mara wakatokea askari wengine, hapo ndipo kilikuwa kipigo kitakatifu. Nilijaribu kuwazuia wasimpige baba kwa kuwa ni mlemavu, wakanikebehi kuwa huyo ni hawara yangu. Walinipiga mpaka mkono na mguu ya kushoto ikavunjika.

Tulikuwa kwenye kibaraza cha nyumba wakati askari wanatupiga. Askari mmoja alirarua gauni langu chini na juu, hadi nikabaki uchi mbele ya baba. Mwingine akakoki bunduki na kuielekeza katikati ya mapaja yangu ili alipue sehemu za siri, wenzake wakamkataza. Mwingine alisema kuwa atanibaka. Baba alinikumbatia akasema watuue wote, mimi niliomba wasituue maana nimeacha mtoto mchanga nyumbani.

Walisema ‘unajifanya wewe CHADEMA, sasa ndiyo utajua kuwa CCM inatawala. Chezea CCM wewe.’ Mimi niliwaambia sina chama chochote nimekuja kumwokoa baba yangu. Wakati huo wote walishanivua hereni, simu wakachukua na fedha zilizokuwa ndani ya pochi na kuitupa chini ikiwa tupu.

Alitusikitikia na kusema, ‘kwa nini mnang’ang’ania kuwa Chadema? Angalieni sasa mlivyoumia na viongozi wenu wamewakimbia.’ Akaokota kanga iliyoachwa uwanjani na kuja kunifunika... Kisha likaja gari la polisi tukabebwa na kuingizwa humo. Mwendo tuliondoka pale ulikuwa wa kasi huku wakiendelea kulipua mabomu na kutukanyaga bila kujali. Tulishtukia tuko Hospitali ya Mount Meru, tukabwagwa hapo na gari hilo likaondoka.
KAULI YA Mzee Malisa
Kilichonisikitisha ni kitendo cha kumpiga na kumdhalilisha mwanangu mbele yangu. Askari wengine walikuwa wakijaribu kuvunja hili gongo ninalotembelea kwa sababu ya ulemavu

Nimesikitishwa na kauli ya Waziri Mkuu Mizengo Pinda aliyoitoa hivi karibuni Bungeni Dodoma ya kuwataka askari waendelee kupiga wananchi. Kwa hali hii sisi wanyonge natuna pa kukimbilia.”
Nukuu kutoka kwenye habari katika gazeti: Mwananchi.
 

 

WATU ZAIDI YA 10 WANUSURIKA KUFA KATIKA AJALI JANA JIONI ENEO LA UYOLE MBEYA

























PICHA ZOTE NA MICHAEL - UYOLE

TAARIFA KAMILI INAKUJA  endelea  kutembelea mtandao huu wa

MBEYAGREENNEWS.BLOSPORT.COM
 

WAHADHIRI WA CHUO KIKUU CHA TEKU WA WEKA MGOMO WA KUTO TUNGA MITIHANI NA HALI SI SHWARI NDAN CHUO HICHO

 

 
 Kaimu Mwenyekiti wa TEKUASA Amani Simbeye akifungua mkutano kati ya waandishi wa Habari na Waahadhiri wa Chuo kikuu cha Teofilo Kisanji(TEKU)
Waahadhiri wa Chuo kikuu cha Teofilo Kisanji(TEKU)  wakifuatilia kwa umakini kikao  hicho wakati kikiendelea
  Kaimu Mwenyekiti wa TEKUASA Amani Simbeye pamoja na katibu wake wakisikiliza kwa umakini wahadhiri wakichangia hoja
  Mmoja wa Waahadhiri wa Chuo kikuu cha Teofilo Kisanji(TEKU) , akikazia jambo  ya yale ambayo yalikuwa yamezungumzwa
 
 
 Waahadhiri wa Chuo kikuu cha Teofilo Kisanji(TEKU)  wakiwa wanaimba wimbo wa Solidarity 
Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo Dr. Daniel Mosses Akiwa anauficha Uso akihofia kupigwa picha na kuhojiwa na waandishi wa Habari kuhusiana na Mgogoro unao endelea  Chuoni hapo 

***************

HALI si Shwari  Ndani ya Chuo Kikuu cha Teofilo Kisanji (TEKU) baada ya Uongozi wa Chama cha Wahadhili wa Chuo hicho (TEKUASA) na wanachama wake kutangaza mgomo wa kutotunga mitihani ya kufungia Mhula, Mitihani ambayo inatarajiwa kufanyika Julai Mosi Mwaka huu kwa kile walichodai Menejimenti ya Chuo kutotoa majibu ya matatizo yao.

Mgomo huo  umetangazwa jana  na Kaimu Mwenyekiti wa Tekuasa Amani Simbeye katika Mkutano na waandishi wa habari uliofanyika katika ukumbi wa Chuo hicho kilichopo  Block T kata ya Iyela Jiji na Mkoa wa Mbeya na kuhudhuriwa na zaidi ya Wahadhili 30.
Simbeye amesema kuna mambo mengi na changamoto za elimu inayotolewa Chuoni hapo ambazo Menejimenti ya 

Chuo inahusika moja kwa moja hivyo kuhatarisha mustakabali wa Elimu Nchini hususani inayotolewa Chuoni hapo ambapo ameongeza kuwa zaidi ya yote ni kukosa ushirikishwaji wa maamuzi yanayohusu Taaluma.

Kwa taarifa zaidi na madai ya Wahadhili hao hadi kupelekea kususia kutunga mitihani ya kumaliza muhula inatarajiwa kufanyika Julai Mosi Mwaka huu yameandikwa kwenye  barua hapo chini lakini habari kamili itawajia baadaye kwa Lugha ya Kiswahili endelea kuwa nasi.




kwa msaada wa MBEYA YETU blog

Monday, 24 June 2013

MBUNGE WA CCM AHOFIA TANZANIA KUWA NA RAIS "SHOGA"


http://www.ippmedia.com/media/picture/large/Ally-Kessy.jpgMBUNGE wa Nkasi Kaskazini, Ali Keissy (CCM), amesema kuwa bila Watanzania kuwa makini na sheria mpya ya ndoa ijayo, huenda nchi ikapata rais, wabunge na madiwani wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja (mashoga).

Keissy alitoa kauli hiyo wakati akichangia mada katika mkutano wa siku tatu wa Chama cha Wabunge cha Kupambana na Ukimwi (TAPAC) uliomalizika jana mjini Dodoma.

Mbunge huyo aliwaomba viongozi wa dini kukemea kwa nguvu vitendo hivyo, pia alipinga hatua ya wazazi kuwapeleka watoto wao wadogo shule za bweni akidai kuwa huko ndiko wanakojifunza vitendo hivyo.

“Mnashindwa kulea watoto wenu, mnawapeleka shule za bweni wakiwa na miaka mitatu ili walelewe kizungu. Huko watapakwa mafuta ya KY na wataingiliwa,” alisema.

Keissy alitolea mfano mkutano mmoja uliofanyika jijini Dar es Salaam kuwa uliwashirikisha mashoga 400, jambo alilodai ni ishara kwamba wanaojihusisha na vitendo hivyo wanaongezeka, na hivyo kuitaka serikali kuwapiga marufuku.

Hata hivyo, baada ya mbunge huyo kuhitimisha mchango wake, mmoja wa vijana wanaojihusisha na mapenzi hayo ya jinsia moja, Abdilah Ally ambaye alikuwa amealikwa na TAPAC, alitetea kuwa jamii inapaswa kukubali kwamba matendo hayo yanafanyika.

“Tunatambua kuwa sheria haziruhusu vitendo hivi, lakini vipo na vinafanyika na tunapata maambukizi kwa kiwango kikubwa. Tunachokitaka tusinyanyapaliwe na jamii, bali tupewe huduma ya afya ya kujikinga na maambukizi.

“Mathalani mimi hapa nina wapenzi wanaume watatu ambao nashiriki nao mapenzi, sasa kama nimeathirika ina maana wote wale nao wamethirika,” alisema.

Akifunga mkutano huo, Naibu Waziri wa Jamii, Jinsia na Watoto, Ummy Mwalimu, aliwasihi wanasiasa wasiwabague makundi ya watu wanaojihusisha na vitendo vya ushoga, usagaji na matumizi ya dawa za kulevya.

Alisema kuwa makundi hayo yanakabiliwa na janga la maambukizi makubwa ya virusi vya ukimwi, hivyo wanahitaji kusaidiwa kuondoka katika makundi hayo badala ya kuwahukumu.
Mwalimu alifafanua kuwa miongoni mwa washiriki wa mkutano huo kutoka katika makundi hayo, alikuwa mtumiaji wa dawa za kulevya, lakini baada ya kupata msaada wa kiafya ameachana na vitendo hivyo na sasa anaendelea vizuri chini ya uangalizi.

Mkutano huo uliratibiwa na Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania (TACAIDS), kama wadau wakuu waliotoa mada mbalimbali kuhusu jinsi wanavyopambana kupunguza maambukizi mapya ya virusi vya ukimwi.

Katika hilo, Mwalimu alisema kuwa serikali dhamira yake ni kufikia maambukizi asilimia sifuri, hasa kwa kutoa msukumo mkubwa kwa makundi ya wanawake, vijana na watoto ambayo yana maambukizi zaidi.

Mbunge wa Chambani visiwani Zanzibar, Yusuf Salam Hussein (CUF), alisema kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imefanikiwa kupunguza maambukizi hayo kwa wanandoa kutokana na sheria ya kuwataka wapime ukimwi kabla ya kufunga ndoa.
CHANZO: TANZANIA DAIMA

KAULI YA MP JOSEPH MBILINYI(SUGU) KUHUSU W/MKUU

Kauli ya Jumamosi, Juni 22, 2013
PictureKauli ya Jumatatu, Juni 24, 2013:
Katuni ya Masoud “Kipanya” ...ghasia za kuleta amani!

HALI YA RAIS MANDELA BADO TETE

 
Hali  ya rais  wa  zamani  wa  Afrika  kusini,Nelson Mandela ,imeendelea kuwa mbaya katika  hospitalini mjini  Pretoria  ikiwa  ni  siku  ya  pili leo tangu  Rais Jacob Zuma alipomtembelea na kusema  shujaa  huyo  wa kupambana  na ubaguzi  wa  rangi  alikuwa  amelala. 
Nelson Mandela

Rais Jacob Zuma  amewaambia  waandishi  habari  wapatao  60 kuwa madaktari  wanafanya kila  linalowezekana  kurejesha hali  yake  kuwa  bora wakati  anatimiza  siku  ya  17 hospiatalini. Mandela  alilazwa  hospitalini  mjini  Pretoria mapema  mwezi  huu  akisumbuliwa  na  maambukizi katika  mapafu. Ni  mara  ya  nne kwa kiongozi  huyo  wa zamani  mwenye  umri  wa  miaka  94 kulazwa hospitali tangu  Desemba  mwaka  jana  akipatiwa  matibabu. 


Zuma pia  amesema  kuwa  madaktari  wamesema  hali  ya  rais huyo  wa  zamani  imekuwa  mbaya  katika  muda  wa  saa 24 zilizopita. Mandela  alifungwa  jela  miaka  27  wakati  wa utawala  wa  kibaguzi . Alichukua  nafasi  ya  juu  katika kuibadilisha  nchi  hiyo  kuwa  ya  kidemokrasia , na amekuwa  rais  wa  kwanza  wa  Afrika  kusini  mwenye asili  ya  nchi  hiyo mwaka 1994.

CHADEMA YASEMA POLISI WANAKAMATA WAFUASI WAKE KWA KUSHINIKIZWA

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimelishutumu kwa Jeshi la Polisi kwamba wafuasi wa chama hicho wanaokamatwa kwa makosa mbalimbali, wamekuwa wakishinikizwa watamke kuwa wametumwa na viongozi wao  waandamizi kufanya vitendo hivyo.

Mkurugenzi wa  Habari na Uenezi wa CHADEMA, John Mnyika, akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, alisema wafuasi wa chama hicho walioshinikizwa ni wale waliokamatwa na polisi hivi karibuni wakihusishwa na kummwagia tindikali kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mussa Tesha, tukio lililotokea mwaka 2011.

Mnyika aliwataja waliokamatwa kuwa ni Oscar Kaijage, aliyekamatwa mkoani Shinyanga, Seif Magesa Kabuta, ambaye alikamatwa mkoani Mwanzai, Evodius Justinian, alitiwa mbaroni mkoani Kagera na Henry Kilewo, ambaye alikamatwa jijini Dar es Salaam.

Alisema wafuasi hao baada ya kukamatwa wameshinikizwa kusema kuwa Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe; Katibu Mkuu, Dk. Willibrod Slaa; Mkurugenzi wa Sheria na Katiba wa Chama hicho na Mbunge wa 
Singida Mashariki, Tundu Lissu na Mkurugenzi wa Habari na Uenezi, Mbuge wa Ubungo, John Mnyika kuwa ndiyo waliowatuma kutenda kosa hilo.

Alisema Evodius Justinian, alikamatwa mjini Bukoba na baadaye akapelekwa mkoani Mwanza na kuletwa jijini Dar es Salaam ambako amefichwa hadi sasa hajulikani aliko.

Mnyika alisema taarifa za kada huyo kuletwa Dar es Salaam zilikuwa za kificho kwani wakili wake Nyaronyo Kicheere, akiongozana na ndugu wa mtuhumiwa huyo walifika Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam na kuelezwa kuwa amepelekwa makao makuu.

Msemaji wa Jeshi la Polisi, Advera Senso,  alipotafutwa jana hakupatikana kutokana na simu yake kuita bila kupokelewa.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kagera, Philip Kalangi, alipoulizwa alithibitisha mtuhumiwa huyo kukamatwa baada ya kupewa taarifa kutoka makao makuu kwamba amefanya kosa Igunga ambako walimsafirisha kumpeleka huko.

Kamanda Kalangi alisema taarifa za kwamba baada ya kukamatwa alishinikizwa awataje viongozi wake waandamizi, hafahamu kama Jeshi la Polisi linaweza kufanya hivyo.

“Polisi hatuwezi kulenga mwanachama wa chama fulani, tunashughulika na wahalifu,” alisema.

Mnyika alisema mtuhumiwa wa pili ni Seif Magesa Kabuta aliyekamatwa Mwanza ambaye baada ya kukataa kukiri kuwa viongozi wake wanahusika na matendo hayo, walimfungia katika chumba maalum wakamleta mke wake, mama yake mzazi na mkwe wake na kumtesa mbele yao.

Kamanda wa Polisi Mkoa Mwanza, Ernest Mangu, alisema hana taarifa za kada huyo wa CHADEMA kwamba alikamatwa katika mkoa wake.

“Kwanza taarifa za kwamba huyo Seif Kabuta, tulimkamata Mwanza sina na kwasababu hiyo siwezi kuwa na majibu kama analazimishwa kuhusika na tukio la kummwagia tindikali kada wa CCM,” alisema.

Mtuhumiwa wa tatu aliyekamatwa mkoani Shinyanga kwa kuhusishwa na tukio hilo la tindikali ni Oscar Kaijage.

Mnyika alisema baada ya mtuhumiwa huyo kukamatwa, awali aliambiwa ni kwa sababu kuna fedha zimepotea kwa njia ya simu na yeye alikuwa anajishughulisha na uwakala wa fedha kwa njia ya mitandao ya M-Pesa, na Z-Pesa.

Alisema baadaye alipokutanishwa na makachero wa polisi makao makuu, alielezwa kuwa amekamatwa kwa kosa la kuhusika na tukio la kummwagia tindikali kada wa CCM,  Mussa Tesha.

Kamanda wa Polisi mkoani Shinyanga, Evarist Mangala, alipoulizwa alisema hana taarifa za kumatwa mtu huyo kutoka katika mkoa huo.

Mtuhumiwa wa nne ni Rajab Kihawa, ambaye anadaiwa kupigiwa simu na mwanamke asiyemfahamu na baadaye akakutanishwa na maofisa wa polisi ambako anadaiwa aliombwa akubali kupewa Sh. milioni 30 ili akubali kusema kuwa Mbowe na wenzake waliwatuma kummwagia tindikali Tesha.

Mtuhumiwa wa mwisho ni Henry Kilewo, Katibu wa CHADEMA wa Wilaya ya Kinondoni na Katibu wa Makatibu wa CHADEMA Kanda Maalum ya Dar es Salaam ambaye anadaiwa aliitwa Polisi bila kuambiwa anakwenda kuhojiwa juu ya suala gani.

Hata hivyo, alipofika makao makuu ya Polisi alidai walisita kumwambia, lakini walishauriana baadaye wakamwambia anatuhumiwa kummwagia Tesha tindikali.

---
Imeandikwa na THOBIAS MWANAKATWE
Imenukuliwa kwenye gazeti la NIPASHE
 

ALITAKA KUJIUWA MARA MBILI KWA HALI ALIYO NAYO YA MARADHI


 Picture


 Ama kwa hakika, wangenga walisema, “Hujafa Hujaumbik
 Sylvester Karanja aliezea masaibu yake ya jinsi alivyozaliwa katika hali ya kawaida kama binadamu wengine wasio na ulemavu wa aina yoyote ile, hadi alipopatwa na kipele katika ujana wake, kipele ambacho kilibadili muonekano wake na kumsababishia sononi ambayo ilimsukuma kutaka kuutoa uhai wake.

Alisimulia kuwa alijaribu mara mbili kufanya hivyo lakini kila mara alipojaribu, alikwama.

Saturday, 22 June 2013

HAFLA FUPI A KUAGWA KWA SPIKA SITTA

 
Picture
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza kabla ya kukabidhi zawadi zake pichani kwa Spika mstaafu. Samuel Sitta katika hafla ya kumuaga Spika huyo kwenye viwanja vya Bunge Mjini Dodoma Juni 21, 2013. Kushoto kwake ni mkewe Tunu na wengine kutoka kulia ni Mkewe Spika Mstaafu, Margareth Sitta, Spika mstaafu, Samuel Sitta na Spika wa Bunge, Anne Makinda. (picha: Ofisi ya Waziri Mkuu)
Mhe. Samuel John Sitta (Mb, W, CCM) alishika wadhifa wa kuliongoza Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mwishoni mwa mwaka 2005 hadi 2010.

Habari nyepesi nyepesi kuhusu halfa ya kumuaga jana zinapasha kuwa Wabunge wa CUF waliohudhuria hafla hiyo walisusia na kuondoka ukumbini baada ya nyimbo zilizopigwa kuwakera, hasa ule wa kuwananga wapinzani wenye kiitikio chenye maneno, "...tuwachanechane tuwatupe!"

Wabunge wa CHADEMA wao inasemekana hawakuhudhuria hata mmoja.

POLISI 7 WA HUKUMIWA MIAKA 5 JELA KWA MAUJI (KIGOMA)

MAHAKAMA Kuu ya Tanzania Kanda ya Tabora imewahukumu kifungo cha miaka mitano jela askari saba wa Jeshi la Polisi mkoani Kigoma ambao walikuwa wakishtakiwa kwa mauaji.

Akitoa hukumu yake katika kikao cha Mahakama Kuu kilichokuwa kikifanyika mkoani Kigoma Jaji wa mahakama hiyo, Sam Mpaya Rumanyika alisema kuwa baada ya kupitia ushahidi mbalimbali Mahakama hiyo imewatia hatiani askari hao kwa kosa la kuua bila kukusudia.

Katika kesi hiyo namba 35 ya mwaka 2012 washitakiwa hao walifikishwa mahakamani hapo na kusomewa shitaka la kumuua Festo Stephano, mkulima wa kijiji cha Rungwe Mpya Wilaya ya Kasulu mkoani hapa katika tukio lililotokea Agosti 6, mwaka 2011.

Askari hao waliohukumiwa ni pamoja na Baraka Hongdi, Koplo Mawazo, Koplo Swahib, D/C Charles, D/C Shamsi, D/C Jerry na D/C Amrani ambao kwa pamoja walikana shitaka lao katika kesi hiyo namba 35 ya mwaka 2012.

Akitoa utetezi kabla ya hukumu hiyo wakili wa washitakiwa, Method Kabuguzi aliiomba Mahakama kuwafutia shitaka washitakiwa hao na kuwaachia huru kwani wote bado vijana na wameoa hivi karibuni.

Sambamba na hilo Kabuguzi alisema kuwa askari hao walikumbwa na mkasa huo wakati wakitekeleza jukumu lao la ulinzi wa taifa ambapo walimkamata mtuhumiwa wa kutumia silaha na ndipo kifo kikatokea wakati wakitekeleza majukumu yao.

Source: wavuti blog

Friday, 21 June 2013

TAARIFA KUHUSU NASARI, LEMA ,MBOWE NA MAJERUHI WA BOMU

Picture
Jeneza lenye mwili wa Mwenyekiti wa BAWACHA kata ya Sokoni, Judith William Moshi, aliyefariki kwa mlipuko wa bomu kwenye viwanja vya Soweto jijini Arusha siku ya kufunga kampeni za chaguzi ndogo tarehe 15.06.2013.
 
Mtoto Fahad Jamal (7) ambaye hali yake ilikuwa mbaya na kulazwa chumba cha Wagonjwa Mahututi (ICU) Hospitali ya Selian, amefariki dunia juzi saa saba mchana hositalini hapo.

Kwa mujibu wa  Kaimu Mganga Mkuu wa Hospitali hiyo, Dk Paul Kisanga alisema mtoto huyo alifariki dunia juzi mchana hospitalini hapo wakati  timu ya madaktari kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili (MOI) pamoja na Madaktari wa Jeshi kutoka Hospitali ya Jeshi ya Lugalo wakijaribu kwa kila hali kuokoa uhai wake.

Alisema majeruhi 14 wamelazwa hospitalini hapo huku wengine watatu wakitibiwa na kuruhusiwa kwenda nyumbani.
Picture
Waombolezaji
Inatipotiwa kwamba askari polisi walivamia nyumbani kwa Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema usiku wa jana kwa lengo la kupekua nyumba yake na kumkamata Mbunge huyo aliyekuwa anatafutwa na polisi.

Taarifa zinasema kuwa Mbunge huyo pamoja na Mbunge mwingine aliyekuwa akitafutwa na jeshi hilo, Freeman Mbowe (Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa) tayari wamejisalimisha kwenye ofisi za jeshi hilo asubuhi ya leo kwa ajili ya mahojiano.
Picture
 
Mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari akiwa amelazwa kwenye ndege akifungwa mkanda tayari kwa kusafirishwa kutoka Arusha na kuamishiwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam jana. (picha: Filbert Rweyemamu/MWANANCHI)
Mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari aliyekuwa amelazwa hospitalini hapo kutokana na kupigwa na kuumizwa mgongoni na shingoni amehamishiwa kwenye hospitali ya Lugalo ya jijini Dar es Salaam.

“Bunge limegharamia kunisafirisha hadi Muhimbili kwa matibabu zaidi, ofisi ya Bunge ndiyo imetafuta ndege ndogo ya kunipeleka,” alisema Nassari.

Alisema hadi jana alikuwa anasumbuliwa na maumivu ya mgongo na nyuma ya shingo, ambako alipigwa rungu na vijana wa Kimasai (Morani) na wafuasi wanaodaiwa kuwa wa CCM.

“Baada ya kunipiga nilifanikiwa kutoroka hadi eneo la Minjingu kunusuru maisha yangu, baadaye ilibidi nitafutiwe pikipiki hadi eneo la barabara kuu ndipo niliwakuta askari wa usalama barabarani, waliniombea usafiri hadi hospitali,” alisema Nassari.


Thursday, 20 June 2013

RAIS MSTAAFU GEOGE W.BUSH KUHUTUBIA WAKE WA MARAIS WA AFRIKA DAR

RAIS mstaafu wa Marekani, George W. Bush na mkewe, Laura, wanatarajiwa kuwasili nchini mwezi ujao ambapo watahutubia kongamano litakalojadili wajibu wa wake za marais katika kuinua wanawake duniani.

Taasisi ya George Bush ndiyo imeandaa kongamano hilo litakalofanyika Dar es Salaam kuanzia Julai 2 hadi 3.

Taarifa iliyotolewa jana na taasisi hiyo kwa vyombo vya habari, ilisema kongamano hilo, litahudhuriwa pia na mke wa Rais Barack Obama wa Marekani, Michelle na muasisi wa Taasisi ya Wanawake ya Cherie, Cherie Blair ambaye ni mke wa Waziri Mkuu wa zamani wa Uingereza, Tony Blair.

Wake wengine wa marais wa Afrika watakaohudhuria ni Mama Salma Kikwete, Chantal Campaore wa Burkina Faso, Roman Tesfaye wa Ethiopia, Maria da Luz Dai Guebuza (Msumbiji), Penehupifo Pohamba (Namibia), Sia Nyama Koroma (Sierra Leone), Janet Museveni (Uganda) na Christine Kaseba wa Zambia.

Kongamano hilo litajikita zaidi katika kujadili masuala ya kuwekeza kwa wake, kuimarisha Afrika lakini pia wajibu wa wake za marais kuhamasisha wanawake katika maeneo ya elimu, afya na kuwakwamua kiuchumi.

“Kongamano hili litakutanisha pamoja wake za marais, maofisa wa Serikali, mashirika binafsi, Asasi Zisizo za Serikali (AZISE) na wasomi kujadili mambo muhimu ya kuchukuliwa hatua ili kunufaisha wanawake,” ilisema taarifa hiyo.

Aidha, mada zitakazowasilishwa na kujadiliwa katika kongamano hilo ni kuinua wajasiriamali wanawake kiuchumi kupitia mafunzo na teknolojia, kupatia fursa wanawake wakulima kwa kupewa mafunzo ya kilimo cha kisasa, mafunzo kuhusu saratani ya matiti na umuhimu wa elimu kwa wanawake.

Kongamano hilo linafanyika sambamba na ujio wa Rais Obama anayetarajiwa kuwasili nchini mwanzoni mwa mwezi ujao.


 

ASKARI WA AUWA MTU MMOJA KUFUATIA VURUGU YA WANANCHI WA KIJIJI CHA LUMBILA WILAYA YA MBOZI (MBEYA)

MMOJA AUWAWA KUFUATIA VURUGU YA WANANCHI WA KIJIJI CHA LUMBILA WILAYA YA MBOZI KUWASHAMBULIA ASKARI WALIOKUWA WANAFANYA OPERESHENI.


MKUU WA WILAYA YA MBOZI MKOANI MBEYA DR. MICHAEL KADEGE AAKIWATULIZA HASIRA WANAKIJIJI HICHO KABLA YA KUANZA KUWASIKILIZA

                                          DIWANI ATHUMANI   - ACP
 KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
MKUU WA WILAYA MBOZI BAADA YA KUWATULIZA WANANCHI HAO SASA WANAELEKEA ENEO LA MKUTANO
MOJA YA WANAKIJIJI HICHO AKIELEZEA JINSI TUKIO HILO LA VURUGU LILIVYOTOKEA
AIDHA KATIKA TUKIO HILIO CHARLES   JOSE  MWAWALO,MIAKA 27,MNYIHA,MKULIMA MKAZI WA KIJIJI CHA LUMBILA ALIJERUHIWA KWA KUPATA MICHUBUKO TUMBONI AMBAPO UCHUNGUZI UNAFANYWA KUBAINI NI KITU GANI KILICHOMJERUHI. 
POLISI WALIFANIKIWA KUCHUKUA MADUMU MACHACHE AMBAYO NI MADUMU MATATU YENYE UJAZO WA LITA 60, MADUMU MAWILI YENYE UJAZO WA LITA 20 NA MADUMU NANE LITA 30 HIVYO UVAMIZI HUO WA WANANCHI NDIO ULIOWAFANYA ASKARI POLISI WASHINDWE KUCHUKUA VIELELEZO VYOTE. 



MNAMO TAREHE 19.06.2013 MAJIRA YA SAA 13:00HRS HUKO KATIKA KIJIJI CHA LUMBILA KATA YA RUANDA WILAYA YA MBOZI MKOA WA MBEYA. RAJABU S/O WILSON MWASHITETE, MIAKA 25, MNYIHA, MKULIMA, MKAZI WA KIJIJI CHA LUMBILA ALIUAWA KWA KUPIGWA RISASI NA ASKARI POLISI WALIOKUWA KATIKA MSAKO DHIDI YA WAHALIFU/WAPORAJI KATIKA ENEO LA MLIMA SENJELE.

CHANZO NI BAADA YA ASKARI POLISI WAKIWA KATIKA OPERESHENI ENEO HILO KUZINGIRWA NA KUNDI LA WANANCHI ZAIDI YA 150 WA KIJIJI HICHO WAKIWA NA SILAHA ZA JADI MAPANGA, MARUNGU, SHOKA NA MAWE WAKIWAZUIA ASKARI HAO KUKAMATA WAHALIFU NA KUANZA KUFANYA VURUGU BAADA YA KUWA WAMEKAMATA MALI INAYODHANIWA KUWA YA WIZI AMBAYO NI MAFUTA  AINA YA DIESEL MADUMU ZAIDI YA 100.

HATA HIVYO KUFUATANA NA VURUGU ZILIZOJITOKEZA WALIFANIKIWA KUCHUKUA MADUMU MACHACHE AMBAYO NI MADUMU MATATU YENYE UJAZO WA LITA 60, MADUMU MAWILI YENYE UJAZO WA LITA 20 NA MADUMU NANE LITA 30 HIVYO UVAMIZI HUO WA WANANCHI NDIO ULIOWAFANYA ASKARI POLISI WASHINDWE KUCHUKUA VIELELEZO VYOTE. 

MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA KATIKA HOSPITALI YA WILAYA YA MBOZI. 

AIDHA KATIKA TUKIO HILI CHARLES  S/O JOSE  MWAWALO,MIAKA 27,MNYIHA,MKULIMA MKAZI WA KIJIJI CHA LUMBILA ALIJERUHIWA KWA KUPATA MICHUBUKO TUMBONI AMBAPO UCHUNGUZI UNAFANYWA KUBAINI NI KITU GANI KILICHOMJERUHI. 

PIA WANANCHI WALIFUNGA BARABARA KUU YA MBEYA/TUNDUMA KWA KUWEKA MAWE NA MAGOGO NA KUSABABISHA MSONGAMANO MKUBWA WA MAGARI BARABARANI. 

HALI ILIKUWA SHWARI BAADA YA KAMANDA WA POLISI KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI KUFIKA ENEO LA TUKIO NA KUZUNGUMZA NA WANANCHI PAMOJA NA VIONGOZI WA ENEO HILO KISHA KUFUNGUA BARABARA . 

ASKARI POLISI WANNE WALIJERUHIWA KATIKA TUKIO HILO KATI YAO WATATU WALIPATIWA MATIBABU NA KURUHUSIWA NA ASKARI MMOJA  AMELAZWA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA KWA MATIBABU ZAIDI . 

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA TABIA YA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI KWANI NI KINYUME CHA SHERIA BADALA YAKE KUWA NA UTAMADUNI WA KUTATUA KERO/MALALAMIKO YAO KWA NJIA YA MAZUNGUMZO KWA KUYAWASILISHA KATIKA MAMLAKA HUSIKA. AIDHA ANAWATAARIFU WALE WOTE WALIOWAHI KUIBIWA/KUPORWA MALI MBALIMBALI YAKIWEMO MAFUTA WAJITOKEZE POLISI KWA AJILI YA HATUA ZINAZOSTAHILI.


Signed By,
                                                            [DIWANI ATHUMANI   - ACP]
 KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.

WATU 48 WAUAWA ZAMFARN NIGERIA

 
Watu waliokuwa wamejihami kwa bunduki wamewaua watu 48 katika shambulizi dhidi ya kijiji kimoja katika jimbo la Zamfara.
Watu hao waliwasili kabla ya macheo wakiendesha pikipiki.
Baadaye walikwea mlima uliokuwa karibu na kijiji hicho na kuanza kuwafyatulia watu risasi kiholela nyumba hadi nyumba.
Shambulizi hilo linasemekana kuhusishwa na mgogoro kuhusu wizi wa Ng'ombe katika jimbo la Kaskazini . Kulikuwa na mashambulizi kama haya mwaka jana.
Jimbo lenye idadi kubwa zaidi ya watu pamoja na kuwa inazalisha mafuta, pia linakabiliwa na tatizo la makundi ya wapiganaji wa kiisilamu wanaofanya mashambulizi mara kwa mara.
Hata hivyo, ghasia za hivi karibuni haziaminiki kuwa na uhusiano wowote na harakati za wapiganaji wa kiisilamu wa Boko Haram.
Miongoni mwa waliouawa ni Chifu, Imamu na kiongozi wa kundi la vijana wanaotoa ulinzi.
Walioshuhudia tukio hilo walisema kuwa wavamizi waliwasili katika eneo la Kizara kabla ya macheo wakiwa kwenye pikipiki na kuwa walijipanga kwa mashambulizi kabla ya kuanza kuwaua wanavijiji.