Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB), Mhe. Bahame Tom Nyanduga (watatu kutoka kulia) akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa warsha ya wadau wa masuala ya haki jinai (criminal justice) kutoka idara mbalimbali za Serikali na Asasi Zisizo za Kiserikali, muda mfupi baada ya kufungua warsha hiyo, iliyofanyika Makao makuu ya ofisi za Tume, jijini Dar es Salaam mapema jana (Aprili 11, 2016).
Warsha hiyo ya siku moja iliandaliwa na THBUB kwa ushirikiano na Chama cha Wanasheria Tanzania Bara (TLS) na Asasi ya Commonwealth Human Rights Initiative (CHRI) ya nchini India. Ililenga pamoja na mambo mengine kuwahamasisha wadau kujiunga na kushiriki katika jukwaa la Haki na Usalama (justice and security forum) linalotarajiwa kuzinduliwa hivi karibuni. Lengo kubwa la jukwaa hilo ni kuunga mkono jitihada za Serikali katika kuboresha mfumo wa haki jinai nchini.
Mkurugenzi wa Asasi ya Commonwealth Human Rights Initiative (CHRI) ya nchini India, Bibi Maja Daruwala akiongea wakati wa warsha ya wadau wa haki jinai, Makao Makuu ya Ofisi za THBUB, jijini Dar es Salaam
Baadhi ya washiriki wakifuatilia mada katika warsha hiyo.
Baadhi ya washiriki wakifuatilia mada katika warsha hiyo.
Picha ya pamoja..
0 comments:
Post a Comment