Thursday 14 April 2016

UCL:Atletico, Bayern zaungana na Real, city nusu fainali, Barca nje! Droo kupangwa kesho april 15


Matokeo:Jumla ya Mabao kwa Mechi Mbili
Jumatano Aprili 13
Benfica 2 Bayern Munich 2 [2-3]
Atletico Madrid 2 Barcelona 0 [3-2]

JANA Atletico Madrid na Bayern Munich zimefuzu kuunga na Real Madrid na Manchester City kwenye Nusu Fainali za UCL, UEFA CHAMPIONZ LIGI.
Wakiwa nyuma kwa Bao 2-1 toka Mechi ya kwanza, Atletico Madrid Jana wakiwa kwao Vicente Calderon waliinyuka Barcelona Bao 2-0 katika Mechi ya Pili ya Robo Fainali na kutinga Nusu Fainali kwa Jumla ya Bao 3-2.
Bao za Atletico hapo Jana zilifungwa na  Antoinne Griezmann katika Dakika za 38 na 88, la Pili likiwa la Penati.Huko Lisbon, Benfica na Bayern Munich zilitoka Sare 2-2 na Bayern kutinga Nusu Fainali kwa vile walisahinda Mechi ya kwanza 1-0.

Bao za Mechi ya Jana zilifungwa na Jimenez Rodriguez, (27' na Souza Conceição,76'’ kwa Benfica na za Bayern kufungwa na Vidal, 38' na Müller, 52'.
Droo ya kupanga Mechi za Nusu Fainali itafanyika Kesho Ijumaa.
UEFA CHAMPIONZ LIGI
ROBO FAINALI
Marudiano
Matokeo:Jumla ya Mabao kwa Mechi Mbili
Jumanne Aprili 12
Manchester City 1 Paris St-Germain 0 [3-2]
Real Madrid 3 Wolfsburg 0 [3-2]

TAREHE MUHIMU:
-Droo ya Nusu Fainali: Aprili 15
**Mechi Aprili 26/27 na Marudiano Mei 3/4
FAINALI
Mei 28
San Siro, Milan, Italy

0 comments: