Saturday 23 April 2016

Liverpool imetangaza kumsimamisha staa wake kwa matumizi ya dawa za kuongeza nguvu









Uongozi wa klabu ya Liverpool leo April 23 2016 umetangaza kumsimamisha staa wake ambaye alikuwa anahusishwa kutumia dawa za kuongeza nguvu michezoni, Liverpoolimeamua kumsimamisha beki wa kimataifa wa Ufaransa anayeichezea klabu hiyo Mamadou Sakho wakati ambao UEFA wanasubiriwa kukamilisha uchunguzi wao.
Sakho ambaye anachunguzwa na UEFA toka March 17 baada ya mchezo wa Europa league kati ya Man United dhidi ya Liverpool Old Trafford, amesimamishwa naLiverpool baada ya kukaa na uongozi na kujadiliana, lakini Mamadou Sakho atakumbana na adhabu kutoka UEFA baada ya uchunguzi wao kukamilika.
Sakho-663761
Mamadou Sakho
Baada ya kuchukuliwa sample na kufanyiwa vipimo Mamadou Sakho anaaminika kutumia ‘Fat Burner’ kwa ajili ya kusisimua misuli, kitu ambacho hakikubaliki michezoni.

0 comments: