Saturday 30 April 2016

MATOKEO YA VPL LEO TOTO 1 2, YANGA YATOKOMEA JUU ZAIDI KILELENI! KESHO, SIMBA v AZAM FC

 LIGI KUU VODACOM

Matokeo:
Jumamosi Aprili 30
Toto Africans 1 Yanga 2    
African Sports 1 Coastal Union 0 
Mwadui FC 2 Stand United 1       
Mtibwa Sugar 1 Mbeya City 0      
Tanzania Prisons 1 JKT Ruvu 1    
      
Mabingwa Watetezi na Vinara wa VPL, Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania, Yanga Leo wamezidi kujongomea juu kileleni baada ya kutoka nyuma kwa Bao 1-0 na kuichapa Toto African 2-1 huko CCM Kirumba, Mwanza.
Toto walitangulia kuifunga Yanga kwa Bao la Dakika ya 39 la William Kimanzi na Yanga kupiga Bao 2 Kipindi cha Pili Dakika za 50 na 78 Wafungaji wakiwa Deus Kaseke na Juma Abdul.
Ushindi huu umeifanya Yanga izidi kupaa kileleni ikiwa na Pointi 65 kwa Mechi 26 ikifuatiwa na Azam FC yenye Pointi 58 na Simba 57  ambao wamecheza Mechi 25 na Kesho Jumapili wanapambana Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.
LIGI KUU VODACOM                             
Jumapili Mei 1
Simba v Azam FC
Jumatano Mei 4
Azam FC v JKT Ruvu
Jumamosi Mei 7
JKT Ruvu v Ndanda FC
Kagera Sugar v Azam FC
Simba v Mwadui FC
Stand United v Coastal Union
Mgambo JKT v Mtibwa Sugar
Jumapili Mei 8
Tanzania Prisons v Majimaji
Jumanne Mei 10
Mbeya City v Young Africans
Jumatano Mei 11
Majimaji v Simba
Jumamosi Mei 14
Mgambo JKT v JKT Ruvu
Jumapili Mei 15
Mtibwa Sugar v Simba
Ndanda FC v Young Africans
Kagera Sugar v Stand United
Mwadui FC v Mbeya City

0 comments: