Thursday 14 April 2016

Kikosi kazi cha JPM sasa kinaingia Wizara ya Mambo ya Ndani baada ya mkataba mbovu wa LUGUMI kubainika.

Ukweli kidogo ila mmeongeza chumvi katika hii habari!
Habari za Uhakika zilizotufikia hivi punde zinasema kuwa kile kikosi kazi cha kushtukiza cha Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuli huenda kikaanza kazi muda wowote kuanzia sasa katika Wizara ya Mambo ya Ndani mara baada ya mkataba mbovu wa LUGUMI kubainika.
Ikumbukwe kuwa Waziri mwenye dhamana ya wizara ya Mambo ya Ndani Waziri Charles Kitwanga ni mmoja wa walionufaika na mkataba huo kupitia kampuni yake ya Infosys. Miezi michache iliyopita Waziri Kitwanga aliwang'oa wote walioshiriki kupitisha mkataba huo mbovu katika operesheni maalum ili isije kubumburuka. Kwa bahati mbaya zaidi hao hao waliong'olewa kiuonevu ndio wametoa hii habari kwenye vyombo vya habari baada ya kuchoka na mabavu yake.
Waziri Kitwanga amekuwa akihusishwa na dosari na kashfa nyingi sana tangia Serikali ya awamu ya tano iingie madarakani. Pia inasemekana huenda report yake iliyotumika kumsafisha na kuchaguliwa kuwa waziri wa Mambo ya Ndani ilitengenezwa na watu walionufaika na nyendo zake mbaya kwa taifa ikiwe huo mkataba wa LUGUMI.
Wiki chache zilizopita,Waziri Kitwanga, alitajwa katika ujumbe uliokuwa ukitembea kwenye mitandao ya kijamii kuwa ni katika genge la watu 6 mashuhuri "UNTOUCHABLES" wanaotaka kuitawala nchi hii kimabavu kwa kutumia nguvu ya pesa (za BOT) na vyeo vyao katika kuwachafua na kuwatoa watendaji wote waliokataa kuwaunga mkono njama zao.
Sambamba na hilo, Waziri Kitwanga, pamoja na ndugu Magori - Mkurugenzi wa Uendeshaji wa NSSF, amehusishwa pia na shutma ya kupanga njama za kumuondoa aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa NSSF. Ikumbukwe kuwa Kashfa iliyomuondoa madarakani ndugu Donata Mgassa aliyekuwa kiongozi wa kitengo cha manunuzi cha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam mara tu baada ya Mheshimiwa Rais kuvunja bodi ya Bandari ndio kashfa hiyo hiyo ilitakiwa imwondoe ndugu Crescentius Magori wa NSSF madarakani kwa sababu wote walihusika kwenye kashfa ya bodi ya Bandari na kupeleka kuvunjwa na mheshimiwa Rais.
Inasemekana pia bodi ya NSSF ilitaka kufanya maamuzi kama ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ndipo Waziri Charles Kitwanga akampa maagizo Katibu Mkuu wa Wizara ya Kazi Ndugu Eric Shitindi kuwa avunje bodi ya NSSF haraka kabla haijakaa. Katika utawala bora inategemewa Prof Kayharara afanye maamuzi yaliyofanywa na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Profesa Mukandala kwani wakati maamuzi hayo yanatoka Profesa Kahyarara alikuwa miongoni mwa walioridhia uamuzi huo kwenye kikao cha manejimenti.
Mbali zaidi, Waziri Kitwanga amehusishwa na kashfa ya kuwa ni mmoja katika wafanyakazi hewa wa BOT. Katika hili na ushahidi ukapatikana ambapo gavana alipelekewa kikosi kazi kumtuliza asitumbue JIPU. Waziri Kitwanga ndio Boss wa vikosi kazi vya Polisi Tanzania.
Haikuishia hapo Waziri Kitwanga amesikika akijisifu yeye ndiye aliyemuweka Rais Magufuli madarakani na yeye ndio mfadhili wake tangia siku ya kwanza Rais wetu mtukufu alipochukua fomu ya kugombea Ubunge. Yeye pekee ndio alidhamini kampeni nzima. Sasa umefika wakati wa kulipwa fadhila zake. Ikumbukwe kuwa kipindi Rais Magufuli alipogombea ubunge kwa mara ya kwanza Waziri Kitwanga alikuwa bado mfanyakazi halali wa BOT, hakuwa HEWA bado.
Taarifa ni kuwa kile kikosi cha kushtukiza cha Mheshimiwa Rais kishampelekea ripoti ya kuhusu ukweli wa Lugumi na wa Israeli waliokuwa wanapewa tenda za jeshi la polisi na baadhi ya vifaa ambavyo vimetoka Israel bado viko kwenye godown la kampuni ya Charles Kitwanga iitwayo INFOSYS


chanzo  Lugumi page.

LikeShow more reactions
Comment
61 comments
Comments
Athumani Athuman Mtengo Ha ha ha hii ndo Tanzania bhana nchi ya masinema mengi
LikeReply17 hrs
David Mayabu unakwenda huko then unalipuka haya rudi ufunguke, ukiwa hapa
LikeReply27 hrs
John William Majanga kitwanga hatufai kumbe fisadi papa
LikeReply37 hrs
Kassim Bingwe Twendeni tu mwisho wa wale wapumbavu na mamuzi yao tutayaona
LikeReply27 hrs
Athumani Athuman Mtengo Tutumbue na jipu hili
LikeReply16 hrs
Samuel Zebedayo Samz Hapa naona donda ndugu.... Lina mlolongo hatari
LikeReply26 hrs
Annety Wangwe Mh!ni hatar xana watu hao!!
LikeReply6 hrs
Hamza Yusuph Mwandawala Said Lugumi. Itisha press conference ueleze kila kitu kabla mambo hayajifikia climax. Ikiwa ushaur huu utapuuzwa Kwa hakika matokeo ya kupuuzwa huko hayatamithilika
LikeReply36 hrs
Melickzeder Paul John Ukweli wako ndo utakuweka huruu bos
LikeReply16 hrs
Christopher Emanuel Nnamashaka na hii akaunti
LikeReply16 hrs
Emmanuel Misigalo Pelekeni Mahakamani.Mkisha tumbuliwa ndio mnajidai kutumbua
LikeReply26 hrs
Kivoon Joseif Pumba zooote hizp
LikeReply16 hrs
Kivoon Joseif Mauongomauongo time
LikeReply16 hrs
Godwin Mwasenga Kwl haka ni kamfumo aise
LikeReply16 hrs
Abel Colman Online
LikeReply16 hrs
Muharami Saidi Endeleeni kuumbuana tu, Dah!! Watanzania tutaendelea kufanywa wajinga, sisi tunalala njaa wengine wanapiga pesa halafu wanatuletea sinema za namna hii....rudi nchini kaka tujue kama unasema ukweli na ukweli wako utakuweka huru, vinginevyo mtakua ni majipuuuuuuu
LikeReply16 hrsEdited
Muharami Saidi Dah!!!, nimeumia sana kumbe kuna watu wapo juu ya sheria? 6 Untachable people, masikini nchi yangu.
LikeReply26 hrs
Bacron Lyimo Uyu janja janja
LikeReply6 hrs
Fredy Donald Acc hacked
LikeReply6 hrs

0 comments: