Kampuni ya simu ya Blackberry imejipanga kuhakikisha mwaka huu wanazindua simu aina mbili zilizo katika mfumo wa Android.
Akizungumza na mtandao wa habari wa Falme za Kiarabu (UAE), Mkurugenzi Mtendaji wa Blackberry, John Chen amesema kampuni yake inataraji kuzindua simu aina mbili moja ikiwa katika mfumo wa kawaida ikiwa na batani na nyingine ikiwa ya kugusa kioo (touch screen).
Chen amesema simu hizo za mfumo wa Adroid zitakuwa za kwanza kutoka kampuni hiyo baada ya wateja wengi kulalamika kuhusu gharama za kununua simu zao na simu hizo zitakuwa na gharama ambazo zitawavutiwa wateja wa bidhaa zao.
“Wateja wetu wengi wamekuwa wakitwambia kuwa wanataka kununua bidhaa zetu lakini Dolla 700 ni kubwa kwa simu kama Blackberry Priv na wanavutiwa zaidi na simu zinazoanzia Dolla 400,” alisema Chen.
0 comments:
Post a Comment