Kamati ya Ulinzi na Usalama wilayani handeni imelazimika kutumia nguvu kuwaondoa baadhi ya wakazi wa kijiji cha Kwamkono kilichopo kata ya Sindeni waliovamia na kujimegea maeneo ya ardhi kwa nguvu zaidi ya hekta 5 zinalomilikiwa na Kanisa Aglikana Dayosisi ya Tanga kisha kujenga nyumba za kuishi na kulima mazao ya chakula.
Sakata hilo linafuatia mmoja kati ya wakazi wa eneo hilo kuwaendea wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wilayani Handeni chini ya mwenyekiti wake
Mkuu wa Wilaya hiyo Husna Msangi na kuwatolea lugha za vitisho kisha kuwaamuru waondoke shambani hapo hatua iliyosababisha viongozi wa kamati hiyo kuingilia kati baada ya kuelezwa kuwa hata padre wa kanisa hilo ni miongoni mwa waliopata kipigo kutoka kwa wananchi.
Awali Katibu wa Mipango na Maendeleo Kanisa Anglikana la Mtakatifu Francis lililopo Kwamkono wilayani Handeni Bwana Daud Mpalahingwe amelalamikia viongozi wa Serikali ya kijiji hicho kwa kuuza kwa makusudi eneo la kanisa kwa kuidhinisha makubaliano baina ya wanakijiji na wageni wanaohitaji kujenga na kulima bila maafikiano na wamiliki wa maeneo hayo.
Kufuatia hatua hiyo Mkuu wa wilaya alilazimika kuwaamuru wakazi waliojenga na kulima eneo la kanisa kubomoa mara moja nyumba zao kabla nguvu za kisheria hazijatumika.
0 comments:
Post a Comment