Wananchi wa kata ya Luhanga wilayani Mbarali wametoa kilio chao cha ubovu wa barabara kwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makala, ambaye pia ameonja adha ya ubovu wa barabara hiyo baada ya msafara wake kukwama kwa zaidi ya saa moja kutokana na magari kunasa kwenye tope.
Obovu wa barabara hiyo umezidi kuongezeka kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha na kufanya maisha kuwa magumu zaidi kwa wakazi wa maeneo hayo.
Diwani wa kata ya Luhanga, Mh.Dira Funika amesema kuwa kutokana na kukatika kwa mawasiliano ya barabara, wananchi wanapata shida kubwa ikiwemo wagojwa kupoteza maisha na wajawazito kuzalia njiani kwa kushindwa kufikishwa hospitalini kwa wakati.
Mwenyekiti wa Bodi ya Barabara ya Mkoa, ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makala amejikuta katika wakati mugumu baada ya msafara wake kukwama kwenye tope katika barabara hiyo, hali ambayo imemfanya atoe siku saba kwa wakala wa barabara nchini TANROAD mkoani Mbeya kukarabati maeneo yote korofi ya barabara hiyo ili iweze kupitika.
0 comments:
Post a Comment