Mke wa Waziri Mkuu, Mama Tunu Pinda kizungumza katika hafla fupi ya watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu kumuaga Waziri Mkuu, Mizengo Pinda iliyofanyika kwenye makazi ya Waziri Mkuu jijjni Dar es salaam Oktoba 16, 2015
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na mkewe Tunu wakigonganisha glass na Watendaji wakuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu katika Hafla fupi ya kumuaga aliyoandaliwana watumishi wa Ofisi yake kwenye makazi yake jijini Dar es salaam Oktoba 16, 2015. Wapili kushoto ni Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu, Dkt. Florens Turuka, kulia ni Naibu Katibu Mkuu, Regina Kikuli na wapili kulia ni Msajili wa Vyama vya siasa, Jaji Francis Mutungi.
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
nae RAIS KIKWETE AAGANA NA WATUMISHI WA WIZARA YA MAMBO YA NJE JIJINI DAR SALAAM-OKTOBA 17, 2015
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na mabalozi pamoja na wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya nje na ushirikiano wa Kimataifa wakati wa hafla ya kumuaga iliyofanyika katika ukumbi wa ukumbi wa Julius Nyerere International Convention Centre(JNICC) jijini Dar es Salaam Oktoba 17, 2015.
(picha na Freddy Maro)
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete pamoja na balozi wa China Mhe. LU Youqing wakifunua kitambaa katika jiwe la msingi katika eneo litakapojengwa jengo la Wizara ya Mambo ya nje na Ushirikiano wa kimataifa jijini Dar es Salaam.
Balozi wa Tanzania Afrika ya Kusini Radhia Msuya na Balozi wa Tanzania nchini India Alan Kijazi wakimkabidhi zawadi Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete kwa niaba ya mabalozi wanaoiwakilisha Tanzania nchi za nje wakati wa hafla ya kutunuku tuzo kwa Mhe.Rais iliyofanyika katika ukumbi wa Julius Nyerere International Convention Centre(JNICC) jijini Dar es Salaam.
0 comments:
Post a Comment