Sunday, 18 October 2015

waandishi wa habari watahadharishwa kuzingatia weledi na maadili ya kazi zao.


Baraza la habari Tanzania MCT limewatahadharisha waandishi wa habari kuzingatia weledi na maadili ya kazi zao hasa wiki hii ya lala salama ya siku chache za kampeni za uchaguzi zilizobaki hadi matokeo yatakapotangazwa kwani taifa linawategemea.

Wito huo umetolewa jijini Dar es Salaam na katibu mtendaji wa MCT Bw Kajubi Mukajanga wakati akizindua tuzo ya 

umahiri wa uandishi wa habari Tanzania EJAT ambayo kwa mwaka huu yameongezeka makundi mapya mawili ambapo amewataka waandishi wa habari kuwa na ujasiri wa kuhoji mambo ambayo yanaweza kusababisha madhara kwa taifa iwe ni polisi, wanasiasa au tume za uchaguzi NEC na ZEC.
 
Kwa upande wa majaji wa tuzo hizo mbali na kutoa dondoo za kazi ambazo ni bora na zina uwezo mkubwa wa kushinda wameeleza kuwa kundi la uandishi wa habari za sayansi na teknolojia ni changamoto kwani waandishi wengi hawatumi kazi zao kama yalivyo makundi mengine.

0 comments: