Tume ya taifa ya uchaguzi imeleta mitambo maalum ya kusaidia walemavu wenye uoni hafifu na wasioona kupiga kura bila kutegemea msaada wowote wa binadamu huku walemavu wa viungo, Albino, wazee, wakinamama wenye watoto na wajawazito wakipewa kipaumbele katika uchaguzi mkuu oktoba 25 mwaka 2015.
Amebainisha h ayo kaimu mwenyekiti wa tume ya taifa ya uchaguzi nchini jaji mkuu mstaaf wa Zanzibar Mh.Himid Hamud katika hotuba yake iliyosomwa kwa niaba yake na afisa uchaguzi kanda ya ziwa Bw.Deogratius Nsanzgwako katika mkutano uliohusisha viongozi wa kisiasa mkoa wa Mwanza.
Wakati huohuo viongozi wa dini na waimbaji wa nyimbo za jijini Mwanza wa kanisa la KKKT usharika wa Galilaya Buhongwa wakishirikiana na mwimbaji wa nyimbo za njili Lucy Haruni wamehimiza jamii kuchagua viongozi waadilifu, kutii sheria bila shuruti siku ya kupiga kura na kuhimiza jamii kuwafichua wahallifu wanaohusika kuuwa wazee na walemavu wa ngozi Albino kutokana na imani potofu za kishirikina.
0 comments:
Post a Comment