Sunday, 18 October 2015

Hali Kipindupindu DSM ni mbaya kutokana na idadi ya wagonjwa kuongezeka.


Hali ya ugonjwa wa Kipindupindu jijini Dar es Salaam bado ni mbaya kutokana na idadi ya wagonjwa wanaopokelewa kwenye kambi maalum kuongezeka kila siku licha ya elimu inayotolewa mara kwa mara juu ya kujikinga na ugonjwa huo.
Afisa muuguzi wa kambi ya Mburahati Amina Mbisu amesema hadi sasa idadi kubwa ya wagonjwa wanaofika katika kambi hiyo wanatokea maeneo ya Mwananyamala, Mburahati, Tandale na Manzese huku akiendelea kutoa elimu ya namna ya kujikinga.
 
Baadhi ya wagonjwa walifika kambini hapo kupata matibabu mbali na kueleza mazingira yaliyo sababisha wapate ugonjwa huo wameviomba vyombo vya habari na manispaa kuendelea kutoa elimu hasa maeneo ambayo yameathirika zaidi ili kuokoa maisha ya watu.

0 comments: