Hatimaye lile tukio la utolewaji wa Tuzo za chama cha waandishi wa habari za michezoTanzania (TASWA) ambazo hutolewa kila mwaka kwa wanamichezo wanaofanya vizuri, zimekamilika usiku wa October 12 kwa wanamichezo, taasisi na viongozi waliofanya vizuri katika kipindi cha miaka 10, Tuzo hizo safari hii zimekuwa tofauti na miaka yote kwani waliopewa Tuzo ni wale waliofanya vizuri katika kipindi cha miaka kumi.
Shadrack Nsajigwa akipokea Tuzo kwa niaba ya timu iliyofanya vizuri katika mashindano ya CHAN
Tuzo hizo ambazo zilikuwa maalumu mwaka huu, kwani zimetumika kumuaga RaisKikwete kwa kumaliza muda wake madarakani na kuheshimu mchango wake katika kuinua michezo nchini katika kipindi cha utawala wake. Ikumbukwe kuwa Tuzo hizo ziligawanyika katika vipengele vinne, Taasisi iliyochangia kuinua michezo katika kipindi cha miaka kumi Tuzo 5.
Francis Cheka akipokea Tuzo yake
Tuzo zimetolewa kwa wanamichezo waliofanya vizuri katika kipindi cha miaka kumi, viongozi waliochangia kuinua michezo katika kipindi cha miaka kumi Tuzo 5 na Tuzo ya heshima kwa Mh Rais Jakaya Mrisho Kikwete kwa kuheshimu mchango wake katika kuinua michezo wakati wa utawala wake, baadhi ya waliopewa Tuzo usiku wa October 12 ni Francis Cheka, Mbwana Samatta, Iddi Kipingu, Abdallah Majura na Hashim Thabiti
Mama yake Hashim Thabiti akichukua Tuzo kwa niaba ya Hashim
Charles Mkwasa akichukua Tuzo ya Twiga Stars kwa kufanya vizuri katika kipindi cha miaka 10.
Wawakilishi wa Mbwana Samatta wakichukua Tuzo kwa niaba yake
Kanali Iddi Kipingu akipokea Tuzo yake ya heshima kwa kusaidia kuinua michezo kwa muda mrefu toka yupo shule ya Makongo
Rais Kikwete akimkabidhi tuzo Dioniz Malinzi kwa kujenga Uwanja wa Gofu Misenyi mkoani Kagera
Rais wa zamani wa TFF Leodger Tenga kapata Tuzo ya kiongozi bora katika kuinua michezo
Abdallah Majura akikabidhiwa Tuzo ya heshima katika kuinua michezo sasa kafungua kituo cha Radio kinachojihusisha na michezo.
Mzee Said akipokea Tuzo ya Taasisi iliyochangia kuinua michezo nchini Azam SSB
Mwenyekiti wa TASWA Juma Pinto akimkabidhi Rais Kikwete Tuzo ya heshima akiwa pamoja na mkuu wa mkoa Dar Es Salaam Meki Sadiki, waziri wa michezo Dk Fenella Mukangara na Dioniz Malinzi.
Nahodha wa Taifa Stars Nadir Haroub akikabidhi jezi ya Taifa Stars kwa Rais Kikwete ikiwa imesainiwa na wachezaji wote.
Baada ya ugawaji wa Tuzo Rais Kikwete alipata nafasi ya kuongea na waandishi wa habari na wageni waalikwa katika Tuzo hizo.
Rais Kikwete katika picha ya pamoja na watu mbalimbali
Rais Kikwete katika picha ya pamoja na washindi wa Tuzo hizo
0 comments:
Post a Comment