Tuesday, 13 October 2015

ANGALIA YANGA SC WALIVYO ENDA BAGAMOYO KWA AJILI YA AZAM FC,

MECHI ZIJZO LIGI KUU YA VODACOM TANZANIA BARA
Okotba 17, 2015
Yanga SC Vs Azam FC
Majimaji FC Vs African Sports
Mbeya City Vs Simba SC
Ndanda FC Vs Toto Africans
Stand United Vs Prisons
Coastal Union Vs Mtibwa Sugar
Oktoba 18, 2015
Mgambo Shooting Vs Kagera Sugar
Mwadui FC Vs JKT Ruvu
Yanga SC watakuwa na kazi na Azam FC Jumamosi Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam

Na Peince Akbar, DAR ES SALAAM
YANGA SC imeingia kambini Jumatatu katika hoteli ya Kiromo, Bagamoyo mkoani Pwani kujiandaa na mchezo wake wa wikiendi wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya Azam FC.
Kocha mpya Msaidizi wa Yanga SC, Juma Mwambusi anatarajiwa kuanza rasmi kesho baada ya kutambulishwa mbele ya wachezaji wote wa timu hiyo.
Yanga SC ilikuwa inasubiri wachezaji wake waliokuwa na timu ya soka ya taifa ya Tanzania nchini Malawi ili kuingia kambini na baada ya kurejea Jumatatu wamekwenda kujichimbia Bagamoyo.
Pamoja na kuweka kambi Bagamoyo, Yanga SC itakuwa ikifanya mazoezi katika Uwanja wa Boko Veterani, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.
Mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu, wamepania kushinda mchezo huo ili kuzidi ‘kuwatoa njiani’ wapinzani wao katika mbio za taji.
Yanga SC ilianza kwa kuifunga Simba SC 2-0 baadaye Mtibwa Sugar pia 2-0 na sasa inakutana na timu nyingine ambayo, haijafungwa kama wao, Azam FC Jumamosi.
Mchezo huo unatarajiwa kuwa na ushindani mkali, kwani tayari msimu huu timu hizo zimekutana mara mbili na kila moja kushinda moja, tena kwa mikwaju ya penalti.  
Azam FC ilianza kuifunga Yanga SC kwa penalti 5-3 kufuatia sare ya 0-0 ndani ya dakika 90 katika Robo Fainali ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na kati, Kombe la Kagame Julai mjini Dar es Salaam.
Na Yanga SC ikalipa kisasi kwa ushindi wa penalti 8-7 baada ya sare ya 0-0 ndani ya dakika 90 katika mchezo wa Ngao ya Jamii Uwanja wa Taifa Agosti mwaka huu.
Jumamosi zikikutana kwa mara ya tatu, utakuwa mchezo wa kuwania usukani wa Ligi Kuu na pia kumaliza ubishi wa nani zaidi baina yao.
Kwa ujumla Ligi Kuu inandelea Jumakosi kwa mechi sita kupigwa kwenye viwanja tofauti na mbali na Yanga SC kumenyana na Azam FC Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam- Majimaji FC wataikaribisha African Sports Uwanja wa Majimaji, Songea na Mbeya City watakuwa wenyeji wa Simba SC Uwanja wa Sokoine, Mbeya
Ndanda FC wataikaribisha Toto Africans Uwanja wa Nangwanda Sijaona, Mtwara, Stand United wataikaribisha Prisons Uwanja wa Kambarage, Shinyanga na Coastal Union watakuwa wenyeji wa Mtibwa Sugar Uwanja wa Mkwakwani, Tanga, wakati Jumapili Mgambo Shooting wataikaribisha Kagera Sugar Mkwakwani na Mwadui FC watakuwa wenyeji wa JKT Ruvu Uwanja wa Mwadui Complex.

0 comments: