Untitled 0
Si jambo geni mtu kuhisi Dar es Salaam ni mji mkuu wa Tanzania, hii ni kutokana na miji mikuu mingi kuwa na idadi kubwa ya watu, vivutio vingi, kukua kimaendeleo na uwepo wa ofisi nyingi za kiserikali.
Dodoma ilijipatia umaarufu wake na kutambulika kama mji mkuu mwaka 1973, hivyo ofisi nyingi zilianza kuhamishia makazi yake ndani ya mji huu, ambapo pia Bunge la Tanzania liliweka makazi yake na kusababisha ongezeko la watu wengi na watumishi wa serikali kutoka mikoa mingine kwa kila msimu wa vikao vya  bunge ndani ya mwaka.
Ukweli ni kwamba Dodoma pamoja na  kuwa na eneo kubwa la 2,576 km2 na idadi ndogo ya watu mara mbili ya Dar es Salaam lakini ina vitu pekee ambavyo vinafanya mji huu uheshimike. Mtu anaweza akahisi akiamua kufanya matembezi yake kipindi hiki cha likizo kinachokuja cha mwisho wa mwaka 2015 atapoteza  muda wake, lakini si kweli. Tuangalie ni vitu gani hasa vinaufanya mji huu uwe wa kipekee.
Majengo ya Bunge la Jamuhuri wa Muungano wa Tanzania.
Untitled 1
Majengo haya yana mvuto, huwezi kupata jengo lolote la vikao vya bunge zaidi ya ndani ya mji huu wa Dodoma, majengo haya yamejengwa kwa ubora wa kukabili tetemeko la ardhi na kubeba idadi kubwa ya watumishi wa serikali.
Mapango ya kondoa Irangi.
Untitled 2
Mapango haya yapo katika wilaya ya Kondoa mkoa wa Dodoma, inachukua Km 9 tu kuelekea mkoa wa Arusha. Histori kubwa ya mapango haya ni michoro iliyochorwa na binadamu wa zamani ikionyesha maumbo yenye maana tofauti, ambapo inasemekana ilichorwa kwa kutumia damu za wanyama na asali bila ya kufutika na kupotea ubora wake kwa kipindi chote cha zaidi ya miaka 1500.
Simba Hill (Mlima Simba).
Untitled 3
Mlima huu ni maarufu kama mlima simba, upo kaskazini mwa mji huu, watalii wengi hupendelea kuupanda  mwinuko huu hasa kipindi cha mwisho wa wiki na msimu wa mwisho wa mwaka,  kama utapendelea kuuona mji mzima wa Dodoma ni vyema ukaupanda mlima huu.
Reli kuu ya kati
Reli hii ilikuwa ndio sababu kubwa kukua kwa mji wa Dodoma tangu mwaka 1800s, ambapo mji huu ulikuwa moja ya kituo cha biashara hiyo haramu kuelekea mji wa Kigoma ambao ni maarufu kama mwisho wa reli.
kilimo na ufugaji
Mji wa Dodoma umekuwa maarufu kwa ufugaji na  kulima zao la zabibu, zabibu hizi zimegawanyika katika makundi manne ambapo  zipo za kula kawaida na kutengenezea mvinyo(wine). Kupitia zao lake la zabibu, zao hili imekuwa ni kivutio cha watalii wengi na jambo la kujivunia kwa wazawa wa eneo hili.
Untitled 4
Hali ya usafiri na malazi
Usafiri na makazi katika mji huu ni kitu rahisi, JovagoTanzania imefanikiwa kuingia ubia na zaidi ya hoteli 35 kama njia ya kurahisisha upatikanaji wa hoteli kupitia tovuti yake kwa kuchagua aina ya hoteli utakayohitaji na kuhifadhiwa kabla ya kuwasili katika mji huo.
Hata hivyo, usafiri wa rahisi ni kupanda mabasi yanayoelekea Dodoma moja kwa moja kutoka mkoa wowote, pia kuna  kiwanja kidogo cha ndege, ambapo serikali bado inajukumu la kuboresha kiwanja hiki kwani inabidi itambue umuhimu na hadhi ya mji huu.