MATUKIO KATIKA PICHA YALIYO WEZA KUVUTIA DUNIANI KOTE

Asante kwa kututembelea mbeyagreennews kwa taarifa zaidi endelelea kututembela kila siku ,saa,dakika usipitwe na matukio kem kemu

MATUKIO KATIKA PICHA YALIYO WEZA KUVUTIA DUNIANI KOTE

Asante kwa kututembelea mbeyagreennews kwa taarifa zaidi endelelea kututembela kila siku ,saa,dakika usipitwe na matukio kem kemu

MATUKIO KATIKA PICHA YALIYO WEZA KUVUTIA DUNIANI KOTE

Asante kwa kututembelea mbeyagreennews kwa taarifa zaidi endelelea kututembela kila siku ,saa,dakika usipitwe na matukio kem kemu

MATUKIO KATIKA PICHA YALIYO WEZA KUVUTIA DUNIANI KOTE

Asante kwa kututembelea mbeyagreennews kwa taarifa zaidi endelelea kututembela kila siku ,saa,dakika usipitwe na matukio kem kemu

MATUKIO KATIKA PICHA YALIYO WEZA KUVUTIA DUNIANI KOTE

Asante kwa kututembelea mbeyagreennews kwa taarifa zaidi endelelea kututembela kila siku ,saa,dakika usipitwe na matukio kem kemu

Saturday, 31 August 2013

ANGALIA BAYERN ILIVYO BEBA SUPER CUP, NA LUKAKU KUKOSA PENERT

 


Bayern Munich imebeba ubingwa wa Super Cup baada ya kuifunga Chelsea kwa mikwaju 5-4 ya penalty.
Katika muda wa kawaida timu hizo zilitoka sare ya mabao 2-2 baada ya Chelsea kuanza kufunga katika dakika ya nane tu kupitia Fernando Torres.


Mechi hiyo ilikwenda hadi dakika 120 kabla ya kusogezwa kwenye mikwaju ya penalti. Kama Lukaku angefunga mkwaju wa mwisho, Chelsea ingekuwa bingwa, lakini akapiga na kipa Neuer akapangua.
Chini angalia vikosi vilivyopangwa na wafungaji.
Bayern Munich: Neuer, Rafinha (Javi Martinez 56), Dante, Boateng, Alaba, Muller (Gotze 70), Lahm, Kroos, Ribery, Mandzukic, Robben (Shaqiri 95).
Subs: Starke, Van Buyten, Contento, Pizarro.
Booked: Ribery
Goals: Ribery (47), Javi Martinez (120)
Chelsea: Cech, Ivanovic, Cahill, Luiz, Cole, Ramires, Lampard, Hazard, Oscar, Schurrle, Torres (Lukaku 97).
Subs: Schwarzer, Azpilicueta, Terry, Essien, Mikel, Mata.
Booked: Cahill, Ramires, Luiz, Torres, Cole, Ivanovic
Sent off: Ramires (84)
Goals: Torres (8) Hazard (93).



HIVYO NDIVYO CHEKA ALIVYO AMCHAPA MMAREKANI NA KUTWAA UBINGWA WA DUNIA (ANGALIA HAPA PICHA)

 

CHEKA Vs WILLIAM...
NYOMI LA DIAMOND, LAKINI KUNA TAARIFA PROMOTA AMEAMBULIA PATUPU KUTOKANA NA KUGUNDULIKA KULIKUWA NA TIKETI FEKI KIBAO.

MMAREKANI ALIKAA KATIKA RAUNDI YA TATU...AKAINUKA NA KUENDELEA



Francis Cheka ameweka rekodi ya kuwa bondia wa kwanza Mtanzania kumtandika Mmarekani katika mchezo wa kuwania taji.

Cheka amefanikiwa kutwaa taji la dunia linalotambuliwa na WBF katika uzito wa Middle baada ya kumchapa bondia Phill Williams kutoka Marekani katika pambano lililomalizika punde kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar.

Cheka amefanikiwa kushinda kwa pointi baada ya majaji wote watatu kumpa ushindi wa ponti kwa kwanza akimpa 116-113, wa pili, 109-108  na wa tatu 117-111.


Pambano hilo lilikuwa kali na la kuvutia na mabondia walilianza kwa umakini mkubwa huku kila mmoja akionyesha kumsoma mwenzake hadi lilipochanganya kadiri raundi zilivyokuwa zinasonga mbele.


Baada ya Cheka kutangazwa bingwa, Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo aliyekuwa mgeni rasmi alimvisha mkanda huo baada ya kutambulishwa na bondia mkongwe, Botha kutoka Afrika Kusini.


Kabla ya hapo, Thomas Mashali naye alifanikiwa kubeba ubingwa wa Afrika baada ya kumchapa Mada Maugo kwa pointi huku majaji wakimpa ushindi wa 95-94, 95-95 na 95-94.


Pambano lilikuwa kali sana hali iliyofanya iwe kazi ngumu kwa mashabiki kutabiri nani ameibuka na ushindi hata baada ya raundi zote 10 kumalizika.


Pambano lingine lisilo la kuwania mkanda kati ya Alphonce Mchumiatumbo dhidi ya Chupaki Chipindi ambalo lilikuwa ni la uzito wa juu kabisa.


Mchumiatumbo alishinda kwa TKO katika raundi ya tano, ikiwa imebaki moja tu pambano hilo kumalizika na wasaidizi wa kona ya Chipindi wakaamua kutupa taulo.


Classic Mawe na Simba wa Tunduru ndiyo walianza kufungua ngumi za utangulizi na mwisho mkongwe Simba wa Tunduru akakubali matokeo kutoka kwa kijana huyo anayetokea Gym ya Ilala chini ya mwalimu wake Super D.

TAZARA YAHAIRISHA KUFUKUZA WAFANYAKAZI YASEMA WAREJEE KAZINI ITAWARIPA MISHAHARA YAO

MAMLAKA ya Reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA) imesitisha kusudio lililotangazwa awali, la kufukuza wafanyakazi wake wapatao 1,067 na kuagiza warudi kazini kuanzia leo.

Kaimu Mkurugenzi wa TAZARA, Ronald Phiri, alisema hayo jana alipozungumza na waandishi wa habari. Aliongeza kuwa mbali na kurudishwa kazini, mishahara yao itaanza kulipwa leo.

“Kwa kuwa hakuna aliyepewa barua ya kusimamishwa kazi mpaka sasa hivi, basi ni halali kusema kuwa hakuna aliyefukuzwa kazi TAZARA. Mazungumzo bado yanaendelea na wafanyakazi wote wanaombwa kurudi kazini kwa sababu tayari tuna fedha na tutaanza kuwalipa mishahara yao kesho (leo),” alisema Phiri.

Hata hivyo Mkurugenzi huyo alionya kuwa ambaye hataripoti kazini leo, atakuwa amejisimamisha kazi mwenyewe na hatohesabika tena kama mfanyakazi wa TAZARA. (kwa hisani ya HabariLeo)

TAZARA imekubali kuwalipa malimbikizo ya mishahara wafanyakazi wake baada ya kuendesha mgomo wa siku saba. Uamuzi huo umefikiwa baada ya TAZARA kukaa na uongozi wa wafanyakazi hao. (kwa hisani yaMWANANCHI)


 

WATANZANIA 18 WATHAMINIWA NA BRAZIL,CHINA KUSOMEA MAFUTA NA GESI

Picture
Katibu Mkuu, Wizara ya Nishati na Madini Eliakim Maswi (watatu kushoto) katika picha ya pamoja na baadhi ya vijana waliopata ufadhili wa masomo ya shahada ya uzamili katika fani ya mafuta na gesi kutoka Serikali ya watu wa China. Pia, wanafunzi wengine 10 wamepata ufadhili wa masomo kama hayo kutoka Serikali ya Brazil. Picha imepigwa mara baada ya kumalizika kwa hafla fupi ya kuwaaga wanafunzi hao iliyofanyika leo katika ukumbi wa mikutano wa Wizara hiyo uliopo jijini Dar es Salaam.

 

Friday, 30 August 2013

ANGARIA PICHA MBALI MBALI ZIKIMUONESHA DIAMOND AKIMZAWADIA MZEE GURUMO GARI


AKIMKABIDHI GARI AINA YA TOYOTA FUNGARCO

MZEE GURUMO NDANI YA MKOKO WAKE

AKIZUNGUMZA KABLA YA KUMKABIDHI GARI MZEE GURUMO

GARI AINA YA FUNCARCO AMBAYO DIAMOND AMEMKABIDHI MZEE GURUMO


Mwanamuziki wa kizazi kipya anae kick kila kona Diamond Platnumz jana aliweka rekodi na kumbukumbu katika maisha yake pale alipomzawadia gari  Maalim Gurumo.

Diamond alimkabidhi mzee Gurumo gari hilo katika uzinduzi wa video ya wimbo wake mpya number 1 katika ukumbi wa hoteli ya kimataifa Serena jijini Dar es Salaam.


Akizungumza wakati wa kumkabidhi gari hilo Diamond alisema alijiskia vibaya pale alipomsikia mzee Gurumo wakati akihojiwa redioni kuwa katika maisha yake ya muziki kwa miaka 53 hadi anastaafu,hajawahi kununua hata baiskeli

ETO'O AKUBALI PAUNI MILIONI 10 NA KUJIUNGA DARAJANI KWA MORINHO


Parading: Eto'o has signed for Chelsea
: Eto'o akiwa na jezi ya Chelsea
Pen to paper: Eto'o signs the contract in the presence of Chelsea club secretary and director David Barnard
SAMWEL ETO'O AKISAINI MKATABA MBELE YA KATIBU WA TIMU YA CHELSEA DAVID BARNARD
Pleased to be here: Eto'o has signed on a free transfer
ETO'O AKIONYESHA JEZI YA DARAJANI

 
 
                                            
 

Top target: Mourinho didn't select any strikers at Old Trafford and is known to be chasing Wayne Rooney
NDOTO ZA MORINHO ZILIANZA KWA ROONEY LAKINI NDOTO HIZO SASA ZIMEKUFA
Treble
ETO'O NA MORINHO WAKISHEREHEKEA FURAHA YA USHINDI WAKTI WAPO NA TIMU YA INTER MILLAN

BAN KI MOON ALAANI KUUAWAWA KWA MLINZI WA AMANI WA TANZANIA DRC

Picture
Walinzi wa Amani wakiwa katika moja ya doria kwenye mitaa ya mji wa Goma
Imeandikwa na Mwandishi Maalum
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa,  Ban Ki Moon  amelaani kuuawa kwa Mlinzi wa Amani kutoka Tanzania  ambapo wengine  kadhaa  wamejeruhiwa baada ya kushambuliwa na   kundi la waasi la M23 katika  katika  eneo la Mashariki ya   Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa   na msemaii wa Katibu Mkuu ,  inaeleza kwamba. “ Katibu Mkuu analaani kwa nguvu zote mauaji  ya mlinzi huyo na  kujeruhiwa kwa walinzi  wengine  10 na anatoa salamu zake za rambirambi kwa familia  za walinzi hao  na  kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  na Jamhuri ya Afrika ya kusini”.

Mashambulizi dhidi ya walinzi hao wa Amani yametokea   siku ya  jumatano katika  Vilima vya Kibati Magharibi ya Kivu ambako Misheni ya   kutuliza Amani   ya  Umoja wa Mataifa katika DRC ( MONUSCO)  ilikuwa ikisaidiana  na majeshi ya  serikali ya   DRC kuwalinda raia katika eneo  la Goma ambalo lina idadi kubwa ya watu.

Kwa mujibu wa taarifa  hiyo,  MONUSCO  ilijibu mashambulizi hayo kwa kutumia zana mbalimbali za kivita yakiwamo makombora, mizinga na helkopta za kivita wakati majeshi ya DRC yalitumia askari wa ardhini,  vifaru

Chanzo wavutiblog

TANGAZO KWA MADAKTARI NA WAUGUZI WALIO OMBA KAZI MUHIMBILI MAJINA YA HAYA HAPA


 
 Tangazo lililotolewa jana Agosti 29, 2012 na Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, limeorodhesha majina ya walioomba nafasi mbalimbali za kazi katika kada na madaraja mbalimbali.

Majina hayo na maelezo muhimu kwa watahiniwa yanapatikana mtandaoni, (bofya hapa).

KIUNGO OLJORO AJISAIDIA UWANJANI SHEIKH AMRI ABEID


 Na Khatimu Naheka, Arusha
Katika hali ya kushangaza, kiungo wa JKT Oljoro, Udda Sorita alijisaidia haja ndogo uwanjani huku sababu kubwa ikatajwa kuwa uchafu wa vyoo vya Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha.

Tukio hilo lilitokea kipindi cha pili cha mchezo wa Ligi Kuu Bara kati ya timu yake dhidi ya Simba, juzi kwenye ambapo Simba ilishinda bao 1-0.


Mchezaji huyo alifanya tukio hilo wakati alipokuwa akipasha misuli huku mechi ikiendelea, ambapo aliketi chini na kujisaidia na alipomaliza alikwenda kwa mwamuzi wa akiba na kuingia uwanjani akichukua nafasi ya Essau Sanu.

Alipouliza juu ya tukio hilo, kiongozi wa JKT Oljoro ambaye hakutaja jina lake litajwe alisema: “Kama kafanya hivyo mimi simlaumu kabisa kutokana na hali ya uchafu iliyopo kwenye vyoo vya uwanja huu, kawaambie viongozi wa uwanja wafanye usafi vyooni.”
 
SOURCE: CHAMPIONI

DAKTARI AMZUIA RASHID MATUMLA KUENDELEA KUCHEZA NGUMI



Bondia mkongwe nchini, Rashid Matumla ‘Snake Man’ ametakiwa kuachana na ngumi mara moja na ikiwezekana astaafu kabisa.
Maagizo hayo yametoka kwa mmoja wa madktari wanaoshughulikia masuala ya michezo nchini.

Akithibitisha suala hilo, Matumla ,44, amesema daktari huyo amemueleza kuachana na mchezo wa ngumi kama mchezaji na badala yake anaweza kuwa mwalimu kwa kuwa afya yake haimruhusu.


“Kweli huyo daktari ambaye nisingependa kumtaja ameniambia hilo, alisema hayo baada ya kunifanyia vipimo.

“Unajua kwa muda mrefu nimekuwa nikusumbiliwa na matatizo ya mgongo. Sasa vipimo vinaonyesha nina matatizo kidogo.
“Hata baadhi ya viungo vyangu vimekuwa havifanyi kazi vizuri kama ilivyokuwa awali,” alisema.

Kuhusiana na kama kweli yuko tayari, Matumla ambaye amewahi kutangaza anastaafu na baadaye akarejea, alisema: “Kweli nahitaji kufanya hivyo, lakini naupenda mno mchezo wa ngumi hadi nachanganyikiwa.


MADAKITARI WA MUHIMBILI WAFANIKIWA KUWATENGANISHA MAPACHA WALIOUNGANA

Picture
Daktari Bingwa wa Watoto katika Hospitali ya Muhimbili, Profesa Karim Manji (wa pili kushoto) akifurahia na wenzake baada ya kufanikiwa kwa operesheni ya kuwatenganisha watoto walioungana, kazi iliyofanywa na jopo la madaktari bingwa saba kwa saa 4. (Picha na Michael Jamson/MWANANCHI)
 
Jopo la Madaktari Bingwa Saba wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) na Taasisi ya Mifupa ya hospitali hiyo (MOI), wamefanikiwa kuwatenganisha pacha waliokuwa wameungana kiwiliwili.

Iliwalazimu mabingwa hao kutumia saa nne kufanikisha upasuaji huo. Mmoja wa watoto hao waliotenganishwa, amelazwa kwenye Wodi ya Uangalizi Maalumu (ICU) Taasisi ya Mifupa Moi wakati kiwiliwili kingine kilifariki.

Jopo la madaktari waliofanikisha upasuaji huo ni; bingwa mstaafu wa watoto ambaye aliitwa maalumu kwa kazi hiyo, Petronila Ngiloi, Dk Robert Mhina (mifupa) na Profesa Karim Manji aliyekuwa akifuatilia kwa karibu mapigo ya
 moyo.

Wengine ni Dk Karima Khalid aliyekuwa akiratibu dawa ya usingizi, Dk Hamis Shaaban (ubongo na uti wa mgongo), Dk Zaitun Bokhary (bingwa upasuaji watoto) na Dk Nyangasa (moyo na mishipa ya fahamu).

Akizungumza baada ya upasuaji huo, Dk Shaaban alisema walimfanyia vipimo mtoto ambaye hakuwa amekamilika na kugundulika kuwa hakuwa amekamilika viungo vyote achilia mbali kutokuwa na kichwa na macho pia hakuwa na moyo, figo, tumbo, maini ila alikuwa na uti wa mgongo.

“Uti wa mgongo ulikuwepo na ndio uliokuwa umeshikana na mwenzake na kuna mshipa mmoja wa fahamu ulikuwa unafanya kazi ndio maana alikuwa ukimgusa anachezesha mguu.”

Alisema kinachoratibiwa kwa sasa ni kuangalia dawa ya usingizi aliyopewa mtoto ambaye anaendelea kupumua na kwamba ndani ya saa 24, dawa ya usingizi waliyomuwekea mtoto huyo itakuwa imeisha na ataanza kunyonya kama kawaida.

Kazi ya upasuaji huo ilianza saa mbili asubuhi kwa mtoto huyo wa jinsi ya kike aliyetimia kuchukuliwa vipimo mbalimbali ikiwemo CT Scan, MRI, Ultra sound na vingine vingi kabla ya upasuaji kamili kuanza saa tano asubuhi.

Dk Shaaban alisema ni mara ya kwanza kwa Moi kufanya upasuaji wa aina ile na kwamba mara nyingi wamekuwa wakifanya upasuaji wa watoto wanaozaliwa na vichwa vikubwa pamoja na mgongo wazi ambao tatizo hilo linasababishwa na upungufu wa madini ya folic acid.

Kabla ya upasuaji kuanza, mama wa mtoto huyo Pili Hija (24) alitumia muda wa nusu saa kufanya maombi maalumu ya kumwombea mtoto wake kisha kuwaruhusu madaktari kuendelea na upasuaji huo.

Akizungumza muda mfupi baada ya kuruhusiwa kumwona mtoto wake, Hija alisema: “Ninamshukuru Mungu kwa yote na nazidi kumwomba amjalie mwanangu apone kabisa, nawashukuru na nitazidi kuwaombea madaktari wanaomtibu mwanangu.”

Alijifungulia nyumbani Agosti 18 maeneo ya Jang’ombe, Zanzibar watoto pacha walioungana mmoja akiwa amekamilika viungo vyote na mwingine akiwa na kiwiliwili. --- 
Kwahisani ya  MWANANCHI

 

KAMANDA KOVA AWAHADHARISHA WANAOBEBA MABURUNGUTU YA FEDHA

 
Dar es Salaam, 29 Agosti, 2013 — Kamanda wa Polisi kanda maalum ya Dar es Salaam, Kamishina Suleiman Kova, amewataka wananchi wenye mazoea ya kubeba fedha nyingi kutoka sehemu moja kwenda nyingine kuacha tabia hiyo kutokana na sababu za kiusalama.

Kamishina Kova ameyasema hayo katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika katika ofisi kuu za polisi kanda maalum ya Dar es Salaam huku akitanabaisha kuongezeka kwa matukio ya watu kuporwa fedha wakiwa wanaelekea au wanatoka katika mabenki na wakati mwingine kutokea kwa vifo.

"Jeshi la polisi linafanya jitihada kubwa kukabiliana na uhalifu wa aina mbalimbali, tunataka wananchi watupe ushirikiano ili tuweze kupunguza matukio ya uhalifu, Kazi kubwa ya polisi ni kuzuia uhalifu na sio kupambana na uhalifu hivyo wananchi wanatakiwa wawe wa kwanza kuzuia uharifu usitokee". Alisema Kova na kuongeza.

"Kwa wadau mbali mbali katika kuhakikisha usalama wa raia wa nchi leo tunayofuraha kushirikiana na kampuni ya mawasiliano ya Vodacom kupitia huduma ya M pesa katika kuleta suluhisho la uvamizi kwa watu 
wenye mazoea yakubeba fedha nyingi kutoka sehemu moja kwenda nyingine,"

Alisema kuwa kuna watu wanadhani kuwa na fedha nyingi ndani au kubeba fedha nyingi ni ufahari, "Kuna watu wanatabia za kushangaza sana, mtu anafurahi kubeba pesa nyingi  akijiona ni ufahari na hata wakati mwingine kuwaita watu na kuwaonyesha pesa zao ili wawaogope au kuwasifia utamaduni huo umepitwa na wakati."

Kova alisema jamii ya sasa inatakiwa kutoka katika mfumo wa matumizi ya fedha taslim, (Cash Sosiety) na kuwa jamii yenye matumizi ya fedha kwa njia za Ki elektroniki (Cashless Society) Ili kuokoa trasilimali za jeshi la polisi na vifo visivyo vya lazima kwa askari au raia.

"Katika usindikizwaji na polisi kunaweza kukatokea uvamizi ambao unaweza kuleta mapambano na hatimaye kusababisha vifo, "Nawasihi wote mtumie mfumo huu maalum wa M pesa katika kuhifadhi pesa zenu na katika kuwalipia wafanyakazi mishahara yao na hata magawio mengine kwasababu ndio njia yenye usalama zaidi kuliko kutoa fedha benki na kutembea nazo. Kwa kufanya hivyo mtakuwa mmelisaidia jeshi la polisi katika operesheni zake kwasababu ni mfumo wa kiusalama zaidi hivyo kupelekea uhalifu kupungua na kutupunguzia sisi gharama za operesheni zetu katika kuhakikisha usalama wa wananchi."

Kwa upande wake Mkuu wa Ukuzaji wa Biashara M-Pesa, Jackson Kiswaga alifafanua zaidi mfumo huo unaotumia M-Pesa kufanya kazi.

"Mfumo huu mpya wa kielektroniki wa kulipa mishahara na magawio kwa njia ya M-Pesa ni rahisi na ya haraka zaidi. Kitakachofanyika hela zitatumwa kutoka akaunti yako ya benki kwenda kwenye akaunti inayoitwa Fast Account ambayo ni ya M- Pesa alafu kwenda kwenye akaunti ya kawaida ya M-Pesa na hapo ndipo unaweza kulipa wafanyakazi wako kwa kuandika tu majina yao nambari zao za simu na kiasi kisha kubonyeza kitufe cha kutumia," alisema Kiswaga.

Alimalizia kwa kusema kuwa kwa mfumo huu unaweza kulipa wafanyakazi zaidi ya mia mbili kwa wakati moja na vilviele kwa wafanyabiashara wanaoingiza zaidi ya billioni moja wanaweza wakajiunga na M-Pesa daraja la tatu (level three)  na kujiwekea fedha zao kwenye akaunti ya M-Pesa na ataweza kulipa shilingi milioni kumi na mbili kwa wakati mmoja na milioni 50 kwa siku.

Source:  wavuti.blog

DK WEGGORO ATEULIWA KUWA MSAIDIZI WA RAIS MASWALA YA USHIRIKIANO WA KIKANDA

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Dkt. Nyamajeje Calleb Weggoro  kuwa Msaidizi wa Rais, Masuala ya Ushirikiano wa Kikanda.

Taarifa iliyotolewa leo, Alhamisi, 29 Agosti, 2013 mjini Dar es Salaam na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Y. Sefue inasema kuwa uteuzi huo umeanza jana Agosti 28, mwaka huu, 2013.

Kabla ya uteuzi huu, Dkt. Nyamajeje Calleb Weggoro alikuwa Mkurugenzi wa Sekta za Uzalishaji (Productive Sectors) katika Sekretarieti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC).
       
                                                        “Mwisho”
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
29 Agosti, 2013


chanzo Ikulu blog

Thursday, 29 August 2013

BREAKING NEWSSS!!!!!!!!!!! MAJAMBAZI WAVAMIA BANK IMETOKEA DAR( KARIAKOO)


RAMANI IKIONYESHA MAHALI ILIYOPO HABIB BANK KARIAKOO
WATU WANAODHANIWA KUWA NI MAJAMBAZI BAADHI YAO WAKIWA WAMEVALIA SARE ZA JESHI LA POLISI WAMEVAMIA HABIB AFRICAN BANK ILIYOPO KARIAKOO JIJINI DAR ES SALAAM NA KISHA KUPORA NA KUTOWEKA NA MAMILIONI YA FEDHA ASUBUHI YA LE

AKAMATWA KWA KUFANYA KAZI KAMA KANALI WA JWTZ (MWENGE JIJINI DSM)

Picture
Mtuhumiwa IBRAHIM Moses
 
Habari na Issa Mnally via GPL, Dar es Salaam — IBRAHIM Moses, mkazi wa Mwenge jijini Dar es Salaam amenaswa na Polisi wa Kituo cha Mwenge kwa madai ya kujifanya askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) mwenye cheo cha Kanali.

Kijana huyo alinaswa na polisi kwa kushirikiana na maafisa wa JWTZ baada ya kuwekewa mtego kutokana na kudaiwa kuwa alikuwa anajiita Kanali Ibra, hivyo kutiliwa mashaka hasa baada ya siku moja kuonekana akiwa na pingu.

Habari za kipolisi zinadai kuwa Ibra alikuwa akifika Kituo cha Polisi Mwenge mara kwa mara na alikuwa 
akipewa heshima zote kama afisa wa jeshi na hasa kwa kuwa alikuwa akitoa ushirikiano wakati wa kunasa wahalifu.

“Alikuwa akija kituoni na kujifanya ni Kanali Ibrahimu akiwa na gari lake, hivyo kupaki na kupatiwa ulinzi mpaka shughuli zake zinapokwisha maeneo hayo. Ilikuwa akikuta watu wamejazana hapa kituoni  alikuwa anakuwa mkali na kuhimiza washughulikiwe haraka kwani hapendi kuona watu wamejaa kwenye kituo,” kilisema chanzo chetu kituoni hapo.

Chanzo hicho kilidai kuwa walianza kumtilia mashaka baada ya siku moja kumuachia mfuko wake askari mmoja ambaye alipoudadisi alikuta kuna pingu, hivyo polisi kuulizana inakuwaje kanali wa jeshi atembee na pingu.

Habari zinasema baada ya hapo mkuu wa kituo hicho cha polisi ilibidi afanye kazi ya ziada kuwasiliana na wanajeshi wa Kambi ya Lugalo ili kujua kama wana afisa wao anayeitwa Kanali Ibrahimu Moses wa Kitengo cha Usalama wa Taifa na Mawasiliano, wakajibu hawakuwa na askari mwenye jina hilo ndipo ulipoandaliwa mtego wa kumnasa.

Imeelezwa kuwa aliitwa kituoni hapo kwa njia ya simu na kuambiwa kulikuwa na kazi ya kiintelejensia na baada ya saa tatu akawa amewasili na kukamatwa kisha kufungwa pingu na kupelekwa Kituo cha Polisi Kijitonyama, Dar kwa mahojiano zaidi ambapo afisa mmoja amesema atafikishwa mahakamani wakati wowote.

Kwa picha zaidi za kukamatwa kwa mtuhumiwa,
                  tembelea GPL

 

NEYMAR ABEBA KOMBE LA KWANZA NA BARCA, MESSI AKOSA PENALTI




Barcelona imefanikiwa kubeba kombe la kwanza msimu huu ikiwa chini ya Kocha Tata Martino.

Mshambuliaji wake mpya, Neymar kutoka Brazil naye amepata baraka ya kombe hilo la kwanza.




Lakini nyota wake, Lionel Messi amejikuta katika ‘bahati mbaya’ baada ya kukosa mkwaju wa penalti ambayo timu yake ilipata.


Pamoja na Messi kukosa penalti hiyo, Barcelona imefanikiwa kubeba kombe hilo dhidi ya Atletico Madrid baada ya timu hiyo kutoka suluhu.

Katika mechi ya kwanza mjini Madrid, Barcelona ikiwa mgeni ililazimisha sare ya bao 1-1 ambalo ndilo limeipa ubingwa.



Kawaida mechi mbili za Super Cup huwakutanisha mabingwa wa Hispania na wale wa Kombe la Mfalme maarufu kama Copa de Rey.

ETO'O ATUA RASMI LEO LONDON KWA JILI YA KUJIUNGA NA CHELSEA



Mshambuliaji nyota wa Cameroon, Samuel Eto’o Fills ametua jijini London tayari kujiunga nayo kwa mkataba wa mwaka mmoja.
Chelsea na Eto’o wamekubaliana mkataba wa mwaka mmoja ambao utagharimu pauni milioni 7.

 

Kikosi hicho chini ya Jose Mourinho kimeamua kumsajili Eto’o baada ya kukubali kushindwwa kumpata Wayne Rooney aneyeonekana sasa atabaki Eld Trafford.

Eto’o aliwasili katika stesheni ya St Pancras jijini London na kupokelewa na wakala maarufu wa kuuza wachezaji, Pini Zahav.
Mshambuliaji huyo anajiunga na Chelsea kama mchezaji huru baada ya kumaliza mkataba na Anzhi Makhachkala ambayo ilikuwa ikimlipa pauni milioni 17 kwa mwaka na kumfanya awe mchezaji anayelipwa zaidi katika soka duniani.
MFANO ATAKAPOANZA KUVAA JEZI YA CHELSEA

Baada ya vipimo, Eto’o anatarajia kusaini mkataba huo na mara moja atajiunga na mazoezi ya kikosi hicho cha Mourinho.

ANGARIA JINSI WAPENZI MPIRA WALIVYO ISHANGIRIA MBEYA CITY BAADA YA KUITANDIKA RUVU SHOOTING BAO 2--1


Mgeni rasmi meya wa jiji laMbeya Athanas Kapunga  akisalimiana na wachezaji wa Mbeya city kabla ya mechi kuanza






Kocha wa timu ya Ruvu shooting Charles Boniface Mkwasa akiongea na waandishi wa habari mara baada ya mpira kwisha

Kocha wa timu ya Mbeya city Mwambusi akiongea na waandishi wa habari



TIMU YA MBEYA CITY IMEISHINDA KWA MAGOLI MAWILI DHIDI YA MOJA YA ROVU SHOOTING WAFUNGAJI WA MBEYA CITY NI PAUL NONGA DK 7 NA STEVEN MAZANDA DAKIKA YA 90 NA GOLI LA KUFUTIA MACHOZI LA RUVU LIMEFUNGWA NA AYUBU KITALA DK 25

kwa hisani ya Mbeya yetublog