……………………………………..
WATANZANIA 2000 watanufaika na uwekezaji wa kampuni ya simu ya mkononi ya Halotel ya nchini Vietnam,kwa kupatiwa ajira mbalimbali.
Hayo yameelezwa Oktoba 16, 2015 na Mkurugenzi wa kampuni ya simu ya Halotel,tawi la Arusha,Tranh Dong,kwenye uzinduzi wa kampuni hiyo jijini Arusha na kusema kuwa kampuni hiyo imeshajenga mtandao wenye urefu wa kilometa 18,000,pamoja na kufunga mkongo wa mawasiliano yaani Fibre.
Dong,amesema kampuni hiyo inayotumia teknolojia ya kisasa zaidi yenye kasi kuliko mitandao mingine inakusudia kuongeza ushindani na kuimarisha uwekezaji kwenye sekta ya mawasiliano nchini kupitia mitandao ya simu za mikononi.
Dong, amesema kuwa kampuni hiyo inatoa huduma za Internet bure kwa shule , jeshi la polisi, hospital, shirika la posta na halmashauri za wilaya nchini kwa lengo la kuharakisha mawasiliano na utoaji huduma kwa wananchi wa vijijini na mijini kwa muda mfupi zaidi .
Amesema kampuni ya Halotel, imewekeza nchini kuanzia mwaka 2014 na tayari imeshaenea katika mikoa 26 ya Tanzania bara na Zanzibar.
Akizindua kampuni hiyo ya simu za mkononi ya Halotel, mkuu wa mkoa wa Arusha, Felix Ntibenda, amesema kuwa hiyo ni fursa pekee ya uwekezaji ambayo inaharakisha maendeleo ya jamii.
Amesema mitandao ya mawasiliano nchini inachangia 6% ya pato la taifa GDP,na akaipongeza kampuni hiyo ya Halotel licha ya uwekezaji wake mkubwa pia imepanga kutoa huduma za Internet bure kwa taasisi mbalimbali.
Akisoma hotuba hiyo, Afisa utumishi mkuu ofisi ya katibu tawala wa mkoa, Richad Kwitega, amesema kupitia kampuni hiyo shule mbalimbali nchini, hospital, jeshi la polisi, halmashauri za wilaya ,shirika la posta zitanufaika na huduma hiyo ya mawasiliano hivyo akazihimiza kujisajili ili kuweza kupata Internet ya bure kwa ajili ya kurahisisha mawasiliano.
Ameongeza kuwa bado kuna pengo kubwa la pato la wananchi wa vijijini na mijini hivyo kupitia uwekezaji huo pengo hilo litapungua.
Amesema kuwa bado mkoa wa Arusha, unahitaji wawekezaji wengi katika sekta mbalimbali ili wananchi wa mijini na vijijini waweze kunufaika na kuboresha maisha na kuwa na maendeleo endelevu
Ameongeza kuwa uwekezaji huo unaongeza ukuaji wa matumizi ya mitandao ya mawasiliano ya simu za mkononi nchini
MAKAMU WA RAIS DKT.BILAL AMWAKILISHA RAIS JAKAYA KUZINDUA HALOTEL TANZANIA
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia wakati wa hafla ya uzinduzi wa mtandao mpya wa simu za Halotel Tanzania, iliyofanyika kwenye Hoteli ya Hyatt Kilimanjaro jana usiku Okt 15, 2015.
Picha na OMR
Waziri wa Sayansi na Tknolojia, Makame Mbarawa, akizungumza kabla ya kumkaribisha Mgeni rasmi Makamu wa Rais,Dkt Bilal, kuzindua rasmi Halotel Tanzania katika hafla hiyo iliyofanyika kwenye Hoteli ya Hyatt Kilimanjaro jana usiku Okt 15, 2015.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Waziri wa Mawasiliano wa Vietnam,Nguyen Bac Son, wakati walipokutana kwa mazungumzo kwenye hafla ya uzinduzi wa Mtandao mpya wa simu za Halotel Tanzania, iliyofanyika kwenye Hoteli ya Hyatt Kilimanjaro jijini Dar es Salaam, jana usiku Okt 15, 2015.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Waziri wa Mawasiliano wa Vietnam,Nguyen Bac Son, wakati walipokutana kwenye hafla ya uzinduzi wa Mtandao mpya wa simu za Halotel Tanzania, iliyofanyika kwenye Hoteli ya Hyatt Kilimanjaro jijini Dar es Salaam, jana usiku Okt 15, 2015.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi zawadi, Waziri wa Mawasiliano wa Vietnam,Nguyen Bac Son, wakati wa hafla ya uzinduzi wa Mtandao mpya wa simu za Halotel Tanzania, iliyofanyika kwenye Hoteli ya Hyatt Kilimanjaro jijini Dar es Salaam, jana usiku Okt 15, 2015.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, (katikati) akiwaongoza viongozi wenzake kupiga ngoma kama ishara ya uzinduzi rasmi wa Mtandao mpya wa mawasiliano wa Halotel Tanzania, wakati wa hafla ya uzinduzi iliyofanyika kwenye Hoteli ya Hyatt Kilimanjaro jijini Dar es Salaam, jana usiku Okt 15, 2015.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, (katikati) akigonganisha glasi na baadhi ya viongozi wa Vietnam kama ishara ya furaha baada ya uzinduzi rasmi wa Mtandao mpya wa mawasiliano wa Halotel Tanzania, wakati wa hafla ya uzinduzi iliyofanyika kwenye Hoteli ya Hyatt Kilimanjaro jijini Dar es Salaam, jana usiku Okt 15, 2015.
0 comments:
Post a Comment