Wednesday, 21 October 2015

Kiongozi Aliyeshindwa Nigeria Ashauri Watakaoshindwa Uchaguzini Tanzania


Kiongozi wa ujumbe wa waangalizi wa uchaguzi wa Tanzania waliotoka Jumuiya ya Madola ametoa wito kwa watakaoshindwa uchaguzini Tanzania kukubali matokeo.
Goodluck Jonathan, ambaye mwenyewe alishindwa uchaguzini na upinzani amesema uchaguzi ni kama biashara.

Kuna kushinda na kushindwa,” amenukuliwa na gazeti la The Citizen la Tanzania.

Amesema kukubali matokeo kutasaidia kuepusha mzozo wa kisiasa.
Kutokana na kupanda kwa joto la kisiasa nchini humo, Watanzania wengi wamekuwa wakifuatilia kwa karibu yanayoandikwa magazetini.
Mwandishi wa BBC Ruth Nesoba aliwapata wengi wakizingira vituo vya kuuzia magazeti Dar es Salaam kujipasha habari.

Jonathan, aliyeshindwa uchaguzini na Muhammadu Buhari mwezi Machi, alikubali matokeo upesi baada ya kushindwa na kupuuzilia mbali ushauri wa waliomtaka kupinga matokeo.
Mwandishi wa BBC aliyeko Zanzbar Aboubakar Famau aliwapata raia huko wakikusanyika mapema vikuo vya kuuzia magazeti kutazama vichwa vya habari.

Jumuiya ya Madola ina waangalizi 14 wa uchaguzi nchini Tanzania na wanatarajiwa kuwa nchini humo hadi Oktoba 31.

0 comments: