Wednesday, 14 October 2015

KASEJA ASEMA SIMBA KICHAPO LAZIMA ,CITY IKO IMARA ZAIDI WAJUAVYO

juma k juma nt
Golikipa mahiri wa Mbeya City Fc, Juma K Juma, amesema anaamimi mchezo ujao wa ligi kuu ya soka Tanzania  bara kati ya timu yake na Simba utakuwa mgumu kutokana na kuzikutanisha timu zenye sura mbili tofauti kwenye vikosi vyake.
Akizungumza mapema leo Juma K Juma  ambaye hapo awali aliwahi kuichezea Simba kwa mafanikio kwa kipindi kirefu alisema kuwa anautizama mchezo huu katika sura tatu tofauti akiamini utakuwa mgumu huku akitoa nafasi kwa timu yake kuibuka na ushindi kufuatia rekondi nzuri mbele ya Simba  katika misimu miwili iliyopita.
“Kwangu mimi huu utakuwa mchezo mgumu, City tutaingia uwanjani tukiwa na rekodi nzuri mbele ya Simba huku pia kikosi chetu kikiwa na nyota vijana  wenye vipaji vikubwa ambao bado wana kiu kubwa ya kucheza na kudhihirisha ubora wao, hivyo sina shaka na sisi kupata ushindi,nafahamu Simba wamekuwa imara msimu huu na wameshinda michezo yao yote ya mwanzo, hilo  halitunyimi nafasi ya ushindi  hasa ukizingatia tutakuwa tunacheza kwenye uwanja wetu wa nyumbani mbele ya mashabiki wetu” alisema.
Akiendelea kipa huyo mzoefu aliweka wazi kuwa kupoteza michezo kadhaa ya awali kwa kikosi chake kumefanya kila mmoja ndani ya kikosi kuwa tayari kupambana kufa na kupona kwenye mchezo huo dhidi ya Simba uliopangwa kuchezwa tarehe 17 mwezi huu kwenye uwanja wa Sokoine ili kurudisha matumaini ya City kusaka nafasi za juu kwenye msimamo wa ligi kabla ya kumalizika kwa mzunguko.
“Tumepoteza michezo minne  mpaka sasa hili ni deni kubwa kwa mashabiki wetu, tutacheza kufa na kupona ili kupata matokeo ni wazi utakuwa mchezo mgumu lakini nia yetu ni kushinda, tunazihitaji pointi tatu kutoka kwao siku hiyo, wao ni timu ngumu lakini sisi tuna kikosi imara” alisema.
Katika hatua nyingine mchezo huu utakuwa wa 8 kwa Juma kucheza dhidi ya Simba ikiwa ni michezo mitano aliyocheza kabla ya kujunga nayo wakati huo akiwa Moro United na pia michezo miwili baada ya kuondoka Msimbazi na kujunga  Yanga  hesabu inayokamilisha michezo 7 huku huu wa tarehe 17 ukitarajiwa kuwa wa 8.
 .

0 comments: