Mambo sasa yanaonekana si mazuri tena kwa ule mfumo wa 4-4-2 ambao amekuwa akiuamini sana Kocha Diego Simeone.
Amekuwa akipoteza mechi mfululizo, jambo ambalo tayari limezua mjadala mkubwa.
Wadau sasa wanamshauri Simeone kutumia mfumo wa 4-3-3 ambao unaweza kubadilisha mambo.
Mara kadhaa amekuwa akishauriwa katika hilo, lakini raia huyo wa Argentina amekuwa akisisitiza kutumia 4-4-2.
Lakini kupoteza mechi mfululizo, kupotea kwa ushindani kutoka katika kikosi chake kunaonekana kumlazimisha kubadili mfumo huo na kuhamia 4-3-3 ambayo inakuwa na washambuliaji watatu mbele.
0 comments:
Post a Comment