Aliyekuwa mgombea Urais wa Zanzibar kupitia Chama cha Wananchi CUF Maalim Seif Sharif Hamad ameamua kutumbua majipu ndani ya Serikali ya Zanzibar baada ya kudai fedha nyingi zilitoroshwa kabla ya uchaguzi na vigogo wengi wa SMZ wana miliki fedha nje.
Maalim Seif Sharrif Hamad ametoa kauli hio hapa Zanzibar wakati akiongea na waandishi habari kuelezea mikakati ya Chama cha Wananchi CUF katika kudai haki ya wananchi wa Zanzibar ambapo amesema kabla ya uchaguzi baadhi ya viongozi walisafirisha fedha nje ya nchi na wengine kununua majumba kwa fedha za umma ingawa hakuwataja viongozi hao.
Akizumgumzia hatua ambazo CUF imezipanga kuchukua maalim Seif ambaye pia ni Katibu Mkuu wa CUF amesisitiza kuwa njia kubwa itaendelea kuwa ya amani na sio fujo wala vurugu ikiwa ni pamoja na kufuata utaratibu wa kwenda mahakama za kimataifa ingawa zina utaratibu wake lakini tayari baadhi ya taasisi za haki za binaadamu wameanza kulishughulikia suala la uvunjaaji wa haki hizo.
Huu ni mkutano wa pili wa CUF kufanya kuelezea msimamo wao wa kutoitambua Serikali ya Dk.Ali Mohamed Shein na harakati wanazozichukua ili kuhakikisha mamauzi ya wananchi ya Ockoba mwaka jana yanaheshimiwa na kutendeka.
0 comments:
Post a Comment