Serikali mkoani Pemba imewaagiza watendaji wake kuhakikisha kuwa baadhi ya wazazi ambao watashindwa kuwahimiza watoto wao kwenda shule wakamatwe na kuchukuliwa hatua kali za kisheria ili kupunguza idadi ya vijana kujihusisha na matumizi ya dawa za kulevya kisiwani humo.
Agizo hilo limetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Pemba katika taarifa yake iliyosomwa kwa niaba yake na Mkuu wa wilaya mkoani katika hafla ya makabidhiano ya jengo la shule ya msingi Matale iliyojengwa kwa msaada wa watu wa marekani kwa gharama ya shilingi milioni 440 kwa lengo la kusaidia sekta ya elimu.
Kwa upande wake Afisa mdhamini elimu na mafunzo ya amani mkoani Pemba Salim Kitwana amewataka wakazi wa Matale na vitongoji vyake kuhakikisha kuwa wanafunzi wanasoma katika shule hiyo ya kimataifa ili kukuza viwango vya elimu katika mkoa wa Pemba.
Kufuatia hatua wakazi wa eneo la Matale wa mkoa wa Pemba wameaswa kulitunza jengo hilo lenye uwezo wa kuongezwa ghorofa nne kwenda juu kulitunza ili iwe msingi bora wa kuibua vipaji vya elimu kwa watoto wa eneo hilo .
0 comments:
Post a Comment