Monday, 19 October 2015

VYAMA VYA SIASA VISIKIMBILE VYOMBO VYA HABARI KATKA KIPINDIKI CHA UCHAGUZI


JAJI Damiani Lubuva mwenyekiti wa tume ya uchaguzi tz 
……………………………….
TUME ya taifa ya uchaguzi, imevitaka vyama vya kisiasa nchini kupeleka malalamiko yao  kwenye kamati za maadili za tume hiyo badala ya kukimbilia kwenye vyombo vya habari ambavyo havina mamlaka ya kutatua changamoto zinazojitokeza wakati huu wa kampeni za uchaguzi mkuu.

Onyo hilo limetolewa leo mjini, Arusha na kaimu mwenyekiti wa tume ya taifa ya uchaguzi, George Kashura,(hayupo pichani) alipokuwa akifungua mkutano wa siku moja wa tume na vyama vya siasa mkoa wa Arusha na kusisitiza kuwa vyama vya siasa kupeleka malalamiko yao kwenye kamati za maadili ili yafanyiwe kazi .
Aidha tume imevitaka vyama vyote vya siasa nchini kutoa taarifa sahihi badala ya kutoa taarifa zisizo sahihi ambazo zinapotosha wananchikuhusu tume .
Tume imesisitiza kuwa mwananchi akimaliza kupiga kura aondoke kwenye kituo cha kupigia kura na kusisitiza kuwa umbali wa mita 200 kutoka kwenye kituo sio umbali unaowaruhusu kukusanyika kwa kisingizio cha kulinda kura.
Tume imewataka wanasiasa kuzingatia sheria  na taratibu za uendeshaji  uchaguzi ,kuepuka lugha zozote za uchochezi ,na endapo chama chochote  kitawaelekeza wanachama wake kubakia vituoni mara baada ya kupiga kura  kuna uwezekano mkubwa wa kutokea vurugu.
Jumla ya watu milioni 23,782,558, kati yao 3870, ambao sio  raia waliandikishwa kwenye daftari la kudumu la wapiga kura na tayari wameshaondolewa kwenye daftari hilo.
Huku watu wengine 231,955, wameondolewa baada ya kubainika kujiandikisha zaidi ya mara moja hivyo watakaopiga kura kwenye uchaguzi mkuu ujao ni watanzania milioni 23, 154, 485.
Zanzibar wapiga kura walioandikishwa kwa ajili ya kupiga kura kwenye uchaguzi mkuu ujao ni 503,193.
Aidha tume imetenga jumla ya vituo 64,736,vitakavyotumika kupigia kura kwenye uchaguzi mkuu ujao  ambapo Tanzania bara ina jumla ya vituo 63,156, na Tanzania Zanzibar ina vituo 1,580 na kila kituo kitakuwa na jumla ya wapiga kura 450.
TUME ya taifa ya uchaguzi imesema chaguzi za marudio kwenye majimbo mbayo wagombea wake wamefariki utafanyika mwezi Novemba 22 mwaka huu.Tume imesema kampeni zitaanza Novemba 13 hadi 21 mwaka huu na uchaguzi utfanyika Novemba 22.
Tume imesema kuwa uteuzi wa wagombea nafasi hizo utafanyika Novemba 12 .
Majimbo hayo ni Ulanga mashariki, Lushoto, Arusha,Ludewa , Masasi.
Taarfa hiyo imesema kuwa uchaguzi huo utafanyika kwa pamoja na uchaguzi wa madiwani kata nne  ambao wagombea wake wamfariki dunia .

Na Mahmoud Ahmad Arusha


0 comments: