Sunday, 10 April 2016

Watu 100 wateketea katika hekalu la wahindu


Image copyrightAFP
Image caption100 watekea hadi kufa katika hekalu la wahindu
Polisi nchini India wanasema kuwa zaidi ya watu 100 wameuawa na wengine 150 kujeruhiwa katika moto uliotokea katika hekalu la Wahindu katika jimbo la Kusini la Kerala.
Moto huo uliotokea katika wilaya ya Kollam ulianza wakati wa sherehe ya mapema asubuhi.
Polisi wanasema huenda moto huo ulianzishwa na fataki.
Waziri wa mashauri ya nchini katika jimbo la Kerala, Ramesh Chentallah, alisema kuwa uchunguzi wa mahakama utaanzishwa.
Image captionPolisi wanasema huenda moto huo ulianzishwa na fataki.
Waziri wa Mashauri ya Ndani, Oommen Chandi, na bwana Ramesh wamesema kuwa watatembelea eneo hilo.
Polisi wamesema kuwa moto huo umedhibitiwa lakini shughuli za uokozi zingali zinaendelea.
Maelfu ya waumini walikuwa wamekongamana ilikushuhudia maonesha haya ya kila mwaka ya fataki.
Image captionWaziri mkuu wa India bwana Narendra Modi amewasili Kerala.
Uchunguzi wa kwanza umebaini kuwa maafisa wakuu katika eneo hilo waliwanyima waratibu wa maonesho hayo leseni ya kuandaa maonesho ya fataki kufuatia hofu kuhusu usalama wa umma.
Waziri mkuu wa India bwana Narendra Modi amewasili Kerala.

0 comments: