Wananchi wa kata ya Ushirika wilayani Tukuyu wameusimamisha msafara wa Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto uliokua ukitoka wilayani Kyela kuelekea Mbarali kwa madai hawana Kituo cha Afya wala Zahanati kwa miaka hamsini sasa.
Wananchi hao ambao walikua wameshika bango kubwa lililoandika hawamtaki mkurugenzi wa halmashauri hiyo kwa madai ya kuwasimamisha ujenzi mara mbili
Akieleza kilio chao katibu.wa kamati ya ujenzi, Fatma Mwandegele alisema eneo hilo limeingia kwenye mgogoro wa ardhi kwa muda mrefu kati ya kijiji cha Mpunguso na aliyekua katibu tarafa wa kata ya Pakati, Bw. Mwakapala
Hata hivyo alisema kesi kuhusu eneo hilo ilishamalizika na wananchi walikusanya nguvu zao kwa kuchangia simenti na mawe hata hivyo simenti hiyo iliharibika.
Waziri Ummy Mwalimu ilimlazimu kwenda kuliona eneo hilo ambalo limechimbwa tayari kwa kuanza msingi huku mawe yakiwa yamerundikwa pasipo kuendelea na ujenzi alimuagiza mganga mkuu wa mkoa ambaye alikua nae kwenye msafara wake, siku ya jumatatu wafike eneo hilo pamoja na mkurugenzi na mganga mkuu wa wilaya ili waeleze kwanini wasiendelee na ujenzi wa zahanati hiyo.
“Nawaomba wananchi muwe watulivu ili tujihakikishie kama kesi hiyo imekwisha na kwanini tusiendelee na ujenzi huu na Jumatatu kabla ya.saa tisa mchana niwe nimepata ripoti ya eneo hili,” alisema Mhe. Mwalimu.
Aidha, Waziri huyo aliwathibitishia wananchi hao kwamba lazima zahanati ijengwe kwenye kijiji hicho ili kiweze kuwahudumia wananchi na kuwaahidi.serikali itawaletea wa huduma pamoja na dawa, vifaa na vifaa tiba.
Na Catherine Sungura, Tukuyu
Wananchi wa kata ya Ushirika-Tukuyu wakiwa wamebeba bango kuonesha kilio chao kwa Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu.
Waziri Ummy Mwalimu akiongea na wananchi hao ambao waliomzunguka kutoa kero yao ya kuzuiwa kuendelea na ujenzi wa Zahanati.
Mmoja wa mwanakamati akimueleza mgogoro wao wa eneo la ujenzi wa zahanati kati yao na mkurugenzi wa halmashauri yao.
Mwanakamati huyo akiendelea na malalamiko hayo.
0 comments:
Post a Comment