Saturday, 9 April 2016

KASHFA YA RUSHWA TFF YATUA TAKUKURU, KAZI IMEANZA.....

 Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (Takukuru) tayari imeanza uchunguzi kuhusu tuhuma za rushwa katika Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).

Hatua hiyo imekuja ikiwa ni siku chache baada ya kunaswa kwa sauti zinazohisiwa kuwa ni za viongozi wa TFF wakipanga matokeo ya mechi ya Ligi Daraja la Kwanza kati ya Geita Gold Sports na JKT Kanembwa.

Shirikisho hilo, tayari limemsi-mamisha kazi msaidizi wa Rais, Juma Matandika huku Kaimu Mkurugenzi wa Mashindano wa TFF, Martin Chacha akitangaza kujiuzulu nafasi yake.

Ofisa Habari wa Takukuru, Tunu Mlei alisema kisheria suala hilo kwa hivi sasa hawaruhusiwi kulizungumza na wataliweka wazi mara baada ya uchunguzi kukamilika.

 “Takukuru tayari imeanza uchunguzi wa hizo tuhuma za rushwa inayodhaniwa TFF inahusika, hivyo hilo suala lipo kwetu na linashughulikiwa kisheria haturuhusiwi kulizungumza hadi pale litakapokamilika, hivyo tunawaomba wadau wa soka kuwa wavumilivu katika kipindi hiki tukisubiria uchunguzi huo utakapomalizika,” alisema Mlei.

0 comments: