Wednesday, 4 November 2015

Mvua iliyoambatana na upepo mkali yabomoa nyumba 96 Bahi, Dodoma.





Mvua kubwa iliyoambatana na upepo mkali imebomoa nyumba 96 zikiwemo ofisi za umma katika kijiji cha Kigwe wilayani Bahi Dodoma ambapo watu zaidi ya 360 hawana mahala pa kuishi huku ikiacha hasara kubwa kwa wakazi wa eneo hilo.
Kwa mujibu wa wahanga wa mvua hiyo wamesema ilianza jioni ya siku ya jumatatu na kuendelea kwa muda mrefu huku upepo mkali ulioambatana nayo ukiezua mabati na kubomoa nyumba ambapo tukio hilo limewaacha katika mazingira magumu kwani wanakosa makazi na chakula hawana kutokana akiba yote waliokuwa nayo kuharibika.
 
Miongoni mwa wahanga wa tukio hilo ni walimu wa shule ya sekondari ya Kigwe ambao nyumba yao iliezuliwa mabati na mara baada ya kutokea waliwasiliana na uongozi wa elimu wilaya lakini katika hali ya kushangaza walimu hao wanadai afisa elimu wa wilaya hiyo akiwataka kutoa pesa zao mifukoni kukarabati nyumba ambapo wanahoji mfuko wa maafa wa wilaya una kazi gani.
 
Kwa upande wake afisa mtendaji wa kata ya Kigwe Mgwala Manala Songola amesema tayari kamati ya maafa ya kata hiyo imefanya tathmini ya madhara yaliyotokana na mvua hiyo huku akibainisha kuwa baadhi ya wahanga wamehifadhiwa kwenye jengo la shirika lisilo la serikali la Kisedet kusubiri taratibu zingine za msaada.
 

0 comments: