MATUKIO KATIKA PICHA YALIYO WEZA KUVUTIA DUNIANI KOTE

Asante kwa kututembelea mbeyagreennews kwa taarifa zaidi endelelea kututembela kila siku ,saa,dakika usipitwe na matukio kem kemu

MATUKIO KATIKA PICHA YALIYO WEZA KUVUTIA DUNIANI KOTE

Asante kwa kututembelea mbeyagreennews kwa taarifa zaidi endelelea kututembela kila siku ,saa,dakika usipitwe na matukio kem kemu

MATUKIO KATIKA PICHA YALIYO WEZA KUVUTIA DUNIANI KOTE

Asante kwa kututembelea mbeyagreennews kwa taarifa zaidi endelelea kututembela kila siku ,saa,dakika usipitwe na matukio kem kemu

MATUKIO KATIKA PICHA YALIYO WEZA KUVUTIA DUNIANI KOTE

Asante kwa kututembelea mbeyagreennews kwa taarifa zaidi endelelea kututembela kila siku ,saa,dakika usipitwe na matukio kem kemu

MATUKIO KATIKA PICHA YALIYO WEZA KUVUTIA DUNIANI KOTE

Asante kwa kututembelea mbeyagreennews kwa taarifa zaidi endelelea kututembela kila siku ,saa,dakika usipitwe na matukio kem kemu

Tuesday, 4 June 2013

MADIWANI WA WILAYA YA MBEYA WAPENDEKEZA MKOA MPYA UITWE MBOZI

KIKAO cha dharura cha Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya Mbeya kimependekeza jina la mkoa mpya wa Mbeya liwe ni Mkoa wa Mbozi badala ya mkoa wa Rungwe kama ilivyopendekezwa na wataalamu,wenye makao yake makuu wilayani Mbozi katika mji wa Vwawa.

Wakizungumza katika kikao hicho Madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Mbeya walisema kuwa azma ya kupendekeza kuwepo kwa mkoa mpya katika wilaya ya Mbozi umezingatia jiografia ya mkoa na fursa za kiuchumi zilizopo badala ya hamasa za siasa.

‘’Sisi ni madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Mbeya, hatuna maslahi yoyote ya kisiasa na wilaya ya Mbozi, tumezingatia fursa za kiuchumi na jiografia ya mkoa ambayo italeta tija na maslahi kwa Taifa,’’alisema Bw. Mashauri Mbembela Diwani wa kata ya Nsalaga.

Awali katika mapendekezo hayo ambayo yaliwasilishwa na Ofisa Uchaguzi wa wilaya kwa niaba ya Kaimu 
Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Mbeya Bi. Marietha Mlozi,Bw.Edward Mwaigombe alisoma taarifa ya mapendekezo ya jina la mkoa mpya kuwa ni Rungwe kama lilivyopendekezwa na wataalamu.

Bw. Mwaigombe alisema kuwa, taarifa ya wataalamu imezingatia vigezo vya idadi ya watu, ukubwa wa eneo, huduma zilizopo na mawasiliano ambayo ni mapendekezo kutoka katika kamati za maendeleo za kata 14 za Ulenje, Lwanjilo, Ikukwa, Swaya, Mshewe, Igale, Iyunga Mapinduzi, Tembela, Bonde la Songwe, Utengule Usongwe, Ilungu, Ilembo na Inyala.

Alisema kuwa kamati zilipendekeza mkoa wa Mbeya ugawanywe katika mikoa miwili ya Mbeya na Rungwe ambapo mkoa wa Mbeya wenye takwimu ya idadi ya watu 1,721,795 na ukubwa wa eneo la kilomita za mraba 41,544 umependekezwa kuundwa kwa wilaya za Chunya,Mbozi,Momba, ambapo makao yake makuu yanatarajiwa kuwa jiji la Mbeya.

Bw. Mwaigombe alisema kuwa mkoa wa pili ambao una takwimu ya watu 985,915 na ukubwa wa eneo wa kilomita za mraba 22,073 unatarajiwa kuundwa na wilaya za Mbarali, Rungwe,Kyela na Ileje na makao yake makuu yanatarajia kuwa katika wilaya ya Rungwe.

Aidha katika taarifa hiyo kwa madiwani wa halmashauri ya Wilaya ya Mbeya, ilipendekezwa kuanzishwa kwa wilaya mpya kutokana na jiografia na kuzingatia mgawanyo mpya wa mkoa kati ya wilaya ya Mbeya na Halmashauri ya Jiji la Mbeya na kupendekezwa wilaya hizo zigawanywe katika wilaya tatu.

Hata hivyo katika mapendekezo ya madiwani wa halmashauri hiyo walisema kuwa mji wa Mbalizi ujigawe kutoka katika halmashauri ya wilaya ya Mbeya na ujitegemee kuwa wilaya kamili.

Katika mapendekezo ya awali madiwani walipendekeza majina mawili ya mkoa wa Mbozi na Mkoa wa Songwe ambapo jina la mkoa wa Mbozi lilipitishwa na madiwani kwa kura 24 dhidi ya kura 3 ambapo baadaye majina mawili ya mkoa wa Rungwe na mkoa wa Mbozi nayo yalipigiwa kura na jina la mkoa wa Mbozi lilipita kwa kura 24 dhidi ya kura tatu za jina la mkoa wa Rungwe.

Akizungumza katika kikao hicho Makamu Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Mbeya Bw. Mwalingo Kisemba alisema kuwa mchakato huo umekuja baada ya ushauri na mapendekezo ya kuugawa mkoa wa Mbeya ambao kwa sasa una jumla ya watu milioni 2.7 na ukubwa wa kilomita za mraba 63,617.
 
 

 

MWANAMKE KAJIFUNGUA WATOTO WATANO 5 KWA MARA MOJA

madakitari wakimfanyia huduma
clip_image001
Alexandra kinava akiwa na ujauzito
Dk akiwa amebeba mtoto













TANZANIA YA TIA SAINI MKATABA WA BIASHARA YA SILAHA

Picture
Naibu Muwakilishi wa Kudumu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Balozi Ramadhan M. Mwinyi akitia sahihi kwa niaba ya Serikali,Mkataba wa Kimataifa wa Kudhibiti Biashara ya Silaha ( ATT) Tanzania ilikuwa kati ya nchi 67 za kwanza ambazo zimetia sahihi katika siku ya kwanza ya uzinduzi wa tukio hilo la kihistoria. Baada ya Mkataba kutiwa sahihi nchi zaidi ya 50 kama sheria zinavyotaka utaanza kufanya kazi rasmi baada ya siku 90. Mkataba huu ambazo umechukua zaidi ya miaka sita hadi kupatikana unalenga katika pamoja na mambo mengine kusimamia na kuratibu biashara ya silaha zikiwamo mizinga ya kivita, magari ya deraya, ndege za kivita, helkopta za mashambulizi, meli za kivita na silaha ndogo na nyepesi. vile vile mkataba unalenga kudhibiti silaha zisiangukie mikononi mwa makundi ya kihalifu yakiwamo ya kigaidi.
Na Mwandishi Maalum — Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imekuwa miongozi mwa nchi za kwanza kutia sahihi Mkataba wa Kimataifa wa  Kudhibiti Biashara ya Silaha Duniani ( ATT)

Utiaji sahihi  wa tukio hilo la kihistoria  umeziduliwa jana jumatatu ( Juni 3) hapa Makao  Makuu ya Umoja wa Mataifa. Ukishuhudiwa na  viongozi  mbalimbali  akiwamo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon.

Katika  tukio hilo Jamhuri ya Muungano wa Tanzania iliwakilishwa na  Balozi Ramadhan M. Mwinyi, Naibu Muwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa.

Utiaji  sahihi  wa mkataba huo  unafanyika ikiwa ni takribani miezi miwili kupita tangu Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa  lilipoupitisha kwa  kuupigia kura 154 za ndiyo na hivyo kuhitimisha majadiliano  ya uundwaji wa  mkataba yaliyodumu kwa takribani miaka sita.
Kutiwa sahihi kwa  Mkataba huo sasa kunafungua  fursa ya  kuanza kufanya kazi rasmi baada ya siku 90, 
kwa sababu  zilikuwa zikihitajika  sahihi    50 ili upate  baraka ya kuanza rasmi. Lakini idadi hiyo imepitiliza katika siku ya kwanza ya utiaji wa sahihi na kufikia nchi 67.

Dhumuni  kuu la  mkataba  pamoja na mambo mengine ni kusimamia na kuratibu biashara ya silaha za aina mbalimbali zikiwamo, mizinga ya kivita, magari ya deraya,  ndege za kivita, helkopta za mashambulizi, meli za kivita, makombora pamoja na silaha ndogo ndogo na nyepesi.

Aidha Mkataba pamoja  masuala mengineyo hautaingilia uhuru wa nchi  kununua silaha kwa matumizi yake  ya ndani na haki ya kujilinda na kulinda mipaka yake, vilevile mkataba hauzui nchi kufanya biashara ya kusafiri aina yoyote ya silaha ilimradi inazingatia sheria na taratibu zilizomo ndani ya  mkataba ikiwa ni pamoja na taratibu ambazo nchi yenyewe imejiwekea.

Matumaini ya Jumuiya ya Kimataifa ni kwamba utekelezaji wa  mkataba na kama utaekelezea ipasavyo utasaidia sana  kudhibiti silaha zisiangukie mikononi mwa makundi mbalimbali ya kihalifu yakiwamo ya kigaidi.

Akizungumza mara baada ya kutia sahihi,  Balozi Ramadhan Mwinyi aliungana na wasemaji wengine katika  kukaribisha hatua hiyo muhimu.  Huku akieleza kwamba  kwa Tanzania kutia sahihi ni uthibitisho wa utayari wake  wa kuutekeleza kwa  kuzingatia masharti na matakwa yanayoendeana na mkataba huo.

Akasema   Tanzania imekuwa miongoni mwa nchi za mwanzo kutia sahihi mkataba huo  kwa kuwa  ilikuwa moja kati ya nchi zilizodhamini Azimio la Kuanzishwa kwa  Mkataba  na pia ilishiriki kikamilifu katika majadiliano yote yaliyozaa mkataba huo.

Balozi Mwinyi akaeleza pia kuwa kufanya kazi kwa  Mkataba  huo kutachangia katika amani ya Kimataifa, amani na  usalama wa Kikanda na pia utachangia sana katika kupunguza   madhara yatokanayo na biashara haramu na holela ya silaha lakini pia  utasaidia katika kukuza na kuimarisha uhusiano mzuri miongoni mwa  nchi wanachama.

Katika  hatua nyingine Muwakilishi huyo wa Tanzania amesisitiza haja na umuhimu wa  uwepo wa fursa sawa  kati ya  wasafirishaji wa silaha na waagizaji wa silaha  na kwamba Mkataba huo usidhibiti au kuzuia biashara ya silaha ambayo ni halali na kwamba mkataba haupashwi kuingilia au kwa namna yoyote  ile au   kuadhiri uhuru na haki ya nchi kujilinda na kulinda watu wake.

Tanzania pia imekaribisha misaada ya kiufundi katika maandalizi ya utekelezaji wa mkataba huo hasa  kwa nchi zinazoendelea.

Nchi  hizo 67 ambazo zimetia sahihi ni   , Albania, Antigua and Barbuda, Argentina, Australia, Austria,  Bahamas, Belgium, Belize, Benin, Brazil,  Burkina  Faso, Burundi, Chile, Costa Rica,  Cote D’ Ivoire, Croatia, Cyprus, Czech Republic , Denmark, Djibout,  na  Dominica Republic.

Nyingine ni  Estonia, Finland, France, Germany, Greece, Grenada, Guyana, Hungary, Iceland, Italy, Jamaica,  Japan, Latvia, Liechtenstein,  Lithuania, Luxembourg, Mali, Malta, Mauritania, Mexico na  Montenegro.

Mataifa mengine ni Mozambique, Netherlands, New Zealand, Norway, Palau, Panama,  Portugal,  Republic of Korea,  Romania, Saint Lucia,  Saint Vincent and the  Grenadines,  Senegal, Seychelles,  Slovenia, Spain, Suriname, Sweden, Switzerland, Togo,  Trinidad and Tobago, Tuvalu, United Kingdom of Great Britain and Northern  Ireland,  United Republic of Tanzania na Uruguay


kwa msaada wa wavuti

WANAFUNZI WA SHULE YA MSINGI BESTA (ENGLISH MEDIUM) WAONDOLEWA SHULENI BAADA YA SHULE KUUZWA KWA AMRI YA MAHAKAMA MBEYA

 

 Hii ndiyo Shule ya Msingi ya Besta Sae Mbeya.
  
 Vibarua waliopewa jukumu la kuhamisha mizigo shuleni hapo
 Viti  vikiwa vimetolewa eneo la shule ya Msingi Besta
 Gari la mizigo likichukua mizigo kuelekea eneo Jengine
 Waliopewa Dhamana ya kuchukua mizigo wakiwa  wanaingia ndani kwa nguvu kutoa vitu katika shule hiyo ya Besta
 Wanafunzi wa Shule ya Besta wakiwa Hawaelewi cha kufanya wakati mizigo yao aikichukuliwa

 Mmiliki wa Kampuni ya Ulinzi  ya Retired Army Bwana Kubaja akiimarisha ulinzi baada ya kupewa jukumu la kulinda shule hiyo na Wamiriki wapya.
 Kipande cha Shule ya Besta
 Polisi wakiwa na watu waliopewa dhamana ya kutoa vitu Besta wakiwa wanaendelea kutoa vitu hivyo
 Baadhi ya vitu ambavyo vilitolewa nje ya Shule ya Besta
Vijana waliopewa Dhamana ya kutoa vitu vya Shuleni hapo wakitoa Magari nje ya Shule hiyo
 Msikiti ambao upo ndani ya shule ya Msingi Besta ambao pia wananchi wa Jirani wanatumia , nao pia umenunuliwa kwa Amri ya Mahakama
 

 Wanafunzi wa Shule ya Msingi wa Besta wakiwa wanakusanya Madftari yake pamoja na Mitihani yao.

 Mmiriki wa Shule ya Besta Ndugu Hamis Othnman akimsihi Askari ampe nakala ya kuondolewa kwake Shuleni Hapo.
  Mmiriki wa Shule ya Besta Ndugu Hamis Othnman akikataliwa na Askari hoja yake yakupewa nakala ya kuondolewa kwake na kutakiwa kumuona Mkuu wa kituo cha Polisi kati au Kumuona msajili wa Mahakama Kuu



Mahakama kupitia dalali wa Mahakama imepiga mnada Shule ya Msingi Besta iliyopo Sae jijini Mbeya kutokana na madai ya mdai katika kesi hiyo .
Mdai wa kesi hiyo namba 212 ya mwaka 2003 ni Kampuni ya Mohamed Enterprises ambapo alikuwa anamdai Hamis Othman kiasi cha Shilingi Milioni 270 ambazo alishindwa kulipa . 
Kesi hiyo namba 27 ilianza kusikilizwa mwaka 2003 huku Othman  akitetewaa na Wakili Mkumbe ambapo hukumu ilitolewa 4.6.2012  majengo ya shule yauzwe, mpaka sasa madai hayo  hayaja jurikana yalikuwa yanahusiana na nini.
Wamiliki wapya wa majengo  hayo ni Mbeya Heritage Company ambao walikabidhiwa majengo hayo na Dalali wa Mahakama Chini ya usimamizi wa mtendji kata ya Ilomba Erasto Mwakapoma  na Mwenyekiti waa Mtaa wa Sae Erias Mwakyusa huku  Jeshi la Polisi Likishuhudia makabidhiano hayoyakifanyika kwa amani.
Zoezi lilisitishwa kwenye Msikiti kutokana na Imani waumini wa Msikiti huo wataalifiwe ili ndani ya siku Mbili wawe wameondoka eneo hilo. 
Adha kubwa ilikuwa ni kwa wanafunzi wliokuwepo shuleni hapo ambapo mitihani yao ilioekana kuzagaa hovyo kutokana  na purukushani zilizo kuwepo bila taarifa yoyote na kutojua Hatma yao  ya masomo yao kutokana na Madarasa kuhodhiwa  na mmiliki mwengine Licha ya kuwepo kwa mabweni kando ya Shule hiyo na kufanya mizigo yote kulundikwa nje ya mabweni.
 
kwa msaada wa kamanga na matukio

MWILI WA MSANII ALBAERT MANGWEAR KUWASILI NCHINI LEO

Mwili wa Msanii Albert Mangwea kuwasili nchini LEO


Wadau wa Afrika Kusini wakiwa katika harakati za kuusafirisha mwili wa msanii wa kizazi kipya aliyefariki Dunia huko nchini Afrika ya Kusini hivi karibuni,marehemu  Albert  Mangwear jioni ya jana huko  Johannesburg, Afrika Kusini. Ratiba zinaonesha mwili huo utawasili leo jijini Dar es salaam. Muda na ratiba kamili zitafuata punde.

SHEIKH PONDA ASEMA MIHADHARA ITAENDELEA




https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEi-oaG-7OIWBe7KqDIg3zFFNsFduXXB2gn0neatQyoOeDahnCBmpd8h0b2MKyCvCQGNb9mAbrMQkMQaPFFcEp5PLg1hpPUdbQJn_RoBig_OYa63H2XDueNpZJyVFT7C467ClzI4iWG8ztXc/s640/DSC_0304.JPGKATIBU wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Ponda Issa Ponda, ameibuka na kutangaza kuendeleza mihadhara iliyokatazwa na kupigwa marufuku na serikali.

Mbali na kutangaza hayo pia amesema watapigania kurudishwa kwa mitihani ya dini ambayo serikali imefuta mitihani hiyo.
 
Hayo ameyasema juzi katika Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es salaam kwenye kongamano la kujadili mada mbalimbali yakiwemo ya mambo yawahusuyo Waislamu nchini

Wakati akitangaza hayo alimtaka Waziri wa Mambo ya Ndani azingatie kauli hiyo kwani ni muhimu waendeleze na kudai hiyo si haki na hiyo ni sawa na kukubali ujinga.

Hivyo alisema mihadhara hiyo itaendelea kama kawaida na atakayejitokeza kukataza mihadahara hiyo watakabiliana nae kwa nguvu zote,” alisema Ponda.

Pia sakata la kufutwa kwa mitihani ya masomo ya dini limeonekena kuwa utata katika kongamano hilo kwani imeonekana kitendo hicho ni kufanya wanafunzi kukosa moyo kujifunza masomo hayo
Hilo limekuja baada ya serikali kufuta mitihani ya masomo ya dini na kuhakikisha kujifunza pekee mashuleni
Hivyo waislamu hao wamesema watahakikisha mitihani hiyo itarudisha kama kawaida kwani wameona kitendo hicho ni kuua elimu ya dini kwa watoto wa kiislamu

Shekhe hivi sasa anatumikia kifungo cha nje alichohukumiwa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kufuatia kupatikana na makosa ya uchochezi

MWENYEKITI WA JUKWAA LA WAHARIRI TANZAANIA KUWASILI LEO




http://www.bongocelebrity.com/wp-content/uploads/2013/03/ABSALOMKIBANDAAVAMIWA6.jpg
MWENYEKITI wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Absalom Kibanda anatarajia kuwasili leo akitokea nchini Afrika Kusini alipokuwa akitibiwa tangu Machi 6, baada ya kushambuliwa na kuumizwa vibaya na watu wasiofahamika usiku wa Machi 5.

Katika taarifa iliyotumwa kwa vyombo vya habari na Katibu Mkuu wa TEF, Neville Meena, Kibanda atawasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere leo saa 7 mchana na atazungumza na waandishi wa habari.

Kutokana na ujio huo, Meena aliwaomba wahariri na waandishi kufika uwanjani hapo kuanzia majira ya saa 6.00 mchana kwa ajili ya kumpokea mwenzao huyo aliyekaa nje ya nchi kwa miezi mitatu.

“Mwenzetu kakaa Afrika Kusini kwa siku 90, hii ni fursa nyingine adhimu ya waandishi wa habari nchini kuonyesha mshikamano na umoja wetu kwa kwenda kumpokea,” alisema.

Kibanda ambaye pia ni Mhariri Mtendaji wa New Habari (2006) Ltd, kuumizwa kwake kuliitikisa tasnia ya habari nchini na kuzua mijadala mbalimbali ndani na nje ya nchi.

WAZIRI SIMBA ATIMULIWA BUNGENI KWA KUVAA VIBAYA





http://www.ippmedia.com/media/picture/large/sophia-simba-jan19-2013.jpg
WAZIRI wa Jamii, Jinsia na Watoto, Sophia Simba, jana alizuiwa na walinzi wa Bunge kuingia ukumbini kutokana na kuvalia mavazi yanayokiuka kanuni zinazoliendesha Bunge.

Simba ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taifa wa Umoja wa Wanawake wa Chama cha Mapinduzi (UWT), alifika bungeni hapo jana akiwa amevalia sketi na shati la mikono mirefu lenye rangi ya kijani na alama za CCM.

Vyombo vya Habari vilimshuhudia Waziri Simba alizuiliwa kuingia bungeni kutokana na vazi lake hilo lenye alama za chama.

Katika kuonesha kuwa Waziri Simba alivalia sare hiyo kwa makusudi, wakati akiingia alijifunika kwa mtandio ili shati hilo lisionekane, lakini walinzi walimshtukia kupitia upande wa mgongoni ambako mtandio huo haukufunika vizuri.

Alipotafutwa kuzungumzia tukio hilo, Waziri Simba alijibu kwa kifupi kwa njia ya ujumbe mfupi wa simu (sms) akisema; “achana na mimi”.

Hatua hiyo inakuja wiki chache tangu Naibu Spika wa Bunge, Job Ndugai kudai kuwa aliandikiwa ujumbe na baadhi ya wabunge wakihoji kama mavazi ya kombati yanayovaliwa na wabunge wa CHADEMA hayakiuki kanuni.

Ndugai katika kauli yake hiyo alisema ziko kombati za rangi mbili, nyeusi na kaki zinazovaliwa bungeni, kwamba na wengine wanataka kuja na kombati za rangi ya kijani.

Hata hivyo, Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA, Zitto Kabwe na Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uenezi wa chama hicho, John Mnyika walipinga kauli ya Ndugai wakidai anafanya porojo za kisiasa bungeni.

Walisema kuwa kombati ni mavazi yanayoruhusiwa na kanuni za Bunge na kufafanua kuwa kwa mujibu wa kanuni, vazi la wanaume linaloruhusiwa ni pamoja na suti za safari zinazovaliwa na CHADEMA.

Kwa mujibu wa kanuni ya 149 (3) (a) kwa wanawake na (b) kwa wanaume kuna aina za mavazi yanayopaswa kuvaliwa bungeni.

Kanuni hiyo inasomeka kuwa kutakuwa na vazi rasmi kwa wabunge (a) kwa wanawake;- (i) Vazi lolote la heshima yaani ambalo si la kubana mwili, lisiloonesha maungo ambayo kwa mila na desturi za Kitanzania hayapaswi kuoneshwa na ni refu kuvuka magoti, (ii) gauni la kitenge au blauzi inayovaliwa na kitenge au sketi ya rangi yoyote (iii) kilemba cha kadiri au mtandio (iv) suti ya kike; au (v) vazi linalovaliwa wakati wa eda.

b) Kwa wabunge wanaume;- (i) suti ya Kiafrika au safari ya mikono mirefu au mifupi yenye ukosi au shingo ya mviringo na yenye fulana au bila fulana ndani, ya rangi moja, isiyokuwa na nakshi, pamoja au bila baraghashia;

(ii) Vazi la kimwambao yaani kanzu rasmi na nadhifu, koti, baraghashia na makubazi au viatu; (iii) suti kamili ya kimagharibi ya rangi kadiri isiyomeremeta; (iv) koti aina ya blazer na tai, pamoja na suruali yoyote ya heshima; au (v) tarbushi na kilemba cha Singasinga, au kilemba chochote kinachovaliwa kwa mujibu wa masharti ya imani au mila.

Utoro bungeni
Katika kile kinachoweza kutafsiriwa wabunge kutotilia maanani umuhimu wa kuhudhuria vikao, mijadala mbalimbali ya hotuba za bajeti imekuwa ikiendelea huku idadi ndogo ikionekana ndani ya ukumbi.

Uchunguzi wa wiki kadhaa, umebaini kuwa wabunge wengi wanahudhuria kipindi cha maswali na majibu asubuhi na baada ya hapo wanatoka nje kuendelea na shughuli zao binafsi au vyama vyao.
CHANZO: TANZANIA DAIMA

Monday, 3 June 2013

BREAKING NEWZ, AJALI MBAYA YA MAGARI IMETOKEA ENEO LA NANENANE DARAJANI

BREAKING NUUZ, AJALI MBAYA YA MAGARI IMETOKEA ENEO LA NANE NANE DARAJANI UYOLE MBEYA MUDA HUU, YAJERUHI VIBAYA NA WATU WANNE WAHOFIWA KUFA HAAPO HAPO.SHUHUDIA


 GARI LA ABIRIA AINA YA HIACE IKIWA IMEGONGANA USO KWA USO NA GARI AINA YA LAND CRUISER
HIZI NI BAADHI YA MAITI ZILIZO OKOLEWA PUNDE BAADA YA AJALI KUTOKEA 
 
HIVI NDIVYO DALADALA HII ILIVYO HARIBIKA BAADA YA AJALI HIYO KUTOKEA 



DALADALA IKIWA IMEUMIA VIBAYA 



HILI NDILO ENEO AMBAPO AJALI HIYO IMETOKEA 






WANANCHI MBALIMBALI WAKIWA KATIKA ENEO LA TUKIO KUSHUHUDIA AJALI HIYO
 
 
 
KWA MSAADA WA MBEYA YETU

UHABA WA VIFAA VYA SABABISHA WAGONJWA WALALA CHINI MKOANI TANGA

  


HOSPITALI ya wilaya ya Lushoto, mkoani Tanga inakabiliwa na Uhaba wa majengo ya wodi ya Mama na Mtoto hali inambayo imesababisha wagonjwa kulala zaidi wawili katika kitanda kimoja.

Pia hospitali hiyo inakabiliwa na upungu mkubwa wa Mashuka na malanketi kwa ajili ya kujifunika wagonjwa hali inawalazimu  wagonjwa hao  kujifunika mashuka yakiwa hayajakauka kutokana na uchache wa mashuka yaliyopo.

Hayo yamebainishwa na, Ofisa tabibu  mkuu wa Hospitali hiyo (Medical officer incharge) Dk Gasto Stephano  wakati wa akipokea msaada wa mashuka yaliyotolewa na umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi (UVCCM) tawi la chuo kikuu cha kumbukumbu ya Sebastian Kolowa (SEKOMU), na kusema kuwa, hospitali hiyo inakabiliwa na uhaba wa wodi ya mama na mtoto kutokana na majengo yake kujengwa tangu mwaka 1961.

Dk. Stefano alisema kuwa majengo yaliyoko kwa sasa hayakidhi mahitaji ya wagonjwa kulingana na idadi ya wagonjwa walioko kwa sasa kuongezeka na kuzidi kiwango kilicho kasimiwa wakati wa ujenzi wa hospitali, hali inayowalazimu  wagonjwa kulala zaidi ya wawili katika kitanda kimoja.

Aidha Dk. Stefano alisema  Hospitali kwa sasa ina mpango mkakati wa kujenga jengo la gorofa mbili ambalo litagharimu kiasi cha bilioni moja hadi mbili ili kuweza kupunguza tatizo la mrundikano wa wagonjwa katika wodi hiyo.

Alisema kuwa jengo hilo litakuwa na sehemu ya upasuaji, sehemu ya mama na mtoto na watoto wanaozaliwa wachanga “njiti” (maternity complex).

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa UVCCM, Tawi la chuo cha kumbukumbu ya Sebastian Kolowa (SEKOMU), Mrisho Kitunga, alisema kama wasomi wameguswa na tatizo lililoko katika wodi ya mama na mtoto hospitalini hapo,  na kuweza kutoa mashuka kumi ya kujifunika pamoja na vitu mbalimbali, vyenye thamani ya shilingi laki tatu.

Naye katibu wa UWT tawi la SEKOMU, Zuhura Maulid,  alisema swala la huduma kwa jamii ni jukumu la kila mmoja wetu kuweza kuwasaidia watu wenye mahitaji na sio kuiachia serikali peke yake.

DK SHEIN AMARIZA ZIARA YAKE NCHINI CHINA

 
 

 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,na Mkewe Mama Mwanamwema Shein,wakiagana na Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Mambo ya Nje ya Serikali ya Jimbo la Xiamen Hong Chengzong,katika uwanja wa Ndege wa Mji huo Nchini china,akirejea Zanzibar baada ya kumalizika ziara yake nchini humo jana
 

MWILI WA MAREHUMU WA KAA MOCHWARI MIAKA 10 SASA

Kenya — Mwili wa mwanamke mmoja umesalia katika mochwari moja ya kibinafsi kaunti ya Machakos kwa miaka kumi kutokana na wanawe na ndugu zao wa kambo wakizozania ardhi ya baba yao huku bili ya kuhifadhi mwili huo katika ufuo huo inakaribia kugonga fedha za Kenya, shilingi milioni mbili.

Wasimamizi wa Machakos Funeral Home mjini Machakos, Jumapili walithibitisha kwamba mwili wa Esther Nzakwa Kitivo, uko katika chumba hicho tangu 2004.

Watoto wa kambo wa Nzakwa aliyekufa Agosti 31, 2004, walikataa mwili huo kuzikwa karibu na kaburi la mumewe katika kipande cha ardhi eneo la  Kitanga, Kalama, Machakos. Walienda mahakamani na kupata agizo la kumzuia mwana wa marehemu, Bw Michael Musau Kitivo, kumzika mama yake katika ardhi hiyo wakidai baba yao, marehemu Gideon Kitivo Ndambuki aliikabidhi kwa Maurice Ndambuki Kitivo, mwana wa mke mwenza wa marehemu Nzakwa.

Katika kesi aliyowasilisha mbele ya mahakama ya Machakos mwaka 2004, iliyopelekea kusimamishwa kwa 
mazishi ya Nzakwa hadi wakati huu, Ndambuki alidai mwili wa mama yake wa kambo haungezikwa kwenye ardhi hiyo kwa sababu ilikuwa yake aliyopata kutoka kwa baba yake kabla ya kuaga dunia.

Alimtaka Musau, amzike mama yake katika ardhi aliyogawiwa na baba yao, lakini Musau akasisitiza kwamba sharti mama yake azikwe kando ya kaburi la mumewe. Alisema kulingana na mila za jamii ya Wakamba, sharti mke wa kwanza azikwe kando ya mumewe.

Lakini mahakama ilikubaliana na Bw Ndambuki na kupuuza madai ya Musau na kusimamisha mazishi.

“Ukoo wa marehemu ulikuwa umeamua eneo la kumzika marehemu, na  mahakama haiwezi kutoa uamuzi mwingine,” akasema aliyekuwa Hakimu Mkazi wa Machakos T. O Okello kwenye uamuzi wake.

Lakini mzozo huo haukukomea hapo na Musau, anayedai anapasa kusimamia mali ya baba yake, akaamua kukata rufaa katika mahakama kuu.

Hata hivyo mahakama kuu iliidhinisha uamuzi wa hakimu kwamba ardhi aliyotaka kumzika mama yake ilikuwa ya nduguye wa kambo, Ndambuki.

“Nguvu nyingi zimeharibiwa kuhusu ufafanuzi wa mila za Wakamba na kwa maoni yangu hayo sio masuala halisi yanayohusu kesi hii,” akasema Jaji Sitati aliyesikiliza rufaa hiyo.

Akipuuza rufaa hiyo, jaji alisema Musau hangeweza kumzika mama yake kwa nguvu katika ardhi hiyo kwa sababu hakuna sheria za jamii ya Wakamba zinazosema mke azikwe kando ya mumewe.

Musau alisema baada ya uamuzi huo wa mahakama ya rufaa, aliwasilisha kesi akitaka mahakama iamue mrithi wa ardhi hiyo anayoshikilia kwamba ilikuwa ya babake na hakumpatia Bw Ndambuki.

Kesi hiyo inaendelea na itatajwa Julai 18 mwaka huu.


Kwa msaada  SwahiliHub

LINDI NA M MTWARA WAPITISHA MAZIMIO 8

Zaidi ya Wananchi 976 kutoka katika mikoa ya Lindi na Mtwara wameitaka serikali iwaombe radhi kwa madai kwamba, imepotosha hoja yao ya msingi kuhusu gesi na hivyo kuwachonganisha na Watanzania wenzao wa mikoa mingine nchini.

Wamesema hoja yao ya msingi iliyopotoshwa ni ya kutaka kuhakikishiwa gesi iliyogunduliwa mkoani Mtwara, inawanufaisha, na hawajawahi kudai isipelekwe katika mikoa mingine nchini.

Hiyo ni miongoni mwa maazimio manane yaliyopitishwa na wananchi wa mikoa hiyo katika kongamano lao lililofanyika katika viwanja vya ofisi za Chama cha Wananchi (CUF), jijini Dar es Salaam jana, ambao 
walichanga Shilingi 352,350/= kwa ajili ya mfuko maalum wa kuwasaidia watu waliokamatwa kufuatia vurugu zilizotokea mkoani Mtwara kuhusiana na gesi.

Kongamano hilo lililohutubiwa na Mwenyekiti wa CUF Taifa, Profesa Ibrahim Lipumba, liliandaliwa maalumu kwa ajili ya wananchi wa mikoa hiyo kujadili gesi.

Akisoma maazimio hayo kwa niaba ya wananchi, Abdulrahman Lugone, alisema wataendeleza makongamano mengine zaidi katika maeneo tofauti nchini ili kueneza taarifa nzuri kuhusu gesi zilizowasilishwa na Profesa Lipumba katika kongamano la jana. Aliyataja maazimio mengine kuwa ni pamoja na:
  • Wanamtaka Rais Jakaya Kikwete kumwajibisha Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, kutokana na nguvu kubwa iliyotumika kudhibiti vurugu za Mtwara na kusababisha vifo vya wananchi, akiwamo mjamzito asiyekuwa na hatia.
  • Kutekeleza matakwa yao, kuanzisha kamati ya watu wa mikoa ya kusini na kuanzisha pia mfuko wa kuchangia gharama za wakili atakayewateteta watu waliokamatwa kufuatia vurugu hizo.
  • Iwapo gesi ya Songosongo haiwanufaishi wananchi wa Wilaya ya Kilwa, mkoani Lindi, basi gesi ya Mtwara isitoke mpaka ‘kieleweke’.
  • Wananchi wa mikoa ya kusini wamebaini kuwa serikali haiwatakii mema na haiwataki, hivyo kwa pamoja watatumia fursa ya chaguzi zijazo kuinyima CCM nafasi za uongozi; kuanzia ngazi ya vitongoji, vijiji, mitaa, udiwani, ubunge hadi urais. 
  • Azimio lingine wamekubaliana kufanya maandamano makubwa ya kitaifa ili kufikisha ujumbe ulio sahihi.

Naibu Katibu Mkuu wa CUF Tanzania Bara, Julius Mtatiro, alisema maandamano hayo yatafanyika Juni 29, mwaka huu, na yataanzia eneo la Buguruni Sheli hadi Ikulu.

Profesa Lipumba, katika hotuba yake alisisitiza haja ya nchi kuwa na umoja wa kitaifa na kwamba chanzo cha mgogoro wa gesi ni serikali kushindwa kutekeleza ahadi zake kwa wananchi wa Mtwara na kusema watahakikisha maandamano hayo yanafuata taratibu zote za kisheria.

---
via NIPASHE
 

Sunday, 2 June 2013

POLISI SUMBAWANGA WAKAMATA MTENGENEZA SILAHA




 
POLISI mkoani Rukwa inamshikilia Samweli Sikazwe(40)kwa kukutwa akimiliki magobore sita kinyume cha sheria.

Mtuhumiwa huyo alikamatwa may 31 kwa operesheni kali ya kusaka wahalifu inayoendeshwa na polisi mkoa Rukwa .

Kaimu kamanda wa polisi Peter Ngusa alisema kuwa uchunguzi wa awali ulibaini kuwa mtuhumiwa alikuwa akijihusisha na utengenezaji wa silaha hizo alizokuwa akiwauzia watu ambao huzitumia kutenda uhalifu.

Katika  tukio lingine mwanamke Lucy kiwi (60)mkazi wa kirando katika wilaya ya nkasi mkoani Rukwa amekamatwa akiwa na pombe ya moshi lita 450 nyumbani kwake.

Mtuhumiwa alikamatwa mnamo may 28 saa 2.30 alikiwa anauza pombe hiyo haramu alimaarufu kama(gongo).

Aidha Operesheni hiyo pia imefanikiwa kumnasa Juma Andrew(25)mkazi wa jangwani kmanispaa ya sumbawanga akiwa na debe 2 za bhangi kavu akiwa katika harakati za kuiuza soko la mandela lililopo mjini hapa.

Watuhumiwa wote wanatarajiwa kufikishwa mahakamani mara tu uchunguzi wa awali utakapo kamilika.


Na Elizabeth Ntambala
  RUKWA

GADDAFI ALIFICHA MALI AFRIKA YA KUSINI PIYA

 
Wizara ya fedha ya Afrika Kusini inachunguza tuhuma kwamba mali ya thamani ya kama dola bilioni moja ya Libya ilifichwa nchini humo.
Rais Zuma na Gaddafi mwezi May mwaka 2011 walipokutana Tripoli, Libya

Wakuu wa Libya wamedai kuna dhahabu, almasi na fedha taslim ambazo kiongozi wa zamani wa Libya, Kanali Gaddafi na familia yake, waliziweka Afrika Kusini.
Serikali ya Libya imekuwa ikijaribu kuzipata mali za Kanali Gaddafi katika sehemu mbali-mbali za dunia tangu alipofariki mwaka 2011.
Mwandishi wa BBC mjini Johannesburg anasema watu wengine wamekisia kuwa mali ya hayati Gaddafi ilioko nchi za nje inaweza kufika dola bilioni 80.

MAELFU WAANDAMANA ADDDIS ABABA

 
Maelfu ya waandamanaji wameandamana katika barabara za mjini Addis Ababa, Ethiopia, wakidai waandishi wa habari na wanaharakati walioko kizuizini wafunguliwe.
Waziri Mkuu wa Ethiopia, Hailemariam Desalegn katika mkutano wa AU hivi karibuni
Waandishi wa habari wanasema ni nadra kuonesha upinzani wa namna hiyo kwa chama tawala ambacho kinadhibiti shughuli za jamii sawasawa.
Makundi ya kutetea haki za kibinaadamu yanasema serikali imetumia sheria za kupambana na ugaidi ili kuwafunga waandishi wa habari.
Waandamanaji- wengi kutoka upinzani - walipiga kelele kudai uhuru na haki.
Haya ni maandamano ya kwanza tangu mwaka wa 2005 ambapo mamia ya waandamanaji waliuliwa katika ghasia zilizofuatia uchaguzi.

Kwa msaada wa bbc

VIGOGO WALIOTIMULIWA BANDARI WAJAZA NAFASI ZILIZOTANGAZWA TPA

 
Nafasi za kazi zilizotangazwa na Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari kwa ajili ya viongozi wa juu wa Mamlaka hiyo, zimedaiwa kuibua vita kubwa ya ajira, imeelezwa.

Habari za uhakika ambazo gazeti la HabriLeo linazo zinasema wengi wa waliojitokeza kuomba  nafasi hizo katika mamlaka hiyo yenye nguvu kubwa kiuchumi ni pamoja na waliokuwa viongozi wa mashirika ya umma, binafsi, serikalini na hata waliopata kuongoza baadhi ya wakala za Serikali.

Lakini kutokana na ushindani kuonekana kuwa mzito, imeelezwa baadhi ya wajumbe wa Bodi ya PTA 
wamekuwa wakidaiwa kuhusika kuwatengenezea waombaji hao mazingira mazuri ya kupata ajira.

Kutokana na baadhi ya wajumbe wa Bodi kudaiwa kuwatafutia wagombea njia za mkato, Mwenyekiti wa Bodi hiyo, Profesa Joseph Msambichaka licha ya kushangazwa, alisema kama kuna wanaojaribu kutumia hila, wanajisumbua kwa kuwa mchakato wa mwisho utafanywa na kampuni binafsi, tena za nje ya nchi.

“Nami ndiyo nasikia, lakini pia inawezekana, maana kuna watu kila kukicha wanahaha kushika nafasi nzito nzito na bandari ni nzito…sasa kwa kulitambua hilo na ili kuzuia mianya ya kuchomekeana watu, sisi tunapitia maombi yao, kisha tutakabidhi kwa  kampuni huru kabisa, tena za kimataifa.

“Wajue Bodi haitahusika na hatua za mwisho za kumpata kiongozi wa TPA, wataalamu ndio watakaoangalia uwezo na sifa za kila anayeomba kazi katika Mamlaka. Narudia, kama wanajipitisha na kutumia hila kupitia Bodi, wanajisumbua,” alisisitiza Profesa Msambichaka.

Mbali ya Profesa, wajumbe wengine wa Bodi ya TPA ni Julius Mamiro, Jaffa Machano, Caroline Kavishe, Asha Nassoro, Dk Kuwe Bakari, Dk Hildabrand Shayo, Abdul Sauko na John Ulanga.

Kwa mujibu wa nyaraka kuhusu mchakato huo, mchakato wa kupitia majina na kutoa mapendekezo unaanza hivi karibuni kabla ya Bodi ya TPA kufanya uamuzi wa mwisho ifikapo mwisho wa mwezi huu.

Nafasi zilizotangazwa ni za Mkurugenzi Mkuu, Naibu Mkurugenzi Mkuu (Miundombinu), Naibu Mkurugenzi Mkuu (Huduma), Meneja wa Bandari ya Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Utawala, Mkurugenzi Huduma za Sheria, Meneja Uhusiano, Meneja Kitengo cha Mafuta, Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Huduma na Mkurugenzi wa Teknohama.

Kutangazwa kwa nafasi za kazi katika ngazi ndani ya TPA mwishoni mwa Aprili mwaka huu kunatokana na kuondolewa na kusimamishwa kazi kwa baadhi ya watendaji waandamizi wa Mamlaka hiyo.
Hivi karibuni, Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe alitangaza kutimua kazi wakurugenzi watatu na mameneja wawili wa TPA.

Wakurugenzi hao walitimuliwa kazi kwa nyakati tofauti baada ya uchunguzi wa tuhuma zilizokuwa zikiwakabili kukamilika na watuhumiwa hao kuhojiwa.

Miongoni mwa tuhuma zilizosababisha vigogo hao kuondolewa ni matumizi mabaya ya madaraka na ubadhirifu wa mali ya umma na kuitia hasara Serikali.

Waliotimuliwa ni aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Ephraim Mgawe, Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Huduma, Hamadi Koshuma, Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Miundombinu, Julius Mfuko, Meneja wa Bandari ya Dar es Salaam, Cassian Ngamilo, Meneja Kituo cha Kupakulia Mafuta (KOJ), Tumaini Massaro.

Baada ya kuondolewa kwa viongozi hao na wengine kusimamishwa, Madeni Kipande aliteuliwa kukaimu nafasi ya Mkurugenzi Mkuu wa TPA.
 
Kwa msaada wa  Ziro99 blog
 

MECHI YA TANZANIA NA SUDANI WATOKA SARE

Na Boniface Wambura, Addis Ababa

TIMU ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, jioni hii imetoka sare ya bila kufungana na Sudan kwenye Uwanja wa Addis Ababa mjini hapa katika mchezo wa kirafiki ulio kwenye kalenda ya Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA).

Taifa Stars ambayo iko Addis Ababa tangu Jumatatu (Mei 27 mwaka huu) imeweka kambi katika hoteli ya Hilton kujiandaa na mchezo wa Kundi C dhidi ya Morocco Juni 8 mjini Marakech kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Kombe la Dunia mwakani nchini Brazil.

Stars, inayodhaminiwa na kampuni ya Bia Tanzania (TBL), kupitia bia ya Kilimanjaro Premium Lager, katika mchezo wa leo, iliwakosa wachezaji wake wawili nyota, Thomas Ulimwengu na Mbwana Samatta ambao walikuwa wanaichezea klabu yao, TP Mazembe ya DRC katika Kombe la Shirikisho Afrika.

Washambualiji wa Stars akina Khamis Mcha ‘Vialli’, Mrisho Ngasa na Amri Kiemba wakiongozwa na John Bocco walilitia msukosuko mara kwa mara lango la Sudan ambalo lilikuwa chini ya beki wa kati Nadir Eltayeb ambaye alifanya kazi ya ziada dakika ya 72 kuokoa mpira uliokuwa ukielekea wavuni.

Stars katika mechi hiyo iliwakilishwa na Juma Kaseja, Nadir Haroub/Vincent Barnabas, Shomari Kapombe, Kelvin Yondani, Aggrey Morris, Frank Domayo, Mrisho Ngasa, Salum Abubakar, John Bocco/Haroun Chanongo, Amri Kiemba/Khamis Mcha na Simon Msuva/Athuman Iddi ‘Chuji’.

Baada ya mechi hiyo, wachezaji wa Stars wamealikwa chakula cha usiku na Balozi wa Tanzania nchini Ethiopia, Joram Biswaro, ambapo watakutana pia na baadhi ya Watanzania wanaoishi Ethiopia kabla ya kuondoka kesho alfajiri kwenda Morocco kwa kupitia Cairo, Misri ambapo inatarajia kuwasili Casablanca saa 8 mchana.

Kocha Kim Poulsen amesema kikosi chake kinaendelea na mazoezi vizuri na kitaimarika zaidi baada ya Samatta na Ulimwengu kujiunga na wenzao kesho huu mjini Marrakech.
 


Na Boniface Wambura, Addis Ababa

UZINDUZI WA RASIMU YA KTIBA KUONYESHWA LIVE NA VYOMBO VYA HABARI NCHINI

 

Ili kuwafikia wananchi wengi, uzinduzi wa Rasimu ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania utakaofanyika kesho, Jumatatu, Juni 3, 2013, kuanzia saa 8:00 mchana katika viwanja vya Karimjee, jijini Dar es Salaam utarushwa moja kwa moja na vituo vya TBC1, TBC Taifa, ITV, Star TV, Channel Ten, ZBC TV na ZBC Redio. Wadau hawa wamekubali kufanya hivyo baada ya kuombwa.
Uzinduzi huo utarushwa moja kwa moja na vituo hivyo kuanzia saa 8:00 mchana.
Rasimu hiyo ya Katiba imetokana na maoni ya wananchi, viongozi na makundi mbalimbali waliyowasilisha kwa Tume kupitia njia mbalimbali zikiwemo mikutano, barua pepe, ujumbe mfupi wa simu za mikononi (sms) na nyinginezo.

MTOTO ATEKELEZWA NA MAMA YAKE BAA

 

KATIKA hali isiyokuwa ya kawaida mwanamke mmoja anayedaiwa kuwa mkazi wa wilayani Tarime, mkoani Mara, amemtelekeza mtoto wake kwenye baa mjini Bunda na kutokomea kusikojulikana.
Tukio hilo lililothibitishwa na jeshi la polisi, limetokea juzi jioni, katika baa moja iliyoko mjini Bunda, baada ya mwanamke huyo kufika katika eneo hilo na kumnunulia mtoto wake soda na andazi na kisha kuondoka akimwacha motto huyo.
Imeelezwa kuwa mwanamke huyo alimwacha mtoto wake huyo wa jinsi ya kike, ajulikanaye kwa jina la Lusia Mwita, anayekadiliwa kuwa na umri wa kati ya miaka mitano hadi sita, pamoja na mfuko wa wa nailoni uliokuwa na nguo za mtoto huyo.
Habari zaidi zinasema baada ya mtoto huyo kutelekezwa alianza kutangatanga, na ndipo akaokotwa kwenye uchochoro na mwanamke mmoja, ajulikanaye kwa jina la Pendo Joseph, mkazi wa mtaa wa Kabarimu mjini Bunda, ambaye alimpeleka kwenye kituo cha polisi.
Polisi wamesema kuwa baada ya mwanamke huyo kutoa maelezo yake, aliruhusiwa kuondoka na mtoto huyo, ambapo sasa anaishi naye akisubiri wazazi wake waweze kumchukuwa.
Akizungumza kwa taabu mtoto huyo amesema kuwa walipanda ndani ya basi kutoka Tarime, ambapo mama yake alimwambia kwamba wanakwenda kwa babu yake mjini Bunda, na baada ya kufika kwenye eneo hilo mama yake alimwacha na kwenda kusikojulikana.


Na Ahmed Makongo, Bunda