Thursday 2 October 2014

MALINZI ASEMA LAZIMA KLABU ZIKATWE ASILIMIA TANO YA FEDHA ZAO,

Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi amesema ni lazima klabu zikatwe fedha zao za udhamini.

TFF iliagiza klabu zote 14 za Ligi Kuu Bara, zikatwe fedha zao za udhamini kutoka Vodacom na Azam TV.
Agizo hilo, liliamsha hisia za klabu ambazo zilisisitiza kwamba haziwezi kukubali hali.
Hali iliyosababisha Mbeya City na Mtibwa Sugar, kutishia kwenda mahakamani.
Akizungumza leo, Malinzi alisema lazima fedha hizo zikatwe kwa ajili ya mfuko wa maendeleo ya soka.
"Hilo suala la kukatwa fedha limeishapita, ni agizo na lazima litekelezwe," alisema Malinzi.
Klabu pia zimekuwa zikikatwa fedha zao za mapato na fedha kwenda kwenye mfuko wa maendeleo.

0 comments: