Sunday 5 October 2014

(FULL TIME): YANGA YAITANDIKA JKT RUVU MABAO 2-1

Dk 90+2
GOOOOOOOO Dk 90, Jabir Aziz anapiga bao kwa shuti kali kutoka umbali wa mita 28.

Dk 90 Msuva anapokea pasi nzuri, lakini anabutua juu ya lango la JKT.

Dk 89, Mgisa anampa pasi nzuri Naftali, lakini anapiga shuti kalii juuuu
Dk 88, Ngassa anaingiza pasi safi kwa Jaja ambaye anajaribu kumpigia Nizar, lakini mabeki JKT wanaokoa

Dk 85, Ngassa anapiga shuti kali baada ya kuiwahi pasi nzuri ya Kelvin Yondani, lakini Chove anaukoa kwa ustadi mkubwa.


Dk 84, Yanga wanamtoa Msuva na nafasi yake inachukuliwa na Nizar Khalfan.


Dk 82, Msuva anapiga krosi safi lakini mabeki wanaokoa na kuwa kona isiyo na madhara.

Dk 77&80 JKT wanashambulia zaidi kwa kupiga krosi tatu mfululizo lakini zinakosa wamaliziaji. Yanga wanaonekana kurudi nyuma na kugongeana mipira mipingi 'kishikaji'.


Dk 76, JKT wanamuingiza Najib Magulu kuchukua Mbaga.

GOOOOOOOOOO Dk 73, Niyonzima anapiga mpira wa adhabu unakwenda moja kwa moja wavuni huku Chove akiwa anaukodolea macho.


Dk 68&69, mechi imechafuka na timu zinacheza kibabe zaidi huku mwamuzi akionekana ameachia kazi iendelee..

Dk 63&67, timu zinaonekana kucheza katikati zaidi, lakini angalau JKT wanafika kumtumia Mgisa.

Dk 61, Mgisa tena anaingia kwenye eneo la hatari lakini Cannavaro anajitahidi kuutoa na Msuva anapiga kichwa unakuwa wa kurushwa.


Dk 60, Yanga wanamtoa Coutinho na kumuingiza Mrisho Ngassa.
Dk 52, Amos Mgisa anajaribu kuuchop mpira, lakini unatoka nje kidogo ya lango la Yanga.


Dk 50, Mbaga anapata pasi nzuri ya Jabir Aziz, lakini anapiga shuti buuuu
Dk 46, Chove analazimika kuokoa mpira wa kurusha wa Mbuyu Twitte.


MAPUMZIKO:
Dk 44 Msuva tena anapiga shuti lakini linapita juu ya lango.


Dk 41, Jaja anapiga shuti kali baada ya kumtoka beki mmoja wa JKT, lakini Chove analidaka kwa ulaiiini na kuanza kutia mbwembwe.


  Dk 36, Yondani anaifungia Yanga bao safi baada ya kupiga bonge la shuti baada ya kupokea pasi nzuri ya Niyonzima aliyekuwa ameiwahi pasi nzuri ya Jaja.

Dk 29, Edward Charles anapiga krosi safi, Chove anafanya kazi nzuri tena na kuupangua.


Dk 25, Coutinho anapiga shuti kali lakini Chove analipangua katikati ya wachezaji wa Yanga.
Dk 16, Mbaga anapiga shuti zuri la chinichini, lakini mpira unatoka nje kidogo.


Dk 14, Chope anadaka vizuri mpira wa Msuva aliyekuwa eneo la hatari.
Dk 6, Chope anafanya kazi ya ziada kuokoa wakati MSuva akipanda kwa kazi.
DK 2, Countinho anaingia lakini shuti lake lina
kuwa nyanya.

0 comments: