Thursday 2 October 2014

HICHI NDIYO KIKOSI BORA CHA MWEZI KATIKA VILABU VYA HISPANIA (LA LIGA)

 

Kikosi bora cha mwezi Septemba katika timu zinazoshiriki Ligi ya Hispania maarufu kama La Liga, kimetangazwa.

Timu zilizotoa wachezaji katika kikosi hicho ni pamoja na Barcelona, Real Madrid, Atletico Madrid, Valencia na Celta Vigo.
Kipa Claudio Bravo amepata kura 37.5% na kuwapiku Iker Casillas na wengine.
Mabeki ni hivi; Juanfran (10.7%), Miranda (20.3%), Nicolás Otamendi (11.6%) na José Gayá (13.3%).
Viungo ni Ivan Rakitic (20.7%) na Luka Modric (14.5%) wakisaidiana na Arda Turan (11.4%) na Fabián Orellana (9.6%).
Wakati safu ya ushambuliaji inaongozwa na wababe wawili duniani Leo Messi (19.2%) na Cristiano Ronaldo (33.1%).

0 comments: