Kocha Mkuu wa Young Africans Marcio Maximo (kushoto) akiongea na waandishi wa habari juu ya mchezo wa kirafiki dhidi ya Big Bullets kutoka Malawi siku ya jumapili, kulia ni Afisa Habari wa timu hiyo Bw Baraka Kizuguto
Timu ya Young Africans itashuka dimba la Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam siku ya jumapili kucheza mchezo wake wa mwisho wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya timu ya Big Bullets FC (zamani Bata Bullets) inayoshiriki Ligi Kuu ya TNM nchini Malawi.Young Africans ambayo imeshacheza michezo minne mpaka sasa ya kirafiki ukiwemo mmoja wa kimataifa katikati ya wiki hii dhidi ya timu ya Thika United kutoka nchini Kenya imeshinda michezo yote.Akiongea na waandishi wa habari leo katika mkutano na waandishi wa habari, kocha mkuu wa Young Africans mbrazil Marcio Maximo amesema mchezo huo wa siku ya jumapili utakua ni kipimo kizuri kwa vijana wake kabla ya kuanza kwa Ligi Kuu ya Vodacom wiki mbili zijazo.
0 comments:
Post a Comment