Monday, 1 September 2014

HOT NEWS KYELA YAANZA KUKAMATA WANAFUNZI WATORO‏

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kyela, Gabriel Kipija, akizungumza na Mbeya yetu kuhusu mikakati ya kuongeza ufaulu kwa Wilaya hiyo.

 Wanafunzi wakiwa Darasani 
 Mmoja wa wanafunzi Livingstone Msusi akielezea jambo kuhusiana na mkakati huo
 Mmoja wa wanafunzi Salome Mwaiposa akielezea jambo kuhusiana na mkakati wa ufauru ulioanzishwa na Wilaya ya Kyela
 Wanafunzi wakiwa Darasani

 Hawa ni Baadhi ya wanafunzi watoro wakiwa wamekamatwa hapa wakipandishwa katika Gari
Huyu ni moja ya wanafunzi watoro, hapa alikuwa amekamatwa amevaa nguo Tano ndani kukwepa viboko, na katika picha hii anaonekana ameshikiria nguo tatu ambazo anazionesha baada ya kuzivua huku zengine akiwa bado amevaa

 Wanafunzi hao wakiwa tayari katika Gari hilo

 Wanafunzi wakisikiliza Mkutano

Wanafunzi wakiwa katika Kituo cha Polisi Kyela
KATIKA kuhakikisha elimu inapewa kipaumbele na kuongeza ufaulu kwa Wanafunzi Wilaya ya Kyela mkoani Mbeya,Halmashauri hiyo imeanzisha mkakati maalumu wa kuwakamata watoto watoro.
Hayo yalibainishwa juzi na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kyela, Gabriel Kipija, alipokuwa akizungumza na Mbeya yetu kuhusu mikakati ya kuongeza ufaulu kwa Wilaya hiyo.
Kipija alisema hali ya utoro kwa wanafunzi ilikithiri sana kwa kutohudhuria masomo na kuzurura ovyo mitaani jambo lililopelekea Halmashauri hiyo kushika nafasi ya mwisho kimkoa katika matokeo ya hivi karibuni ya kidato cha Nne.
Alisema katika Operesheni iliyofanyika wiki mbili zilizopita ikiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Kyela, Magreth  Malenga, yeye mwenyewe na Mkurugenzi wa Halmashauri walifanikiwa kuwakamata wanafunzi 500 wa shule za Sekondari ndani ya siku moja.
Alisema katika siku hiyo Wanafunzi wa shule mbali mbali za Sekondari Kyela Mjini walikamatwa kwa uzururaji wengi wao wakiwa kwenye sare za shule lakini hawakuhudhuria masomo na kuwafikisha kituo cha polisi kwa kosa la utovu wa nidhamu.
Alisema kitendo cha kuwafikisha polisi wanafunzi hao kimeibua mwamko mkubwa wa wanafunzi kuhudhuria masomo darasani pamoja na kuwahi ambapo hivi sasa hakuna mwanafunzi anayeonekana barabarani kuanzia saa moja asubuhi tofauti na awali.
Baadhi ya Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Keifo iliyopo Wilayani Kyela ambao walikumbwa na mkasa huo, mbali na kukiri kufanya vitendo hivyo tofauti na matarajio ya wazazi pia walipongeza kitendo cha Halmashauri cha kuwakamata na kuwapeleka Polisi.
Livingstone Msusi(15) mwanafunzi wa kidato cha Kwanza Keifo Sekondari alisema yeye binafsi alikumbwa na kamata kamata hiyo lakini hivi sasa amejirekebisha na kuwa wa kwanza kuwahi shule tofauti na awali ambapo alikuwa hafiki kabisa.
Salome Mwaiposa(14) alisema tangu operesheni hiyo ifanyike amekuwa na maendeleo mazuri darasani kutokana na kuhudhuria vipindi vyote na kwa wakati unaostahili.
Aidha baadhi ya wanafunzi waliwatupia lawama wazazi kwa kutofuatilia maendeleo ya watoto wao mashuleni ikiwa ni pamoja na kuwahimiza kwenda shule jambo lililochangia kuongezeka kwa utoro na kujiingiza katika shughuli hatarishi mitaani.

Walisema ili kukomesha kabisa utoro wa wanafunzi mashuleni ni bora wazazi wakatoa ushirikiaono kwa Serikali kwa kutoa taarifa endapo wanakuwa na watoto ambao husumbua kusoma na kuwaletea kesi wazazi kutokana na kujiingiza katika magenge ya uhalifu.

Na Mbeya Yetu

0 comments: