KUFUATIA AJALI MBAYA ILIYOTOKEA
THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
Telephone: 255-22-2114512, 2116898
E-mail: ikulucommpress@googlemail.com
Website : www.ikulu.go.tz
Fax: 255-22-2113425 |
PRESIDENT’S OFFICE,
STATE HOUSE,
1 BARACK OBAMA ROAD,
11400 DAR ES SALAAM.
Tanzania.
|
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amemtumia Salamu za Rambirambi
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Mheshimiwa Abbas Kandoro kuomboleza vifo vya watu
10 vilivyotokea Mbalizi, Mkoani Mbeya tarehe 29 Agosti, 2014 baada ya
basi dogo la abiria aina ya Toyota Hiace maarufu kama Daladala Na. T 237
BFB kugongana na lori aina ya Tata Na. T 158 CSV. Katika ajali hiyo,
watu saba wengine walijeruhiwa na kukimbizwa hospitali kwa matibabu.
“Nimesikitishwa
na kuhuzunishwa mno na taarifa za vifo vya watu 10 na wengine saba
kujeruhiwa katika ajali hii iliyotokea siku chache baada ya ajali
nyingine kutokea Mkoani Tabora iliyoua watu 19 na wengine 81
kujeruhiwa”, amesema Rais katika salamu zake.
Rais
Kikwete amesema mfululizo wa ajali hizi unaonyesha dhahiri kuendelea
kuwepo kwa tatizo la ukosefu wa umakini miongoni mwa madereva, hivyo
jitihada zaidi zinatakiwa kufanywa kusimamia kikamilifu Sheria ya
Usalama Barabarani na kufuatiliwa kwa karibu kwa mienendo ya
wanaoendesha vyombo vya moto, ili ajali hizi ziweze kupunguzwa na hata
kudhibitiwa kabisa katika barabara zetu.
“Naomba upokee salamu zangu za rambirambi kutoka
dhati ya moyo wangu kutokana na ajali hiyo, na kupitia kwako naomba
unifikishie salamu zangu za pole kwa wafiwa wote kwa kupotelewa ghafla
na wapendwa wao”Ameongeza.
Rais
Kikwete amesema anatambua machungu waliyo nayo wanafamilia, ndugu na
jamaa wa watu waliopoteza maisha yao kwenye ajali hiyo, lakini anawaomba
wote wawe wavumilivu na wenye subira wakati huu wanapoomboleza vifo vya
ndugu na jamaa zao.
“Ninawaombea
kwa Mola majeruhi wote wa ajali hiyo waweze kupona haraka na kurejea
katika hali zao za kawaida ili waweze kuungana tena na familia, ndugu
na jamaa zao”, amemalizia kusema Rais Kikwete katika salamu zake.
Imetolewa na;
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu – Dar es Salaam.
31 Agosti,2014
0 comments:
Post a Comment