MATUKIO KATIKA PICHA YALIYO WEZA KUVUTIA DUNIANI KOTE

Asante kwa kututembelea mbeyagreennews kwa taarifa zaidi endelelea kututembela kila siku ,saa,dakika usipitwe na matukio kem kemu

MATUKIO KATIKA PICHA YALIYO WEZA KUVUTIA DUNIANI KOTE

Asante kwa kututembelea mbeyagreennews kwa taarifa zaidi endelelea kututembela kila siku ,saa,dakika usipitwe na matukio kem kemu

MATUKIO KATIKA PICHA YALIYO WEZA KUVUTIA DUNIANI KOTE

Asante kwa kututembelea mbeyagreennews kwa taarifa zaidi endelelea kututembela kila siku ,saa,dakika usipitwe na matukio kem kemu

MATUKIO KATIKA PICHA YALIYO WEZA KUVUTIA DUNIANI KOTE

Asante kwa kututembelea mbeyagreennews kwa taarifa zaidi endelelea kututembela kila siku ,saa,dakika usipitwe na matukio kem kemu

MATUKIO KATIKA PICHA YALIYO WEZA KUVUTIA DUNIANI KOTE

Asante kwa kututembelea mbeyagreennews kwa taarifa zaidi endelelea kututembela kila siku ,saa,dakika usipitwe na matukio kem kemu

Tuesday, 28 May 2013

HII NDIO TANZANIA RISASI 227 ZA KAMATWA MKOANI MWANZA


https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjOAwy5Z_c346dmgfaEVt1k3_bFM5Q_c3CNtuhrh0X2Bq6XEuprP-djcbLfOrUXSDVozS8hpJC7kHlPjTPDDNUltxKmqFesTD2Tzd0z-Dx3KnE9tIhAVN_xmVdVUGfBLQWbztla9vGUN9A/s1600/E.J.+MANGU.jpgPOLISI mkoani Mwanza inashikilia risasi 277 zilizookotwa vichakani na raia wema katika eneo la Lumala, wilayani Ilemela mkoani hapa.

Akizungumza na waandishi wa habari, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Ernest Mangu alisema juzi walipokea taarifa kutoka eneo hilo kuwa zimeokotwa risasi 277 za silaha ya kivita aina ya SMG.

Kwa mujibu wa Kamanda, risasi hizo zilitupwa katika eneo hilo na zilikutwa kwenye galoni ya lita tano baada ya kuokotwa na raia wema.

Inasadikiwa zilitupwa na wahalifu ambao jeshi hilo bado linaendelea kuwasaka katika
operesheni yake inayoendelea kwenye wilaya za Sengerema, Kwimba na Magu.

Kamanda Mangu amezihusisha risasi hizo na majambazi mawili waliouawa wiki iliyopita wakati wakirushiana risasi na polisi walipotaka kufanya uporaji katika duka la wakala wa Kampuni ya Bia (TBL) katika eneo la Igoma.

“Itakumbukwa kuwa Mei 18, Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na wananchi waliwaua majambazi wawili waliojaribu kufanya uporaji eneo la Igoma ambao walikuwa na silaha aina ya SMG,” alisema Kamanda Mangu.

Alisema baadaye ilifahamika kuwa majambazi hao walikuwa ni wahalifu sugu ambapo waliwahi kukamatwa wakiwa na risasi 597 za SMG kisha kufungwa jela. 
 
 
CHANZO: HABARILEO

Monday, 27 May 2013

WANAO TETEA HAKI NCHINI WATAJWA NA SITTA

Sitta awataja marafiki wanaotetea nchi kwa haki

 
 
Na Sheilla Sezzy, Mwananchi 

Mwanza. Katika kile kinachoonekana ni mbio za urais 2015, makada wanne wa  Chama Cha Mapinduzi (CCM) wameunganisha nguvu tayari kwa kinyang’anyiro hicho.
Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta ni kama ametangaza timu yake ingawa si rasmi pale alipoweka hadharani majina ya makada hao akisema kuwa ni marafiki zake wa karibu ambao wana mikono misafi.
Sitta ambaye anatajwa kuwa  mmoja wa makada watakaowania urais 2015, aliwataja marafiki zake hao juzi wakati wa harambee ya kuchangia ujenzi wa Kanisa Katoliki la Josephen Bakita, Parokia ya Igoma Mwanza.
Waliotajwa kuwa ni marafaki wa Sitta ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Benard Membe, Waziri wa Ujenzi, Dk John Magufuli na Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe.
“Membe, Magufuli na Mwakyembe ni marafiki zangu wa karibu ambao wana mikono safi na wameniunga mkono siyo wengine walafi, waongo wanaotutumbukiza katika mikono ya Dowans na Richmond ambao siyo waadilifu na wazalendo;
“Tuwakatae maana ukiwapa madaraka wataweka vibaraka wao na nchi itaelekea pabaya na hiyo ndiyo inaweza kuzusha vurugu kwani ukimnyonya maskini na akiona unamnyonya atataka kufurukuta...Huo ndiyo mwanzo wa vurugu, nchi haiwezi kutulia kwa hiyo tuwakatae watu wa namna hiyo,” alisisitiza Sitta.
Hii ni mara ya kwanza kada huyo wa CCM ambaye amewahi kuliongoza Bunge la Jamhuri wa Muungano kuwataja hadharani marafiki zake hao ambao wamekuwa na ushawishi mkubwa katika duru za kisiasa nchini.
Katika harambee hiyo Sitta aliwasilisha zaidi ya Sh25 milioni ambazo alisema kati ya fedha hizo Sh5 milioni zilitoka kwa Waziri Membe, Sh5 milioni zingine zilichangiwa na Dk Mwakyembe na Dk Magufuli huku yeye (Sitta) akichangia Sh5 milioni  na pesa zilizobaki zilichangwa na wabunge wanaowaunga mkono.
Sitta alitaja viongozi wengine ambao wanashirikiana vizuri na wamemsadia katika harambee  hiyo kuwa ni Anna Kilango, Merry Nagu, William Geleja, Aden Rage, Catherin Majige, James Lembeli, Mark Mwandosya pamoja na Victor Mwambalaswa ambao wao wote walimchangia Sh500,000  kila mmoja huku Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Lazaro Nyalandu akitoa Sh1 milioni.
Awali Sitta aliwataka Watanzania kuthamini kura zao ili wasiangukie katika mikono ya viongozi mafisadi

 Na Sheilla Sezzy, Mwananchi 

KEZI YA UPORAJI WA MIL 239 ZA NMB KUTOLEWA JUNE 4

Hukumu kesi ya uporaji wa Sh239 mil za NMB sasa kutolewa Juni 4

 

 


Moshi. 
Usikilizwaji wa kesi ya wizi wa Sh239 mali ya Benki ya NMB, Tawi la Mwanga sasa umefikia ukingoni baada ya jopo la mahakimu watatu kupanga Juni 4 kuwa siku ya kutoa hukumu.
Kesi hiyo inawakabili raia wawili wa Kenya, Samwel Saitoti na Peter Kimani na Watanzania watano wanaotuhumiwa kuvamia benki hiyo Julai 2007 na kupora fedha hizo chini ya mtutu wa bunduki.
Katika uporaji huo, polisi mmoja wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) aliyekuwa lindo aliuawa.
Jopo hilo la Mahakimu waandamizi watatu, Pantrine Kente, Aziza Temu na John Nkwabi wamepanga tarehe hiyo baada ya mawakili wa pande zote mbili kukamilisha uwasilishaji wa majumuisho.
Tarehe ya kutolewa kwa hukumu hiyo inayovuta hisia za wananchi wengi ndani na nje ya Mji wa Moshi ilitangazwa wiki iliyopita na Hakimu Mkazi Mfawidhi, Simon Kobelo wakati akiahirisha kesi hiyo.


Na Daniel Mjema, Mwananchi gazeti

WALIOFELI KIDATO CHANNE SASA WAMEFAULI

Waliofeli kidato cha nne waula, ufaulu sasa waongezeka



Katibu Mtendaji wa NECTA, Dk. Joyce Ndalichako 

Dar es Salaam. Idadi ya watahiniwa waliofaulu mtihani wa kidato cha nne mwaka jana imeongezeka kwa kati ya asilimia 20 na 23 baada ya Baraza la Mitihani la Taifa (Necta), kufanya marekebisho alama za viwango vya ufaulu, Mwananchi limebaini.
Habari ambazo gazeti hili imezipata zinasema matokeo hayo ambayo yamewezesha kiwango cha ufaulu kupanda na kufikia asilimia kati ya 54 na 57, huenda yakatangazwa wiki hii pamoja na yale ya kidato cha sita ambayo pia yamechelewa kutangazwa.
Chanzo cha habari kutoka Necta kimesema matokeo hayo mapya yanaonyesha kuwa, ufaulu wa kuanzia daraja la kwanza hadi la nne umeongezeka kutoka asilimia 34.5 kwa matokeo yaliyotangazwa awali na huenda yakafikia asilimia 57. Hii inamaanisha kwamba watahiniwa wapatao 82,000 ambao awali walikuwa wamepata sifuri katika matokeo ya awali sasa wamepanda na kupata madaraja ya ufaulu katika matokeo mapya.
Kwa matokeo hayo, watahiniwa wa mwaka 2012 watakuwa wamefanya vizuri kuliko wa mwaka 2011, ambao watahiniwa 225,126 sawa na asilimia 53.37 ya 349,390 waliofanya mtihani huo walifaulu.
Msemaji wa Necta, John Nchimbi alisema upangaji wa matokeo hayo ulikuwa bado unaendelea. “Ninachojua kwa sasa ni kuwa mchakato unaendelea na matokeo yatatangazwa mapema tu ili watoto waweze kujiunga na shule mapema,” alisema Nchimbi.
Pia alisema usahihishaji wa mitihani ya kidato cha sita umekamilika.
Matokeo ya awali
Matokeo ya awali yaliyotangazwa na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk Shukuru Kawambwa yalionyesha kuwa kati ya watahiniwa 367,756 waliofanya mtihani wa kidato cha nne mwaka jana, waliokuwa wamefaulu kwa daraja la kwanza mpaka la tatu walikuwa 126,847 sawa na asilimia 6.4. Waliopata daraja la nne walikuwa ni 103,327 sawa na asilimia 28.1.
Katika matokeo hayo, watahiniwa 240,909 sawa na asilimia 65.5 walipata sifuri, hesabu ambayo imebadilika katika matokeo mapya ambayo yanaonyesha kuwa sasa waliopata daraja hilo ni 158,100 ambayo ni asilimia 43.
Hata hivyo, habari kutoka Necta zinasema kuwa licha ya kuwezesha kuongezeka kwa waliofaulu, matumizi ya kanuni mpya ya kukokotoa matokeo hayo yalisababisha zaidi ya wanafunzi 2,500 kushuka ufaulu ikilinganishwa na awali.
Maofisa mbalimbali wa Necta pamoja na wale wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi na taasisi zake, walikutana mwishoni mwa wiki iliyopita kukubaliana masuala mbalimbali juu ya matokeo hayo pamoja na suala la matokeo ya wanafunzi hao 2,500 kabla ya kutangazwa wiki hii.
“Baada ya wajumbe kujadili suala lile, busara ilibidi itumike kwa hiyo hakuna mwanafunzi ambaye alama yake itashuka, kwa kawaida isingewezekana mtoto ambaye matokeo yalitoka akiwa amefaulu leo umwambie ameshuka,” kilieleza chanzo chetu.

chanzo (gazeti la mwananchi jumatatu)

OMBA OMBA ALIYEIGIZA MLEMAVU WA MIGUU NA MIKONO APATA KICHAPO ATIMUA MBIO IRINGA

  ,OMBAOMBA ANAYETAPELI WATU KWA KUIGIZA HANA MKONO MMOJA NA MGUU ACHEZEA KICHAPO AONYESHA MIKONO YOTE NA MIGUU

Omba omba tapeli anayejifanya hana  mikono akikamatwa na  wananchi  baada ya  kukimbia
Hapa  akibanwa  kuonyesha  mikono yake  yote  miwili
Wananchi eneo la Miyomboni  wakiwa  wamembana omba omba  huyu tapeli kuonyesha  mikono yake  yote
'' Huwa  unasema wewe  ni  mlemavu  huna mkono mmoja   hii nini ....nyosha  juu  watu waone utapeli  wako"
Hapa  kipigo  kilipoanza  kwa  mzee  huyo tapeli  anayejifanya  hana  mkono  mmoja na mguu
Hapa  ni  kipigo  kikiendelea
Tapeli  huyo akitaka  kujinasua  kutoka  mikono ya  wananchi  wenye hasira  kali
Hapa  baada ya  kupata upenyo akivaa nguo  zake
Hapa  akiwa ameachiwa  na kuanza kutimua mbio
Baada ya  kuchezea kichapo  tapeli huyo  sasa anajaribu  kuficha aibu

OMBA OMBA ALIYEIGIZA MLEMAVU WA MIGUU NA MIKONO ATIMUA MBIO

Huyu ni omba omba anayeigiza kutokuwa na mkono mmoja na mguu akiwa ameka eneo la M.R akisubiri kuomba chochote kutoka kwa wapita njia leo
Hapa akisubiri msaada kutoka kwa wasamaria wema leo
Hapa akitimua mbio kukwepa kamera ya mtandao huu leo

  Mwisho  wa  utapeli ni aibu  kubwa      leo kwa  wakazi  wa Miyomboni mjini Iringa wamepata  kushuhudia  kituko cha mwaka  baada ya watu  waliochoka  kuvumilia vitendo vya  kitapeli  vinavyofanywa mzee  mmoha ambae amekuwa akiigiza ni mlemavu asiye na mguu mmoja na mkono mmoja.
Tapeli  huyo  mbali ya  kuumbuliwa kwa  kutakiwa  kuonyesha miguu  yake  yote  pamoja na mikono  yake  yote  bado amepata  kuchezea  kichapo  kiasi cha  kunusurika  kuuwawa na wananchi   wenye hasira  kali.
Tukio la mzee  huyo  kubainika kama ni tapeli kwa mara  ya kwanza  chanzo chetu kikuucha  habari  na kubaini kua anaigiza ndio ulipata  kufichua siri  hiyo ya omba omba  huyo kuwa si omba omba kutokana na kumnasa akijiweka mfano  wa mlemavu .
Kutokana na kufichuliwa kwa  siri  hiyo ya  kujiigiza  kuwa ni  omba omba mlemavu wananchi wamekuwa  wakimtimua kila kona anayokaa tapeli huyo na  kumtimua  mbio kabla ya leo wananchi hao kuamua  kumkimbiza  kutoka eneo la Hazina  Ndogo  hadi miyomboni na kuanza  kumpa  kichapo hadi alipoamua kuonyesha viungo  vyote kuwa  si mlemavu
Tapeli  huyo mbali ya  kujifanya ni mlemavu  wa  viungo  wakati mwingine huwa anajifanya  ni mtu asiyeongea (bubu) asiye na viungo kama  mikono na miguu ila wakati mwingine akijifanya ni hana mguu  mmoja na  kuwaomba  watu fedha za matibabu .

Hata hivyo baada ya mmoja kati ya wananchi kufika eneo hilo alionyesha kufichua mbinu hiyo chafu ya mzee huyo kujifanya ni mlemavu wakati asubuhi alikutana maeneo akiwa mzima wa afya njema na katika kumhoji zaidi ndipo kamera ya mtandao huu ilipoamua kufanya kazi yake ya kunasa kituko hicho na ndipo mzee huyo alipoanza kuongea kwa sauti vizuri tofauti na alivyokuwa akijifanya kuwa hawezi kuongea kabisa (bubu)

Wakati mabishano yakiendelea eneo hilo ghafla mzee huyo alisimama kwa miguu yake yote miwili pamoja na awali kujifanya ni mlemavu asiye na mguu mmoja ila baada ya watu kutaka apigwe picha ndipo mzee huyo alipoanza kutimua mbio huku ulemavu aliokuwa nao akiusahau hapo  kutokana na  kichapo alichokipata  na kuumizwa  vibaya usoni .
Hata  hivyo  inasemekana  mzee  huyo  amekuwa akiadhibuwa katika maeneo mbali  mbali kutokana na mbinu yake ya  kufuru anayoifanya  kuwa ni mlemavu  wakati si mlemavu na  kuwa ni heri kuomba kama mtu mwenye matatizo ya  kiuchumi kuliko  kuwaigiza  walemavu na  kuwa iwapo atarudia na  kukutwa akifanya  hivyo watamvunja kweli mkono ili kuwa mlemavu walisema  wananchi hao ambao hata hivyo mtandao huu uliwaomba kufanya  hivyo .
Aidha  anadaiwa chanzo cha  kichapo  cha  leo kwa mzee  huyo tapeli ni mmoja kati ya  mpenzi  wake ambae  alikuwa amemsusa na  kuhamia kwa mpenzi mwingine  kuueleza umma kuwa  huyo ni tapeli na yeye ni mpenzi  wake ambae anamtambua kuwa na miguu yote,mikono na si bubu kama anavyoigiza jambo lililopelekea  wananchi kufanya udadisi .
Kabla kufukuzwa na kuchezea  kichapo tapeli huyo alifukuzwa  eneo ambalo alikuwa amekaa barabara eneo la Santona na kutoka kuondoka haraka na mmoja kati ya  vijana  wanaofanya kazi ya kusafisha na kushona  viatu na kupuuza na ndipo mtiti ulipoanza.
Baadhi ya wananchi wameuomba uongozi wa Manispaa ya Iringa kuwabana omba omba hao ambao wamekuwa wakidanganya watu kuwa wao ni walemavu kumbe ni wazima na kutaka kuwepo kwa utaratibu maalum wa watu kuomba misaada. 
kwa msaada wa
 francisgodwin.blogspot.com

MWANAMKE MCHAWI ADONDOKA KANISANI DAR

MWANAMKE MCHAWI ADONDOKEA KANISANI AKIWA NA BIBLIA MKONONI, WAUMINI WAHAHA, YEYE MWENYEWE ANENA MAZITO 


clip_image001
Wakati Mtwara kukilipuka kwa vurugu za gesi na kusababisha maafa, jijini Dar kumeibuka taharuki ya aina yake baada ya mwanamke aliyetajwa kwa jina moja la Anna kudaiwa kuwa ni mchawi na kudondokea kanisani.
Tukio hilo lililochukua saa kadhaa lilitokea katika Kanisa la Yesu Kristo la Huduma ya Maombezi na Uponyaji linaloongozwa na Nabii Flora Peter lililopo Mbezi Beach Salasala, Dar hivi karibuni.
Taarifa kutoka kwa mashuhuda wa tukio hilo ambao ni waumini wa kanisa hilo inadai kuwa mwanamke huyo, mkazi wa Bunju, Dar alifika kanisani hapo saa 4:45 asubuhi huku akiwa amebeba Biblia na pochi lake akionekana kuwa sawa waumini wengine.
WAUMINI WABAKI VINYWA WAZI
Ilidaiwa kuwa muda mfupi baada ya maombi kuanza, katika hali isiyo ya kawaida, mwanamke huyo aliruka kupitia dirishani akapotea na kuacha waumini vinywa wazi.
Habari zilidai kuwa kuna baadhi ya watu walimuona kwenye paa ya nyumba ya watu waliojenga karibu na kanisa hilo, hali iliyozidi kusababisha mkusanyiko mkubwa wa watu wakiwemo askari wa Jeshi la Wananchi (JWTZ) waliokuwa wakimshangaa.
Wakati taharuki hiyo ikiendelea, mwanahabari wetu alitonywa kuwepo kwa tukio hilo ambapo aliwasha ‘tukutuku’ yake na kuwahi eneo la tukio.
NI SIMULIZI NDEFU
Akizungumzia tukio hilo, mmoja wa viongozi wa kanisa hilo aliyejitambulisha kwa jina la Octavian Mahembe alikuwa na haya ya kusema:
“Nakumbuka kulikuwa na waumini wengi kanisani, walikuja kwa ajili ya maombi, huyo mwanamke naye alikuja hapa kama waumini.
“Ilipofika saa 5:00: asubuhi watu wakawa wanasubiri maombi, baadaye nabii naye akawa amefika na kuanza kutoa maombi. Baada ya maombi kuanza, yule mwanamke alianza kuhangaika, akawa anahamahama, hatulii sehemu moja.
“Watu waliokuwa wanataka kuombewa waliambiwa wapite mbele.
“Yule mwanamke alikurupuka na kurukia ukuta wa futi sita na nusu, akadondoka nje.
“Nabii alisema afuatwe ili aombewe, alidai kwa kuwa si mtu mwema ni hatari na anaweza kuliangamiza kanisa na waumini kwa jumla kwani alikuwa na nguvu za giza.
“Alipochukuliwa akapelekwa kwa Nabii, akaombewa sala ya toba huku akikataa kwa kusema hana dhambi.
“Aliendelea kuombewa na baada ya maombi alitoka nje kupitia mlangoni. Akiwa nje alivua nguo na kubaki na ile ya ndani tu, akapanda juu ya paa la nyumba jirani na kanisa, akarukia nyumba nyingine juu kwa juu bila kushuka.
“Hakuishia hapo, akawa amerukia mti huku akionekana kama mtu wa ajabu kiasi kwamba hata watu wengine hawawezi kufanya yale aliyokuwa akiyafanya.
“Watu wengi walikusanyika wakiwemo polisi na wanajeshi. Baada ya kupotelea mitini, ghafla kilisikika kishindo kanisani baada kudondoka eneo hilo.
“Baadaye alipelekwa ofisi ya serikali ya mtaa kwa usalama wake kwani watu walitaka kuchukua sheria mikononi wakidai ni mchawi,” alimaliza kusimulia kiongozi huyo wa kanisa.
ATANGAZA ALIYOKUWA AKIFANYA
Hata hivyo, habari nyingine zilidai kwamba kabla ya mwanamke huyo kupelekwa serikali ya mtaa, wakati akiombewa alikuwa akitangaza mambo mengi aliyokuwa akiyafanya yasiyoeleweka kwa watu wasiojua mambo ya kilozi.
SERIKALI YA MTAA
Mwandishi wetu hakuishia hapo, alikwenda hadi ofisi za serikali za mtaa kutaka kujua kama mwanamke huyo alifikiswa hapo na sehemu alipo kwa sasa.
Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Salasala, Monica Timba alikiri kutokea kwa tukio hilo akidai kuwa siku hiyo hakuwepo ofisini lakini alipigiwa simu na mkazi wa eneo lake kujulishwa juu ya tukio hilo.
“Niliambiwa kuna vurugu kubwa katika mtaa wangu na kwamba kulikuwa na mchawi amedondoka kanisani,” alisema mwenyekiti huyo.
Kiongozi huyo aliendelea kusema kuwa  baada ya kupewa taarifa hiyo alimpigia simu mtendaji wake, Ramadhan Juma ili mwanamke huyo aokolewe na walifanya hivyo.
HADI KITUO CHA POLISI
Alisema kuwa baadaye mwanamke huyo alipelekwa kituo kidogo cha polisi kilichopo eneo hilo cha Mtongani.
Risasi Jumamosi lilibisha hodi kituoni hapo na kuzungumza na askari aliyekuwa zamu ambaye hakutaka jina lake liandikwe gazetini kwa kuwa siyo msemaji wa jeshi hilo ambaye alikiri kuripotiwa kwa tukio hilo kituoni hapo.
“Ni kweli huyo mwanamke alifikishwa hapa akidaiwa ni mchawi lakini baadaye tulimwachia kwa sababu sisi hatuamini mambo ya uchawi,” alisema.


Kwa msaada wa lindiyetu blog

BOMU LALIPUKA LA JERUHI WANAFUNZI MAKAMBAKO (NJOMBE)

BOMU LALIPUKA MAKAMBAKO MKOANI NJOMBE, WANAFUNZI SABA WAJERUHIWA

 

clip_image001

Baadhi ya Maeneo walimo jeruhiwa wanafunzi hao na Mmoja kupatwa na Mshtuko wa Mlipuko wa Mabaki ya Mabomu hayo kutokana na Tatizo lake la Moyo alilonalo na hivyo kupelekea wanafunzi Watano kulazwa Ilembula Hospitali.Mkuu wa Wilaya ya Njombe Bi.Sarah Dumba akiwajulia Hali wanafunzi hao katika Hospitali ya Lutherani ya Ilembula.Mwanafunzi Evance Joseph[16]kidato cha Kwanza ambaye alikuwa akifanya Majaribio ya Kuchoma Mabaki hayo ya Bomu huku Mengine akiyahifadhi kwenye Tranka lake la Nguo.Wanafunzi wakiwa wanaendelea kufanyiwa Vipimo vya Mionzi ya Jua kutambua ukubwa wa Tatizo  katika Hospitali ya Ilembula Wilayani Wanging'ombe Mkoani Njombe.DC Njombe na Msafara Wake wakiwatazama Wanafunzi waliojeruhiwa na Mabaki ya Mabomu hayo. Mwanafunzi aliyejeruhiwa Katika maeneo Mbalimbali ya Mwili wake ikiwemo Miguuni.Hapa Mkuu wa Wilaya na Msafara wake ukiongozwa Na JWTZ Makambako.Msafara ukiwasili katika Shule ya Sekondari NABOTI Iliyopo katika Halmashauri ya Mji wa Makambako.
Wanafunzi wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Njombe.Mkuu wa Wilaya ya Njombe Bi.Sarah Dumba akizungumza na Wanafunzi wa Shule ya Sekondari NABOTI Mara baada ya kutoka katika Hospitali ya Ilembula kuwajulia Hali wanafunzi Watano waliolazwa kwa Matibabu.Wanafunzi wa NABOTI Sekondari wakimsikiliza DC na Msafara wake.Wanafunzi Wanne wa shule ya sekondari NABOTI iliyopo katika Halmashauri ya Mji wa Makambako wamejeruhiwa na Mlipuko wa Mabaki ya Bomu huku mmoja akipata Mshtuko wa Moyo kutokana na Mlipuko huo Baada ya Wanafunzi Takribani saba wa Kidato cha Kwanza kwenda kuyaokota Mabaki hayo kwenye Mlima uliopo Jirani na maeneo ya Jeshi.

SOURCE       lindiyetu blog

MTOTO MCHANGA WA SIKU 4 AKAA NDANI YA SHIMO SIKU 6 AKIWA HAI

HUYU NDO MTOTO MCHANGA WA SIKU 4 ALIYEKAA NDANI YA SHIMO SIKU 6 AKIWA HAI


Ndugu yangu ukishangaa ya Mussa basi shangaa na ya Filauni, Methali hiii methibitika Songea baada ya Mtoto Bahati Upendo mwenye siku 3 toka azaliwe alipo wekwa na mama yake kwenye mfuko wa mbolea na kutumbukizwa kwenye shimo...
 
Ndani ya shimo hilo amekaa siku 6 bila kula wala kunywa hadi alipo okotwa na wasamalia wema...
Hivi sasa yuko Hospitali ya Mkoa wa Ruvuma akiwa Salama  Salimini .
Yeyote Mwenye nafasi ya kumsaidia mtoto huyu anaweza kwenda moja kwa moja Hospitali au wasiliana na namba zifuatayo,  mchango  utafuatwa 0755061588 au 0755 731 234.
Dawati la Police Wanawake Mkoa wa Ruvuma wakiwa na Wauguzi kuangalia usalama wa Mtoto huyo aliye Tupwa. Kutoka kulia ni Muguzi Rukia Twahili anaye fuata Devota Umbela na aliye mshika mtoto Mwenyekiti wa Mtandao wa Police Wanawake Fadhila Chacha na wa mwisho kushoto ni A nna Chaima 

Sunday, 26 May 2013

TAIFA STARS YAONDOKA JANA USIKU KWENDA ADDIS ABABA

  TAIFA STARS KWENDA ADDIS ABABA LEO



Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars)  imeondoka jana(Mei 26 mwaka huu) usiku kwenda Addis Ababa, Ethiopia ambapo itaweka kambi na kucheza mechi moja ya kirafiki kabla ya kwenda Morocco.
 https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhncC2QHp6r1zbw5KyEwX5MsjM5uoh-LXstYRwd_74y4iuq8O82l8wnTRhustwhVUWLz8zmPOsFZLgIcNCs48PVrtVu5DTTLV6IfMNXhl9s-IEpytf4gDvkOjLrKksJ2qn_C_qvzHM0zgdf/s640/IMG_6274.JPG
Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager imeondoka saa 5 usiku kwa ndege ya EgyptAir ikiwa na kikosi cha wachezaji 21 chini ya nahodha wake kipa Juma Kaseja.
Timu hiyo ikiwa Ethiopia, Juni 2 mwaka huu itacheza mechi ya kirafiki dhidi ya Sudan ambapo siku inayofuata itaondoka kwenda Marrakech, Morocco kwa kupitia Cairo, Misri. Mechi hiyo ya mchujo ya Kombe la Dunia dhidi ya wenyeji Morocco itachezwa Juni 8 mwaka huu jijini Marrakech.
Mbali ya nahodha Kaseja, wachezaji wengine wanaoondoka katika kikosi hicho ambacho kina wiki sasa tangu kingie kambini jijini Dar es Salaam ni Mwadini Ally na Ally Mustafa ambao wote ni makipa.
Wengine ni Shomari Kapombe, Kevin Yondani, Aggrey Morris, Haroub Nadir, Mwinyi Kazimoto, Frank Domayo, Mrisho Ngasa, Khamis Mchana, Amri Kiemba, Salum Abubakar, Simon Msuva, John Bocco, Vicent Barnabas, Mudathiri Yahya, Athuman Idd na Haruni Chanongo.
Wachezaji Mbwana Samata na Thomas Ulimwengu ambao wako na timu yao ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo watajiunga moja kwa moja na Stars jijini Marrakech, Juni 4 mwaka huu wakitokea Maputo, Msumbiji mara baada ya mechi yao ya Kombe la Shirikisho dhidi ya Liga Muculumana ya huko.
Katika msafara huo wa Ethiopia benchi la ufundi la Stars linaundwa na Kim Poulsen (Kocha Mkuu), Sylvester Marsh (Kocha Msaidizi),Juma Pondamali (Kocha wa makipa), Leopold Tasso (Meneja wa timu), Dk. Mwanandi Mwankemwa (Daktari), Frank Mhonda (Mtaalamu wa tibamaungo) na Alfred Chimela (Mtunza vifaa).
Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

SIASA YA TANZANIA (BONGO)PROFESA LIPUMBA AIBUA JIPYA NA ZITO

PROFESA LIPUMBA AIBUA JIPYA NA ZITO



http://www.ippmedia.com/media/picture/large/Lipumba(30)(2).jpgMWENYEKITI wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba, ameibua suala zito akikihusisha chama chake na “kumnusuru” Rais Jakaya Kikwete katika uchaguzi mkuu uliopita.

Tanzania Daima limefahamishwa kuwa Profesa Lipumba alitoboa siri hiyo katika Msikiti wa Idrissa, Kariakoo, jijini Dar es Salaam, alikokwenda kuswali swala ya Ijumaa, miezi kadhaa iliyopita.

Kwa mujibu wa video ya tukio hilo, ambayo gazeti hili lina nakala yake, Profesa Lipumba alikaribishwa kuzungumza na waumini hao mara baada ya utangulizi uliotolewa na Imamu wa msikiti huo, Sheikh Ali Basaleh, aliyemtaka awaeleze Waislamu hali ya kisiasa nchini kuelekea Uchaguzi Mkuu wa 2015.

Huku akisisitiza juu ya umuhimu wa mshikamano wa kiimani, Profesa Lipumba alianza kwa kuzungumzia matokeo ya uchaguzi mkuu wa 2010, na ushindani mkali wa kisiasa uliokuwapo.

Alisema hawaoni matunda ya jitihada walizofanya kumnusuru Rais Kikwete asishindwe, kwani hata chini ya uongozi wake, Waislamu wameendelea kutothaminiwa.

“Ninyi masheikh mnajua vizuri zaidi hali ya kisiasa ilivyokuwa, kwamba ilibidi zifanyike juhudi za makusudi ili kuokoa jahazi. Lakini pamoja na kuliokoa jahazi, hali halisi inaonyesha mpaka sasa hakuna matunda yoyote yaliyopatikana, na tupo katika mtihani mgumu zaidi,” alisema.

Katika hali ambayo inasemekana ushindi wa Rais Kikwete ulipatikana kwa mbinu, huku wengine wakiituhumu Tume ya Taifa ya Uchaguzi kuwa ilimnusuru mgombea wa CCM, kauli hii ya Profesa Lipumba inadokeza kwamba anajua mkakati zaidi wa kazi ya Tume ya Uchaguzi.

Katika hali isiyo ya kawaida, Profesa Lipumba anaonekana kuhamasisha Waislamu kujipanga akisema “wenzetu wameanza kujipanga” kuelekea 2015.
 
CHANZO: TANZANIA DAIMA JUMAPILI
 

PACHA WATANO WAFARIKI DUNIA RUVUMA

 PACHA WAFARIKI DUNIA


WATOTO pacha wote watano waliozaliwa juzi katika Hospitali ya Mkoa wa Ruvuma wamefariki dunia.
Pacha hao walizaliwa salama juzi kwa kufanyiwa upasuaji kutoka kwa mama yao Sophia Mgaya (28), mkazi wa Ruhuwiko mjini hapa.
Mganga Mkuu Mfawidhi wa Hospitali ya Mkoa wa Ruvuma, Dk. Benedict Ngaiza, alisema kuwa watoto hao wameishi kwa saa kumi tu na kufariki dunia kutokana na kuzaliwa na uzito mdogo wa chini ya kilo moja.
Dk. Ngaiza alibainisha kuwa watoto wote wanaozaliwa wakiwa na uzito mdogo, nafasi yao ya kuishi ni ndogo sana.
Hata hivyo, hali ya mama wa watoto hao inaendelea vizuri ingawa bado amelazwa katika hospitali ya mkoa akiendelea kupata matibabu.
Tukio la kuzaliwa kwa pacha hao ambalo halijawahi kutokea katika hospitali hiyo lilitokea juzi majira ya saa 4 asubuhi, huku mtoto wa kwanza akiwa na uzito wa gramu 730, wa pili 810, wa tatu 670, wa nne 820 na wa tano 430.
Watoto watatu walikuwa wa kiume, wawili wa kike na huu ulikuwa mzao wa pili kwa mwanamke huyo.
Katika mzao wa kwanza wa mama huyo ambaye ni mwalimu, alijifungua mtoto mmoja.

MLUGO APIGA MARUFUKU WANAFUNZI WANAO TUMIA SIMU MASHULENI

NAIBU Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Philipo Mulugo, amesema atafanya ziara katika shule zote za msingi na sekondari ili kuwabaini wanafunzi wanaotumia simu za mkononi shuleni.

Mulugo alitoa kauli hiyo mjini hapa juzi alipokuwa akizindua mpango mkakati wa elimu ya haki za binadamu na kuongeza ataanzia Mkoa wa Dodoma na atakaowabaini atawanyang’anya na kuzichoma moto.

Alisema suala la utandawazi limechangia kwa kiasi kikubwa wanafunzi kuharibika na kuwa na nidhamu mbovu, ikiwa ni pamoja na kuwadharau walimu na wazazi.

Mulugo alisema kitendo cha wanafunzi kwenda na simu shuleni kimesababisha mmomonyoko mkubwa wa maadili, ambapo pia kimechangiwa na baadhi ya wazazi kujifanya wanawapenda watoto wao: “Hivi sasa limekuwa ni jambo la kawaida kuwakuta wanafunzi wa ngazi zote wakiwa na simu shuleni. Mimi sikubaliani nalo, nimeamua nitafanya 

ziara shule moja baada ya nyingine nikimkagua mwanafunzi mmoja baada ya mwingine nikianzia na Mkoa wa Dodoma katika kipindi hiki cha Bunge. Ole wake mwanafunzi nitakayemkuta na simu nitamnyang’anya na kuichoma moto maana walimu wanawalea sana… halafu na mimi mniimbie ‘tunataka haki zetu’,” alisema Mulugo.

Naibu Waziri huyo alisema suala la wanafunzi kuwa na simu limesababisha kujiingiza katika vishawishi na kuanza vitendo vya ngono wakiwa na umri mdogo.

Aidha, alisema mpango huo uliozinduliwa unawawezesha wanafunzi kujua wajibu na kudai haki zao.

Mulugo aliwaasa wanafunzi wote wakiwemo wa vyuo vya elimu ya juu kuacha kudai haki ikiwemo mikopo kwa kufanya vurugu na maandamano na badala yake watumie vyombo vya sheria pale wanapoona haki imepindishwa.

---
Imeandikwa na Happiness Mtweve
 
Source TanzaniaDaima

AKAMATWA NA NYARA ZA SELIKALI KOBE 70 MKOANI DODOMA

 
Picture
Kamanda wa polisi Mkoa wa Dodoma, David Misime akiwaonyesha waandishi wa habari nyara za Serikali, kobe zaidi ya 70 waliokuwa wamefungwa kwenye mifuko na mtuhumiwa Moses Nyawaje (42), akiwa anawasafirisha kinyume cha sheria. (Picha: John Banda, Dodoma)

VIKONGWE WATATU WAUAWA KIKATILI KWA KUCHOMWA MOTO MARA

VIKONGWE WATATU WAUAWA KIKATILI KWA KUCHOMWA MOTO HUKO BUNDA

 
clip_image001
MAUAJI ya kikatili yametokea usiku wa kuamkia leo wilayani Bunda, mkoani Mara baada ya watu wenye hasira wa kijiji cha Kasaula kuwauwa kwa kuwachinja kama Kuku kisha kuwachoma moto vikongwe watatu kwa kuwatuhumu wanajihusisha na vitendo vya kishirikina.
Pia watu hao mbali na kuwaua kikatili vikongwe hao kwa tuhuma kwamba walimuua kijana mmoja aitwaye Sale Ligolo, walichoma moto na kuteketeza nyumba walizokuwa wakiishi wazee hao pamoja na kupora kuku waliokuwa wakiwafuga na kuwatafuna kumaliza hasira zao.
Kwa mujibu wa wa taarifa ya mwandishi Masau Bwire aliyepo Bunda kwa sasa, tukio hilo limetokea usiku wa kumakia leo baada ya watu hao wenye hasira kuwasaka ajuza hao baada ya kuwepo tuhuma kwamba walishirikiana kumuua kijana huyo hivi karibuni.Kijana huyo alikufa kwa kugongwa na gari, lakini dereva aliyemgonga alidai hakuona kama alimgonga mtu ila mbwa na pia inaelezwa  tangu azikwe kijana huyo alikuwa akirejea kwa mkewe na kumuita nyakati za usiku pamoja na kusumbua familia yao akitaka apewe chakula na ndipo wanafamilia hao walipoamua kwenda kwa mganga kuchunguza tukio hilo.
Wakiwa kwa mganga,wanafamilia hao walitajiwa majina ya wanakijiji watatu wa kijiji hicho ambao hata hivyo walitoroka kwenda vijiji vya jirani pamoja na familia zao kabla ya usiku wa leo kuvamiwa walipokuwepo na kuangushiwa adhabu hizo za kinyama.
Wa kwanza kushambuliwa na kuuwa ni bibi aitwaye Bi Mgala ambaye alikimbilia kijiji cha jiorani kwa rafiki yake aitwaye Bi Laya, ambapo walimkata miguu yote miwili na kumtenganisha kichwa na kiwiliwili kabla ya kumchoma moto ambapo hata hivyo kitu cha ajabu ni kwamba ziliungua nguo zake tu huku mwili ukiwa upo vile vile.
Baadaye walimgeukia Bi Laya aliyekuwa akitaka kuwatoroka na kumfanyia unyama kama rafikie kwa kosa la kumhifadhi Bi Mgala kwa kuamini huenda wanafanya shughuli za kishirikina pamoja na baadaye kurudi Kasaula na kumnasa Bi Chausiku na kumfanyia kama walivyowafanyia ajuza hao wengine kisha kuchoma nyumba tatu.
Bibi wa tatu wanayemtuhumu pia kwa ushirikina, ametimka kijijini hapo, lakini nyumba yake imeteketezwa pamoja na kuku waliokuwa wakiwafuga kuporwa na watu hao na kutumia moto waliouwasha katika nyumba hizo kuwachoma na kuwala kwa hasira.
Kamanda wa Polisi wa Bunda, Mika David Nyange amethibitisha juu ya tukio hilo la kusikitisha na kwamba wanedelea na upelelezi kwa nia ya kuwasaka waliohusika na kitendo hicho cha kujichukulia sheria mikononi.
 

BAYERN MUNICH MABINGWA ULAYA JANA 2013/2014

UCL-FAINALI: BAYERN MUNICH MABINGWA ULAYA!


Robben ajifuta machozi Wembley.
>>BAO LA DAKIKA YA 89 LA ROBBEN NI MUUAJI!!
BAO LA DAKIKA YA 89 la Arjen Robben limefuta gundu kwake na Bayern Munich katika Fainali za UCL, UEFA CHAMPIONZ LIGI, baada ya Bao hilo kuipa ushindi wa Bao 2-1 Bayern dhidi ya wenzao wa Germany Borussia Dortmund katika Mechi iliyochezwa Wembley Stadium Jijini London Jumamosi Usiku.
Bayern walipoteza Fainali mbili za UCL katika Miaka mitatu iliyopita, ikiwemo kutolewa kwa Mikwaju ya Penati na Chelsea Mwaka jana tena katika Uwanja wao wenyewe Allianz Arena, lakini safari hii waliibuka Washindi wa Kombe hili kwa mara ya 5.
Ni Real Madrid, mara 9, na AC Milan, mara 7, ndio wameshinda Kombe hili mara nyingi kupita Bayern Munich.
Kwa Kocha wao, Jupp Heynckes, huu ni ushindi mtamu kwa vile anastaafu na nafasi yake kuchukuliwa na aliekuwa Kocha wa Barcelona, Pep Guardiola kwa ajili ya Msimu ujao.

MAGOLI:
Bayern Munich 2
-Mandzukic Dakika ya 60
-Robben 89
>>BAO LA DAKIKA YA 89 LA ROBBEN NI MUUAJI!!

Borussia Dortmund 1
-Mandzukic Dakika ya 68 [Penati]

Mara baada ya Filimbi ya mwisho kulia, Arjen Robben alitokwa machozi kwani alikuwepo wakati Bayern Munich inapoteza Fainali mbili kwa Inter Milan, Mwaka 2010, na Chelsea, 2012, ambapo alikosa Penati katika Mikwaju ya Penati iliyoipa Chelsea Ubingwa, na vile vile akiwa na Chelsea katika Miaka ya 2005 na 2007 walitolewa kwenye Nusu Fainali ya Mashindano haya na mara zote hizo walikuwa ni Liverpool ndio waliowabwaga.
Mechi hii ilitangaza vyema Soka la Kushambulia la Germany.
VIKOSI:
BAYERN MUNICH: Neuer; Lahm, Boateng, Dante, Alaba; Martinez, Schweinsteiger; Robben, Muller, Ribery; Mandzukic.
Akiba: Starke, Van Buyten, Shaqiri, Luiz Gustavo, Tymoshchuk, Pizarro Gomez
BORUSSIA DORTMUND: Weidenfeller; Pisczcek, Subotic, Hummels, Schmelzer; Bender, Gundogan; Blaszczykowski, Reus, Grosskreutz; Lewandowski.
Akiba: Langerak, Kirch, Santana, Kehl, Leitner, Sahin, Schieber.
REFA: Nicola Rizzoli [Italy]
 
 Bayern Munich yatwaa Ubingwa wa Ulaya.

UCL-MABINGWA WALIOPITA:
MSIMU
BINGWA
1955–56 Real Madrid
1956–57 Real Madrid
1957–58 Real Madrid
1958–59 Real Madrid
1959–60 Real Madrid
1960–61 Benfica
1961–62 Benfica
1962–63 Milan
1963–64 Internazionale
1964–65 Internazionale
1965–66 Real Madrid
1966–67 Celtic
1967–68 Manchester United
1968–69 Milan
1969–70 Feyenoord
1970–71 Ajax
1971–72 Ajax
1972–73 Ajax
1973–74 Bayern Munich
1974–75 Bayern Munich
1975–76 Bayern Munich
1976–77 Liverpool
1977–78 Liverpool
1978–79 Nottingham Forest
1979–80 Nottingham Forest
1980–81 Liverpool
1981–82 Aston Villa
1982–83 Hamburg
1983–84 Liverpool
1984–85 Juventus
1985–86 Steaua BucureČ™ti
1986–87 Porto
1987–88 PSV Eindhoven
1988–89 Milan
1989–90 Milan
1990–91 Red Star Belgrade
1991–92 Barcelona
1992–93 Marseille
1993–94 Milan
1994–95 Ajax
1995–96 Juventus
1996–97 Borussia Dortmund
1997–98 Real Madrid
1998–99 Manchester United
1999–2000 Real Madrid
2000–01 Bayern Munich
2001–02 Real Madrid
2002–03 Milan
2003–04 Porto
2004–05 Liverpool
2005–06 Barcelona
2006–07 Milan
2007–08 Manchester United
2008–09 Barcelona
2009–10 Internazionale
2010–11 Barcelona
2011–12 Chelsea