Mwanamke
wa Mexicana, Leandra Becerra mwenye umri wa miaka 127 anaetajwa kuwa
mtu mwenye umri mkubwa zaidi duniani ameeleza siri ya kuishi miaka mingi
zaidi.
Kwa
mujibu wa mjukuu wake mwenye umri wa miaka 45, bibi huyo alimueleza
kuwa siri ya ‘yeye’ kuishi miaka mingi ni kula vizuri, kulala kwa muda
mrefu na kuishi bila kuolewa.
Bi Leandra ambaye alizaliwa August
31, 1887 alikuwa mpiganaji wakati wa mapinduzi ya Mexico mwaka 1910-1919
na alikuwa kiongozi wa kundi la ‘Adelitas’ ambalo lilikuwa linaundwa na
wanawake wanaoenda vitani na waume zao.
Bibi huyo ambaye ana wajukuu wengi huku mjukuu wake mkubwa akiwa na umri wa miaka 73, tayari ameshawazika watoto wake watano.
Mjukuu wake aliiambia gazeti la El Hozizonte la Mexico kuwa bibi huyo hivi sasa anatatizo la kubwa la kusikia.
Ameeleza kuwa bibi huyo mara nyingine hulala mfululizo kwa muda wa siku tatu huku akipewa chakula pale anaposhituka.
Lakini akiamka hupenda kula mlo
kamili kwa uhakika, kuimba, kutaniana na kusimulia hadithi mbalimbali
zinazohusu maisha na mapambano ya mapinduzi ya Mexico.
Tofauti na wazee wengi, bi Leandra yeye hana tatizo la sukari hivyo anakula vitu vya sukari na chocolate kadri awezavyo.
0 comments:
Post a Comment