Idara ya upelelezi ya nchini marekani FBI imetoa tamko kuwa inachunguza kwa ukaribu madai ya maelfu ya accounts za watu maarufu kutekwa,na kinachotafutwa hasa ni picha za utupu za watu hao maarufu ambazo zimekua zikianikwa mitandaoni bila ya muwekaji kujulikana.
Katika tamko la FBI liliripotiwa na NBC News, wameeleza kuwa walikuwa wanafahamu kuhusu vitendo vya wezi wa njia za mtandao kuhack mafaili ya watu maarufu waliyoyatunza kwenye simu zao kwa application za kutunza mafaili mtandaoni na kwamba wameanza kufanya uchunguzi.
"The FBI is aware of the allegations concerning computer intrusions and the unlawful release of material involving high profile individuals and is addressing the matter.” Inaeleza sehemu ya tamko hilo.
Sakata
hili limemkumba mshindi wa tuzo ya Oscar Jennifer Lawrence ambaye picha
zake za uchi ziliachiliwa mtandaoni pamoja na Kate Upton na Mary Elizabeth Winstead.
Nae msemaji wa Apple anaehusika na applications za kutunza mafaili online ameeleza kuwa kampuni hiyo imeanza pia kufanya upelelezi juu ya tukio hilo ili kubaini kama uvujaji wa picha hizo umesababishwa na iCloud .

0 comments:
Post a Comment