HII
NI SEHEMU ALIYOKUWA AKIFANYIA KAZI MAREHEMU BUTUNGO MBUGANI KATIKA
KITONGOJI CHA NTEGELE KIJIJI CHA IGULWA WILAYANI BUKOMBE MKOANI GEITA.
Kijana mmoja aliyefahamika kwa jina la Butungo Mbugani mkazi wa kitongoji cha Ntegele kijiji cha Igulwa kata hiyo
wilayani Bukombe mkoani Geita amechukua
jukumu la kujinyonga kwa kutumia kamba
ya katani baada kuugua kwa muda wa miaka 18 ugonjwa wa kifua kikuu (TB).
Kijana huyo ambaye alianza kuugua maradhi hayo akiwa na umri
wa miaka miwili alishindwa kupona na
badala yake alichukua uamuzi wa kujinyonga huku akiacha ujumbe ulioandikwa
kwenye karatasi kuwa “kwa heri baba
nimeamua kujinyonga sababu ya
kuugua muda mrefu nakwenda kuanza maisha mapya ahera”.
Kwa mujibu wa maelezo
ya baba wa marehemu Mbugani
Maleka alisema kuwa mwanaye alikuwa
akisumbuliwa na maradhi hayo tangu akiwa na
umri wa miaka miwili na kumfanya asisome ,ambapo alieleza kuwa kifo
hicho kimekuwa na mshtuko mkubwa kwani hawakufikiria kama angechukua uamuzi
huo.
Alisema katika uhai wake licha ya kuugua muda mrefu alikuwa
akitibiwa katika hospitali ya wilaya ya
Bukombe na vituo vya afya tofauti tofauti na
kupata unafuu ikiwa ilimfanya dawa
alizokuwa akipewa kuendeleza hata shughuli zake ili kuweza kujipatia kipato.
Ofisa mtendaji wa kijiji hicho Andrew Tungu baada ya kupata
taarifa majira ya saa 4 asubuhi kwa
kutokea kifo hicho alisema kuwa baadhi
ya wananchi wenye maradhi ya kusumbua muda mrefu wanatakiwa kumuona mtaalamu
mara kwa mara na sio kuchukua jukumu zito kama hilo huku akiwataka wazazi na
walezi kuzingatia chanjo maalumu kwa watoto na sio kupuuza.
Kamanda wa jeshi la polisi mkoani Geita Joseph Konyo alithibitisha kutokea kwa
tukio hilo katika kitongoji hicho ambapo alieleza kuwa fiko cha kijana huyo kinatakiwa kuchunguzwa kitaalamu
zaidi .
|
0 comments:
Post a Comment