MATUKIO KATIKA PICHA YALIYO WEZA KUVUTIA DUNIANI KOTE

Asante kwa kututembelea mbeyagreennews kwa taarifa zaidi endelelea kututembela kila siku ,saa,dakika usipitwe na matukio kem kemu

MATUKIO KATIKA PICHA YALIYO WEZA KUVUTIA DUNIANI KOTE

Asante kwa kututembelea mbeyagreennews kwa taarifa zaidi endelelea kututembela kila siku ,saa,dakika usipitwe na matukio kem kemu

MATUKIO KATIKA PICHA YALIYO WEZA KUVUTIA DUNIANI KOTE

Asante kwa kututembelea mbeyagreennews kwa taarifa zaidi endelelea kututembela kila siku ,saa,dakika usipitwe na matukio kem kemu

MATUKIO KATIKA PICHA YALIYO WEZA KUVUTIA DUNIANI KOTE

Asante kwa kututembelea mbeyagreennews kwa taarifa zaidi endelelea kututembela kila siku ,saa,dakika usipitwe na matukio kem kemu

MATUKIO KATIKA PICHA YALIYO WEZA KUVUTIA DUNIANI KOTE

Asante kwa kututembelea mbeyagreennews kwa taarifa zaidi endelelea kututembela kila siku ,saa,dakika usipitwe na matukio kem kemu

Tuesday, 30 September 2014

WAIBA JENEZA MSIKITINI NA KULIPELEKA KWA AFISA MTENDAJI WA KIJIJI



Jeshi la Polisi mkoani Ruvuma linawasaka watu wasiofahamika wanaotuhumiwa kuingia msikitini na kuiba jeneza, Wilaya ya Namtumbo, mkoani Ruvuma.

Baada ya kuiba jeneza hilo, watu hao wanadaiwa kwenda nyumbani kwa Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Kitanda, wilayani humo, Fidea Mbawala (30) na kuliweka mlangoni, likiwa limesheheni matofali.

Kamanda wa Polisi Mkoa huo, Mihayo Msikhela, alisema  tukio hilo lililotokea juzi, saa 12:00 asubuhi, katika kijiji hicho.

Alisema tukio hilo limesababisha kuwapo utata na kwamba uongozi wa msikiti umedai kuwa tukio hilo ni la aina yake, ambalo halijawahi kutokea.

Alisema tukio hilo liligundulika wakati waumini wa msikiti huo walipokwenda kuswali swala ya alfajiri na kushtuka baada ya kusikia kuwa jeneza hilo limekutwa kwenye mlango wa nyumba ya afisa mtendaji wa kijiji hicho.

Alisema kwa mujibu wa Katibu wa Msikiti huo, Khalifa Ngonyani, tukio hilo limezua mtafaruku mkubwa kwa waumini wa msikiti huo.

 Kamanda Msikhela alisema taarifa za awali zinaonyesha kuwa  tukio hilo limefanyika baada ya afisa huyo kuwaeleza wananchi wa kijiji chicho kuwa wanatakiwa kuchangia asilimia 75 ya ujenzi wa shule ya kutwa ya sekondari ya Mkomanile.

Alisema ujenzi wa shule hiyo ni utekelezaji wa agizo lililotolewa na Rais Jakaya Kikwete na kwamba, wanakijiji waligoma kutoa michango hiyo kwa madai kwamba, agizo hilo ni la ghafla na kuomba wachangie mwaka 2015, kwani kwa sasa nguvu zao wameelekeza kwenye kilimo.

Msikhela alisema hakuna mtu aliyekamatwa na kuwa polisi wanaendelea na uchunguzi.


via>>Nipashe

WAZIRI MKUU ACHAPWA VIBOKO HADHARANI

Hali ya taharuki iliibuka katika mkutano wa hadhara katika jimbo la Kwale nchini Kenya, baada ya mwanamume mmoja kwenda ukumbini na kuanza kutandika bakora kiongozi wa upinzani Raila Odinga pamoja na wanasiasa wengine.
Raila alikuwa amejiunga na kikundi cha wanawake waliokuwa wanacheza densi ya kitamaduni kuwatumbuiza wageni, pamoja na gavana wa jimbo la Kwale Pwani ya Kenya Salim Mvuruya katika mkutanmo wa kisiasa.
Walikuwa wameambatana na viongozi wengine, wakiwemo, Seneta Juma Boy, Hassan Omar, Agnes Zani, James Orengo, Johnstone Muthama na wengineo.
Mwanamume huyo alimshambulia Odinga ambaye ni waziri mkuu wa zamani na kumchapa mara mbili kabla ya kumgeukia gavana wa jimbo hilo na pia kumchapa mara mbili. 
Hata hivyo mwanamume huyo alishindwa nguvu na walinzi wa Raila Odinga.
Polisi walithibitisha kuwa walimkamata mwanamume huyo na kumwachilia baada ya kugundua kuwa alikuwa na matatizo ya kiakili.
Haijulikani kwa nini mwanammume huyo alimshambulia Raila ila baadhi wanasema ni kwa sababu alighadhabishwa pale waziri mkuu alipocheza densi na mwanamke aliyesemekana kuwa mke wake ambaye alikuwa katika kikundi cha wanawake waliokuwa wanawatumbuiza wageni waheshimiwa.
Viongozi waliofika walilazimika kusitisha densi hiyo kabla ya mwanamume huyo kushindwa nguvu.
via>>BBC

UEFA CHAMPIONZ LIGI: BAYERN YASHINDA UGENINI! ANGLIA RATIBA NA MATOKEO


MATOKEO:
Jumanne Septemba 30
KUNDI E
CSKA Moscow 0 Bayern Munich 1
Man City VS Roma
KUNDI F
APOEL Nicosia VS Ajax
Paris St-Germain VS Barcelona
KUNDI G
FC Schalke 04 VS NK Maribor
Sporting Lisbon VS Chelsea
KUNDI H
BATE Borisovs VS Athletic Bilbao
Shakhtar Donetsk VS FC Porto

Penati ya Dakika ya 22 iliyopatika baada ya Mario Gotze kuangushwa ndani ya Boksi na Fernandez na Thomas Muller kufunga, imewapa Bayern Munich ushindi wa Bao 1-0 Ugenini huko Moscow Urusi.
Hii ni Mechi ya Pili ya Kundi E baada ya Bayern kuichapa Man City Bao 1-0 huko Munich.
VIKOSI:
CSKA MOSCOW: Akinfeev, Fernandes, A. Berezutski, Ignashevich, Schennikov; Natcho, V. Berezutski; Tosic, Eremenko, Milanov; Musa.
Akiba: Chepchugov, Nababkin, Efremov, Bazelyuk, Doumbia.
BAYERN MUNICH: Neuer; Lahm, Benatia, Dante, Bernat; Alonso, Alaba; Robben, Muller, Gotze; Lewandowski.
Akiba: Shaqiri, Rafinha, Pizarro, Boateng, Rode, Reina, Hojbjer
REFA: W. Collum [Scotland]
UEFA CHAMPIONZ LIGI
RATIBA MECHI ZIJAZO
**Mechi zote kuanza Saa 2145, Bongo Taimu, isipokuwa inapotajwa
Jumatano Oktoba 1
KUNDI A
Atlético Madrid VS Juvsentus
Malmö FF VS Olympiakos
KUNDI B
FC Basel VS Livserpool
Ludogorets Razgrad VS Real Madrid
KUNDI C
1900 Zenit St Petersburg VS Monaco
Bayer 04 Levserkusen VS Benfica
KUNDI D
Arsenal VS Galatasaray
RSC Anderlecht VS Borussia Dortmund

MAKOCHA WA AFRIKA WAICHAMBUA BRAZIL 2014

PrintPDF
FIFA-AFRIKAFIFA na CAF imewaalika Makocha wa Timu za Taifa za Afrika kuhudhuria Kongamano la Siku mbili unaoanza hii Leo huko Cairo, Misri kuzichambua Fainali za Kombe la Dunia za Mwaka 2014 zilizochezwa huko Nchini Brazil Mwezi Juni na Julai Mwaka huu.
Kongamano la aina hii pia ulifanyika huko Panama na Saint-Petersburg kwa Nchi Wanachama wa FIFA wa Mabara ya Amerika na Ulaya na kudhuriwa na Makocha na Maafisa wa Mabenchi ya Ufundi ya Nchi hizo.
Lengo kuu la Mikutano ya aina hii ni kujifunza mbinu za Ufundi kutoka kwenye Kombe la Dunia ili kuendeleza Soka katika ngazi zote Duniani.
Mbali ya michango ya Jopo maalum la Ufundi la FIFA, Mkuu wa Marefa wa FIFA, Massimo Busacca, na Mwakilishi kutoka, IFAB [Bodi ya Kimataifa ya Vyama vya Soka ambalo ndio Kundi waanzilishi wa Soka Duniani], Washiriki watajadili mbinu mpya za huko Brazil, mambo ya Kitaalm ya Utabibu katika Soka na matumizi ya Teknolojia Mstarini Golini na Rangi inayoyeyuka kwa ajili ya Frikiki.
Mikutano ya aina hii inatarajiwa kuhudhuriwa na Wanachama wote 209 wa FIFA.

HII NDIYO LISTI YA MAJERUHI MAN UNITED YAONGEZEKA, HERRERA NJE WIKI 3 BAADA KUVUNJIKA MBAVU

PrintPDF
ANDER-HERRERA-RASMI-MAN-UNITEDKIUNGO wa Manchester United Ander Herrera atakuwa nje kwa Wiki 3 baada kuvunjika mfupa wa mbavuni.
Herrera, ambae alijiunga na Man United mwanzoni mwa Msimu huu akitokea Athletic Bilbao na kuifungia Bao 2 katika Mechi 4 za Ligi Kuu England, anaungana na Listi ndefu ya Majeruhi ya Timu hiyo wakiwemo Jonny Evans, Chris Smalling, Phil Jones, Jesse Lingard, Michael Carrick, Marouane Fellaini na Ashley Young.
Ingawa Carrick, Fellaini na Young wameanza tena Mazoezi hawatarajiwi kuwa fiti kwa Mechi ijayo ya Ligi Jumapili na Everton na hao wanaungana na Nahodha Wayne Rooney ambae atazikosa Mechi 3 baada ya kupewa Kadi Nyekundu walipocheza na West Ham Mechi iliyopita.
Herrera aliumia na kutolewa katika Dakika ya 74 Man United walipocheza na West Ham na awali ilidhaniwa ameumia Mgongo hadi uchunguzi wa kina ulipofanywa.
Jumapili Man United watapambana na Everton na kisha Ligi itaenda Mapumziko ya Wiki mbili kupisha Mechi za Kimataifa na baada ya hapo zitafuata Mechi za Ligi dhidi ya West Brom, Chelsea na Manchester City.

MAN UNITED - MECHI ZIJAZO
**Saa za Bongo
Oktoba 5 Saa 1400: Man United v Everton
Oktoba 20 Saa 2200: West Brom v Man United
Oktoba 26 Saa 1900: Man United v Chelsea
Novemba 2 Saa 1630: Man City v Man United
**Zote Ligi Kuu England

NOOIJ WA STARS AITA 26 WA KUIVAA BENIN YANGA YAVUNJA REKODI KATIKA KIKOSI


Na Boniface Wambura, DAR ES SALAAM
KOCHA Mkuu wa timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Mholanzi Mart Nooij ameteua wachezaji 26 kwa ajili mechi ya Kalenda ya Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) dhidi ya Benin itakayochezwa Oktoba 12 mwaka huu jijini Dar es Salaam.
Kocha Nooij ambaye yuko Cairo, Misri kwenye kongamano la makocha la Shirikisho la Soka Afrika (CAF), safu ya ulinzi itaendelea kutegemea mabeki wa Yanga SC kwa mujibu wa kikosi alichoteua ambacho kitaingia kambini Oktoba 6 mwaka huu jijini Dar es Salaam.
Kikosi cha Taifa Stars kitaendelea kutegemea safu ya ulinzi ya Yanga SC

Wachezaji walioitwa ni makipa Deogratias Munishi (Yanga), Aishi Manula (Azam), na Mwadini Ali (Azam).
Mabeki ni Said Moradi (Azam), Shomari Kapombe (Azam), Oscar Joshua (Yanga), Nadir Haroub (Yanga), Kelvin Yondani (Yanga), Aggrey Morris (Azam), Miraji Adam (Simba), Charles Edward (Yanga) na Emmanuel Simwanda (African Lyon).
Viungo ni Erasto Nyoni (Azam), Mwinyi Kazimoto (Al Markhiya, Qatar), Amri Kiemba (Simba), Himid Mao (Azam), Salum Abubakar (Azam), Said Ndemla (Simba) na Haruna Chanongo (Simba).
Washambuliaji ni Khamis Mcha (Azam), Simon Msuva (Yanga), Thomas Ulimwengu (TP Mazembe, DR Congo), Mbwana Samata (TP Mazembe, DR Congo), Mrisho Ngasa (Yanga), Mwegane Yeya (Mbeya City), na Juma Liuzio (Zesco, Zambia).

BAADA YA MATOKEO YA SIMBA KUA HABA PHIRI AHAMISHIA KAMBI DAR



Kocha Mkuu wa Simba, Patrick Phiri amesema ulikuwa ni wakati mwafaka wa kuhamishia kambi jijini Dar.
Simba imehamishia kambi yake Changanyikeni jijini Dar na leo jioni imefanya mazoezini Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Phiri amesema kwa muda waliokaa Zanzibar unatosha pia ni jambo jema kufanya mazoezi Dar es Salaam kwa kuwa wana mechi mbili ndani ya wiki mbili na zote zitapgwa Dar es Salaam.
"Mechi zote zitakuwa Dar es Salaam, wiki zote mbili tutacheza hapa. Hatuna sababu ya kurudi Zanzibar.
"Hivyo tutabaki hapa, naamini hata wakati wa mechi dhidi ya Yanga tunaweza kuendelea kubaki hapa," alisema Phiri.
Simba ilikuwa imeweka kambi mjini Zanzibar ambako ilikuwa ikisafiri kuja Dar es Salaam kila inapokuwa na mechi.
Chini ya Phiri, Simba imeanza mechi zake za ligi, zote kwa kutoka sare ya 2-2 dhidi ya Coastak Union na baadaye 1-1 dhidi ya Polisi Moro.

BODI YA LIGI YATOA KAULI YAKE KUHUSU TFF KUCHUKUWA FEDHA ZA KLABU

MWAKIBINGA (KUSHOTO) AKIWA NA BOSI MKUBWA WA AZAM TV, RHYS TORINGTON AMBAO NI KATI YA WADHAMINI WA LIGI KUU BARA.

Bodi ya Ligi Tanzania imetoa msimamo wake kuhusiana na lile sakata la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kutaka lipewe fedha za udhamini za klabu kwa ajili ya shughuli zake lilizoziita ni za maendeleo ya soka.



TFF imeiagiza bodi ya ligi kukata kiasi cha asilimia tano tano kutoka kwenye udhamini wa Vodacom na Azam TV ili ipewe yenyewe.

Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi, Silas Mwakibinga amesema wao ni wawakilishi wa klabu, hivyo wanabaki upande wa klabu.

"Bodi inazaliwa kutoka kwenye ubavu wa klabu, sisi ni wawakilishi wa klabu. Hivyo automatikale tunabaki upande wa klabu," alisema Mwakibinga.
Kama bodi hiyo itabaki upande wa klabu hizo 14, maana yake utakuwa umeziokoa kunyongwa fedha zao za udhamini.

Tayari klabu kupitia mwanasheria Dk Damas Ndumbaro zimepinga suala hilo na Mbeya City na Mtibwa Sugar zimetishia kwenda
mahakamani.

SIMBA SC YAUNDA SEKRETARIETI MPYA KUWA NA MAJUKUMU YA KITAWALA

KLABU ya Simba SC imetangaza Sekretarieti yake mpya ambayo itakuwa na majukumu ya kiutawala na kuratibu shughuli zote za uendeshaji wa klabu.
Taarifa iliyotolewa na Rais wa Simba SC, Evans Aveva imesems kwamba Sekretarieti hiyo itakuwa ikifanya kazi zake chini ya kamati ya utendaje ambayo imeundwa na Rais wa klabu, makamu wake na wajumbe wengine wa kuteuliwa na kuchaguliwa kupitia uchaguzi mkuu wa klabu ya simba.
Ameutaja muundo wa sekretarieti hiyo kuwa ni Katibu Mkuu Stephen Ally, Mhasibu Amos Juma Gahumeni, Ofisa Habari Humphrey Nyasio, Ofisa Operesheni, Stanley Philipo, Ofisa Utawala Hussein Mozzy, pamoja na Mtunza ofisi, Juma Issa Matari. 


Aveva amesema kwamba Sekretarieti hiyo imeshaanza kazi kuanzia Septemba 1, hivyo Kamati ya Utendaji inawaomba wanachama, washabiki na wadau wote wa michezo kuipa sekretarieti hiyo ushirikiano wa kutosha katika utekelezaji wa majukumu yake katika klabu.
Na Samira Said, DAR ES SALAAM

MKOSI WAIKUMBA MAN UNITED BAADA YA ANER HERRERA ACHANIKA MBAVU,

Ander Herrera anatarajiwa kuwa nje kwa wiki kadhaa baada ya kuchanika mbavu akiichezea Manchester United dhidi ya West Ham Jumamosi.

Kiungo huyo wa kimataifa wa Hispania alimpisha Antonio Valencia baada ya kuumia katika mchezo huo uliofanyika Uwanja wa Old Trafford.
Taarifa iliyotolewa na United leo mchana imesema: "Kiungo wa Manchester United, Ander Herrera amechanika mbavu wakati wa mechi na West Ham United Jumamosi. 
Herrera akiwa ameshika ubavu wake wakati akiondoka uwanjani Old Trafford baada ya kuumia

NYOTA ANAOWAKOSA VAN GAAL MAN UNITED

Wachezaji tisa wa kikosi cha kwanza cha Man United waio nje kwa majeruhi na wengine kutumikia adhabu ni;
Ander Herrera, Jonny Evans, Phil Jones, Chris Smalling, Michael Carrick, Marouane Fellaini, Ashley Young, Jesse Lingard na Wayne Rooney. 
"Mspanyola huyo alitolewa dakika ya 74 na klabu hiyo itaendelea kuangalia hali yake kwa karibu katika wiki kadhaa,". 
Herrera anakuwa mchezaji wa tisa wa kikosi cha kwanza cha Louis van Gaal kuwa nje ya Uwanja kwa sababu ya maumivu na wengine wakitumikia adhabu wakati inajiandaa na mechi dhidi ya Everton Jumapili. 
Haifahamiki ni muda gani mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 atakuwa nje kwa maumivu hayo, ambayo ni pigo lingine kwa kocha wake.
Herrera amekuwa katika kiwango kizuri United tangu ajiunge nayo kutoka Athletic Bilbao mwishoni mwa Juni mwaka huu.
Amecheza mechi za Ligi Kuu ya England dhidi ya Swansea City, Queens Park Rangers, Leicester City na West Ham.
Alifunga bao la pili la United katika ushindi wa 4-0 dhidi ya QPR na akaifanya United ionize 3-1 mbele ya Leicester, kabla ya kufungwa 5-3.

Monday, 29 September 2014

DIDIER KAVUMBAGU KUTAMBA KUHUSU UFUNGAJI BORA LIGI KUU YA TANZANZNIA BARA

 
Mshambuliaji wa kimataifa wa Azam FC, Mrundi, Didier Kavumbagu, ametamba kuwa sasa atahakikisha anafunga kila mechi ili kuisaidia timu yake kuibuka na ushindi na hatimaye kutwaa ubingwa.

Kavumbagu ameianza Ligi Kuu Bara kwa mkwara baada ya kufunga mabao manne katika michezo miwili ya awali. Kila mchezo akitupia mawilimawili.

Akizungumza na Championi Jumatatu baada ya kuifungia timu yake mabao mawili katika ushindi wa 2-0 dhidi ya Ruvu Shooting juzi kwenye Uwanja wa Chamazi, Kavumbagu alisema anafurahi kuona amekuwa katika wakati mzuri ndani ya kikosi hicho lakini akasisitiza kuwa ataendelea kufunga kila anapopata nafasi.


“Cha msingi ni kufunga tu, hilo ndilo suala pekee linaloipa timu mafanikio, kwa hiyo nitajitahidi kufunga katika kila mechi kadiri ninavyopata nafasi ili kuhakikisha naisaidia timu katika mbio za kutwaa ubingwa, kisha hayo mambo ya ufungaji bora yatakuwa baadaye,” alisema Kavumbagu, mchezaji wa zamani wa Yanga.

TIMU YA MBEYA CITY KUFUNGUA MADUKA YA JEZI,NA VIFAA VYA MICHEZO NDANI YA DAR


Mbeya City ina mpango wa kubadili jezi zake za awali kutokana na kutaka kuweka nembo ya mdhamini mpya Bin Slum na kuachana na zile za awali.

Katibu Mkuu wa Mbeya City, Emmanuel Kimbe, alisema wapo katika hatua za mwisho kukamilisha mchakato wa usambazaji wa jezi mpya ambapo watasaka mawakala wa kuwasaidia kazi hiyo.

“Tupo katika mikakati ya kubadili jezi zetu ambapo zitauzwa katika maduka mawili jijini Dar, moja lipo maeneo ya Sinza na lingine litakuwa katikati ya mji, Posta.


“Tunawatafuta mawakala ambao watasimamia kazi hiyo kwa kuhakikisha tunadhibiti hali ya watu wengine kuuza jezi hizo na hatua kali zitachukuliwa kwa mtu yeyote atakayehusika na utoaji wa jezi zetu bila ruhusa,” alisema Kimbe.

KIBOKO AVAMIA KIJIJI WANANCHI WASHINDA JUU YA MITI KUTWA

 
Baadhi ya wakazi wa Kitongoji cha Kashalami Kata ya Mashimboni  wilaya ya Mlele Mkoa wa Katavi wamelazimika kushinda juu ya miti kwa kuhofia kushambuliwa na Kiboko  aliyevamia kijiji hicho  na kuhatarisha uhai wa Wanachi 
 Kwa mujibu wa Diwani wa Kata hiyo ya Mashimboni  Raphael  Kalinga  tukio hilo lilitokea hivi karibuni mwezi huu
 Akielezea tukio hilo alisema  Kiboko huyo baada  ya kuvamia kijiji hicho  alielekea kwenye nyumba ya mkazi  mmoja  aitwaye Joseph  Kashamakula  ambae alinusurika  kushambuliwa na Biboko huyo wakati alipokuwa  akitokea chooni kujisaidia 
  Diwani  Kalinga alisema  ndipo Kiboko huyo ambae  alionekana kuwa na hasira alipoanza  kukanyaga  kanyanga na vuvivunja vyombo vya mwanakijiji huyo ambavyo vilikuwa  nje ya nyumba yake na kuviharibu kabisa  hari ambayo ilimfanya wananchi huyo apige mayowe ya kuomba msaada kwa majirani 
 Majirani walifika kwenye eneo hilo  hata hivyo walilazimika  kutimua mbio  baada ya kiboko huyo  kuanza  kuwafuata  hari ambayo ilipelekea  kukimbia na kisha kupanda juu ya miti kwa kuhofia kushambuliwa na mnyama huyo ambae aliendelea kuvunja vyombo kwenye nyumba mbalimbali 
  Alisema  Kiboko huyo aliendelea kuzunguka kwenye eneo la kijiji hicho na  taarifa za  zilifika kwenye Idara ya Maliasili ya Halmashauri ya  Nsimbo  ambao  walituma Akari wao wa wanyama pori kwenda huko 
 Baada ya  Askari wa Maliasli kufika kijijini hapo  walianza msako wa kumtafuta kwa kushirikiana na wananchi  ambapo walifanikiwa kumwona na kisha  walimuuwa kwa kumpiga Risasi  tumboni na kichwani 
 Diwani   Kalinga  alieleza  baada ya Kiboko kuuwa  wananchi  licha ya hapo awali kumkimbia kiboko huyo  walianza  kugombea  nyama  ya  mnyama huyo  kwa kuchukua  kitoweo cha mboga na  baada ya nusu saa wakawa wamemmaliza 

Na  Walter  Mguluchuma 
 Mpanda Katavi 

HUYU NDIYO MTANZANIA ALITESWA DUBAI, AKI SAFIRISHA DAWA ZA KULEVYA



 


Mwanaisha Athuman Pinde(36) , mzaliwa wa mkoa wa Morogoro, Novemba 25, 1978 kama pasi yake ya kusafiria inavyoonyesha.


USALAMA  wa watanzania wanaopelekwa nchini Dubai  falme za kiarabu kujaribu fursa za ajira upo shakani kutokana na baadhi ya waajiri nchini humo kuwafanyia vitendo visivyokuwa vya kibinadamu ikiwamo kupokwa pasi zao za kusafiria na wengine kujikuta wakiswekwa jela bila hatia.
Uchunguzi uliofanywana mtandao wa www.kalulunga.blogspot.com kwa zaidi ya mwezi mmoja sasa, umebaini kuwa mbali na hilo,watanzania hao wamejikuta wakifanya kazi kwa mali kauli pasipo kulipwa mishahara yao kama ambavyo mikataba ya ajira inavyoonesha.
Mmoja wa wahanga hao ni Mwanaisha Athuman Pinde(36) ,Mwanaisha mzaliwa wa mkoa wa Morogoro, Novemba 25, 1978 kama pasi yake ya kusafiria inavyoonyesha.
Kwa mujibu wa nyaraka tulizonazo, Mwanaisha aliondoka Jijini Dar e s salaam, kwenda Dubai  Februari 17 mwaka huu,  na ndege ya shirika la ndege la Qatar yenye namba QR1350.
Uchunguzi umebaini kwamba alisafiri kwa msaada wa kampuni ya Bravo Job Centre Agency Ltd ya Jijijini Dar es salaam, inayojihusisha na kuwatafutia fursa za ajira watanzania katika nchi mbalimbali na kupokelewa na wakala aitwaye Oriental Int,Labour Supply aliye na mkataba na Bravo.
Baada ya binti huyo kupokelewa na kupelekwa kwa mwajili wake, alijikuta akiingia kwenye mgongano na mama mwenye nyumba na kulazimika kusitisha mkataba na kupelekwa kwa mwajili mwingine.
Kwa mujibu wa dada wa binti huyo, Zena Athuman Pinde, mdogo wake huyo baada ya kupelekwa kwa mwajili mwingine alipokwa pasi yake ya kusafiria, simu pamoja na nyaraka nyingine huku akinyimwa kufanya mawasiliano na ndugu zake.
Zena amesema, mdogo wake alikuwa akiishi bila kulipwa mshahara na pale alipodai mshahara wake alijikuta akiambulia kauli chafu kutoka kwa mwajili wake.
Kwa upande wake Mwanaisha akiongea na mwandishi wa habari hizi  kwa njia ya simu kutoka Abu Dhabi hivi karibuni, alisema alijikuta akiswekwa jela na maofisa wa polisi wa huku baada ya mwajiri wake kumtelekeza na kushindwa kumrejesha nyumbani huku pasi pake akiwa ameishikilia pamoja na simu yake ya kiganjani.
Akizungumza kwa msaada wa ofisa wa polisi mwenye asili ya Tanzania, mwanaisha amedai kuwa,chanzo cha kutofautiana na mwajili wake ni hatua ya bosi huyo kutaka kumgeuza kitega uchumi kwa kumbadilisha kazi za ndani na kutaka kumtumia katika biashara haramu za dawa za kulevya.
Amedai baada ya kugoma, alijikuta katika mgogoro na bosi wake na hapo upepo ukawa mbaya kwake kwani alijikuta akipokwa kila kitu huku akiwa hajalipwa mshahara wake kwa muda wa miezi sita sasa.
kwa mujibu wa mwanaisha, tangu awasili Abu Dhabi, amekuwa hana mawasiliano na ndugu zake kutokana na simu yake kuwa mikononi mwa bosi wake japo amefanikiwa kurejea nyumbani kwa msaada wa ubalozi mdogo wa tanzania huko Abu Dhabi baada ya kupatiwa hati ya muda ya kusafiria.
Akizungumza muda mfupi baada ya kurejea nchini hivi karibuni na ndege ya shirika la ndege la Kenya na kupokelewa na ndugu zake, Mwanaisha anadai kwa sasa anakamilisha tararibu za kisheria kuifikisha mahakamani kampuni ya Bravo kwa kile alichodai kushindwa kumsadia kupata haki zake.
Hata hivyo,msemaji wa kampuni hiyo ya Bravo, Heri Mtemvu, akizungumza na www.kalulunga.blogspot.com hivi karibini ofisini kwake, Keko Bora jijini Dar es salaam, alitetea hatua ya waajiri huko Dubai ya kuwapoka simu na pasi za kusafiiria watanzania wanaokwenda kufanya kazi huko.
Kwa mujibu wa Mtemvu, hatua ya kupokonywa pasi na simu ni katika juhudi za kuzima majaribio ya watumishi hao kutoroka pindi wanapopata vibali vya kuwawezesha kufanyakazi nchini humo.
Mtemvu hata hivyo alisema,kampuni yake ipo katika hatua za mwisho kwenda nchini Dubia kufuatilia haki za mtanzania huyo ikiwamo mishahara yake pamoja na pasipoti yake ya kusafiria ambayo ingali mikononi mwa tajili yake.
Kwa mujibu wa nyaraka tulizonazo, safari za watanzania kwenda katika nchi za falme za kiarabu zimekuwa zikipata baraka kutokana wakala wa Huduma za ajira Tanzania(TaESA) ambako mhusika hulipia ada ya sh,100,000/=.
Nyaraka hizo zinaonyesha kuwa,mwanaisha alikuwa na mkataba  wa kufanyakazi za ndani kwa  mfanyabiashara Mohamed Saleh Yeslam Alameri ulioidhinishwa februari 5 mwaka huu na kutiwa saini na Omary Mjenga kutoka TaESA.
"Mtajwa hapo juu mwenye pasipoti namba AB474488 amethibitishwa na ubalozi wa Tanzania ulioko Dubia, UAE kwamba amepata kazi nchini humo,wakala wa huduma za ajira Tanzania umeridhia utaratibu uliotumika kwa kumuunganisha  mtajwa hapo juu na fursa ya ajira",inasema barua ya TaESA.
Barua hiyo iliyotumwa uhamiaji kwa taratibu zaidi ya kiuhamiaji, ilisainiwa na K.V.Kilindu  februari 12 mwaka huu kwa niaba ya mtendaji mkuu wa TaESA huku ikiwa imebandikwa picha ya mwanaisha.
Kwa mujibu wa mkataba ambao nakala yake tunayo,mwanaisha alikuwa alipwe mshahara wa AED 1100  sawa na sh,460,000 za Tanzania lakini kwa mujibu wa maelezo yake,alielezwa kuwa atalipwa AED 800 sawa na sh,360,000 ambazo hata hivyo alidai hajawahi kulipwa 

KWA HISANI YA.Kalulunga media, correspondent