MATUKIO KATIKA PICHA YALIYO WEZA KUVUTIA DUNIANI KOTE

Asante kwa kututembelea mbeyagreennews kwa taarifa zaidi endelelea kututembela kila siku ,saa,dakika usipitwe na matukio kem kemu

MATUKIO KATIKA PICHA YALIYO WEZA KUVUTIA DUNIANI KOTE

Asante kwa kututembelea mbeyagreennews kwa taarifa zaidi endelelea kututembela kila siku ,saa,dakika usipitwe na matukio kem kemu

MATUKIO KATIKA PICHA YALIYO WEZA KUVUTIA DUNIANI KOTE

Asante kwa kututembelea mbeyagreennews kwa taarifa zaidi endelelea kututembela kila siku ,saa,dakika usipitwe na matukio kem kemu

MATUKIO KATIKA PICHA YALIYO WEZA KUVUTIA DUNIANI KOTE

Asante kwa kututembelea mbeyagreennews kwa taarifa zaidi endelelea kututembela kila siku ,saa,dakika usipitwe na matukio kem kemu

MATUKIO KATIKA PICHA YALIYO WEZA KUVUTIA DUNIANI KOTE

Asante kwa kututembelea mbeyagreennews kwa taarifa zaidi endelelea kututembela kila siku ,saa,dakika usipitwe na matukio kem kemu

Wednesday, 3 December 2014

WAYNE ROONEY KUPIMWA GOTI LEO, DELAY BLIND APONA!


ROONEY-LVG-KICHEKO-18OCTWAKATI Nahodha wa Manchester United Wayne Rooney Leo hii atapimwa Goti lake kuthibitisha undani wa maumivu yake na pia atakuwa nje kwa muda gani, Klabu hiyo imepata habari njema baada ya Kiungo Daley Blind kupata nafuu na huenda akawa fiti kabisa kabla ya mwisho wa Mwezi huu baada nae kuumia Goti.
Rooney hakucheza Mechi ya Ligi Kuu England Jumanne Usiku Uwanjani Old Trafford wakati Man United inaifunga Stoke City 2-1 baada kuumia Goti Jumamosi iliyopita wakati wanaifunga Hull City.
Meneja wa Man United, Louis van Gaal, amesema: “Rooney atachunguzwa zaidi Goti lake Jumatano. Natumai hakuumia sana.”
Nae Blind alieumia Goti akiichezea Timu ya Taifa ya Netherlands anatarajiwa hivi karibuni kurejea Mazoezini.
Tangu aanze kuifundisha Man United, Van Gaal amekumbwa na Majeruhi wengi na kwenye Mechi na Stoke City Mastaa wake wakubwa kina Angel Di Maria, Luke Shaw na Daley Blind vile vile hawakucheza.

Manchester United-Listi ya Wachezaji walioumia Msimu huu:
Kipa: David De Gea
Viungo: Angel Di Maria, Juan Mata, Michael Carrick, Daley Blind, Ashley Young, Ander Herrera, Antonio Valencia, Anderson, Marouane Fellaini, Jesse Lingard
Mabeki: Rafael, Luke Shaw, Phil Jones, Marcos Rojo, Jonny Evans, Chris Smalling, Paddy McNair, Tom Thorpe
Mafowadi: Radamel Falcao, Wayne Rooney, Robin van Persie, James Wilson

Van Gaal amethibitisha kuwa Rooney na Di Maria hawataweza kucheza Mechi yao ijayo ya Ligi Jumatatu Ugenini na Southampton kwani ni mapema mno kwao.
Hata hivyo, Van Gaal amesema majeruhi wao wengi sasa wanapona na wameanza kurejea Mazoezini.
LIGI KUU ENGLAND
RATIBA:
**Saa za Bongo
Jumatano Desemba 3
2245 Arsenal v Southampton               
2245 Chelsea v Tottenham         
2245 Everton v Hull         
2245 Sunderland v Man City                
Jumamosi Desemba 6
1545 Newcastle v Chelsea           
1800 Hull v West Brom               
1800 Liverpool v Sunderland                
1800 QPR v Burnley          
1800 Stoke v Arsenal       
1800 Tottenham v Crystal Palace          
2030 Man City v Everton            
Jumapili Desemba 7
1630 West Ham v Swansea                   
1900 Aston Villa v Leicester                  
Jumatatu Desemba 8
2300 Southampton v Man Utd

MWAMUZI TANZANIA AFUZU KUCHEZESHA AFCON YA VIJANA, SASA AWANIA YA WAKUBWA

 

Mwamuzi kutoka Tanzania, Samwel Mpenzu, amefuzu kuchezesha michuano mikubwa itakayoandaliwa na Shirikisho la Soka Afrika (Caf) ikiiwemo ya Mataifa ya Afrika kwa vijana chini ya umri wa miaka 20 (Afcon U-20).

Mpenzu, ambaye ni mwamuzi mwenye beji ya Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa), amefuzu baada ya kupita kwenye mchujo wa kupata nafasi hiyo ambao ulifanyika Cairo, Misri wiki iliyopita pamoja na waamuzi wengine kutoka nchi mbalimbali barani Afrika.
Mwamuzi huyo alisema kuwa baada ya kupita kwenye hatua hiyo, kwa sasa anachoangalia ni kupita kwenye hatua inayofuata ‘Elite A’ ambayo itamfanya aweze kuchezesha michuano ya wakubwa ya Afcon pamoja na Kombe la Dunia.

Alisema kuwa lengo lake kubwa ni kuchezesha Kombe la Dunia, kwani hakuna Mtanzania aliyefika huko.

ANGALIA:DI MARIA AKIJIBU BARUA WALIZOMTUMIA MASHABIKI WAKE

 
KIUNGO WA MANCHESTER UNITED, ANGELO DI MARIA AKIJIBU BARUA ZA MASHABIKI. KWA SASA MUARGENTINA NI MAJERUHI.

ILO NA TUCTA WANDAA SEMINA YA MAFUNZO BURE JIJINI MBEYA IJUMAA HII


Mkugenzi wa wise and mercy compani Clemence Busara Akiwa ofisini kwake


Shirika la kazi duniani  ILO  na chama cha wafanyazi Tanzania TUCTA kwa kushirikiana na wise and mercy company ameandaa  Semina kubwa ya mafunzo ya kuelimisha juu ya kujua msingi ya  na sheria  za kazi kwa mwajiri na majiriwa

Akizungumza na mtandao huu wa green media ofisini kwake  Mkurungenzi wa wise and mercy company ambao ni ndiyo waratibu wa mafunzo haya Mh Clemence Busara amesema kuwa lengo kubwa la semina  hii ni kumjengea uwezo mfanyakazi  kueleawa misingi ya kazi kwa mwajiri na mwajiriwa ,kutambua wajibu wa mwajiri na mwajiriwa katika majukumu ya kila siku,  kuwongeza  ujuzi zaidi mfanyakazi  kufanya kazi kwa Ufanisi na Ubunifu wa hali ya juu.na jinsi mwajiri anavyo weza kuboresha mazingira kwa wafanya kazi wake.
Mkugenzi wa wise and mercy compani Clemence Busara Akiongea na mwandishi wa Habari wa Green Media Group {Abdul Marwa Abdallah} 
Mh busara ameongaza kuwa ILO na TUCTCA wameona kuna umuhimu mkubwa wa kuandaa mafunzo haya kwa kuwa wanyakazi wengi hawatambui sheria za kazi zinazo walinda wakiwa kwenye ajirazao, wajiri kukiuka miko  na sheria za kazi kwa wajiriwa, busara amesema kupitia mafunzo haya  yanaweza kuondoa hali ilipo hivi sasa
 Mkugenzi huyu amesema mafunzo haya yamewalenga   Wajasiriamali Wadogo na wakubwa, wafakazi wa umma nawa mashrika binafsi ,wakurungenzi wa kampuni na tasisi mbalimbali, hivyo ametoa wito kwa watu wote kuhudhuria kwa  kwa wingi kwa kuwa mafunzo hayo kwa kuwa semina hiyo ni bure
Mafunzo hayo yatafanyika   nyanda ya juu kusini mkoa wa mbeya Siku ya Ijumaa 5/12/2014  katika ukumbi wa JM MOTEL, karibu na shule ya st merry kuanzia 10:00 kamili asubuhi  na  kingilio cha mafunzo haya ni bure kwa mtu yeyote Yule ,semina ya mafunzo hayo itahudhuliwa na wa wawakilishi wa sirika la kazi duiani (ILO) ,chama cha wafanya kazi Tanzania TUCTA , wawakilishi wa wizara ya kazi  mkoa wa mbeya  na wadau mbalimbali  hapa nchini Tanzania.
clemence busara akiwa ofisini kwake
Ikumbuke kwa semina hii ya mafunzo inaratibiwa na kusimamiwa na wise and mercy company kwa kuwezeshwa na ILO na TUCTA kushirikiana  wizara ya kazi mkoa.

Tuesday, 2 December 2014

POLISI MORO , MWADUI YA SHINGA ZA MTAKA BEKI SIMBA MIRAJ ADAM

POLISI ya Morogoro na Mwadui FC ya Shinyanga zimewasilisha barua kumuomba beki wa pembeni Miraj Adam wa Simba SC kwa mkopo.

Polisi ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania inapambana na Mwadui FC, inayopigania kupanda Ligi Kuu pia kuwania huduma za beki huyo aliyetokea timu ya vijana ya Wekundu hao wa Msimbazi.
Mwadui wanaamini wanaweza kumpata kwa urahisi beki huyo kwa sababu ya mahusiano mazuri ya kocha wao, Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ na klabu ya Simba SC.
Miraj Adam kushoto anatakiwa na Polisi Moro na Mwadui ya Shinyanga baada ya kushushwa Simba B

Julio ni mchezaji na kocha wa zamani wa Simba SC, ambaye pia ni mwanachama wa klabu hiyo aliyegombea nafasi ya Umakamu wa Rais katika uchaguzi wa katikati ha mwaka na kuangushwa na Geoffrey Nyange ‘Kaburu’. 
Lakini Polisi nayo inaamini inaweza kumpata kwa urahisi beki huyo wa kulia, Miraj, kwa sababu inacheza Ligi Kuu kwa sasa na Morogoro si mbali sana na Dar es Salaam anakoishi mchezaji huyo.
Kwa sasa, Miraj ameshushwa kikosi cha pili baada ya mechi saba za awali za Ligi Kuu, lakini Simba SC bado haijaamua kumtoa kwa mkopo hadi hapo itakapofanikisha kusajili mchezaji mwingine wa nafasi hiyo.

Tuzo Fifa:Ronaldo,Messi,Neuer nani bora?


Lionel Messi
Shirikisho la Mpira wa miguu duniani Fifa limewataja Cristiano Ronaldo, Lionel Messi na Manuel Neuer kuwania Tuzo ya mchezaji bora wa Dunia.Nyota hawa watatu wameteuliwa toka katika kundi la Wachezaji 23 waliokua wakiwania tuzo hii ya mchezaji bora itakayotolewa tarehe 12, Januari.
Nadine Kessler(Ujerumani) , Marta(Brazil) na Abby Wambach(Marekani) watawania tuzo ya mchezaji bora wa dunia kwa upande wa Wanawake.
Kwa upande wa Makocha watakaochuana katika kuwania Kocha bora wa mwaka ni pamoja na kocha wa mabigwa wa dunia Ujerumani Joachim Low,kocha wa Real Carlo Ancelotti,na Diego Simeone kocha wa Atletico Madrid.
Manuel Neuer
Kwa upande wa kocha bora wa kike ni pamoja na kocha wa Wolfsburg Ralf Kellermann,kocha wa timu ya Taifa ya Ujeruman chini ya miaka 20 Maren Meinert,na Norio Sasaki kocha wa Japan.
Cristiano Ronaldo 29, atakuwa akiwania tuzo hii kwa mara ya tatu mara baada ya kuitwaa mara mbili. Lionel Messi 27 akitaka kuweka historia ya kutwaa tuzo ya mchezaji bora kwa mara ya tano.huku kipa Manuel Neuer akiwania tuzo hiyo kwa mara ya kwanza na iwapo atatwaa tuzo hii ataweka historia kuwa mchezaji bora golikipa toka ilipowekwa historia na kipa Lev Ivanovich Yashin mwaka 1963.
Nyota wengine waliokuepo katika kinyanganyiro hiki kabla ya kuenguliwa ni pamoja na Angel di Maria,Eden Hazard,Yaya Toure,James Rodrigues,Zlatan Ibrahimovic ,Gareth Bale na Neymer.

MATIC AWAONYA WACHEZAJI WENZAKE AWAKUMBUSHA KILICHOMKUTA BENFICA


Kiungo wa Chelsea, Nemanja Matic amesema pamoja na kucheza mechi 20 bila kupoteza, lakini anawaonya wenzake.
Amesema kucheza mechi hizo bila ya kupoteza, si sababu kwamba wana uhakika wa kutwaa ubingwa.
Kwa LIgi Kuu England, wameishacheza mechi 11 bila ya kupoteza.
Matic amesema wakati akiwa Benfica walicheza mechi 28 bila ya kupoteza, lakini mwisho wakakosa ubingwa.
“Umakini ndiyo jambo muhimu na tunalazimika kuwa makini sana,” alisema Matic.
Matic ndiyo jembe kwenye kiungo cha ukabaji cha Chelsea kwa sasa.

AFCON 2015-EQUATORIAL GUINEA: DROO MAKUNDI FAINALI JUMATANO

 

WASHIRIKI 16 wa Fanali za Kombe la Mataifa ya Afrika, AFCON 2015, ambazo zitachezwa huko Nchini Equatorial Guinea kuanzia Januari 17, watajua nani Wapinzani kwenye Makundi yao hapo Jumatano baada ya hii Leo Vyungu Vinne vya Timu 4 kila moja kutajwa kwa ajili ya Droo hiyo na CAF.
Droo hiyo itafanyika Mjini Malabo Nchini Equatorial Guinea.
Timu hizo 16 zimepangwa kwenye Vyungu Vinne vya Timu 4 kila moja na kwenye Droo kila Chungu kitatoa Timu moja ili kupanga Makundi Manne.
CHUNGU 1
Equatorial Guinea, Ghana, Zambia, Burkina Faso
CHUNGU 2
Ivory Coast, Mali, Tunisia, Algeria
CHUNGU 3
Cape Verde, South Africa, Gabon, DR Congo
CHUNGU 4
Cameroon, Senegal, Guinea, Congo

YASINE BRAHIMI ASHINDA TUZO YA BBC YA MCHEZAJI BORA AFRIKA


Yacine Brahimi akiwa na tuzo yake ya BBC.

MSHINDI wa tuzo ya BBC ya mchezaji bora wa mwaka 2014 Afrika imekwenda kwa mchezaji wa Algeria na nyota wa Porto, Yacine Brahimi.
Hapajawahi kutokea katika miaka 23 ya historia ya shindano hilo kwa mchezaji bora kutoka Algeria kuishinda tuzo hiyo, lakini Brahimi amefanikiwa kutwaa tuzo hiyo baada ya mwaka uliokuwa na mbwembwe nyingi.
Brahimi amewabwaga wachezaji wengine nyota wakiwemo, Pierre-Emerick Aubameyang wa Gabon, Vincent Enyeama wa Nigeria, Gervinho wa Ivory Coast.

Aliyewakosoa watoto wa obama Sasha na Malia ajiuzulu

Mfanyakazi katika chama cha Republican nchini Marekani amejiuzulu baada ya kukosolewa kwa kuwatuhumu wanawe Rais wa Marekani Barack Obama , Sasha na Malia kwa kuwaambia kuwa wamekosa ustaarabu.
Elizabeth Lauten, afisaa mkuu wa mawasiliano wa mwanasiasa mkuu wa chama hicho, Stephen Fincher, alijiuzulu Jumatatu.
Bi Lauten, aliwakosoa watoto wa Obama Sasha na Malia kwenye ukurasa wake wa Facebook baada ya watoto hao kuonekana wakiwa wamevalia sketi fupi kwenye hafla ya jioni.
Rais Obama na mkewe wamejitahidi sana kuwalinda watoto wao kutokana na ndimi kali za vyombo vya habari
Baadaye Lauten alifuta maandiko yake ambayo baadaye aliyataja ya kuumiza moyo na kuudhi.
Bi Lauten pia alikuwa amewakosoa Sasha na Malia kwa kusema walionekana wasio na furaha walipokuwa wamesimama na baba yao katika hafla ya maankuli katika Ikulu ya White House.
Wakati watu wengi walihisi kwamba Sasha na Malia hawakua na furaha kuwa na baba yao katika hafla ile na hata kulizungumzia swala hilo kwenye mitandao ya kijamii,Bi Lauten aliamua kujitoa kimasomaso na kuwakosoa wasichana hao kupitia kwa Facebook.
Sasha na Malia ni miongoni mwa vijana wadogo sana kuwahi kuwa katika ikulu ya White house
Mwanamke huyo akiomba msamaha, alisema baada ya kufanya maombi na hata kuzungumza na wazazi wake na kisha kusoma maandiko yake kuwahusu Sasha na Malia, alihisi kweli aliwakera wasichana hao.
"ningependa kuomba radhi kwa wote niliowaudhi kwa matamshi yangu, na nina ahidi kujifunza na kubadilisha mwenendo wangu, '' alisema Lauten.

YAYA TOURE NA ASAMOAH GYAN KWENYE KINYANGANYIRO CHA TUZO YA MWANASOKA BORA AFRIKA


SHIRIKISHO la Soka Afrika leo limetoa orodha fupi ya wachezaji watano walioingia katika fainali ya kuwania Tuzo ya Mwanasoka Bora Afrika kwa mwaka 2014.
Taaria ya CAF iliyoifikia BIN ZUBEIRY imetoa orodha fupi mbili za wawania tuzo ya Mchezaji Bora wa Afrika kwa ujumla na Mchezaji Bora wa Afrika anayecheza hapa barani.
Wanaowania tuzo ya Mchezaji Bora wa Afrika kwa ujumla ni Ahmed Musa wa Nigeria na klabu ya CSKA Moscow, Asamoah Gyan wa Ghana na Al Ain, Pierre – Emerick Aubameyang wa Gabon na Borussia Dortmund, Vincent Enyeama wa Nigeria na Lille na Yaya Toure wa Ivory Coast na Manchester City, ambaye ndiye anashikilia tuzo hiyo kwa sasa.
 
Kwa upande wa tuzo ya Mwanasoka Bora wa Afrika anayexheza hapa barani walioingia ni Akram Djahnit, El Hedi Belamieri wote wa Algeria na E.S. Setif, Fakhreddine Ben Youssef wa Tunisia na C.S. Sfaxien, Firmin Mubele Ndombe wa DRC na AS Vita na Senzo Robert Meyiwa (marehemu) aliyekuwa akichezea Afrika Kusini na Orlando Pirates.

CHADEMA YASEMA WANANCHI KUCHAGUA VIONGOZI WAADILIFU




Mwenyekiti wa chama cha Demokrasia na maendeleo Mbeya mjini John Mwambigija aliyesimama katikati aliyevaa kofia upande wa kulia ni Samweli Ndoni Mwandishi wa habari wa Highlands fm

 Baadhi ya wananchi waliokuwa wakimsikiliza mwenyekitti huyo kwa wakati akifanya uzinduzi huo



Baadhi ya wananchi wakimshangilia  mwenyekiti huyo wakati wa uzinduzi.


Chama cha demokrasia na maendeleo mkoani mbeya  kimewataka wananchi kuacha  dhana ya kuamini kuwa vyama vyote vya siasa ni viadilifu na vinalengo moja la kuwatumikia  wananchi kulingana na sera ya chama husika.

Hayo yamesemwa na mwenyekiti wa chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) mbeya mjini  John Mwambigija alipokuwa akizungumza na mtandao huu katika uzindua wa kampeni za uchaguzi wa viongozi wa vitongoji, vijiji na mitaa katika kitongoji cha ilongoboto kijiji cha mpandapanda kata ya kiwira wilaya ya rungwe mkoani mbeya.
\
Mwambigija amesema chama cha Chadema kimekuwa na uwezo wa kuwawajibisha viongozi wake wanaokwenda kinyume na sera ya chama, tofauti na vyama vingine vimekuwa vikiwakumbatia viongozi wake ambao si waadilifu.

Aidha Mwambigija amesema dhana ya wananchi kuamini kuwa wanapaswa kuchagu mtu na si chama ni kujinyima haki hao ya mingi. “wananchi wanatakiwa kuchagua chama chenye uwezo wa kuwawajibisha viongozi wake ambao si waadilifu kwakufanya hivyo watakuwa wamepata haki yao ya msingi, mimi nawaambia wananchi wa kijiji cha mpandapanda na Taifa kwa ujumla kama mtachagua viongozi wa vyama vuinavyo wakumbatia viongozi wanaokula kodi yenu kisha wanawakatetea basi mtaendelea kuchangishwa michango isiokuwa na tija kila wakati” alisema Mwambigija.

Hata hivyo Mwambigija amesema chama cha Mapinduzi CCM kimekuwa ni moja kati ya vyama vinavyowakumbatia viongozi wake ambao ni mafisadi ikiwa wanafahamu wazi kuwa viongozi wake wanakula kodi za wananchi pasipo huruma yeyote.

Akitolea mfano wa sakata la fedha shilingi bil. 321 zilizoibiwa katika akaunti ya Tegeta Escrow kwamba viongozi wa CCM ndio wahusika wakubwa lakini jambo la kushangaza tuhuma hizo zimefunikwa funikwa bila majibu sahii hivyo inaonesha kuwa chama hicho kinashindwa kuwawajibisha viongozi wake.

Monday, 1 December 2014

NMB BENKI YA YATOA ZAWADI KWA WASHINDI WA PROMOSHENI YA WEKA NA USHINDE.


Meneja wa NMB Kanda ya Mbeya, Lecrisia Makiriye akimpongeza moja ya washindi walioshinda pikipiki katia pomosheni ya weka na ushinde




Baadhi ya wateja waliobahatika wakishangilia kupata zawadi walizopewa katika promosheni hiyo







Picha ya pamoja
WATANZANIA wametakiwa kuwa na utaratibu wa kuweka fedha zao benki hususani Benki ya NMB kutokana na kuwa na promosheni ya Weka na ushinde ambapo wateja hujishindia Bajaji, Pikipiki na baiskeli.

Wito huo ulitolewa na Meneja wa NMB Kanda ya Mbeya, Lecrisia Makiriye, alipokuwa akizungumza na wateja waliojishindia Bajaji, Pikipiki na Baiskeli kutoka Matawi ya benki hiyo mkoani Mbeya.

Makiriye alisema ni vema watanzania waendelee kuweka fedha kwenye akaunti zao ili washinde kupitia matawi ya NMB zaidi ya 160 yaliyotapakaa nchi nzima kwa kupitia mawakala wa tigo pesa na mpesa pamoja na NMB Mobile kupitia simu za mkononi.

Alisema katika Droo ya nane iliyochezeshwa nchi nzima tayari wameshapatikana washindi 34 wa bajaji, 32 wa pikipiki na washindi wa baiskeli 264 ambapo alitoa wito kwa wateja wengine kuendelea kuweka fedha kwenye akaunti zao.

Alisema kwa Kanda ya Mbeya ina jumla ya washindi 26 ambapo washindi 3 walijipatia Bajaji, washindi watatu wameshindia pikipiki na wateja 20 wamejipatia baiskeli na kuongeza kuwa zimetengwa zaidi ya shilingi Milioni 500.

JENGO LISILOKALIWA NA WATU LAPOROMOKA HUKO ZANZIBAR

 

Askari wa zima moto wakiwa eneo la tukioa baada ya jengo moja kuporomoka mjini Zanzibar jana asubuhi huko maeneo ya Shangani karibu na Kijiwe cha 'Jaws Corner', Jengo hilo lililokuwa wazi bila kukaliwa na watu kwa kipindi kirefu cha takriban miaka 10, halikusababisha kifo wala majeruhi katika ajali hiyo, na chanzo cha kuanguka kwake bado hakijaweza kujulikana kwa haraka.

MHE. ABDULLAH MWINYI ASHEREHESHA MAZOEZI YA TMK JOGGING

 

 Mh. Abdullah Mwinyi (wa pili kulia) akishiriki Jogging na baadhi ya viongozi wa Temeke Jogging Association, wakati alipokuwa mgeni katika mbio hizo zilizofanyika jana asubuhi Mbagala.

 Akishiri mazoezi ya viungo.
 Akifuatilia ratiba zilizokuws zikiendelea mahala hapo baada ya mazoezi.
Sehemu ya vijana washiriki wa Jogging wa kikundi hicho wakimsikiliza mgeni rasmi wakati akizungumza.

TAIFA STARS MABORESHO YAINGIA KAMBINI

KIKOSI cha pili cha timu ya soka ya taifa ya Tanzania, maarufu kama Taifa Stars Maboresho kimeingia kambini leo (Desemba 1 mwaka huu) Bulyanhulu mkoani Shinyanga kujiandaa kwa mechi ya kirafiki dhidi ya Burundi itakayochezwa Desemba 9 mwaka huu jijini Dar es Salaam.
Ikiwa chini ya Kocha Mart Nooij, Stars Maboresho itapiga kambi mkoani humo hadi Desemba 6 mwaka huu ambapo itarejea jijini Dar es Salaam tayari kwa ajili ya mechi hiyo itakayochezwa Uwanja wa Taifa.
Kocha wa Taifa Stars, Mholanzi Mart Nooij

Wachezaji walioingia kambini ni Abubakar Ally (Coastal Union), Abubakar Ally Mohamed (White Bird), Aishi Manula (Azam), Andrew Vicent (Mtibwa Sugar), Atupele Green (Kagera Sugar), Edward Charles (Yanga) na Emmanuel Semwanda (African Lyon).
Gadiel Michael (Azam), Hashim Magoma (Stand United), Hassan Banda (Simba), Hassan Mwasapili (Mbeya City), Joram Mgeveke (Simba), Kassim Mohamed Simbaulanga (African Lyon), Kelvin Friday (Azam) na Makarani Ally (Mtibwa Sugar).
Miraji Adam (Simba), Mohamed Hussein (Simba), Muzamir Ally (Mtibwa Sugar), Omari Nyenje (Ndanda), Pato Ngonyani (Yanga), Rashid Mandawa (Kagera Sugar), Said Hamisi (Simba), Salim Hassan Mbonde (Mtibwa Sugar) na Shiza Ramadhan (Mtibwa Sugar).
Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) linaishukuru kampuni ya kuchimba madini ya Acacia Mining PLC (zamani African Barrick Gold PLC) kwa kufadhili kambi ya Stars kupitia mgodi wa Bulyanhulu