MATUKIO KATIKA PICHA YALIYO WEZA KUVUTIA DUNIANI KOTE

Asante kwa kututembelea mbeyagreennews kwa taarifa zaidi endelelea kututembela kila siku ,saa,dakika usipitwe na matukio kem kemu

MATUKIO KATIKA PICHA YALIYO WEZA KUVUTIA DUNIANI KOTE

Asante kwa kututembelea mbeyagreennews kwa taarifa zaidi endelelea kututembela kila siku ,saa,dakika usipitwe na matukio kem kemu

MATUKIO KATIKA PICHA YALIYO WEZA KUVUTIA DUNIANI KOTE

Asante kwa kututembelea mbeyagreennews kwa taarifa zaidi endelelea kututembela kila siku ,saa,dakika usipitwe na matukio kem kemu

MATUKIO KATIKA PICHA YALIYO WEZA KUVUTIA DUNIANI KOTE

Asante kwa kututembelea mbeyagreennews kwa taarifa zaidi endelelea kututembela kila siku ,saa,dakika usipitwe na matukio kem kemu

MATUKIO KATIKA PICHA YALIYO WEZA KUVUTIA DUNIANI KOTE

Asante kwa kututembelea mbeyagreennews kwa taarifa zaidi endelelea kututembela kila siku ,saa,dakika usipitwe na matukio kem kemu

Sunday, 18 May 2014

MBEYA YATAHADHARISHWA KUHUSU UGONJWA WA DENGUE


 
 

WATEJA WA TANESCO WALIA NA MITA MPYA ZA LUKU, ZATHIBITIKA HAZINA UBORA. NI NCHI YA KITU KIDOGO!


Waziri wa Nishati na madini Mh Sospeter Muhongo.
* Wawafungia wateja mita zinazokata umeme kila baada ya dakika tano kuanzia saa moja na dakika 34 usiku.

* Mteja hawezi kuweka namba kupitia mita husika, anapatiwa kifaa kingine kilichoandoka Inhemeter customer interface unit. Model CIU(PDHO).

* Kina VOT 230V. 2013, kinatumia betri za Nne za gharama na umeme.

 * Mita ni MOdel DDZ.

* mafundi wa dharula wathibitisha kuwa hazina ubora.

* Wakutana na kikosi kazi cha kalulunga Media eneo la CCM Ilomba Jijini Mbeya, usiku wa saa 2 na dakika 23, wakiwa na gari lenye namba za usajili SM 37781.

* Wasema zimetengenezwa India, hazifai na usiku huo walipata malalamiko ya wateja wawili. 
Habari na kalulunga media

KIKWETE AMFARIJI JAJI WARIOBA KWA KUFIWA NA MKWE WAKE

 
w1
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiweka saini katika kitabu cha kumbukumbu alipokwenda kuhani msiba wa mama mkwe wa Waziri Mkuu Mstaafu Jaji Joseph Sinde Warioba, Marehemu Hedwig Laurent Ojjik, Oysterbay jijini Dar es salaam   Mei 17, 2014.
w2
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa mama mkwe wa Waziri Mkuu Mstaafu Jaji Joseph Sinde Warioba, Marehemu Hedwig Laurent Ojjik, Oysterbay jijini Dar es salaam 
w3
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akifariji wanafamilia bada ya kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa mama mkwe  wa Waziri Mkuu Mstaafu Jaji Joseph Sinde Warioba, Marehemu Hedwig Laurent Ojjik,  Oysterbay jijini Dar es salaam .
w4
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma Kikwete wakiwa na Jaji Joseph Warioba na mkewe Mama Evelyne Warioba walipokwenda kuhani na kutoa heshima za mwisho katika msiba wa mama mkwe wa Waziri Mkuu Mstaafu Jaji Joseph Sinde Warioba, Marehemu Hedwig Laurent Ojjik,   Oysterbay jijini Dar es salaam 
w5
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimfariji Mama Evelyne Warioba  alipokwenda kuhani msiba wa mama yake mzazi Marehemu Hedwig Laurent Ojjik  Oysterbay jijini Dar es salaam  (Picha na IKULU).
W6

KIONGOZI WA UPINZANI AKAMATWA SUDANI

 
kiongozi wa upinzani nchini Sudan Sadiq Al Mahdi

Kiongozi wa upinzani nchini Sudan Sadiq al Mahdi amekamatwa kutokana na madai ya kuchochea chuki dhidi ya serikali.
Bwana Al Mahdi, kiongozi wa chama cha Umma na ambaye aliwahi kuhudumu kama waziri mkuu katika serikali ya kidemokrasia ya Sudan alikamatwa baada ya kuzikosoa sera za serikali katika jimbo la Darfur na kuvishtumu vikosi vya Sudan kwa ukiukaji mkubwa wa haki za binaadamu mbali na kutekeleza ubakaji katika eneo hilo.
Chama chake tayari kimevunja mazungumzo na serikali ya kutaka kubuni serikali ya muungano ili kumaliza mgogoro unaokumba uchumi wa taifa hilo huku kikiwataka wafuasi wake kuandamana.
Jimbo la Darfur limeshuhudia miaka kumi ya umwagaji damu na rais wa Sudan Omar el Bashir anasakwa na mahakama ya kimataifa ya ICC kwa shtaka la uhalifu wa kivita. CHANZO BBC

GUINEA BISSAU YAFANYA UCHAGUZI WA PILI

 
Wagombea wafanya kampeni nchini Guinea Bussau kabla ya uchaguzi wa awamu ya pili.

Taifa la Magharibi mwa Afrika ,Guinea Bissau linafanya awamu ya pili ya uchaguzi wa urais hii leo.
Aliyekuwa waziri wa maswala ya kigeni Jose Mario Vaz alipata kura nyingi katika raundi ya kwanza ya uchaguzi huo lakini akashindwa kupata kiwango cha kura zinazohitaji ili kuibuka mshindi.
Hatahivyo anakabiliwa na upinzani mkali kutoka kwa Nuno Gomez Nabiam ambaye waandishi wanasema anaungwa mkono na jeshi.
Jeshi nchini humo lilifutilia mbali uchaguzi wa kidemokrasi mnamo mwaka 2012 na taifa hilo limekuwa na rekodi ya mapinduzi ya kijeshi.
Hakuna kiongozi aliyechaguliwa na raia ambaye amemaliza kipindi chake cha miaka mitano tangu taifa hilo lijipatie uhuru wake kutoka kwa Ureno miaka 40 iliopita.

WATU 70 WAUAWA KATIKA VITA NCHINI LIBYA

 
Mwanamgambo nchini Libya
Maafisa nchini Libya wanasema kuwa idadi ya watu waliofariki katika vita mjini Benghazi imeongezeka na kufikia zaidi ya 70.
Jeshi limetangaza kwamba hakuna ndege itakayoruhusiwa kupaa juu ya mji huo huku spika wa bunge akisema kuwa mtu anayeongoza vita hivyo Khalifa Haftar anajaribu kufanya mapinduzi.
Bwana Haftar amesema kuwa ataendelea na kampeni yake ya kuwaondoa wale aliowataja kama magaidi nje ya mji wa Benghazi huku akiongezea kuwa anaungwa mkono na raia wengi wa mji huo ambao ni wa pili kwa ukubwa nchini Libya.
Hatahivyo familia nyingi zinahamia magharibi mwa mji huo kufuatia vita vikali kati ya vikosi vya Haftar na wanamgambo. CHANZO BBC SWAHILI

RAIA WA UCHINA WAJERUHIWA NCHINI VIETINAM

 
Shirika rasmi la habari nchini Uchina Xhinua limesema kuwa serikali imewaondoa zaidi ya raia wake 3000 kutoka nchini Vietnam kufuatia ghasia dhidi raia wa Uchina nchini humo.
Wafanyikazi wawili wa Uchina wameuawa kufuatia ghasia hizo zilizosababishwa na hatua ya Uchina kupeleka meli yake ya kuchimba mafuta katika eneo linalozozaniwa kusini mwa bahari ya Uchina.
Mapema hii leo takriban raia 16 wa Uchina waliojeruhiwa vibaya waliondoshwa nchini humo kupitia usafiri wa ndege maalum.
Serikali mjini Beijing inaandaa safari nyingine za ndege huku naibu waziri wa maswala ya kigeni Liu Jianchao akizuru Vietnam kwa mazungunmzo na mamlaka.
Aidha waziri huyo amewatembelea baadhi ya raia wa Uchina waliojeruhiwa hospitalini.
Wanaharakati nchini Vietnam wameitisha maandamano zaidi dhidi ya raia wa Uchina hii leo licha ya mwito wa serikali wa kutaka kusitishwa kwa maandamano hayo

HONGERA ZAKO DIAMOND KWA KUTTEULIWA KUWANIA TUZO ZA BET

 
Nyota ya Tanzania katika sanaa imepata mwangaza na msukumo mpya baada ya msanii wake mahiri, Naseeb Abdul au Diamond kuteuliwa kuwania tuzo maarufu za BET zitakazofanyika baadaye mwaka huu kule Marekani.
Tuzo hizo ambazo zilianza rasmi 2001, zinalenga katika kuwaunganisha wasanii wote wenye asili ya Afrika nchini Marekani na tangu kuanzishwa kwake zimekuwa zikiwashirikisha wasanii mbalimbali kutoka sehemu nyingi duniani ikiwamo nchi za Afrika
Uteuzi huu wa Diamond ambaye anashiriki kwa mara ya kwanza ni sifa kwa Tanzania na pia ukanda wa Afrika Mashariki kwa jumla.
Tunapenda kumpongeza msanii huyu kijana ambaye mwezi huu pia ametwaa tuzo saba kwenye tuzo za Kilimanjaro, jambo ambalo linaifanya nchi yetu kuingiza mshindani halisi.
Hata hivyo, Diamond ambaye anashiriki pia tuzo za MTV pamoja na zile za Kora, anachuana na wakali wengine kutoka barani Afrika kama vile, Mafikizolo (Afrika Kusini), Davido, Tiwa Savage (Nigeria) na wasanii wengine kadhaa kutoka Ghana na Togo.
Tunatambua kuwa huu ni mtihani mkubwa si kwake kama Diamond, bali kwa Tanzania na Afrika Mashariki kwa jumla, lakini tunatambua kuwa ushindi wake unamtegemea kila mmoja wetu.
Hata hivyo, imekuwa ni kama bahati mbaya kwetu sisi Watanzania kwani hatuna utamaduni wa kuwapigia kura washiriki wetu kwenye matukio mbalimbali ya kimataifa, jambo ambalo hatuna budi kulibadili sasa ili kumwezesha Diamond awe mshindi. Tumeona, huko nyuma kwa mfano kwenye shindano la Big Brother Africa, tuzo za filamu bora ya Kiafrika kwa Kiswahili zilizofanyika Nigeria mwaka huu ambako wasanii wetu waliangushwa si kwa kukosa sifa, vigezo bali kwa kukosa kura.
Hivyo, tunasema wakati ukifika, kushiriki kwetu na kupiga kura zetu kwa njia ya mtandao, bila shaka tutakuwa tumemwezesha kijana wetu huyu kushiriki, kushindana na pengine kufanya vizuri mwaka huu kwenye tuzo hizo.
Tuna imani kwamba vijana ambao ni wengi na ambao siku hizi wanaishi kwenye mitandao ya kijamii bila shaka watakuwa mabalozi wazuri wa kumwezesha Diamond kuwa mshindi na pia balozi mzuri wa nchi yetu huko Marekani.
Tunadhani, Wizara ya Habari, Utamaduni, Vijana na Michezo na hata balozi zetu zilizoko nje pia zitashiriki katika kuhakikisha kuwa Diamond anaibuka mshindi kwani hakuna kisichowezekana chini ya jua na washindi siku zote hutengenezwa.
Inawezekana hata sisi kumtengeneza mshindi etu, ambaye ni Diamond kwani yeye ndiye pekee kutoka Tanzania, ingawa ukanda wa Afrika Mashariki unaye pia Lupita Nyong'o kutoka Kenya ambaye mapema mwaka huu alishinda tuzo za Oscars kwenye uigizaji.
Tunapenda kutoa ushauri kwa wasanii wengine wa fani mbalimbali waige kutoka kwenye mafanikio ya mwenzao huyu na kuamini kuwa inawezekana kuwa mshindi, hasa kwa kufanya kazi kwa nidhamu, kujiamini na kujituma..

MAKALA HII IMEANDKWA NA(Martha Magessa)

Saturday, 17 May 2014

BALOTELLI AVAMIWA NA KUAKUIBA GARI NA MAZAGAZAGA KIBAO

WEZI wameiba gari la Mario Balotelli aina ya Porsche pamoja na dhahabu na saa baada ya kuingia kwenye nyumba ya mshambuliaji huyo wa Italia na AC Milan. 

Balotelli alitoka kwa chakula cha usiku pamoja na kaka yake, Enoch na aliporejea nyumbani kwake eneo la Limido Comasco akakuta masela wamefanya yao. Hata hivyo, gari hilo lilipatikana baadaye likiwa limetelekezwa. 
Balotelli aliandika Jumamosi kwenye ukurasa wake wa Twitter: "Najisikia mtupu! Hakuna hasira... Lakini wakati wore napambana kwa ajili ya watu wachache wanaonipenda. Wanastahili hii,". 
Wiki mbaya: Balotelli alimuangusha chini mwizi aliyekuwa anajaribu kumpora simu

Tukio hilo lilitokea muds mfupi baada ya Balotelli kumuangusha chini mwizi aliyekuwa anataka kumpora simu née ya klabu ya usiku.
Pamoja na hayo, Balotelli alipata habari nzuri wiki hii baada ya kutajwa katika kikosi cha awali cha wachezaji 30 wa Italia kwa ajili ya Kombe la Dunia kilichotajwa na kocha Cesare Prandelli. 
The Azzurri itaanza kampeni yake katika Kundi D dhidi ya England mjini Manaus Juni 14, kabla ya kucheza na Uruguay na Costa Rica.

WANANCHI MBOZI WALALAMIKIA UCHELEWESHAJI WA KESI

 
mdau_83a94.jpg
Mmoja wa wadau wa mahakama katika Wilaya ya Mbozi, mkoani Mbeya, Brighton Simwinga (kushoto) akibainisha baadhi ya changamoto zinazoikabili idara ya mahakama wilayani humo ikiwa ni pamoja na ucheleweshwaji wa kesi kunakopelekea wananchi wengi kukosa haki (Justice delayed is justice denied) wakati wa mahojiano maalum na mwandishi wa habari na mtangazaji wa KwanzaJamii Redio, Sagini Edward Majura hivi karibuni. Hata hivyo mdau huyo alipendekeza kuwepo na chombo cha usimamizi wa mahakama ngazi ya wilaya kama vile Baraza la Wazee cha kuwabana mahakimu wanapokosea kutenda haki kwa wananchi.(PICHA NA FRIDAY SIMBAYA)

HOT NEWS; KOCHA BARCA ABWAGA MANYANGA BAADA YA KUKOSA UBINGWA SIKU YA MWISHO

KOCHA Gerardo Martino amesema anaondoa Barcelona baada ya kumaliza msimu wake wa kwanza kazini vibaya akikosa ubingwa wa Ligi Kuu ya Hispania katika sikh ya mwisho. 

Kocha huyo Muargentina amefikia makubaliano ya kuacha kazi baada ya Barcelona kulazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na mabingwa wapya, Atletico Madrid usiku huu. 
Martino aliteuliwa kuifundisha Barca msimu huu ili kuendeleza wimbi la mafanikio Barcelona lililoanzishwa na Pep Guardiola mwaka 2008.  
Anaondoka: Gerardo Martino anaondoka Barcelona baada ya msimu mmoja tu kazini

Lakini Barcelona imemaliza msimu bila taji lolote kwa mara ya kwanza tangu msimu wa 2007-08. 
Mchezaji wa zamani wa Barcelona, Luis Enrique anatarajiwa kuchukua nafasi ya Martino, ambaye anaondoka akiwa amebakiza mwaka mmoja katika mkataba wake. 
Enrique anaachia ngazi ukocha wa Celta Vigo baada ya kukutana na Barcelona wiki iliyopita.

BAADA YA KUINUA KOMBE LA FA WENGER ASEMA ANABAKI ARSENAL

KOCHA wa Arsenal, Arsene Wenger ameamua kubaki katika klabu hiyo baada ya kuiongoza Gunners kumaliza ukame wa miaka tisa wa mataji kufuatia kuilaza Hull City mabao 3-2 na kutwaa Kombe la FA usiku huu Uwanja wa Wembley.

Hull iliwavunja nguvu mashabiki wa Gunners kwa mabao mawili ya haraka ya kuongoza ndani ya dakika nane, lakini timu ya Wenger ikazinduka na kusawazisha yote kabla ya Aaron Ramsey kufunga la kuongeza ndani ya dakika 30 za nyongeza.
Wenger amesema kwamba matokeo hayo ya Wembley hapaa shaka yanamfanya ajisikie faraja kubakia Emirates na amethibitisha haondoki. 

Raha imerejea: Lukas Podolski akimwagia bia Wenger baada ya kutwaa Kombe la FA

"Wakati wore nimesema mustakabali wangu hautegemei hili, lakini wakati wore nimesema nilitaka kubaki," alisema Wenger alipoulizwa na ITV kama atabaki, kabla ya kusema , "Ndiyo, nitabaki.'
"Tulitaka kuweka historia usiku huu na kushinda mechi na tumefanya hivyo, hizo ni namna zote - namna ya kuianza fainali ya Kombe na namna ya kuzinduka," alisema Wenger.
Silver service: Wenger lifts the FA Cup much to the delight of his Arsenal players
Furaha tupu: Wenger akiinua Kombe la FA kusherehekea na wachezaji wake
Match winner: Aaron Ramsey scored the crucial goal which saw Arsenal win the FA Cup
Mshindi wa mechi: Aaron Ramsey alifunga bao la ushindi na hapa anasherehekea na Kombe la FA

BAYERN MUNICH WAMFUNGA BORUSSIA DORTMOND NAKUBEBA 'NDOO' YA PILI UJERUMANI

MABAO ya Arjen Robben na Thomas Mueller katika dakika za nyongeza baada ya dakika 90 za kawaida, yametosha kuipa Bayern Munich ushindi wa 2-0 dhidi ya Borussia Dortmund na kutwaa Kombe la Ujerumani usiku huu, hilo likiwa taji la pili kwa timu hiyo katika msimu wa kwanza wa kocha Pep Guardiola kazini.
Robben alifunga dakika ya 107 baada ya kuunganisha krosi ya Jerome Boateng aliyemtoka Roman Weidenfellert kabla ya Mueller kumzunguka Weidenfeller kufunga la pili dakika za majeruhi.
Robert Lewandowksi aliichezea Dortmund mechi yake ya mwisho kabla ya kuhamia Bayern Munich Julai 1, mwaka huu na usiku huu aliwekewa ulinzi mkali na Boateng na Dante.
Kifaa; Arjen Robben akisherehekea baada ya kufunga bao la kwanzaClinical: Arjen Robben scores Bayern Munich's first goal against Borussia Dortmund
Kitaalamu: Arjen Robben akiifungia Bayern Munich bao la kwanza dhidi ya Borussia Dortmund