MATUKIO KATIKA PICHA YALIYO WEZA KUVUTIA DUNIANI KOTE

Asante kwa kututembelea mbeyagreennews kwa taarifa zaidi endelelea kututembela kila siku ,saa,dakika usipitwe na matukio kem kemu

MATUKIO KATIKA PICHA YALIYO WEZA KUVUTIA DUNIANI KOTE

Asante kwa kututembelea mbeyagreennews kwa taarifa zaidi endelelea kututembela kila siku ,saa,dakika usipitwe na matukio kem kemu

MATUKIO KATIKA PICHA YALIYO WEZA KUVUTIA DUNIANI KOTE

Asante kwa kututembelea mbeyagreennews kwa taarifa zaidi endelelea kututembela kila siku ,saa,dakika usipitwe na matukio kem kemu

MATUKIO KATIKA PICHA YALIYO WEZA KUVUTIA DUNIANI KOTE

Asante kwa kututembelea mbeyagreennews kwa taarifa zaidi endelelea kututembela kila siku ,saa,dakika usipitwe na matukio kem kemu

MATUKIO KATIKA PICHA YALIYO WEZA KUVUTIA DUNIANI KOTE

Asante kwa kututembelea mbeyagreennews kwa taarifa zaidi endelelea kututembela kila siku ,saa,dakika usipitwe na matukio kem kemu

Thursday, 24 April 2014

VIKOSI VYA ULINZI NA USALAMA VYAENDELEA NA MAZOEZI KWA AJILI YA MAADHIMISHO YA MUUNGANO

Vikosi vua ulinzi na usalama vikiwa katika mazoezi makali kwenye uwanja wa Uhuru leo kwa ajili ya maadhimisho ya miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania  ulioasisiwa na Baba wa Taifa Mwalimu Julius K. Nyerere na Mzee Abeid Amani Karume waliounganisha Tanganyika na Zanzibar mwaka 1964 na kuwa Tanzania huru , Sherehe hizo zitaadhimishwa Aprili 26 mwaka huu kwenye uwanja wa Uhuru Mgeni rasmi akiwa Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dr. Jakaya Mrisho Kikwete.  2Katibu Mkuu Kiongoziwa Tano kutoka kulia ni Naibu Katibu Mkuu Kiongozi Dr. Frolence Turuka wa nne kutoka kulia na maafisa mbalimbali wa majeshi ya ulinzi na usalama wakijumuika pamoja kushuhudia mazoezi hayo ya vikosi vya ulinzi na usalama kwenye uwanja wa Uhuru leo. 4 
Mazoezi ya vikosi hivyo yakiendelea. 6 
Kikosi cha Askari wa msituni kikifanya mazoezi ya kutoa heshima kwa Amiri jeshi mkuu. 7 
Kikosi cha makomandoo kikitoa heshima8 
21

RAIS JAKAYA KIKWETE AWEKA JIWE LA MSINGI UJENZI WA TERMINAL 3 UWANJA WA NDEGE WA KIMATAIFA J.K.NYERERE

23 
 Rais Jakaya Kikwete akikata utepe huku Balozi wa Uholanzi hapa nchini Mhe Jaap Frederiks na Waziri wa Uchukuzi Dr. Harrison Mwakyembe wakiwa wameshikilia utepe huo wakati wa uzinduzi wa mradi mkubwa wa upanuzi wa Uwanja mkubwa wa ndege wa J.K.Nyerere Terminal 3 utakaoweza kuhudumia abiria milioni 7.500.000 kwa mwaka, Ujenzi huo umefadhiliwa na serikali ya Uholanzi na unatarajiwa kukamilika mwezi oktoba mwaka huu, kutoka kulia ni Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya bunge Miundo mbinu Peter Serukamba, Makamu Mwenyekiti wa kamati hiyo Profesa Juma Kapuya na Mkurugenzi wa Mamlaka ya viwanja vya Ndege Injinia Suleiman Suleiman na kutoka kushoto ni Didas Masaburi Meya wa jiji la Dar es salaam, Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Meck Sadik na Naibu waziri wa Uchukuzi Mh. Dr. Charles Tizeba (PICHA NA   FULLSHANGWE-DAR ES SALAAM) 24 
Rais Jakaya Kikwete na  Balozi wa Uholanzi hapa nchini Mhe Jaap Frederiks wakifunua pazia huku  Waziri wa Uchukuzi Dr. Harrison Mwakyembe katikati na viongozi wengine wakipiga makofi wakati wa uzinduzi wa ujenzi wa uwanjahuo   25 
Rais Jakaya Kikwete akisalimiana na viongozi mbalimbali huku akiwa ameongozana na   Balozi wa Uholanzi hapa nchini Mhe Jaap Frederiks 26 
Waziri wa Uchukuzi Dr. Harrison Mwakyembe  akisalimiana na baadhi ya viongozi baada ya kuwasili katika uzinduzi huo kulia ni Mkurugenzi wa Mamlaka ya viwanja vya ndege Injini Suleiman Suleiman. 27 
 Waziri wa Uchukuzi Dr. Harrison Mwakyembe akisalimiana na Mkurugenzi wa Mamlaka ya viwanja vya ndege Injini Suleiman Suleiman mara baada ya kuwasili katika uzinduzi  . 28Mwenyekiti wa kamati ya kudumu  bunge Miundo mbinu Peter Serukamba akizungumza na Naibu Waziri wa Uchukuzi Dr. Charles Tizeba huku  Makamu Mwenyekiti wa kamati hiyo Profesa Juma Kapuya akiwasilkiliza, kulia ni  na Mkurugenzi wa Mamlaka ya viwanja vya Ndege Injinia Suleiman Suleiman na  kushoto ni  Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Silaa. 29 
Wafanya kazi wa kampuni zinazojenga uwanja huo wakiserebuka na muziki wa Msondo 30 
Baadhi ya wafanyakazi mbalimbali wa uwanja wa ndege wakiwa katika hafla hiyo ya uzinduzi. 31 
Wananchi wamejitokeza kwa wingi katika uzinduzi huo. 32Mwanamuziki Diamond Platnum akifanya vitu vyake katika uzinduzi huo. 35 
Naibu Waziri wa Uchukuzi Dr. Charles Tizeba akizungumza na Mkurugenzi wa Mamlaka ya viwanja vya Ndege Injinia Suleiman Suleiman na mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Meck Sadik 36 
Baadhi ya wafanyakazi wa Mamlaka ya viwanja vya Ndege wakiwa katika hafla hiyo. 37Mkurugenzi wa Mamlaka ya viwanja vya Ndege Injinia Suleiman Suleiman akizungumza katika uzinduzi huo 39 
Rais Jakaya Kikwete akizungumza na wananchi wakati wa uzinduzi huo 40 
Rais Jakaya Kikwete akipata maelezo ya ujenzi wa uwanja huo kutoka kwa Mkurugenzi wa Mamlaka ya viwanja vya Ndege Injinia Suleiman Suleiman 42Mkurugenzi wa Mamlaka ya viwanja vya Ndege Injinia Suleiman Suleiman akitoa maelezo kwa Rais Jakaya Kikwete 43 
Rais Jakaya Kikwete akipiga picha ya pamoja na viongozi mbalimbali waliohudhuria katika uzinduzi huo. 44 45 
Rais Jakaya Kikwete akiagana na Mkurugenzi wa Mamlaka ya viwanja vya Ndege Injinia Suleiman Suleiman mara baada uzinduzi huo.

Saturday, 19 April 2014

KIGOGO TANESCO ASHTAKIWA KWA KUISABABISHIA SERIKALI HASARA YA MIL. 200/=


tanescologo_e4d1c.jpg
Aliyekuwa Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), Robert Semtutu na wenzake wanne, wamefikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kujibu mashitaka mawili yakiwamo ya kuisababishia serikali hasara ya zaidi ya Sh. milioni 200.
Washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni aliyekuwa Afisa Ugavi wa Tanesco, Hanin Mahambo, Mkurugenzi wa Fedha, Lusekeo Kasanga, Mwanasheria Godson Ezekiel na Mkandarasi Martin Abraham.
Mwendesha Mashtaka wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Isdore Kyando alidai kuwa washtakiwa walifanya makosa hayo katika tarehe tofauti mwaka 2011.
Kyando alidai kuwa katika shitaka la kwanza, Desemba, mwaka 2011 katika ofisi za Tanesco Ubungo jijini Dar es Salaam washtakiwa walitumia madaraka yao vibaya kwa kufanikisha malipo kwa msambazaji M/S Young Dong Electronic Co Ltd bila kuhakikisha Mkandarasi anafika katika kituo cha mwisho.
CHANZO: NIPASHE

MECHI YA 77 SIMBA NA YANGA LIGI KUU TANGU 1965

Yanga_65a60.jpg
Picha kwa hisani ya sw-ke.facebook.com
Na Daniel Mbega
"KITIMTIMU, mtakiona leo, nyumba ya shetani mwendawazimu kaingiaje!" Naam, hilo ni chagizo la wimbo maarufu wa mashabiki wa Yanga kila wanapoishangilia timu yao, hasa inapocheza na Simba.
Lakini chagizo hilo litakumbana na kibwagizo cha mashabiki wa Simba, maarufu kama Mchacho Group (ambao sasa wameongezewa sapoti na tawi la Mpira Fedha) watakaokuwa wakiimba "Amesimama kidedea, eeee kidedea!"
Timu hizo mbili zinapopambana katika mechi ya Jumamosi hii Aprili 19, kukunja jamvi la Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara kwa msimu wa 2013/2014, kila mtu anatazama nini kitatokea, iwe uwanjani ama nje ya uwanja.
Mechi baina ya timu hizi mbili kongwe katiba katika historia ya kandanda nchini huwa zinatawaliwa na vituko vingi mno. Kuvunja nazi, kuoga maji ya maiti, kuruka ukuta, kuingia uwanjani kinyumenyume na mengine kama hayo hutajwa kwamba ni sehemu ya kuhanikiza ushindani.
Hata hivyo, kwa sasa hawawezi kuruka ukuta kama ilivyokuwa miaka ile ya zamani, wala hawawezi kuoga maji ya kuoshea maiti au kuvunja nazi hadharani, kwa sababu Sheria za Soka haziruhusu ushirikina na tayari timu hizo mbili zimekwishawahi kutozwa faini kwa vitendo hivyo.
Simba ikiwa inatokea Zanzibar, na Yanga ambayo ilikuwa Kawe jijini Dar es Salaam, zinapambana Jumamosi hii zikitaka kulinda heshima tu, kwa sababu ubingwa tayari umekwishachukuliwa na Azam FC iliyofikisha pointi 59 ambazo haziwezi kufikiwa na timu nyingine.
Ushindi wa Azam wa mabao 2-1 nyumbani kwa Mbeya City Jumapili iliyopita uliifanya iweke rekodi mpya kwa kuwa timu ya nane katika historia ya soka nchini kunyakua ubingwa huo ambao umekuwa ukitwaliwa na Simba na Yanga pekee. Mara ya mwisho kwa timu nyingine kutwaa ubingwa (mbali ya Simba na Yanga) ilikuwa mwaka 2000 wakati Mtibwa Sugar ilipotwaa kwa mara ya pili mfululizo ubingwa huo wa Bara.
Lakini pia ushindi wa Azam ulivunja rekodi ya kutofungwa ya Mbeya City kwenye uwanja wake wa nyumbani katika msimu huu, huku Azam ikiendelea kushikilia rekodi yake nyingine ya kutopoteza hata mechi moja katika msimu huu. Sijui leo hii hali itakuwaje.
Yanga yenyewe imeshika nafasi ya pili kwa ushindi wa mabao 2-1 ilioupata kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha dhidi ya JKT Oljoro na sasa inahitaji vitu viwili tu – kulipa kisasi cha kufungwa mabao 5-0 msimu wa 2011/2012 pamoja na kulinda hadhi yake, huku Simba ikitaka kuendeleza ubabe kwa vijana hao wa Jangwani kwa kuwa hakuna itakachopoteza katika nafasi yake ya nne iliyoifikia.
Lakini kwa upande mwingine ushindi ni muhimu sana kwa Simba ikiwa inataka kulinda hadhi yake japo kwa kumaliza ikiwa ya nne, kwa sababu ikiwa itapoteza mchezo huo, basi inaweza kujikuta ikimaliza ikiwa ya sita msimu huu. Hii ni kwa sababu mpaka sasa ina pointi 37 wakati nyuma yake kuna timu mbili za Kagera Sugar na Ruvu Shooting ambazo zina pointi 35 kila moja.
Kagera Sugar inayoshika nafsi ya tano ikishinda ugenini kwa Coastal Union na Ruvu Shooting ikiwalazama maafande wa Rhino Rangers ambao tayari wamekwishashuka daraja, zinaweza kuipiku Simba kimzaha mzaha tu.
Kelele za: "Simba! Simba! Simba!" na zile za: "CCM! CCM! CCM!" zitasikika kwenye Uwanja wa Taifa, lakini zitahitaji kuangalia matokeo ya uwanjani yakoje, vinginevyo upande mmoja unaweza kuzizima.
Hapo hakuna ugomvi, ni burudani ya jukwaani huku mashabiki wakiendelea kutazama buradani nyingine ndani ya uwanja wakati vijana walio katika jezi nyeupe na nyekundu wakipelekeshana puta na wenzao walio kwenye jezi za kijani na manjano.
Mandhari haya ndiyo yaliyokuwepo Jumapili Oktoba 20, 2013 kwenye Uwanja Mkuu wa Taifa, wakati Simba na Yanga zilipoumana katika mchezo wa kwanza wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu wa 2013/2014.
Wakati Yanga, ambayo ilikuwa inatetea ubingwa wake huku ilikiwa katika nafasi mbaya kwenye msimamo, ilikuwa inatafuta ushindi ili kukwea kileleni lakini pia kulipa kisasi cha mabao 5-0 ilichokipata mwaka 2012 katika mchezo wa mwisho. Jambo hili lilionekana kuwa ni ndoto baada ya kushindwa kuyalinda mabao yake matatu iliyoyapata katika kipindi cha kwanza, hivyo kuifanya Simba isawazishe na kuleta matokeo ya ajabu ya sare ya 3-3.
Simba wao walikuwa na mambo mawili: Kwanza, walitaka kulipa kisasi cha kufungwa katika mchezo wa mwisho wa Ligi Kuu Mei 17, 2013, lakini pili, walikuwa wanatafuta ushindi ili kujiweka sawa zaidi na kutwaa ubingwa baada ya kukosa hata nafasi ya pili.
Kama wachezaji wa timu hizo watatulia na kutandaza soka, huku wakiacha ubabe na kufuatisha kelele za mashabiki jukwaani, hakika hii itakuwa burudani safi ya kufungia msimu.
Mechi zao
Hii itakuwa mechi ya 77 kuzikutanisha Simba na Yanga kwenye Ligi Kuu tangu mwaka 1965 ilipoanzishwa Ligi ya Taifa na aliyekuwa kocha wa Taifa Stars, Milan Celebic.
Katika kipindi chote hicho, msisimko wa kuelekeza mechi hizi umekuwa mkubwa, bila kujali nani anawania kitu gani.
Hata hivyo, katika mechi 76 zilizopita, Watanzania wameshuhudia Yanga ikitawala zaidi kwa kushinda mara 29, wakati Simba imeshinda mara 22. Timu hizo zimetoka sare mara 25 huku mabao 162 yakifungwa. Kati ya mabao hayo, Yanga imefunga 86 na Simba imefunga 75. Ikumbukwe kwamba, mechi hizi hazihusishi mechi za Ligi ya Muungano.
MECHI YA 77 SIMBA NA YANGA LIGI KUU TANGU 1965

ZAIDI YA WASICHANA 14 WAWATOROKA BOKO HARAM

 
140307165520_nigeria_military_640x360_bbc_nocredit_7c518.jpg
Kamishna wa elimu katika jimbo la Borno nchini Nigeria amesema kuwa wasichana 14 zaidi wamefanikiwa kutoroka katika mikono ya wanamgambo wa kiislamu waliowatekanyara Jumatatu usiku.
Musa Inuwo Kubo, amesema wasichana 44 sasa wamewatoroka watekaji hao na kwamba wasichana wengine 85 hawajulikani walipo
Vikosi vya Usalama,makundi ya vijana wa kuweka usalama mitaani pamoja na familia za wasichana hao wanaendelea kuwatafuta.
Wasichana hao wanaaminika kutekwanyara na kundi la wanamgambo wa kiislamu wa Boko Haram.
Mwandishi wa BBC nchini Nigeria amesema kuwa wasichana wamekuwa wakitekwanyara na kundi hilo lakini sio katika kiwango kama cha sasa.
Amesema kuwa wapiganaji hao wanapinga kuwepo kwa elimu ya kidunia na kwamba wanataka kuanzisha serikali ya kiislamu.CHANZO BBC

KIINGILIO CHA CHINI YANGA vs SIMBA NI 7,000/-


944155_584386034916133_328594498_n_4c470.jpg
VS
images_c523e.jpg

Taarifa yetu tuliyotuma hivi punde ilionesha kiingilio cha chini mechi ya Yanga na Simba ni sh. 5,000. Usahihi ni kuwa kiingilio hicho ni sh. 7,000 kama kinavyooneshwa kwenye tiketi.
Boniface Wambura
Ofisa Habari na Mawasiliano

SITTA AHAHA KULINUSURU BUNGE MAALUMU LA KATIBA


Mwenyekiti wa Bunge Maalumu la Katiba, Samuel Sitta anahaha kulinusuru Bunge hilo, baada ya wajumbe ambao ni wanachama wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) kususia vikao vinavyoendelea mjini Dodoma.
Habari ambazo zimelifikia gazeti hili zilisema Sitta anawasaka viongozi wa Ukawa kwa lengo la kukaa nao katika meza ya mazungumzo, kutafuta maridhiano yatakayowezesha kundi hilo kurejea bungeni.
Sitta jana aliliambia Mwananchi kuwa wako njiapanda, kwa sababu hawafahamu kama wajumbe hao wa Ukawa wametoka tu nje ya ukumbi na watarudi au wamejiuzulu.  

"Hapa ninapozungumza na wewe nimesitisha kwenda mapumziko ya Pasaka... Nimewapigia simu Lipumba (Ibrahim) na Mbowe (Freeman), lakini hawapokei simu," alisema Sitta na kuongeza;
"Niliyempata ni Mbatia (James) peke yake na ameniambia yeye yuko na wenzake na hana uamuzi wa pamoja...Nataka nikutane nao ana kwa ana nasubiri kama inawezekana tufanye mazungumzo."
Aliongeza: "Nasubiri hata kama watatuma mwakilishi wao tukae tuzungumze hili jambo, lakini mpaka sasa sijaona mwakilishi yoyote...huwezi kuamini sijaenda Pasaka niko hapa Dodoma."
Sitta alisema pamoja na viongozi hao wawili wakuu wa Ukawa hawapokei simu, lakini amefanya jitihada ikiwamo kuwatumia ujumbe mfupi wa maneno (SMS), lakini hadi jana mchana alikuwa hajajibiwa.
"Sitaki kuongeza chochote kuhusu hili jambo kwa sababu kwa mazingira yenyewe nikisema chochote ninaweza kuharibu japo nina maoni yangu binafsi kuhusu hili, lakini sitaki kusema sasa," alisema Sitta.
Jana gazeti hili lilimtafuta Mbatia ambaye alikiri kuzungumza na Sitta. "Ni kweli amenipigia simu na nimemwambia kwamba nimemsikia, lakini siwezi kufanya uamuzi peke yangu, lazima nishuriane na wenzangu."
Hata hivyo, Mbatia alisema kwa mtizamo wake hadhani kama Sitta anaweza kutatua mvutano uliopo na kwamba wanaopaswa kusimamia suala hilo ni viongozi wa vyama vya siasa vinavyovutana.
"Mimi naamini katika maridhiano, lakini vyama vya siasa ndivyo vinaweza kutatua mzozo huu, kwa hiyo viongozi wa CCM ndiyo wanaweza kuonyesha nia ya kuzungumza, Sitta ni kiongozi wa Bunge ambaye kazi yake ni kusimamia uendeshaji wa vikao, hivyo suala la maridhiano kwake ni kumtwisha mzigo mzito ambao hapaswi kuubeba," alisema Mbatia.
Kanuni za uendeshaji wa Bunge hilo za 2014, zinasema kuwa ili ibara au Rasimu ya Katiba iweze kupitishwa itahitaji kuungwa mkono na theluthi mbili ya wajumbe kwa pande zote za Muungano.Soma zaidi>>>>>

Thursday, 17 April 2014

ATLETICO MINEIRO YATISHIA KUMPELEKA MAHAKAMANI ANELKA KWA KUGOMA KWENDA BRAZIL

264816-nicolas-anelka-1 Atletico Mineiro wamejibu shutuma kwamba Nicolas Anelka hakuwa anajua chochote kuhusu suala la uhamisho wa kujiunga na klabu hiyo ya Brazil na hata kufikia hatua ya kutishia kumfungulia mashtaka ya kumdai fidia mchezaji huyo.
Anelka, 35, aliposti video kwenye mtandao wa kijamii wa Facebook jana Jumatano asubuhi ambapo alionekana kukataa kwamba alikuwa amesaini kujiunga na mabingwa Copa Libertadores .
Hata hivyo,  raisi wa Atletico Mineiro, Alexandre Kalil, amepingana na Anelka, ambaye alimtangaza kumsaini tarehe 6 mwezi huu.
“Tutaelelezea kila kitu kuhusu uhamisho huu, kwa sababu tuna ushahidi wa kila kitu,” Kali aliwaambia waandishi wa habari.
“Tutakwenda FIFA. Itabidi atulipe fidia kwa kila kitu tulichotumia katika gharama za malazi na usafiri.”
Atletico Mineiro walitangaza wiki iliyopita kwamba wamefuta mpango wa kumsajili Anelka baada ya msjambuliaji huyo kushindwa kwenda kwa wakati Brazil.

MPIGA GITAA SKYLIGHT BAND CHIRI CHALLA AFARIKI GHAFLA

 10173726_10152036323227864_1413106576404088176_n
Mpiga Gitaa wa Skylight Band maarufu kwa jina la Chiri Challa(pichani) amefariki dunia ghafla usiku wa kuamkia April 17 katika Hospitali ya Muhimbili.
Taarifa za awali zimethibitishwa na uogonzi wa bendi hiyo kuwa mpiga gitaa huyo machachari amefariki baada ya kuugua kwa siku mbili ugonjwa wa kupooza nusu ya mwili wake na kuepelekea kutofanya kazi ipasavyo.
Kwa mujibu wa Meneja wa bendi hiyo Aneth Kushaba AK47 Ugonjwa wa kupooza ulipelekea mishipa ya damu kichwani kupasuka hivyo na kumsababishia maumivu makali sehemu kichwani.
10268531_10152035773597864_7736400417218686840_n
Kutokana na msiba huo uongozi unapenda kutoa taarifa kuwa Show ya Escape One iliyokuwa ifanyike Alhamis ya April 17 imeahirishwa hata hivyo uongozi unasikitika kumpoteza msanii huyo ambaye alikuwa ni kiungo muhimu wa bendi na inaungana na familia ya marehemu Chiri Challa kuomboleza kifo cha mpendwa wao na inatoa pole kwa familia na mashabiki wa Skylight Band na wapo bega kwa bega katika kipindi hiki kigumu.
Msiba na shughuli za mazishi zinafanyika maeneo ya Mwanyamala Ujiji mtaa wa Mpunga.
Kwa mawasiliano zaidi namba ya
 Meneja wa Bendi +255 715 677 499.