Ni utaratibu wa millardayo.com kukupatia
stori kubwa za Magazeti ya Tanzania kila siku kabla ya saa mbili kamili
asubuhi kutoka kwenye kurasa za kila gazeti kuanzia ya Udaku, Michezo
na hardnews kurasa za mwanzo na mwisho.
MATUKIO KATIKA PICHA YALIYO WEZA KUVUTIA DUNIANI KOTE
Asante kwa kututembelea mbeyagreennews kwa taarifa zaidi endelelea kututembela kila siku ,saa,dakika usipitwe na matukio kem kemu
MATUKIO KATIKA PICHA YALIYO WEZA KUVUTIA DUNIANI KOTE
Asante kwa kututembelea mbeyagreennews kwa taarifa zaidi endelelea kututembela kila siku ,saa,dakika usipitwe na matukio kem kemu
MATUKIO KATIKA PICHA YALIYO WEZA KUVUTIA DUNIANI KOTE
Asante kwa kututembelea mbeyagreennews kwa taarifa zaidi endelelea kututembela kila siku ,saa,dakika usipitwe na matukio kem kemu
MATUKIO KATIKA PICHA YALIYO WEZA KUVUTIA DUNIANI KOTE
Asante kwa kututembelea mbeyagreennews kwa taarifa zaidi endelelea kututembela kila siku ,saa,dakika usipitwe na matukio kem kemu
MATUKIO KATIKA PICHA YALIYO WEZA KUVUTIA DUNIANI KOTE
Asante kwa kututembelea mbeyagreennews kwa taarifa zaidi endelelea kututembela kila siku ,saa,dakika usipitwe na matukio kem kemu
Thursday, 5 June 2014
UKUAJI WA DENI LA TAIFA LA UMIZA VICHWA HIKI NDICHO KIASI AMBACHO KIRA MTANZANIA ANADAIWA!
Bunge la bajeti linaendelea bungeni mjini Dodoma ambapo sasa ni zamu ya wizara ya fedha na uchumi. Bajeti yake imewasilishwa na waziri wa fedha Saada Mkuya Salum ambapo bajeti yake imepita huku suala la deni la taifa likiendelea kuumiza vichwa vya wabunge wengi kwa kuendelea kukua siku hadi siku.
Suala hilo limeonekana kuwashtua wabunge wengi akiwemo Mheshimiwa Christina Lissu ambaye anasema fedha zinazokopwa na kuongeza deni la taifa zimekuwa hazitumiki katika miradi ya maendeleo.

Mhe. Lissu anasema “Mheshimiwa spika deni la taifa, tumeangalia hotuba ya kamati ya wizara hii ikieleza kwamba deni la taifa limekua kutoka trilioni 21 hadi 29 ikiwa ni ongezeko la trilioni 8 tu kwa miaka 7, kukopa ni sahihi na nchi yoyote inakopa lakini je fedha tunazokopa zinaenda katika miradi ya maendeleo? Mbona ukuaji huu wa deni hauendani na fedha zinazoelekezwa katika miradi ya maendeleo?.”
“Kwa mwaka huu karibu miradi yote ya maendeleo imepelekewa fedha chini ya asilimia 50, mbona ukuaji wa deni hauendani na fedha zilizoenda kwenye matumizi ya maendeleo? inawezekana tunakopa na tuaambiwa deni ni stahimilivu lakini kama fedha haiendi kupunguza matatizo ya wananchi inakuwa haina maana kukopa.”
Suala la kuchelewesha fedha zinazotengwa kwa ajili ya bajeti ya miradi mbalimbali limeonekana kuwagusa wabunge wengi ambapo Mhe. Asupta Mshana anasema;
“Kumekuwepo na tatizo kubwa la fedha tunazoidhinisha kama bunge kutotolewa kwa wakati na kufanya kazi kama zilivyopangiwa, tatizo ni kwamba tunaandaa bajeti kwa kutabiri bila kuwa na fedha mkononi. Ni vyema tukabadilisha utaratibu wa kuandaa bajeti zetu badala ya kuwa na Cash bajeti tuwe na Capital bajeti”
Pamoja na jitihada za serikali kupitia kukusanya kodi je mikakati ya ukusanyaji kodi inatosha? Mhe. David Kafulila anasema;
“Tufike mahala tuwe na mkakati wa kutosha kuhakikisha maeneo yote ambayo hatukusanyi kodi tunakusanya. Tumezungumza mara kadhaa juu ya watanzania kuashiriki kwenye uchumi wa nchi yao kwa kupitia masoko ya mitaji katika soko la hisa DSE ili watanzania washiriki kwenye uchumi wao, tusiwanyime fursa wazawa kushiriki katika uchumi wao.”
Wakati Serikali ikiendelea kubanwa juu ya suala hilo, Waziri Kivuli wa Fedha, James Mbatia amesema ukiligawanya deni hilo kwa idadi ya Watanzania milioni 45, kila mwananchi atakuwa anadaiwa Sh600,000.
KAMATI YA RUFANI YA UCHAGUZI KUKETI JUNI 9
Kamati
ya Rufani ya Uchaguzi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
inakaa Jumatatu (Juni 9 mwaka huu) kusikiliza rufani moja inayopinga
uamuzi wa Kamati ya Uchaguzi ya Simba.
Michael
Wambura amewasilisha rufani yake TFF akipinga uamuzi wa Kamati ya
Uchaguzi ya Simba iliyomwengua katika kinyang’anyiro cha kuwania urais
katika uchaguzi wa klabu hiyo unaotarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwezi
huu.
Kamati
hiyo inayoongozwa na Wakili Julius Lugaziya itakutana saa 5 asubuhi
kwenye hoteli ya Courtyard iliyopo Upanga, jijini Dar es Salaam.
NYOTA WAWILI COPA WAENDA BRAZIL
Wachezaji
wawili waliochaguliwa kwenda kwenye kambi ya Copa Coca-Cola ya Dunia
nchini Brazil wamekabidhiwa bendera tayari kwa safari hiyo inayofanyika
leo (Juni 4 mwaka huu).
Hafla ya kukabidhi bendera
hiyo kwa Ali Shabani Mabuyu na Juma Yusuf imefanyika leo katika hoteli
ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam. Naibu Mkurugenzi wa Maendeleo ya
Michezo katika Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Juliana
Yassoda ndiye alikabidhi bendera.
Wakati
Mabuyu kutoka Ilala alikuwa mchezaji bora wa michuano ya Copa Coca-Cola
kwa vijana wenye umri chini ya miaka 15 kwa mwaka 2013/2014, Yusuf
kutoka Zanzibar ndiye aliyeibuka mfungaji bora katika michuano hiyo.
Wachezaji
hao watakuwa katika kambi hiyo itakayokuwa katika Jiji la Sao Paulo kwa
siku kumi ambapo watafundishwa masuala mbalimbali ya mpira wa miguu.
Pia watashuhudia mechi ya ufunguzi ya Fainali za Kombe la Dunia katika
ya wenyeji Brazil na Croatia itakayochezwa Juni 12 mwaka huu.
BONIFACE WAMBURA
OFISA HABARI NA MAWASILIANO
SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)
. TANZANIA YA KWANZA AFRIKA MASHARIKI KATIKA USAFIRI WA MABASI YAENDAYO KASI -

Mh Pinda
WAZIRI
MKUU Mizengo Pinda amesema Tanzania ni miongoni mwa nchi za kwanza
katika Jumuiya ya Afrika Mashariki kuingia kwenye ubia na sekta binafsi
katika mradi mkubwa wa usafirishaji abiria.
Ametoa kauli hiyo leo mchana (Jumanne,
Juni 3, 2014) wakati akifungua Mkutano wa Majadiliano yenye lengo la
kuutangaza mradi wa mabasi yaendayo kasi kwenye ukumbi wa Mlimani City.
Mkutano huo wa siku mbili, utamalizika kesho (Jumatano, Juni 4, 2014).
Waziri Mkuu amesema kutèkelezwa kwa
mradi huo kutatoa fursa za ubunifu utakaowezesha kupatikana kwa
suluhisho la usafiri mijini na hasa kwenye miji inakua kwa kasi barani
Afrika.
"Mbali ya kutoa huduma za hali ya juu,
za haraka na ambazo siyo ghali kwa wakazi wa Jiji la Dar es Salaam, nia
ya Serikali ni kuona mfumo mpya wa matumizi ya kadi kwenye mpango huu wa
usafiri unatumika ipasavyo," alisema.
Alisema ni matumaini ya Serikali kwamba
wadau kutoka sekta binafsi ambao ni wazawa na wa kutoka nje ya nchi
watashiriki kwenye mradi huu ili uweze kuboresha matumizi ya kadi ambayo
mtu hatatakiwa kulipia fedha taslimu akiwa ndani ya basi bali kutumia
kadi anayoilipia kabla ya kuingia ndani ya basi husika.
Akizungumza na waandishi wa habari mara
baada ya kufungua mkutano huo, Waziri Mkuu alisema Serikali iliamua
kuanzisha mradi huo ili kupunguza msongamano wa magari kwenye barabara
za Jiji la Dar es Salaam.
"Hii ni awamu ya kwanza ambayo
inakaribia kukamilika na inaanzia Kimara hadi Kivukoni na itakuwa na
matawi mawili ya Morocco na Karikoo. Mradi wote una awamu sita za ujenzi
kuelekea maeneo tofauti ya Jiji," alisema.
Mbali na mradi huo wa mabasi yaendayo
kasi, Serikali inaangalia uwezekano wa kutumia usafiri wa majini kwa
kutumia boti kati ya Dar es Salaam na Bagamoyo kama njia mojawapo ya
kupunguza msongamano wa magari jijini Dar es Salaam.
“Vilevile tutaimarisha usafiri wa reli
kama njia nyingie ya kupunguza tatizo hili. Dk. Mwakyembe (Waziri wa
Uchukuzi) ameanza na sote tumeona ni jambo linalowezekana. Cha msingi ni
kuimarisha tu usafiri huu,” aliongeza Waziri Mkuu.
Mapema, akiwakaribisha wajumbe wa
mkutano huo, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI), Bibi Hawa
Ghasia alisema Serikali imedhamiria kuhakikisha kuwa mradi huo
unafanikiwa.
Pia
alitumia fursa hiyo kuishukuru Benki ya Dunia ambayo alisema imetoa
kiasi cha dola za Marekani milioni 200 kwa ajili ya kufadhili mradi huo.
Mkutano huo unawashirikisha wadau
mbalimbali wakiwemo wa ndani na wa nje wanaotarajiwa kutoa huduma za
mabasi makubwa na madogo, utoaji tiketi, ulinzi, usafi na huduma za
maduka.
TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI
MTU MMOJA ALIYETAMBULIKA KWA JINA LA DANIEL JOSEPH (20) FUNDI REDIO, MKAZI WA MTAA
WA MWAKA WILAYANI MOMBA ALIFARIKI DUNIA WAKATI ANAPATIWA MATIBABU
KATIKA KITUO CHA AFYA TUNDUMA BAADA YA KUPIGWA NA KUNDI LA WANANCHI
WALIOAMUA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI WAKIMTUHUMU KUWA NI MWIZI.KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA WANANCHI KUACHA TABIA YA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA BADALA YAKE WAJENGE TABIA YA KUWAFIKISHA WATUHUMIWA WANAOWAKAMATA KWA TUHUMA MBALIMBALI KATIKA MAMLAKA HUSIKA KWA HATUA ZAIDI ZA KISHERIA.
TAARIFA ZA MISAKO:
MSAKO WA KWANZA:
JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LAKAMATA SILAHA/BUNDUKI MBILI AINA YA GOBOLE ZENYE NAMBA CH 777 NA CH 1031.
SILAHA HIZO ZILIKAMATWA KATIKA MSAKO ULIOFANYIKA MNAMO TAREHE 04.06.2014 MAJIRA YA SAA 14:00 MCHANA KATIKA KITONGOJI CHA MTAKUJA, KIJIJI CHA MWIJI, KATA YA LUALAJE, TARAFA YA KIPEMBAWE, WILAYA YA CHUNYA, MKOA WA MBEYA. AIDHA, WATUHUMIWA WAWILI WAWINDAJI HARAMU WALIOFAHAMIKA KWA MAJINA YA SURUALI MWAIKONYOLE NA SAMSON TUNTUMA WOTE WAKAZI WA KIJIJI CHA MWIJI WALIKIMBIA MARA BAADA YA KUWAONA ASKARI. JUHUDI ZA KUWATAFUTA ZINAENDELEA.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII KUTOA TAARIFA KATIKA MAMLAKA HUSIKA ZA MTU/WATU WANAOMILIKI SILAHA KINYUME CHA SHERIA ILI WAKAMATWE NA SHERIA ICHUKUE MKONDO WAKE.
MSAKO WA PILI:
JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA WATU WAWILI WALIOFAHAMIKA KWA MAJINA YA 1. JOSEPH PETER (55) NA 2. DAIMON MWALUKASA WOTE WAKAZI WA ITEZI WAKIWA NA POMBE HARAMU YA MOSHI [GONGO] UJAZO WA LITA SABA [07].
WATUHUMIWA WALIKAMATWA MNAMO TAREHE 04.06.2014 MAJIRA YA SAA 10:45 ASUBUHI KATIKA ENEO LA UYOLE, KATA YA IGAWILO, TARAFA YA IYUNGA, JIJI NA MKOA WA MBEYA. WATUHUMIWA NI WAUZAJI NA WATUMIAJI WA POMBE HIYO, TARATIBU ZA KUWAFIKISHA MAHAKAMANI ZINAFANYIKA.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII HASA VIJANA KUACHA TABIA YA KUTUMIA POMBE HARAMU YA MOSHI KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI.
Imesainiwa na:
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA
Sunday, 1 June 2014
DIAMOND AWEKA HISTORIA NEW JERSEY NCHNIN MAREKANI
All
Star Club Elizabeth New Jersey Diamond akikamua licha ya show kuchelewa
kuanza na wapenzi wa Diamond kushikwa na jazba wakitaka aendelee lakini
ikashindika kutokana na muda wa kufunga club kufika. Picha zote na Vijimambo Blog
AJ nae akifanya yake baada ya kupewa nafasi ya ufunguzi katika show hiyo iliyofanyika New Jersey.
AJ
Ubao na Dirty Hary wakishambulia jukwaa kwenye show ya kufubgua pazia
iliyoanyika New Jersey na baadae Prezidaa wa Wasafi, Diamond Plutnumz
kuwapagawisha mashabiki wake wa ukanda wa pwani ya mashariki.
Ni
Rais wa Wasafi akishambulia jukwaa akiwa na madancer wake kwenye show
ya kukata na shoka iliyofanyika New Jersey na kuvuta mashabiki kutoka
kila kona ya pwani ya mashariki ambayo ni DC, PA, NJ, NY, CT, MA na
kwingineko.
Diamond
mwanamuziki wa kizazi kipya anayekimbiza vibaya mno kwenye anga za
Bongo Flava akipagawisha mashabiki wake New Jersey nchini Marekani.
Diamond na madancer wake wakijaribu kukata kiu ya mashabiki wake wa pwani ya mashariki.

Wapenzi wa Diamond wakipagawa na show ya Diamond iliyofanyika All Star Club Elezabeth NJ.

Shabiki akidata na show ya pezidaa wa wasafi.

Shabiki akidatishwa na moja ya wimbo wa Diamond na kushindwa kujizuia kupanda jukwaani.

Mashabiki wa Diamond wakipagawa huku wengine wakipata taswira za hapa na pale. kwa picha zaidi BOFYA HAPA

Wapenzi wa Diamond wakipagawa na show ya Diamond iliyofanyika All Star Club Elezabeth NJ.

Shabiki akidata na show ya pezidaa wa wasafi.

Shabiki akidatishwa na moja ya wimbo wa Diamond na kushindwa kujizuia kupanda jukwaani.

Mashabiki wa Diamond wakipagawa huku wengine wakipata taswira za hapa na pale. kwa picha zaidi BOFYA HAPA
HIVI NDIVYO KILI MUSIC TOUR ILIVYO VUNJA REKODI JIJINI MWANZA
Msanii
wa Bongo flava, Ben Pol akitumbuiza maelfu ya wakazi wa Mwanza wakati
wa show ya Kilimanjaro Music Tour iliyofanyika katika Uwanja wa Kirumba
na kuwavutia maelfu ya mashabiki. Ziara hii inadhaminiwa na Kilimanjaro
Premium Lager.
Msani
wa muziki wa dance, Christian Bella akikonga nyoyo za wakazi wa Mwanza
katika show ya Kilimanjaro Music Tour iliyofanyika katika Uwanja wa
Kirumba na kuwavutia maelfu ya mashabiki. Ziara hii inadhaminiwa na
Kilimanjaro Premium Lager.
Msanii
wa bongo flava, Fid Q akizungumza na wakazi wa Mwanza wakati
akitumbuiza katika show ya Kilimanjaro Music Tour iliyofanyika katika
Uwanja wa Kirumba na kuwavutia maelfu ya mashabiki. Ziara hii
inadhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager.
Msanii
wa Bongo Flava Izzo Biznez akifanya vitu vyake wakati wa show ya
Kilimanjaro Music Tour iliyofanyika katika Uwanja wa Kirumba na
kuwavutia maelfu ya mashabiki. Ziara hii inadhaminiwa na Kilimanjaro
Premium Lager.
Wakazi
wa Mwanza wakiwa wamefurika kwa maelfu huku wakishangilia wakati kundi
la Weusi likitumbuiza katika show ya Kilimanjaro Music Tour
iliyofanyika katika Uwanja wa Kirumba na kuwavutia maelfu ya mashabiki.
Ziara hii inadhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager.
Vanessa
Mdee na Ommy Dimpoz wakimakinika katika show ya Kilimanjaro Music Tour
iliyofanyika katika Uwanja wa Kirumba na kuwavutia maelfu ya mashabiki.
Ziara hii inadhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager.
Msanii
wa muziki wa kizazi kipya, Rich Mavoko akipagawisha wakazi wa Mwanza
katika show ya Kilimanjaro Music Tour iliyofanyika katika Uwanja wa
Kirumba na kuwavutia maelfu ya mashabiki. Ziara hii inadhaminiwa na
Kilimanjaro Premium Lager.
Vanessa
Mdee na Fid Q wakishirikiana kutoa burudani wakati wa show ya
Kilimanjaro Music Tour iliyofanyika katika Uwanja wa Kirumba na
kuwavutia maelfu ya mashabiki. Ziara hii inadhaminiwa na Kilimanjaro
Premium Lager.
Wakazi
wa Mwanza wakiwa wamefurika kwa maelfu huku wakishangilia wakati kundi
la Weusi likitumbuiza katika show ya Kilimanjaro Music Tour
iliyofanyika katika Uwanja wa Kirumba na kuwavutia maelfu ya mashabiki.
Ziara hii inadhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager.
Msanii
wa miondoko ya Bongo flava, Young Killer akimtambulisha mama yake mzazi
wakati wa show ya Kilimanjaro Music Tour iliyofanyika katika Uwanja wa
Kirumba na kuwavutia maelfu ya mashabiki. Ziara hii inadhaminiwa na
Kilimanjaro Premium Lager.
MTOTO Nasra Said aliyekuwa akiishi kwenye box kwa miaka minne afariki Dunia

MTOTO
Nasra Said aliyekuwa akiishi kwenye box kwa miaka minne akidaiwa
kuteswa na mama yake mkubwa baada ya mama yake kufariki, huku akikosa
uangalizi wa karibu, chakula, tiba na huduma nyingine muhimu AFARIKI
DUNIA katika Hospitali ya Taifa MUHIMBILI usiku wa kuamkia leo majira ya
saa saba, tatizo ni Nimonia na homa ilipanda sana.
R.I.P NASRA wewe mbele sisi nyuma tutakufuata, Tulikupenda lakini Mungu amekupenda zaidi.
MSIBA ,WAZIRI LUKUVI AFIWA NA BABA MKWE WAKE
MAMA MZAZI WA MH ZITTO KABWE AFARIKI DUNIA

Mbunge
wa Jimbo la Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe, asubui hii amefiwa na mama
yake mzazi Bi Shida Salum, aliyeugua kwa muda mrefu.
Pichani ni Mama mzazi wa Zitto Kabwe enzi za uhai wake.
Taarifa
ya msiba huu imethibitishwa na yeye mwenye Zitto Kabwe kupitia mtandao
wa kijamii wa Twitter kama inavyosomeka hapo chini.

mbeyagreennewsblog tunatoa pole kwa Zitto Kabwe, familia na wote walioguswa na msiba
huu Mwenyezi Mungu awatie nguvu katika kipindi hiki kigumu.
MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AHANI MSIBA WA BABA YAKE ROSTAM AZIZI JIJINI DAR JANA
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akisalimiana na Rostam Azizi, wakati alipofika nyumbani kwake Oysterbay
jijini Dar es Salaam, leo Mei 31, 2014 kwa ajili ya kumpa pole kwa
kufiwa na Baba yake mzazi aliyefariki katikati ya wiki hii.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akijumuika na waombolezaji waliofika nyumbani kwa Rostam Azizi,
Oysterbay jijini Dar es Salaam, leo Mei 31, 2014 kwa ajili ya kumpa pole
kwa kufiwa na Baba yake mzazi aliyefariki katikati ya wiki hii. Picha
na OMR
Sheikh
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa, akitoa mawaidha wakati wa
dua maalum iliyofanyika nyumbani kwa Rostam Azizi Oysterbay kumuombea
Baba mzazi wa Rostam, aliyefariki katikati ya wiki hii.
Baadhi ya waombolezaji walioshiriki dua hiyo maalum nyumbani kwa Rostam Azizi.
OFFICIAL: KOCHA MPYA WA YANGA NI MARCIO MAXIMO

Official: Kocha mpya wa Yanga ni Marcio Maximo - Yusuph Manji kathibitisha
Tutakuletea habari zaidi endelea kutembelea mtandao huu wa mbeyagreennews
ENGLAND WAELEKEA MIAMI KUWEKA KAMBI YA MANDALIZI YA KOMBE LA DUNIA

Tabasamu kubwa: Alex Oxlade-Chamberlain (kushoto) akiwa amekaa na Daniel Sturridge na nyuma yao ni Raheem
Sterling (kushoto) na Danny Welbeck

Wanakwea pipa: Kikosi cha England kimesafiri kwa ndege kwenda Miami kuendelea na maandalizi ya kombe la dunia

Wachezaji wa England wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya kwenda Miama.
Imechapishwa Juni 1, 2014, saa 11:32 jioni
KUNA
mdahalo mkubwa kama England wapo tayari kwa kombe la dunia, lakini
vijana wa `simba watatu` hawana wasiwasi kabisa kama walivyoonekana
katika picha ya pamoja kabla ya kwend Brazil.
Kikosi
cha Roy
Hodgson kilipiga picha ya pamoja kabla ya kupanda ndege kwenda Miami
kuweka kambi yao ya maandalizi ya kombe la dunia mwezi huu na watacheza
mechi mbili za kirafiki kabla ya kuwasili rasmi Marekani kusini.
GHANA YATAJA KIKOSI CHA WACHEZAJI 23 WATAKAO CHEZA KOMBE LA DUNIA BRAZIL,

Imechapishwa Juni 1, 2014, saa 11: 45 jioni
KOCHA mkuu wa timu ya taifa ya Ghana, Kwesi Appiah ametaja kikosi chake cha mwisho cha wachezaji 23 kwa ajili ya fainali za kombe la dunia zinazoanza kushika kasi mwezi huu nchini Brazil.
Kikosi hicho cha Appiah kinajumuisha wachezaji 16 wanaokwenda kucheza fainali hizo kwa mara ya kwanza, huku nahodha Asamoah Gyan na Sulley Muntari wakiwa wakongwe wanaokwenda kucheza fainali zao za tatu mfululizo, wakati Jonathan Mensah, Michael Essien, Kwadwo Asamoah, Andre Ayew na Kevin-Prince Boateng wanakwenda kucheza fainali hizo kwa mara ya pili.
Kocha huyo mwenye miaka 53 amewaacha majeruhi Jerry Akaminko, Jeffrey Schlupp na David Accam katika kikosi hicho kinachoelekea Miami kuweka kambi ya maandalizi ya mwisho ambapo kitacheza mechi ya kirafiki juni 9 dhidi ya Korea kusini
Akaminko alipata majeruhi jana jumamosi katika kipigo cha bao 1-0 dhidi ya Uholanzi kwenye mechi ya kirafiki na atafanyiwa upasuaji utakaomfanya akae nje ya uwanja kwa miezi mitatu.
Ghana iliyofika robo fainali mwaka 2010 ipo kundi G pamoja na nchi za Marekani, Ujeruman na Ureno.
Kikosi kamili:
Walinda Mlango:Fatau Dauda (Orlando Pirates), Adam Kwarasey (Stromsgodset), Stephen Adams (Aduana Stars)
Mabeki: Samuel Inkoom (Platanias), Daniel Opare (Standard Liege/Porto), Harrison Afful (Esperance), John Boye (Rennes), Jonathan Mensah (Evian), Rashid Sumalia (Mamelodi Sundowns)
Viungo: Michael Essien (AC Milan), Sulley Muntari (AC Milan), Rabiu Mohammed (Kuban Krasnodar), Kwadwo Asamoah (Juventus), Emmanuel Agyemang-Badu (Udinese), Afriyie Acquah (Parma), Christian Atsu (Vitesse), Albert Adomah (Middlesbrough), Andre Ayew (Marseille), Mubarak Wakaso (Rubin Kazan)
Washambuliaji: Asamoah Gyan (Al Ain), Kevin-Prince Boateng (Schalke 04), Abdul Majeed Waris (Valenciennes), Jordan Ayew (Sochaux
BAADA YA KUTEMWA, NAVAS AWATAKIA KILA LA KHERI HISPANIA KUTETEA KOMBE LA DUNIA

Imechapishwa Juni 1, 2014, saa 12:01 jioni
BAADA ya kuachwa na Vicente del Bosque, Jesus Navas na Daniel Carvajal wamewatakia kila la heri
wachezaji wenzao wa timu ya taifa ya Hispania kueleka kutetea ubingwa wao wa
kombe la dunia mwaka huu nchini Brazil.
Navas aliachwa katika kikosi chake na kocha
alieleza kuwa sababu ni kutokuwa fiti baada ya kupona majeruhi ya kifundo cha
mguu siku za karibuni.
Nyota huyo mwenye miaka 28 akucheza mchezo wa mwisho
wa ligi kuu nchini England mwezi aprili, lakini amesema amafurahi sana
kwasababu ameimarika.
“Ninajivunia kuimarika kwangu kwa wakati muafaka
na nilitegemea kulitetea taifa langu nchini Brazil”. Ameandika Navas katika
mtandao wake wa Twita.
“Nawatakia kila la kheri wachezaji wenzangu na
kocha wangu mafanikio makubwa katika kutetea ubingwa”.
Naye beki wa Real Madris, Carvajal alikuwa
miongoni mwa wachezaji wa kikosi cha awali cha wachezaji 30 kabla ya kuachwa
katika kikosi cha mwisho.
Beki huyo ametwiti: “ Ni aibu kukosekana katika
kikosi cha mwisho, lakini najivunia kwasababu nilikuwa karibu kutajwa. Nawatakia
Hispania kila la heri”.
Wakati huo
huo kiungo wa Atletico Madrid, Koke amefurahi kujumuishwa katika kikosi cha
Hispania baada ya kufanya vizuri katika michuano ya UEFA na kwenda kushiriki
fainali zake za kwanza za kombe la dunia.
“Nimefurahi kuchaguliwa kwenda Brazil, nitakuwa
makini kuisaidia timu yangu”.
TAIFA STARS YASONGA MBELE BAADA YA KUTOA SARE YA 2-2 SASA KUKUTANA NA MSUMBIJI

Na Baraka Mpenja
Imechapishwa Juni 1, 2014, saa 16:31 jioni
Goooo!. Hivyo ndivyo watangazaji walitangaza mara nne katika uwanja wa Taifa wa Harare nchini Zimbabwe.
Taifa stars ya Mart Nooij itakabiliana na Msumbiji
katika mchezo wa mwisho wa mtoano kuwania kupangwa hatua ya makundi kusaka
tiketi ya fainali za mataifa ya Afrika mwakani nchini Morroco.
Hii imetokana na sare ya 2-2 waliyopata jioni hii
dhidi ya wenyeji wao, timu ya taifa ya Zimbabwe.
Zimbabwe walioripotiwa kuwafanyia hujuma vijana wa
Tanzania wameambulia patupu leo hii baada ya kuoneshwa soka safi na vijana wa
Tanzania.
Haikutegemewa kuwa mechi ya mabao mengi kiasi
hiki, lakini Zimbabwe ndio walianza kuamsha `mizimu` ya vijana wa Taifa stars waliokuwa
wanamtazama kiongozi wao wa msafara, Rais wa TFF, Jamal Malinzi akiwa jukwaani.
Bao la dakika ya 10 walilopata Zimbabwe kupitia
kwa Phiri D liliwashitua mashabiki wa Tanzania, lakini nahodha wa Taifa Stars,
Nadir Haroub Canavaro katika dakika ya 21 aliwazisha bao hilo na kuufanyaubao
wa matangazo kusomeka 1-1 mpaka kipindi cha kwanza kinamalizika.
Wakati Zimbabwe wakiwa katika presha ya kusaka bao
la pili, dakika ya 46 kipindi cha pili walifanya makosa na Thomas Emmanuel
Ulimwengu hakufanya makosa na kuwaadhibu
goli la pili.
Dakika ya 55 kipindi hicho cha pili, Katsande W
aliifungia Zimbabwe bao la pili la kusawazisha.
Baada ya hapo mpira ulianza kuchezwa kwa timu zote
kutafuta mabao zaidi, lakini wenyeji ndio walikuwa kwenye presha kubwa zaidi
kwasababu tayari Stars walikuwa na mtaji wa mabao zaidi.
Taifa stars ya Mart Nooij ilionesha kiwango safi
na upinzani mkubwa ugenini na kuwafurahisha watanzania wachache waliokuwa
uwanjani na waliokuwa wanaangalia kupitia televisheni.
Haikuwa kazi nyepesi kwa vijana wa Tanzania
kuwafunga Zimbabwe, lakini jitihada kubwa walizofanya na kutambua kuwa
mamilioni ya watanzania wapo nyuma yao, ilitosha kuwapa morali kubwa.
Mechi ya kwanza ambayo Stars ilishindi bao 1-0
uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, tatizo kubwa lilionekana katika safu ya
kiungo, lakini leo vijana walijidhatiti na kuonesha kandanda zuri.
Canavaro amekuwa kiongozi wa kuigwa kwani
alionesha ushupavu wa kuwaelekeza njia wenzake ikiwemo kufunga bao muhimu la
kusawazisha.
Beki kazi yake ni kulinda, inapofika wakati
anafunga, basi amejiongezea majukumu kwa lengo la kuisaidia timu yake ipate
mafanikio.
Kuwa nahodha sio kuvaa kitambaa tu bali ni pamoja
na kuisaidia timu kama wanavyofanya akina Sergio Ramos. Kazi nzuri Nadir Haroub
`Canavaro`.
Ulimwengu ni mchezaji wa TP Mazembe. Kuna faida ya
kuwa na wachezaji wa kimataifa kama yeye. Kudhihirisha umuhimu wake, alifunga
bao safi na kuwavusha watanzania hatua inayofauta. Kazi nzuri kijana.
Kwa matokeo ya leo, Taifa stars imefuzu hatua ya
mwisho ya mtoano kwa wastani wa mabao 3-2 kuwania kupangwa hatua ya makundi
kusaka tiketi ya kucheza fainali za mataifa ya Afrika.
Hii inatokana na ushindi wa bao 1-0 iliopata
uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam katika mchezo wa kwanza na matokeo ya 2-2
mjini Harare jioni hii.
Kwa maana hiyo, Taifa Stars inajiandaa kuutafuna
mfupa wa Msumbiji katika hatua ya mwisho ya mtoano.
Msumbiji walifuzu hatua hiyo kwa wastani wa mabao
5-0 baada ya juzi kutoka suluhu ya bila kufungana na Sudan Kusini Ugenini,
wakati waliibuka na ushindi mnono wa mabao 5-0 mjini Maputo.
Msumbiji wana historia ya kuwaharibia Taifa stars
katika michezo muhimu ya mashindano, hivyo ni jukumu la wachezaji na kocha
Nooij kupanga mikakati kabambe ya kuwanyamazisha `Mamba hao weusi`.
Mechi nyingine iliyomalizika jioni hii ni baina ya
Lesotho na Liberia na kushuhudia Lesotho wakiibuka na ushindi wa mabao 2-0.
Mechi nyingine zinaendelea na utapata matokeo yake
baadaye.













































































